Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 45,867
- 65,206
- Thread starter
- #81
Hiyo ndio maana ya magic, huwezi kujua kila trick inabidi ibaki inakufikirisha, ukielewa magic tricks katika hali ya kawaida inakuwa sio tena mazingaombwe. Hapa inawezekana aliwaaminisha anachotafuna ni chupa wakati ni kitu kingine kabisa, inawezekana ni chupa kweli ila namna ya utafunaji na umezaji wake ndio haimletei madhara.Nimeshawahi kuona mazingaombwe mtu anatafuna glass mpaka vile vipande vya chupa vinasagika na anameza na kushushia na maji huku mdomo wake ukitoka damu kiasi. Naomba uniambie ni saikolojia na ujanja gani alioutumia hapo? Nahitqji kujua nini cha ziada anachofanya ili kuwapumbaza wanaomuangalia maana katika hali ya kawaida haiwezekani kumeza vipande vya chupa unawezaweza kupoteza maisha.