HEKIMA KWANZA
JF-Expert Member
- Mar 31, 2015
- 2,942
- 3,937
Watanzania tuna tatizo la kumbukumbu? Hivi TCU imeanza kulalamikiwa baada ya Prof Ndalicheko kuwa Waziri? Kuna malalamiko lukuki humu JF kuhusu hiyo TCU, sijui utetezi unatoka wapi?
Huo uamuzi ulikuwa ni wa TCU au wa serikali ya Kikwete kupitia wizara ya elimu?Hivi akili zenu zikoje?Ukweli gani wakati makosa yako wazi kabisa watu wana division four wanakwenda kusomea ualimu pale St Josephu....watu wameishia Form fou wana kwenda kujiunga na degree! Hivi mna hitaji nini?
yaani hatuna jemaWatanzania tuna tatizo la kumbukumbu? Hivi TCU imeanza kulalamikiwa baada ya Prof Ndalicheko kuwa Waziri? Kuna malalamiko lukuki humu JF kuhusu hiyo TCU, sijui utetezi unatoka wapi?
Kwani yeye ni kasisi au sheikh?UDINI TU NDICHO KILICHONYUMA YA PAZIA; KWANI HATUMJUI
Hapa tatizo siyo usomi wa Ndalichako, hapa tunahoji busara iliyotumika kuwahukumu vijana wetu zaidi ya 7000 kwani nao ni moja ya watanzania wenye haki ya kuishi na kuheshimiwa kama ulivyo wewe,leo hii kuna baadhi ya hao vijana wameamua kujiuza miili yao ili wapate angalau nauli ya kurudi majumbani mwao,wewe hapo unacho shangilia ni kitu gani?
Ukishakuwa Waziri usiye na maneno mengi kama unavyosema, basi uwaziri huwezi ni bora ukapewa ukatibu mkuu wa wizara.
Waziri ni mwanasiasa. kila kona utatakiwa kuzungumza na kutoa ufafanuzi. Lazima uwe mwepesi wa kufikiri na hapa hakuna kampeni ya uzuri wa mtu. akikosea lazima ashike adabu. Inaingiaje akilini kuwapelekea askari polisi wanafunzi waliokujulisha kwamba hawajasoma kwa miezi kadhaa? Unatoa masaa 24, ili iweje? wakome kukujulisha taarifa kama hizo? Kwani angesema tunatoa likizo hadi tutakapomalizana na hawa waalimu wanaogoma, kuna kosa gani?
Unatamani elimu iboreshwe lakini huenda huyu siyo mtu sahihi. Huu siyo mwanzo mzuri hata kidogo. Tuliza kichwa hata kama ni rafiki yako, mpe ukweli aelewe maamuzi ya kikorofi siyo ushujaa.
Tunataka kuona watu wanawajibika kwa uzembe huu maana wanafunzi hawa hawakujipeleka chuoni wenyewe. Rudisheni na hela zilizopotea tangu serikali iwafikishe hapo UDOM maana walikuwa wanalipiwa ada na hela ya kujikimu(boom).Hivi mnajua utawala nyie mnaotaka wanafunzi waombwe kistaarabu,mnadhani serikali ilikua haijui fukuto pale Udom? Acheni umbumbu wa div 4 na 3 zenu.Dalili za riot tayar zilikuwepo na kundi la watu 7000 ni hatari kwa usalama,sio kazi ya serikali kujua una nauli au huna,waliosoma shule za bweni za serikali watakubaliana na mie kwamba utaratibu uliotumika kuwaondoa pale Udom ni kawaida kabisa na hakuna kosa hapo
Tabby huna haja ya kulaumu hawa aina ya viongozi wetu wa bunge sababu hata wao wanatekeleza kile wanacho kiamini kama wewe unavyo amini kuwa kujiuza ni tabia ya mtu,hivi ingetokea hata wewe unafukuzwa usiku wa manane wakati huna hata senti tano na unaambiwa unatakiwa kuyaacha mazingira ya chuo muda huo na mfukoni huna hata senti tano,kwenu labda ni bukoba,au mtwara au ni sumbawanga ungefanyaje?Kujiuza ni tabia zao za umalaya. Hakuna solutioin ya tatizo mtu atatafuta nje ya fikra zake.
Nimesikia akisema kwamba wamerudishwa nyumbani kwa mgogo wa walimu. Masuala mengine yanahitaji ufafanuzi na mchango wa kuyaboresha na si lazima mtu afutwe kazi. Mimi nitamlaumu Naibu spika wa bunge kwa kugomea mjadala badala ya kuuongoza kitaalam ili pia Waziri apate nafasi ya kutoa ufafanuzi badla ya kuwaacha watu wakilalamika na kuongzea mitafaruk.
Udini udini udini udini udini udini udini udini udini udini!!!!!!!!!!Niliandika humu kuwa Ndalichako ana agenda ya siri.
Ukweli ukidhihiri uongo hujitenga.
Punguza ugoro wako huo,na nikupe tahadhari tu ni kuwa kwa umri ulio nao na hii tabia mbaya ya ubaguzi wa kidini ukifikisha miaka 60 wewe utakuwa ni mchawi mkubwa sanaHivi mkubwa wa TCU anaitwa nani? Na mkubwa wa UDOM anaitwa nani?