Lowassa achomoza Kamati Kuu ya CCM Dodoma

Sababu? Kama ni hofu ya kutumbuliwa, Magu ni wa Watanzania na siyo wa CCM. Hoja yako hiyo hiyo i-reverse kama kura za siri zitapigwa ndani ya CHADEMA au kwa watanzania wote, LOWASSA ataambulia nini?
Hapa tunazungumzia kikao cha chama ambacho kinakuja na agenda kuzungumzia mwanachana wao wa zamani aliye wakimbia. Inaonyesha bado anao umaarufu kuliko yule aliyeteuliwa na jina kutokea mfukoni kwa mtu
 
Mkuu huyo Mzee Throw Throw (wa Pull- Push) ni pandikizi la Fisadi Lowasa siku nyingi, na si ajabu kesha fungashiwa kitu kidogo kuleta habari ambazo hazina mbele wala nyuma.

Hapana Masopakyindi,ukisikia sauti ujue kuna watu wananong'ona au kuna kiota cha ndege.Hivyo tumesikia sauti ni haki yetu kujua ni ndege au minong'ono?Tusijemjeruhi mleta habari kwamba kuna minong'ono nje,tujiandae tu.

Pili ndani ya CCM kuna zaidi ya Lowassa lakini tunaogopa kuwasema.
 
Lowassa ni smart boy,game zake anazijua Kikwete na sishangai kwa kutoa kwake tahadhari hizo.
Ila nimecheka sana walipomuonya JPM kupunguza ukali kidogo,ina maana hatowafukuza tena akina Sofia,Nchimbi na wengineo 'waliokihujumu' chama kama ilivyokuwa imepangwa awali?

Nifah UDA na ESCROW plus Lugumi lazima upate jipu lake
 
Lowassa au mgombea mwingine wa upinzani hawezi kuwa rais wa Tanzania chini ya mazingira ya sasa.

Na CCM imenuia kukaa madarakani milele. Njia iliyobaki ni kuitoa tu madarakani kama alivyotolewa Hosni Mubarak.
 
Ukimya wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa UKAWA,Edward Lowassa umezua mjadala kwenye mkutano wa Kamati Kuu ya CCM.Kikao cha Kamati Kuu kimefanyika jana hapa Dodoma.

Mjadala ulianza pale Mwenyekiti Kikwete alipochagiza maelezo yake ya chama kuendelea kufanya maandalizi ya chaguzi zijazo na kutobweteka. Mwenyekiti alisema kuwa Lowassa bado ana uungwaji mkono na nguvu ya kisiasa na hutumia ukimya kujijenga zaidi.

Mwenyekiti alionya kuwa Lowassa hakufika mwisho na chama chapaswa kuutazama ukimya wake wa kuchangia na kutoa hoja juu ya Serikali ya Rais Magufuli kwa jicho la tatu. Wajumbe wote wa KK walikubaliana na Mwenyekiti Kikwete.

Wakati huohuo,Rais Magufuli ameaswa kuwa 'mpole kiasi' atakapoukwaa uenyekiti wa taifa wa CCM mnamo mwezi Juni mwaka huu. Imesemwa kuwa wanachama wa chama cha siasa hutendewa mambo kwa upole ili wabaki chamani na kukijenga chama. KK imeunga mkono hatua za Rais na Serikali yake kutumbua majipu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Kibaraka wa Lowassa katika ubora wako...

Kazi unayo....Hamia tu CHADEMA badala ya kuendelea na unafiki wa kujifanya u mwana CCM wa Lumumba...
 
Wewe panya mdogo kabisa unasema haya ilhali tembo na wenye chama chao hawapati usingizi juu ya huyo unayemkejeli.
Tumia akili wewe,huijui Tanzania wala siasa kuliko Kikwete & co.
Wakiwa mnachachawa sana...tatizolenu mnakariri sana, hamjui kuwa "time and tide has turned"...there's a new sheriff in town...JK is no longer running the show..hii ni serikali mpya na ina mtazamo tofauti kabisa na serikali iloyopita..jifunzw kuzoea hilo
 
Lowassa ni smart boy,game zake anazijua Kikwete na sishangai kwa kutoa kwake tahadhari hizo.
Ila nimecheka sana walipomuonya JPM kupunguza ukali kidogo,ina maana hatowafukuza tena akina Sofia,Nchimbi na wengineo 'waliokihujumu' chama kama ilivyokuwa imepangwa awali?

