Kwa nini nawaelewa ambao Wanaanza kutafuta Pesa ndio wajenge na SIO kujenga ukiwa na kipato kidogo

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
8,160
19,732
Kwanza kupanga sio jambo la ajabu au aibu. US zaidi ya watu wazima Mil 45 wamepanga.

Wengi wanalazimisha kujenga wakiwa hawana kipato cha kueleweka wanaishia kuishi nje ya matarajio yao.

Unakuta mtu anafanya kazi kkoo anajenga kisarawe kijijini KWA DC Machachari KWA gharama nafuu. Unakuta karibu nusu ya maisha yake anaishia kusafiri na kugombania daladala.

Unakuta mtu amekaa kanyumba hakuna hewa, haijaisha vizuri, anarisk ya kuumwa na tandu, nyoka na wadudu watambaao lakini anajifariji " kwako ni kwako".

Pia kujenga haraka ukiwa na kipato kidogo inaondoa morali ya utafutaji. Unajiona umefika. Kuna watu baada ya kujenga Nyumba maendeleo yao ni tofauti na wakati wamepanga. Wengi wanaona wamefika.

Pia utafiti unaonyesha kuingia kwenye Nyumba ambayo haijaisha wengi huwa wanakaa miaka mingi bila kuimaliza, na hata wakimaliza inakuwa haina mvuto maana kule kuungaunga kunaonekana.

Hakuna haja ya kuishi KWA hofu KWA kukimbilia kujenga wakati kipato unachopata kinakutosha kula, kulipa Kodi na ada.

Anza polepole tengeneza mifumo ya kuingia fedha. Watu waliopanga IQ yao huwa Iko juu sana na uwezo wa kutafuta Pesa uko juu. Tumia hii kama fursa ya kubuni vyanzo vya mapato vya ziada ili angalau ununue kiwanja kikubwa, mahala pa heshima KWA makuzi ya watoto na kufikika. Mahala unaweza hata kupanda miti ya kupata hewa, kufuga kuku ule mayai OG, kupanda hata vibustani vya matembele mchicha, ukizeeka unakuwa bizebize kidogo.

Anza kujenga Nyumba ndogomdogo iishe kabisa SIO kuhamia kwenye pagale.

Pia Mungu akikubariki itakusaidia kujenga mahala unapotaka SIO maisha yatakakokupeleka hata kama hukuwa na huo mpango.

Lakini tukumbuke, Kujenga Nyumba nzuri ni amri ya Mungu.

Ni hayo tu.

Mtumishi Matunduizi
 
Mtazamo mzuri.
Ukilipia Kodi SIO ya mwanaume mwenzio umo humo KISHERIA. Labda ukome kulipa uhesabike mvamizi kwenye Nyumba ya mwenzako.
Kwahiyo ukilipa kodi unaweza kupanda na maua bila idhini ya baba mwenye nyumba? Unaweza kupaka rangi uipendayo kisa umelipa kodi?
Unaweza kupanda hata papai hapo kwa mwanaume mwenzio?
 
Kwanza kupanga sio jambo la ajabu au aibu. US zaidi ya watu wazima Mil 45 wamepanga.

Wengi wanalazimisha kujenga wakiwa hawana kipato cha kueleweka wanaishia kuishi nje ya matarajio yao.

Unakuta mtu anafanya kazi kkoo anajenga kisarawe kijijini KWA DC Machachari KWA gharama nafuu. Unakuta karibu nusu ya maisha yake anaishia kusafiri na kugombania daladala.

Unakuta mtu amekaa kanyumba hakuna hewa, haijaisha vizuri, anarisk ya kuumwa na tandu, nyoka na wadudu watambaao lakini anajifariji " kwako ni kwako".

Pia kujenga haraka ukiwa na kipato kidogo inaondoa morali ya utafutaji. Unajiona umefika. Kuna watu baada ya kujenga Nyumba maendeleo yao ni tofauti na wakati wamepanga. Wengi wanaona wamefika.

Pia utafiti unaonyesha kuingia kwenye Nyumba ambayo haijaisha wengi huwa wanakaa miaka mingi bila kuimaliza, na hata wakimaliza inakuwa haina mvuto maana kule kuungaunga kunaonekana.

Hakuna haja ya kuishi KWA hofu KWA kukimbilia kujenga wakati kipato unachopata kinakutosha kula, kulipa Kodi na ada.

Anza polepole tengeneza mifumo ya kuingia fedha. Watu waliopanga IQ yao huwa Iko juu sana na uwezo wa kutafuta Pesa uko juu. Tumia hii kama fursa ya kubuni vyanzo vya mapato vya ziada ili angalau ununue kiwanja kikubwa, mahala pa heshima KWA makuzi ya watoto na kufikika. Mahala unaweza hata kupanda miti ya kupata hewa, kufuga kuku ule mayai OG, kupanda hata vibustani vya matembele mchicha, ukizeeka unakuwa bizebize kidogo.

Anza kujenga Nyumba ndogomdogo iishe kabisa SIO kuhamia kwenye pagale.

Pia Mungu akikubariki itakusaidia kujenga mahala unapotaka SIO maisha yatakakokupeleka hata kama hukuwa na huo mpango.

Lakini tukumbuke, Kujenga Nyumba nzuri ni amri ya Mungu.

Ni hayo tu.

Mtumishi Matunduizi
Kupanga ni kuchagua. Maisha ya kupanga africa hayajawahi kuwa na maana kabisa
 
Kwahiyo ukilipa kodi unaweza kupanda na maua bila idhini ya baba mwenye nyumba? Umaweza kupaka rangi uipendayo kisa umelipa kodi?
Unaweza kupanda hata papai hapo kqa mwanaume mwenzio?
Utapanda kwako mkuu. Kulazimsha kujenga wakati kipato Kiko chini ni hofu tu. Unaweza kupanga ukaendelea kujitafuta ukae kwako penye kukufanya hata ukiwa kazini unaona unachelewa kufikia nyumbani.
 
Utapanda kwako mkuu. Kulazimsha kujenga wakati kipato Kiko chini ni hofu tu. Unaweza kupanga ukaendelea kujitafuta ukae kwako penye kukifanya hata ukiwa kazini unaona unachelewa kufikia nyumbani.
Mtu hadi anajenga maana yake kipato kinamtosha mkuu.

Hizo nyumba ni sawa na magari unaweza kujitutumua wee ukadhani kwamba nawewe umejenga ila ukienda kwa wenzako hata Choo chake tu hakilingani thamani na nyumba yako ya chumba vitatu!!

Hivyo jenga kulingana na kipato chako wewe una hangaika na sofa la laki6 wenzio wana masofa ya m15!

Sasa ukiwaza hayo yte je utaweza?
 
Kila mtu anafanya anachoona Kipaumbele kwake,
Mi nikiwa na Miaka 25, Nimemiliki Nyumba yangu, Dar Hapa Hapa mjini kwenda kariakoo nauli 700 kwa Bei ya Leo hii 24/4.2024. Kutoka Home kwenda kariakoo Faster tu.
Sasa Cha kushangaza Mimi Sina Tv.
 
Mimi nimejenga ila naendelea kupanga. Nilikojenga nimempangisha mtu mwingine. Siwezi kushinda kwenye mafoleni ya kipuuzi kisa natokea kwangu.
 
Kuiondoa sisiemu ni kuiweka katika Panic mode Kama ilivyo sasa .
Haaaaa, Unajua Mimi ni mtu mdogo Sana Ktk Hii Nchi, ila nilifanya uchunguzi wangu Binafsi nikaona Mizizi ya sifsi ni Mikubwa, Vyombo vyote na Taasisi zote, zipo ktk Mikono yao Sasa hapo kutoboa Haliwezekani, pia Ukiwa miongoni mwao lazima ufuate mfumo.
Ni jambo gumu kubadilisha mfumo ndugu.
 
Mimi nimejenga ila naendelea kupanga. Nilikojenga nimempangisha mtu mwingine. Siwezi kushinda kwenye mafoleni ya kipuuzi kisa natokea kwangu.
Kuna watu wamepanga kkoo wakati wananyumba dar vijijini. Kupanga kwao ndio imekuwa njia Bora.
Kukibwa ni flexibility. Huwezi kukomaa lazima nitokee kwangu au nikae kwangu wakati kukaa kwako kunakupa gharama mara 10 ya kukaa karibu na eneo lako la uzalishaji.
 
Kwenye maisha hatuwezi kufanana. Kila mtu na kipaumbele chake. Wakati tunaanza kazi nilikuwa na rafiki yangu yeye alikuwa na familia kubwa wanaishi kwenye upangaji. Hivyo tukaamua kuchukua mkopo. Tulipopata yeye akaenda kujenga familia yake ikapata pa kuishi. Binafsi sikuwa na familia hela yangu nikawekeza kwenye biashara. Japokuwa sijajenga lakini nina miradi ambayo inaniingizia fedha. Kwa hiyo kwenye maisha inachotakiwa ni focus na kufanya kitu kulingana na kipaumbele na malengo ambayo umejiwekea. Na sio kubeza watu kwa vipaumbele vyao walivyochagua.
 
Back
Top Bottom