Lowassa achomoza Kamati Kuu ya CCM Dodoma

Naomba unifafanulie kidogo mkuu....
Hii ikoje?
Hilo jipu ni nani?

Jamani NIfa hujanifahamu kweli hapo?Escrow Scandle+UDA Scandle+Lugumi Scandle= MAJIPU...........Yanayohitaji kupasuliwa maana yapo sehemu nyeti.
 
Kuna namna mbalimbali za kuelewa kwanini Lowassa anaendelea kuwa tishio kubwa kwa CCM. Tulitazame suala hili kwa jicho la Kiuchumi.

1. Deni la Taifa na Umaskini wa Watanzania

Kwa miaka 47 ya uhuru (1961-2008), jumla ya Deni la taifa lilikuwa ni TZS Trilioni 15.

· Je Deni hili lilitumikaje?


Katika kipindi chote cha uhuru, serikali ya CCM (hasa chini ya Mwalimu Nyerere) iliwekeza vyema mikopo hii kwa kujenga miradi mikubwa ya umeme kwa mfano (hydro power plants), reli ya Tazara, bomba na mafuta kwenda Zambia (TAZAMA), Viwanda mbalimbali, na pia kuboresha hali za maisha ya wananchi. Mengi ya haya leo ni ‘water under the bridge’. Gone! Huduma za kijamii (hasa elimu na afya) zinazidi kuzorota licha ya kinachoshangiliwa “kasi kubwa ya kukua kwa uchumi”, hakuna umeme wa uhakika, umaskini umezidi kuongezeka miongoni mwa wananchi, nk. Haya ni masuala ambayo katika kampeni za Urais, Lowassa aliahidi kuyatafutia ufumbuzi. Baada ya CCM kutangazwa ‘mshindi’, mikakati ya serikali ya awamu ya tano ikalenga kuhakikisha kwamba yale yote aliyo ahidi Lowassa kwa wananchi yanapatiwa ufumbuzi. Pengine kuna nia njema chini ya serikali ya sasa, lakini changamoto kubwa kwa serikali hii ni kwamba kutokana na ‘root-cause’ ya umaskini nchini, ambayo inaenda sambamba na ‘elites in CCM’ kunufaika, ukweli unaendelea kubakia kwamba ‘mabadiliko ya kweli ni lazima yatokee nje ya CCM’. Ni vigumu kwa CCM kuleta mabadiliko ya kweli bila ya kugusa maslahi ya wakubwa ndani ya chama ambao ndio waliotufikisha hapa.

2. Sera ya ‘Ubinaifishaji’:

Wana CCM na wananchi wengi kwa ujumla wake kamwe hawatasahau kauli ya Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana (akiongozana na Mwenezi wake Nape Nnauye) aliyoitoa katika moja ya ziara zake zilizobatizwa maneno “Uimarishaji wa Chama”. Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu (CCM) alieleza kwa uwazi, ukweli na masikitiko makubwa na kukiri kwamba matatizo yanayowakabili wananchi yametokana na CCM. Kinana akaenda mbali na kutoa mfano kwamba:

“Tulikosea sana katika sera yetu za ‘Privatization’. Athari za sera hii mbovu ni pamoja na:

· Ajira nyingi kwa wananchi kutoweka.

· Mashirika mengi yaliyojengwa kwa fedha za walipa kodi kuuzwa kwa bei chee, nk.

· Hata mashirika ya umma ambayo bado yalikuwa yanaendeshwa kwa faida na kuchangia pato la taifa (GDP) na pato la serikali (tax revenues), nayo yakauzwa kwa bei ya karanga. Mifano ni pamoja na NBC, TBL, TCC n.k.

Ubinaifisishaji holela wa mashirika ya umma ni moja ya jipu kubwa linalopaswa kutumbuliwa. Jipu hili linarudi kwa kasi lakini kwa sura tofauti kidogo. Sura mpya ni ile ya miradi ya ubia baina ya sekta binafsi na sekta ya umma, yani - Public Private Partnerships (PPPs).

Miradi ya PPPs ina athari kubwa katika deni la taifa. Kwa mfano miradi hii inatoa fursa kwa wawekezaji wa nje kuwekeza katika mradi Fulani lakini mara nyingi wawekezaji huwa wanafanya hivyo pale tu serikali inapokubali ‘to guarantee’ malipo au inapo commit to bail out the investor incase investment fails. Kwa maana hii, miradi mingi ya PPP ina same fiscal impact kama ya serikali kukopa moja kwa moja. Lakini kitu kibaya zaidi ni kwamba ‘payment obligations are not included in debt figures’. Serikali ikijumuisha hizi obligations kwenye mahesabu ya deni la taifa, kiwango tunachodaiwa nje ya nchi kitakuwa ni kikubwa zaidi ya kile tunachoelezwa na takwimu za serikali.

