Kwanini Mandela anasifiwa wakati hakuwapa Uhuru Waafrika wa asili wa Afrika Kusini

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,095
Sifa anazopewa hazilingani na uhalisia, nawe kama unsmuona shujaa pengine umekuwa brainwashed

Alihamasisha forgiveness dhidi ya makaburu kwamba waendelee kumiliki ardhi takribani asilimia 85 yenye rotuba, kabla ya kutetea naomba ujibu swali rahisi, hilo shamba lako ama mashamba ya huko kijijini kwenu ungefurahi wazungu wangeendelea kuyamiliki ? ungejipiga kifua kusifia Nyerere katupa uhuru ?

Alihamasisha forgiveness dhidi ya makaburu kwamba waendelee kumiliki migodi,

Alihamasisha forgiveness dhidi ya makaburu kwamba waendelee kuendesha mifumo ya uchumi

Leo hii Waafrika wa asili waliokuwepo Afrika Kusini kabla hata ya ukoloni ni masikini sana, Afrika kusini ndio inaongoza kwa uhalifu Afrika sababu waafrika wengi ni masikini huku wazungu wakiwa matajiri sana kwa rasilimali za Afrika kusini, waafrika wengi wanaishi kwenye shacks (Nyumba ndogo zenye kuta za mabati)
 
Nelson Mandella ni Baba wa Afrika hii,huwezi mfananisha ni kiongozi yoyote ndani ya bara hili.Ni upumbavu kuamini mtu ili awe mwafrika lazima awe mweusi.Afrika kusini ilijengwa na Makaburu ambao mpaka leo ni nguzo muhimu ndani ya Afrika kusini.

NAC wameiharibu SA kama walivyo fanya wakina Mugabe, Nyerere, Nkrumah nk,katika mataifa yao.
 
Utachagua moja; uwaache wazungu kwenye miundombinu, ajira, madini, kilimo, ulinzi, afya na huduma nyingine za jamii. Au ufukuze wazungu wote uwanyanganye mali zao.

Aliyewaacha wazungu mfano ni South Africa na jirani yake Namibia. Aliyefukuza wazungu mfano ni Zimbabwe
1000265285.png


Kwa mbali mfano mwingine ni Uganda ambapo Idd Amin alifukuza Wahindi, wakaacha biashara zao wakaenda mikono mitupu. Wakarudi enzi za Museveni wakakuta biashara zao zimeuwawa na weusi, wakakuta weusi na makapuku, Wahindi wakaanza upya na sasa pale Kampala na Entebbe ndio wanaishi "uhindini".
 
Kuna mzulu nilikutana nae Chuo alisema hi kauli, #Mandela sold us akendelea kusema kwamba the one who control means ya Uchumi wa nchi ndiye anayecontrol hata Uongozi wa nchi.
Kwani hapa Bongoland watu weusi ndo wanao miliki uchumi? Mandella alikuwa kiongozi mzuri ni mpumbavu pekee ndo hawezi tambua umuhimu wa Mandella kule SA.

Leo hii watawala ni NAC wamefanya nini kwa weusi wenzao,kama sio wizi wa Mali za umma kama Jacob Zuma.
 
Utachagua moja; uwaache wazungu kwenye miundombinu, ajira, madini, kilimo, ulinzi, afya na huduma nyingine za jamii. Au ufukuze wazungu wote uwanyanganye mali zao...
Hata Tanzania Wahindi na waarabu ndo wanao miliki uchumi,weusi wamebaki kushabikia mpira wa Yanga na Simba,kuwaza ngono nk.

Ukweli lazima usemwe weusi ni waharibifu Tanganyika ya mkoloni ilikuwa bora kuliko Tanganyika ya Nyerere.
 
Mandela alikuwa na chaguo hilo la kuwaacha makaburu waendelee na maisha yao kiuchumi au awanyang'anye mali zao kuzuke vita vya wenyewe kwa wenyewe kati weusi na wazungu.
 
Km Nyerere tu, akipewa sifa huwezi jua kua ilifika hatua nchi ilimshinda, hali ikawa mbaya.
Harakati zenyewe za uhuru kafanya kukalibisha.

Ila sasa, kila kitu utasikia nyerere. Unafiki mwingi sana
Binafsi huwa naona kitendo Cha SA kuchelewa kupata uhuru,kilitoa funzo kwao,kwa kuangalia mataifa yaliyo wahi pata uhuru nini kinaendelea.Nadhani hapa ndo maamuzi magumu na yenye busara yalimfanya Mandella kuona Kuna baadhi ya vitu waafrika hatuwezi.
 
Sifa anazopewa hazilingani na uhalisia, nawe kama unsmuona shujaa pengine umekuwa brainwashed

Anasifiwa kwa lipi wakati hata baada ya uhuru Makaburu wachache waliendelea na wanaendelea kuimiliki ardhi asilimia 80 yenye rotuba ya kulima na madini

Bungeni, jeshini, taasisi za serikali kuna Makaburu wabaguzi wengi sana wanaoamua mustakabali wa taifa
Nelson Mandela kama binadamu mwingine yoyote yule ana mazuri yake lakini pia ana mabaya yake. Mojawapo ya mazuri yake ni kwamba amefanikisha suala la Co-habitation Kati ya watu Weusi na watu Weupe nchini Afrika ya Kusini
 
Nelson Mandela kama binadamu mwingine yoyote yule ana mazuri yake lakini pia ana mabaya yake. Mojawapo ya mazuri yake ni kwamba amefanikisha suala la Co-habitation Kati ya watu Weusi na watu Weupe nchini Afrika ya Kusini
Na demokrasia imara zaidi barani Africa
 
Binafsi huwa naona kitendo Cha SA kuchelewa kupata uhuru,kilitoa funzo kwao,kwa kuangalia mataifa yaliyo wahi pata uhuru nini kinaendelea.Nadhani hapa ndo maamuzi magumu na yenye busara yalimfanya Mandella kuona Kuna baadhi ya vitu waafrika hatuwezi.
"Tuliwakataa, tuliwatenga na kuwaengua kabisa watu Weusi katika mchakato wa maendeleo ya nchi na ujenzi wake kwa sababu hawana akili nzuri, endapo kama tungewajumuisha wangetuharibia mambo yetu mazuri yaliyopo Afrika ya Kusini leo hii."

Pieter W. Botha, Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini enzi za utawala wa Ubaguzi wa rangi
 
Nelson Mandela kama binadamu mwingine yoyote yule ana mazuri yake lakini pia ana mabaya yake. Mojawapo ya mazuri yake ni kwamba amefanikisha suala la Co-habitation Kati ya watu Weusi na watu Weupe nchini Afrika ya Kusini
Kivipi waakati wazungu ambao wapo asilimia 8 wanaendelea kumiliki ardhi asilimia 80
 
Mandela alikuwa sahihi 100% kuwaacha makaburu. Angewaachia hao wazulu Afrika kusini ingekuwa kama Zimbabwe. Hata hapa kwetu kulikuwa na maamuzi ya hovyo sana kuwanyang'anya watu hasa weupe mali zao wakati wa awamu ya kwanza. Matokeo yake ni nchi kurudi nyuma sana.
jaribu tu kuwaza ingekuwaje hapa Tanzania karibu kila sehemu unayotafuta shamba tayari inamilikiwa na wazungu
 
Kivipi waakati wazungu ambao wapo asilimia 8 wanaendelea kumiliki ardhi asilimia 80
Wazungu (Whites) na watu Weusi (Blacks) wote hadi leo hii wanaishi pamoja nchini Afrika ya Kusini. Hakuna watu waliofukuzwa kutoka ktk nchi hiyo hata baada ya kuanguka kwa utawala wa Wazungu wachache/Makaburu
 
Wazungu (Whites) na watu Weusi (Blacks) wote hadi leo hii wanaishi nchini Afrika ya Kusini. Hakuna watu waliofukuzwa kutoka ktk nchi hiyo hata baada ya kuanguka kwa utawala wa Wazungu wachache/Makaburu
jaribu tu kuwaza ingekuwaje hapa Tanzania karibu kila sehemu unayotafuta shamba tayari inamilikiwa na wazungu wachache huku sisi wengi wa asili hatuna ardhi
 
Back
Top Bottom