Kwanini maonyesho mazingaombwe yaliacha kuonyeshwa shuleni na nchini?

Comrade, Mazingaombwe ni saikolojia na akili tu. Hakuna cha mazingara, wala uchawi.
Nimeshawahi kuona mazingaombwe mtu anatafuna glass mpaka vile vipande vya chupa vinasagika na anameza na kushushia na maji huku mdomo wake ukitoka damu kiasi. Naomba uniambie ni saikolojia na ujanja gani alioutumia hapo? Nahitqji kujua nini cha ziada anachofanya ili kuwapumbaza wanaomuangalia maana katika hali ya kawaida haiwezekani kumeza vipande vya chupa unawezaweza kupoteza maisha.
 
Bado haujaktana na "mazingambwa" wewe!
Niambie mazingaombwe gani ambayo hayapo Youtube..., na kinachovutia sio mazingaombwe (ile trick) but the power of performance na katika performance ndio huko tumeamia kwa kina Zuchu, Diamond et al....

Sasa kama watu hata hizi wanazielewa ukiwaletea issue za kukata vichwa kwenye sinia wakati mtu yupo kwenye shimo inabidi uwe more of a performer zaidi ya trickster...

View: https://youtu.be/QfDX-a7MQPM?si=Qtwz_T0PF_xcx0ux
 
Wakati nasoma shule ya msingi kulikuwa na watu mbalimbali wanakuja shuleni kufanya maonyesho ya mazingaombwe, yale maonyesho yalikuwa na buradani ya aina yake, wanafunzi wengi walikuwa wanalipia pesa ya kiingilio cha kuingia kutazama na wanafanya juu chini kupata siti za mbele katika ukumbi mdogo wa shule uliokuwepo.

Miaka mili ya kumalizia shule ya msingi haya maonyesho ya mazingaombwe yalikuja kupotea kabisa na siku hizi sidhani kama bado yapo kokote nchini, sijui kitu gani kilitokea kikaipoteza hii burudani.
Gentleman,
wanamazingaumbwe walijibadilisha majina saivi wanajiita manabii,

kwahiyo mazingaumbwe yamehamia kwenye maombi na maombezi kamavile kula keki ya upako ili mtu apate mtoto au nguvu za kijinsia, kukanyaga mafuta ya alizeti ya upako ili upate gari,

kwahiyo mazingaumbwe yapo ila yamejibrand kivingine tu 🐒
 
Nimeshawahi kuona mazingaombwe mtu anatafuna glass mpaka vile vipande vya chupa vinasagika na anameza na kushushia na maji huku mdomo wake ukitoka damu kiasi. Naomba uniambie ni saikolojia na ujanja gani alioutumia hapo? Nahitqji kujua nini cha ziada anachofanya ili kuwapumbaza wanaomuangalia maana katika hali ya kawaida haiwezekani kumeza vipande vya chupa unawezaweza kupoteza maisha.
Kuangalia kwako tu huku wewe huwezi alichofanya hadi leo ndiyo cha ziada kilichokupumbaza hadi leo unakisimulia huku unakumbuka damu"kidogo" ilivyomtoka mzee baba.
 
Wakati nasoma shule ya msingi kulikuwa na watu mbalimbali wanakuja shuleni kufanya maonyesho ya mazingaombwe, yale maonyesho yalikuwa na buradani ya aina yake, wanafunzi wengi walikuwa wanalipia pesa ya kiingilio cha kuingia kutazama na wanafanya juu chini kupata siti za mbele katika ukumbi mdogo wa shule uliokuwepo.

Miaka mili ya kumalizia shule ya msingi haya maonyesho ya mazingaombwe yalikuja kupotea kabisa na siku hizi sidhani kama bado yapo kokote nchini, sijui kitu gani kilitokea kikaipoteza hii burudani.
Sisi tumeacha kufanya mazingaumbwe wenzetu nchi za Ulaya ndio yanashika kaso
 
Badala ya ku embrace Technological innovations Mna kazania mazingaombwe, li nchi limelaaniwa hili.
Ila wabongo kwa ujuaji bwana, hujui kuwa Magic show ni mchezo kama ilivyo michezo mingine kama mpira na ni sekita inayo ingiza pesa nyingi?
 
Sasa,hapo kakuonesha ujuaji au kaeleza asivyoupenda mchezo huo?Au hauelewi maana ya ujuaji?Na kwa nini umuite mtu ni mjuaji?Wewe nani kakukataza kujua?
 
Morogoro miaka ya 80's mpaka 90's kulikuwa na Mkuu mmoja wa kuitwa Nyonganyonga alikuwa anajifanya anaonyesha Mazingaombwe kumbe mzushi tu,alikuwa anajifanya anakalia misumari kumbe matakoni kavaa kipande cha ngozi,alafu mazingaombwe yake anatoa vitu vya mtaani tu kama Vibagia,gubiti,mabumunda,viladu,hamna vitu vya dukani kama pipi.Yule Mkuu alikuwa mzushi sana.Naskia kadedi,.Apumzike kwa amani Mkuu Nyonganyonga.
 
Wakati nasoma shule ya msingi kulikuwa na watu mbalimbali wanakuja shuleni kufanya maonyesho ya mazingaombwe, yale maonyesho yalikuwa na buradani ya aina yake, wanafunzi wengi walikuwa wanalipia pesa ya kiingilio cha kuingia kutazama na wanafanya juu chini kupata siti za mbele katika ukumbi mdogo wa shule uliokuwepo.

Miaka mili ya kumalizia shule ya msingi haya maonyesho ya mazingaombwe yalikuja kupotea kabisa na siku hizi sidhani kama bado yapo kokote nchini, sijui kitu gani kilitokea kikaipoteza hii burudani.
Nakumbuka kuna mtu alichemshiwa chai kichwani
 
Back
Top Bottom