In fact, gharama ya miradi hii ya PPP kwa serikali ni kubwa kuliko gharama ambayo serikali ingeingia kwa kuwekeza yenyewe moja kwa moja. Hii ni kwa sababu mikopo ya sekta binafsi (tofauti na concessional loans) ina gharama zaidi kwa walipa kodi, private contractors demand more profits, na muhimu zaidi, negotiations kati ya serikali na wawekezaji katika miradi hii kwa kawaida huwa inapendelea zaidi mwekezaji kuliko serikali. Kwa maana nyingine, mwekezaji huwekeza pale tu maslahi yake yote yanapo angaliwa na serikali.

The elites in CCM wanapenda sana miradi ya aina hii kwa sababu, kwanza huwa wanapata 10%, lakini muhimu zaidi, such projects enable debt payments to be hidden from public view. Wananchi wengi hawana uelewa juu ya jinsi gani miradi ya PPP kama ile inayotangazwa katika mpango wa pili wa maendeleo wa taifa (2016-21) inaweza kuwa na athari kubwa katika kodi zao.

Edward Lowassa na PPPs

Lowassa anarekodi ya kutumbua jipu hili, suala ambalo limekitikisa CCM sio chini ya mara mbili. Tujadili hilo kwa undani.

· “City Water” Public Private Partnership.

Mradi wa City Water ulihusisha mkopo kwa serikali wa zaidi ya Dola Milioni 80. City Water ilikuwa ni consortium of: Biwater (UK) & HP Gauff Inegnieue (Germany),na ulihusisha mmaji safi na maji taka kwa jiji la Dar-es-salaam na vitongoji vyake. Akiwa Waziri wa Maji, Edward Lowassa alinusa uozo katika mradi huu kwani kwa tathmini yake, mradi ule haukuwa na ‘value for money’ kwa sababu, pamoja na mengine, mradi haukuwa na uwezo wa kufikia malengo yake mengi kwa sababu wawekezaji husika hawakuwekza the ‘equity they promised’. Kwahiyo ili kuokoa fedha za walipa Kodi zisipotee kwa mradi usiokuwa na tija kwa wananchi, Lowassa akauvunja mkataba huu na kuibuka shujaa. Jambo hili halikuwapendeza viongozi wengi ndani ya CCM kwa sababu tulizojadili huko juu (vested interests by elites).

Katika kampeni za urais 2015, pamoja na mengineyo, Lowassa aliahidi kufumua uozo wote unaotokana na miradi ya aina hii.

· Lowassa na Richmond's PPP

Serikali ya awamu ya nne (2005) iliingia kwa kasi kubwa ya kuletea mabadiliko wananchi. Moja ya vipaumbele vya serikali ile mara tu baada ya kuingia madarakani ikawa ni uwekezaji katika sekta ya nishati. Kampuni ya Richmond ikaingia mkataba na Serikali kwa nia ya kuzalisha umeme wa dharura. Mengine kuhusu Lowassa na Richmond, historia itakuja kueleza, lakini kilicho muhimu ni kwamba:

Vyama vya Upinzani ulimhusisha Lowassa na ufisadi kwa sababu ya sakata la Richmond. Kutokana na sakata hili, Lowassa akajiuzulu Uwaziri Mkuu huku Mamlaka ya uteuzi ikisema kwamba kilichotokea ni “ajali ya kisiasa”, na sio vinginevyo. Lowassa alitoa ahadi kuzungumza ukweli wa suala hili mbele ya safari. Lakini ukimya wake ukafanya upinzani uendelee kumhusisha na sakata la “Richmond”. Lowassa aliamua kukaa kimya pengine kutokana ili kuzuia kupasua jipu ambalo lingeathiri chama chake cha CCM.

Lowassa Kuondoka CCM

Lowassa alipoamua kuhama CCM alikabiliwa na wakati mgumu wa kuelezea wananchi nini hasa kilijiri katika sakata la Richmond. Kilichofuatia ni kwamba Lowassa akajieleza ufasaha kwa uongozi wa UKAWA. Kama vile haitoshi, Lowassa akaenda mbali na kujieleza mbele ya UMMA jinsi gani alikuwa amechoka kusingiziwa kitu ambacho hahusiki nacho. Lowassa akaeleza kwamba baada ya kupata ushauri kutoka kwa wataalamu kwamba kampuni ya Richmond ilikuwa ni ya kubabaisha, aliamrisha mradi husika usiendelee kwa sababu ni jipu. Lowassa akaendelea kuelezea umma kwamba lakini kilichotokea baada ya yeye kutoa maagizo yale kama Waziri Mkuu, Katibu Kiongozi alimwambia kwamba ‘amri kutoka juu imesema mradi usifutwe, na uendelee’. Lowassa akahitimisha kwa kusema kwamba kwa anayetaka sheria ifuate mkondo wake, ‘waende mahakamani wakakutane nao huko’. Lowassa hayupo tena CCM, Lowassa ameelezea nani ni jipu la Richmond, na Serikali ya CCM ina nafasi nzuri sasa ya kumshitaki kwa suala husika kwa sababu hiyo ndio njia pekee ya kummaliza kisiasa na . Lakini badala yake, hilo halitokei, na CCM kwenye umma inaendelea kujiuma uma, kwenye vikao vyake, CCM inaendelea kupata wakati mgumu la Lowassa.


Baada ya Lowassa kuondoka serikalini Mwaka 2008.

Awali tuliona kwamba kwa kipindi chote cha miaka 47 ya uhuru (1961-2008), serikali ya CCM ilikopesha jumla ya TZS Trilioni 15 kama deni la taifa. Lakini kwa kipindi cha miaka mitano tu, hasa Lowassa alipoondoka serikali (2009-2013), Serikali ya CCM ikakopa zaidi ya TZS trilioni 20. Kwa maana nyingine rahisi, ndani ya miaka mitano tu, Serikali ya CCM ilikopesha kiasi kikubwa cha fedha (TZS trilioni zaidi ya ishirini) kuliko jumla ya fedha iliyokopesha kwa miaka 47 ya uhuru (1961-2008), trilioni kumi na tano.

Swali linalofuata ni Je:

Mikopo hii imewasaidia nini wananchi ambao wanawajibika kulipa deni hili kupitia kodi zao? CCM haina majibu. Badala yake wananchi wanazidi kupigwa na butwaa pale wanapoona serikali ya awamu ya tano ikitumia zaidi ya nusu ya makusanyo ya kodi zao kulipa madeni yanayoiva badala ya kwenda kwenye miradi ya kuboresha maisha yao, madeni ambayo hayajawa na manufaa yoyote kwa wananchi.

Hakuna dalili yoyote kwamba indirect debts (PPPs) itasaidia kuboresha maisha ya wananchi, sana sana hali za maisha ya wananchi walio wengi zinazidi kuzorota. CCM inatambua kwamba hili ni jipu kubwa ambalo Lowassa ana historia ya kukabiliana nalo tangia enzi za City Water.

Miradi mikubwa ya PPP ambayo inapaswa kutumbuliwa ni pamoja na IPTL na Songas. Ripoti ya CAG 2007/2008 iliweka wazi jinsi gani miradi hii ni jipu lakini hakuna hatua iliyochukuliwa na serikali ya ccm hadi leo.
 
Kwani Obama ni mwenyekiti wa Democratic? Sasa kama Magufuli mnataka kumpa uenyekiti chama kitaisimamia vipi serikali? Upuuzi huu upo Tanzania peke yake.

Hivi huyu Uhuru Kenyatta naye ni mwenyekiti kwenye chama kilichompa ugombea urais?
Kwani lazima tufanane nao kila kitu?acha ulimbukeni.
 
Ukimya wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa UKAWA,Edward Lowassa umezua mjadala kwenye mkutano wa Kamati Kuu ya CCM.Kikao cha Kamati Kuu kimefanyika jana hapa Dodoma.

Mjadala ulianza pale Mwenyekiti Kikwete alipochagiza maelezo yake ya chama kuendelea kufanya maandalizi ya chaguzi zijazo na kutobweteka. Mwenyekiti alisema kuwa Lowassa bado ana uungwaji mkono na nguvu ya kisiasa na hutumia ukimya kujijenga zaidi.

Mwenyekiti alionya kuwa Lowassa hakufika mwisho na chama chapaswa kuutazama ukimya wake wa kuchangia na kutoa hoja juu ya Serikali ya Rais Magufuli kwa jicho la tatu. Wajumbe wote wa KK walikubaliana na Mwenyekiti Kikwete.

