Lwakatare aomba Bukoba wapunguziwe kodi vifaa vya ujenzi, Magufuli amjibu ajenge kiwanda awapunguzie

Sasa roho mbaya ipi mdau unajua sisi watanzania tunapenda sana kudanganywa hivyo vifaa haagizi yeye wala bei yake haijui yeye achojua lipa kodi na yule mfanyabiashara analeta kwa ajili ya kupata faida leo hii uje umwambie akushushe bei kivipi
Kama kweli walikuwa na nia ya kupata vya raisi wangechangishana wananchi pamoja na wanabukoba , kagera walio nje ya huo mji kwa umoja wao wangenunua material za ujenzi hapo Dubai ambazo ni bora na ni rais wakakodi kontena la pamoja halafu likifika hapo bandarini hapo sasa ndio mtaweza kuongea kiswahili na Rais na mkaelewana lakini vinginevyo ni ngumu
Stop that nonsense acha kushabikia utumbo wa wakubwa.Hivi mtu akikwambia ninaumwa njaa sasa hivi anakuomba msaada,wewe kwa akili zako utamwambia achukue mkopo wa tractor na mbegu alime shamba?Si atakufa hata kabla ya kuanza kulima?

Tin iliachwa kuchimbwa tokea uhuru ,ni kazi ya serikali kuweka mazingira safi,Je Magu anajua kwanini wazungu walifunga mgodi au ndio kupayuka tu jukwaani
 
Kinachonihuzunisha mbunge anawaombea wananchi wake vifaa vya ujenzi vishuke bei....cha ajabu rais anajibu kisiasa tena amesahau kuwa hiyo ni moja ya ahadi zake katika kampeni.....cha kushangaza zaidi ni pale rais anapotoa majibu na wananchi wanashangilia
 
Mbunge wa Bukoba Wilfred Lwakatare kwenye mkutano wa Magufuli na Bukoba aliomba Bukoba wapunguziwe vifaa vya ujenzi kama bati na simenti kwa kuwa serikali haiwezi kumjengea kila mwananchi nyumba

Akitolea mfano Kikwete kuwapa fidia ya ng'ombe wafugaji waliopatwa na janga la Ukame walipewa ng'ombe na Nyerere alivyofanya kwa CDA dodoma kwa kuwapa msaada wa kodi

Magufuli alimjibu kwa kumpa changamoto ya kujenga kiwanda Kyelwa wauze mabati hata kwa 1,000 kwa sababu kuna madini ya bati Kyelwa na sio mabati ya kutoka Dar na China na ni ya wafanyabiashara.


Hata kubadili matumizi ya misaada ya wahanga kuwa ya kujengea miundo ni mkomoeni tu ili watu waone upinzani hauwezi kuwasaidia, sasa sote tukiwa na mawazo mamoja tutajifunza kutokea wapi?
 
Kuna clip moja iliwahitolewa ya huyu jamaa akisema akiwa igwee watu watalimia meno! Kwa mbaliiiiii naona anatembea kwenye maneno Yake.
 
Huyo ndio Magufuli hakopeshi.!
Ubaguzi tu! na dhambi hii ina haki iwatafune kabla ya 2020 mtakuwa mmepotezana hata kama mnafikiri wananchi hawawezi kuwafanya chochote Mungu mwenyewe atawakomboa kwa mkono wake, waisrael walikaa utumwani miaka 430 kipindi kirefu kuliko utawala wowote kupata kutokea lakini wakati ulipofika walitoka ndivyo itakavyo kuwa hata kwenu hata kama wewe na mimi hatutakuwepo, ni heri leo mngetumia dhamana hiyo kurekebisha mlipokosea mpaka mkapelekea watu waliokuwa wamoja chini ya utawala wa Mwalimu Nyerere wagawanyike kuliko kuwakebehi, mbegu mnayopanda ndiyo mtakayo vuna nawaambia, nyie sinzieni na kipisi cha sigara tu mchome kibanda!!
 
Kamjibu VIZURI SANA akili ya VYA BURE SI KWA ZAMA HIZI.......kwenye hili acheni UNAFIKI
Wewe ndio uache unafiki mbona mnatoa tax holiday kwa wanaojiita wawekezaji na kuruhusu kuchezewa akili kwa kubadili usajili kila baada ya muda kwisha na wala hamna ujasiri wa kusema kwamba hapana ila kukebehi waafrika wenzenu ndio mahodari poor Africa, ndio maana wengine wanafikiri kulitawala tena bara hili kwani kwa aibu hizi tunasibitisha maneno yao! Shame on you!
 
Back
Top Bottom