matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 8,160
- 19,732
Kwanza kupanga sio jambo la ajabu au aibu. US zaidi ya watu wazima Mil 45 wamepanga.
Wengi wanalazimisha kujenga wakiwa hawana kipato cha kueleweka wanaishia kuishi nje ya matarajio yao.
Unakuta mtu anafanya kazi kkoo anajenga kisarawe kijijini KWA DC Machachari KWA gharama nafuu. Unakuta karibu nusu ya maisha yake anaishia kusafiri na kugombania daladala.
Unakuta mtu amekaa kanyumba hakuna hewa, haijaisha vizuri, anarisk ya kuumwa na tandu, nyoka na wadudu watambaao lakini anajifariji " kwako ni kwako".
Pia kujenga haraka ukiwa na kipato kidogo inaondoa morali ya utafutaji. Unajiona umefika. Kuna watu baada ya kujenga Nyumba maendeleo yao ni tofauti na wakati wamepanga. Wengi wanaona wamefika.
Pia utafiti unaonyesha kuingia kwenye Nyumba ambayo haijaisha wengi huwa wanakaa miaka mingi bila kuimaliza, na hata wakimaliza inakuwa haina mvuto maana kule kuungaunga kunaonekana.
Hakuna haja ya kuishi KWA hofu KWA kukimbilia kujenga wakati kipato unachopata kinakutosha kula, kulipa Kodi na ada.
Anza polepole tengeneza mifumo ya kuingia fedha. Watu waliopanga IQ yao huwa Iko juu sana na uwezo wa kutafuta Pesa uko juu. Tumia hii kama fursa ya kubuni vyanzo vya mapato vya ziada ili angalau ununue kiwanja kikubwa, mahala pa heshima KWA makuzi ya watoto na kufikika. Mahala unaweza hata kupanda miti ya kupata hewa, kufuga kuku ule mayai OG, kupanda hata vibustani vya matembele mchicha, ukizeeka unakuwa bizebize kidogo.
Anza kujenga Nyumba ndogomdogo iishe kabisa SIO kuhamia kwenye pagale.
Pia Mungu akikubariki itakusaidia kujenga mahala unapotaka SIO maisha yatakakokupeleka hata kama hukuwa na huo mpango.
Lakini tukumbuke, Kujenga Nyumba nzuri ni amri ya Mungu.
Ni hayo tu.
Mtumishi Matunduizi