Wakati huohuo,Rais Magufuli ameaswa kuwa 'mpole kiasi' atakapoukwaa uenyekiti wa taifa wa CCM mnamo mwezi Juni mwaka huu. Imesemwa kuwa wanachama wa chama cha siasa hutendewa mambo kwa upole ili wabaki chamani na kukijenga chama. KK imeunga mkono hatua za Rais na Serikali yake kutumbua majipu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Mh Edo bado ni tishio kubwa kwa uhai wa ccm hilo lipo wazi ni mbumbu na wachumia tumbo ndio watakaobeza.
 
Lowassa ni smart boy,game zake anazijua Kikwete na sishangai kwa kutoa kwake tahadhari hizo.
Ila nimecheka sana walipomuonya JPM kupunguza ukali kidogo,ina maana hatowafukuza tena akina Sofia,Nchimbi na wengineo 'waliokihujumu' chama kama ilivyokuwa imepangwa awali?
Hawana uthubutu huo. Kama ni kufukuza wachafu waanze na mwenyekiti wao na yule nyoka wa makengeza(chenge) mzee wa kila kashfa hakosi kuwepo.
 
Sasa Mzee Tupatupa hiyo ya kumjadili Lowassa ilikuwa ajenda yenu pia?Kuna ile kauli ya wale wapendao kuzungumzia watu na si Mambo yenye faida wanaitwaje vile....................Mwambie JK ameshatoka CCM asiendelee kumzungumzia Lowassa...............
Tetty upo!
 
Sasa Mzee Tupatupa hiyo ya kumjadili Lowassa ilikuwa ajenda yenu pia?Kuna ile kauli ya wale wapendao kuzungumzia watu na si Mambo yenye faida wanaitwaje vile....................Mwambie JK ameshatoka CCM asiendelee kumzungumzia Lowassa...............
Jasiri haachi asili.
 
Maamuzi yapi tena jamani.Mbona mie bado Mbunge viti maalum Jimbo la Nyumbani kwangu?:oops::oops:
Labda nimekosea kuna tetty aliaga kuwa hatakuwepo tena jf..im sorry labda nimechanganya
 
Akili inagoma.jpg
 
Lowassa bado ataendelea kuwanyima usingizi magamba siku zote. Lowassa Mungu ampa hekima na busara sana
 
Ukimya wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa UKAWA,Edward Lowassa umezua mjadala kwenye mkutano wa Kamati Kuu ya CCM.Kikao cha Kamati Kuu kimefanyika jana hapa Dodoma.

Mjadala ulianza pale Mwenyekiti Kikwete alipochagiza maelezo yake ya chama kuendelea kufanya maandalizi ya chaguzi zijazo na kutobweteka. Mwenyekiti alisema kuwa Lowassa bado ana uungwaji mkono na nguvu ya kisiasa na hutumia ukimya kujijenga zaidi.

Mwenyekiti alionya kuwa Lowassa hakufika mwisho na chama chapaswa kuutazama ukimya wake wa kuchangia na kutoa hoja juu ya Serikali ya Rais Magufuli kwa jicho la tatu. Wajumbe wote wa KK walikubaliana na Mwenyekiti Kikwete.

Wakati huohuo,Rais Magufuli ameaswa kuwa 'mpole kiasi' atakapoukwaa uenyekiti wa taifa wa CCM mnamo mwezi Juni mwaka huu. Imesemwa kuwa wanachama wa chama cha siasa hutendewa mambo kwa upole ili wabaki chamani na kukijenga chama. KK imeunga mkono hatua za Rais na Serikali yake kutumbua majipu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Were was 22222222w2w22w22w222ww22ww222222222222ww2222ww2222222q
 
Kwani Dr Mashinji alivyomtaja Dr Slaa kule Mwanza, inaamaana bado Dr Slaa Ana nguvu katika CHADEMA, au Ukimya wa Dr Slaa nao unaleta wasiwasi ndani ya CHADEMA..

Mambo mengine ya Kitoto, habari ya Lowasa katika siasa za Tanzania zimeshaisha.. Na mstari umeshacholwa.. Hakuna jipya lolote kutoka kwa Edo, wamebaki wafia CHADEMA kushelehesha Na kuleta Mubalagha TU.. Ili kumfariji Edo..

SIASA za kufarijiana kwa wapinzani zinashika Hatamu, na itakapo fika 2020 mtamgeuka, Edo..

Baada ya uchaguzi mkuu 2010 mlikuja na kelele kua mmeibiwa kura na Dr Slaa mshindi, ilipofika 2015 Dr Slaa ambae CHADEMA walisema ni mshindi mwaka 2010, akaambiwa Hatoshi hana uwezo wa kuitoa CCM, wakaitaji mtu mwingine.. Haya maneno yatajiludia 2020
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom