Nadhani kuna kitu fulani hivi, labda tumelogwa na kama tumelogwa basi hakuna mwingine aliyetuloga isipokuwa ni Shetani mwenyewe. Rais Mstaafu Ben Mkapa aliwahi kusema na nakuu; " Umasikini na maradhi ni watoto wawili mapacha wanaowatesa Watanzania na Ujinga ndiye mama yao mzazi"
Msemo huu naupenda sana na nakubaliana na Mkapa! Kwa hiyo hatuna maadui watatu wanaotutesa kama Nyerere alivyotuambia. Ni wawili tu. Huyu mwingine (wa Nyerere) kumbe ni mzazi tu wa wale watesaji wenyewe! Dawa ni kumuua huyu mzazi, mambo yote yatakuwa barabara!