Kwenye swala la wasaliti, mimi ningeomba CCM (kwa mara ya kwanza) wa adopt sera za chadema za kikambale....wafukuzwe tu
 
huyu mzee anachokisema hapa sio kweli; anaandika tu mambo ya kufikirika yasiyo na uhalisia wowote ili kumfufua mzee aliyekwisha kisiasa
Na kama ni kweli pia sio vibaya Wapinzani Mkatumia Miaka 5 hii Kujipanga ifikapo 2020 Muhakikishe Mnaingia katika Uchaguzi na Tume huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya vinginevyo Wa TZ, Watawachukulia kama wachumia Tumbo tu
 
Kibaraka wa Lowassa katika ubora wako...

Kazi unayo....Hamia tu CHADEMA badala ya kuendelea na unafiki wa kujifanya u mwana CCM wa Lumumba...

Naam, ukisikia mtu mnafik, fataani na mzandik ni kama huyo anaejiita Tupatupa.

Huyo ni kiwanda cha uongo.
 
Kwenye swala la wasaliti, mimi ningeomba CCM (kwa mara ya kwanza) wa adopt sera za chadema za kikambale....wafukuzwe tu
Kama tulivyokutimua wewe msaliti CDM?

Hebu tusubiri na tuone.
Maana 'nyeti' nilizopenyezewa kipindi kile zilikuwa kama nilivyosema awali.
 
Wakiwa mnachachawa sana...tatizolenu mnakariri sana, hamjui kuwa "time and tide has turned"...there's a new sheriff in town...JK is no longer running the show..hii ni serikali mpya na ina mtazamo tofauti kabisa na serikali iloyopita..jifunzw kuzoea hilo
My dear, huna unachokijua.
Hebu nitafute kwa muda wako nikueleze hali halisi.
Otherwise...endelea kujidanganya.
 
Safi sana endeleeni kumjadili kwenye vikao vyenu vya juu ili muendelee kumuongezea umaarufu, hongera sana mzee wa msoga kutupa uzi wa kuujadili kwa leo

Chonde chonde raisi wetu Magufuli asikufundishe yeyote iwe toka kwa viongozi waliokutangulia wala wapambe wao namna ya kuongoza nchi wala chama.Sikatai kupokea ushauri wao na si lazima uutekeleze kwani kwa miaka yao ufisadi na wizi wa rasilimali za watanzania zilitamalaki.Amani wanayoweza kujivunia tunayo tu na watanzania kwa ujumla hawakulelewa na Nyerere katika vurugu.Ukishapokea kofia ya m/kiti chama taifa ni kuwa umekamilika kuongoza nchi na chama na tenda kadri yote kwa manufaa ya wananchi unaowaongoza na ndivyo ulivyokuwa unawaahidi katika mikutano yako ya kampeni na wananchi wakakupa ridhaa kwa imani hiyo.Nakuhakikishia hadi sasa una asili mia 85 ya imani ya watanzania kwa uongozi wako wa miezi sita tu.Wasikudanganye kuwa asilimia hizo ni za wanaccm wenzako tu na wapinzani wapo.Ushari wa kuwa tunakubali utumbuaji majipu anaoufanya raisi ila akisha pewa kofia ya chama taifa apunguze ukali ili wanachama wabaki ndani ya chama hauna manufaa kwako na watanzania huo pengine ni upotoshaji.Mtamshaurije awe mpole wakati hata yeye mwenyewe anajua fika waovu na mafisadi ndiko walikojificha?Hivi hadi leo hamjiulizi sababu za kuepuka sana kujinadi kwa kutumia chama kwenye kampeni zake?Namshauri raisi aanzie huko huko kwenye chama chake mafisadi na wasiotenda kuenenda na taratibu za chama sio tu kuwatimua na kuanza nao kwenye mahakama ya mafisadi mwezi July bali awanyanganye na kadi za chama.Chama kisicho safi kitaongozaje serikali?Pia mapema tu kabla moto haujapoa alirudishe na azimio la Arusha na kuachana na la Zanzibar walikokwenda kuhalalisha ulaji wa wakubwa na viongozi serikalini kumiliki mabiashara makubwa kuanzia maduka,mahoteli,meli kubwa kubwa hadi migodi.Pili atoe agizo bunge la katiba kuheshimu mawazo na matakwa ya wananchi na kuipitisha rasimu ya judge Warioba na kuachana na matakwa ya wabunge wachache wa ccm na wateule wachache kwa manufaa yao na chama chao.Ukishatekeleza hayo ndio mwisho wa wewe na viongozi kuhangaika na utumbuaji maana yatakuwa yamejitumbua yenyewe kwenye azimio na katiba.Nakuhakikishia mwaka 2020 kampeni zako zitakuwa kidogo sana na utaongoza kwa raha.Hayo ndiyo wanayoyataka wananchi na mwenyezi Mungu kwa waja wake.
 
M
Chonde chonde raisi wetu Magufuli asikufundishe yeyote iwe toka kwa viongozi waliokutangulia wala wapambe wao namna ya kuongoza nchi wala chama.Sikatai kupokea ushauri wao na si lazima uutekeleze kwani kwa miaka yao ufisadi na wizi wa rasilimali za watanzania zilitamalaki.Amani wanayoweza kujivunia tunayo tu na watanzania kwa ujumla hawakulelewa na Nyerere katika vurugu.Ukishapokea kofia ya m/kiti chama taifa ni kuwa umekamilika kuongoza nchi na chama na tenda kadri yote kwa manufaa ya wananchi unaowaongoza na ndivyo ulivyokuwa unawaahidi katika mikutano yako ya kampeni na wananchi wakakupa ridhaa kwa imani hiyo.Nakuhakikishia hadi sasa una asili mia 85 ya imani ya watanzania kwa uongozi wako wa miezi sita tu.Wasikudanganye kuwa asilimia hizo ni za wanaccm wenzako tu na wapinzani wapo.Ushari wa kuwa tunakubali utumbuaji majipu anaoufanya raisi ila akisha pewa kofia ya chama taifa apunguze ukali ili wanachama wabaki ndani ya chama hauna manufaa kwako na watanzania huo pengine ni upotoshaji.Mtamshaurije awe mpole wakati hata yeye mwenyewe anajua fika waovu na mafisadi ndiko walikojificha?Hivi hadi leo hamjiulizi sababu za kuepuka sana kujinadi kwa kutumia chama kwenye kampeni zake?Namshauri raisi aanzie huko huko kwenye chama chake mafisadi na wasiotenda kuenenda na taratibu za chama sio tu kuwatimua na kuanza nao kwenye mahakama ya mafisadi mwezi July bali awanyanganye na kadi za chama.Chama kisicho safi kitaongozaje serikali?Pia mapema tu kabla moto haujapoa alirudishe na azimio la Arusha na kuachana na la Zanzibar walikokwenda kuhalalisha ulaji wa wakubwa na viongozi serikalini kumiliki mabiashara makubwa kuanzia maduka,mahoteli,meli kubwa kubwa hadi migodi.Pili atoe agizo bunge la katiba kuheshimu mawazo na matakwa ya wananchi na kuipitisha rasimu ya judge Warioba na kuachana na matakwa ya wabunge wachache wa ccm na wateule wachache kwa manufaa yao na chama chao.Ukishatekeleza hayo ndio mwisho wa wewe na viongozi kuhangaika na utumbuaji maana yatakuwa yamejitumbua yenyewe kwenye azimio na katiba.Nakuhakikishia mwaka 2020 kampeni zako zitakuwa kidogo sana na utaongoza kwa raha.Hayo ndiyo wanayoyataka wananchi na mwenyezi Mungu kwa waja wake.[/QUOTE MAGUFULI:- " Mimi sipendi Mavyama vyama haya"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom