Kwa maelezo haya, Ndalichako anapaswa kujiuzulu kupisha uchunguzi

Ukimsema yule mama kuwa ni mdini basi jipime mara mbili kama unastahili hata kuchangia maada jamiiforums.
 
Ukweli gani wakati makosa yako wazi kabisa watu wana division four wanakwenda kusomea ualimu pale St Josephu....watu wameishia Form fou wana kwenda kujiunga na degree! Hivi mna hitaji nini?
Mleta mada ni Mlowassa na sio Bavicha.Japo Bavicha baadhi nao wameathirika na lowassaism.
 
Ikumbukwe kwamba ni sisi tuliopiga kelele humu mpaka rais akakuteua na hata kipindi anasoma jina lako alitabasamu akimaanisha yule mnaemtaka nimewaletea.

Bila wanaJF kupiga kelele ulikuwa umesahaulika kwenye siasa za Tanzania hasa baada ya kuondoka pale NECTA, ila kwa matukio haya unatutia aibu wanaJF ingawaje tuna mengi tunajivunia kutoka kwako.

1. Mh. Ndalichako mitihani ya kidato cha sita imevuja mno. Binafsi baada ya kuona hoja hiyo ya kuvuja mitihani imeletwa humu nilifikiri ni wale wabaya wako wasiokutakia mema wanakutafutia sababu, ndipo nikajitosa mtaani nikagundua kuwa ni kweli mitihani ilikuwa imevuja. Nimeongea na wanafunzi wa shule za sekondari Tabora na Shinyanga wamekiri kuwa walikuwa wanapata mitihani toka kwa wenzao. Mh hii aibu karne hii mitihani inavuja tunatengeneza Taifa gani?

2. Ni namna unavyolitatua suala la wanafunzi wa UDOM. Kama mzazi hukutakiwa kuruhusu wanafunzi wale kufukuzwa chuoni kwa haraka namna ile bila kuwa na tatizo, ikumbukwe kuwa kosa ni lenu serikali sasa kwanini wanafunzi watimuliwe chuoni bila kuwapa pesa za nauli na kuwaambia hatma yao?

Kushindwa kwako ni aibu yetu wanaJF.
 
una ushahidi kuwa mwandishi amenunuliwa?
Kama yupo apelekwe TAKUKURU kwa rushwa. Ila kama Ndalichako alikurupuka ili kupata unafuu wa kutafuta kiki ya kupitisha bajeti ya Wizara na aonekane anashughulika kumbe amelikoroka inabidi apishe uchunguzi.
 
una ushahidi kuwa mwandishi amenunuliwa?

Kwa upuuzi huu wa kusema hasara sio shilingi milioni 700 bila kusema hasara ni sh ngapi, ni wazi kama sio kanjanja basi amenunuliwa kwa manufaa na maslahi anayoyafahamu yeye!
 
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, anadaiwa kulikoroga kutokana na uamuzi wake wa kuwasimamisha viongozi wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

Profesa Ndalichako anadaiwa kuikanyaga Sheria ya Vyuo Vikuu ya Mwaka 2005 na Kanuni zake za mwaka 2013 ambazo zinaipa Tume mamlaka ya kuteua watendaji na kuwawajibisha inapobidi.

Inaelezwa kwamba majukumu ya Waziri hayahusiani na masuala ya utendaji wa Tume kwa mujibu wa sheria, ila Tume ina jukumu la kumshauri Waziri katika masuala ya elimu ya juu nchini na kwingineko.

Sheria hiyo inaeleza kuwa endapo Waziri hataafiki ushauri wa Tume kwa jambo lolote kuhusu masuala ya elimu ya juu, ni budi aeleze kwa maandishi sababu za kutofautiana na ushauri wa Tume.

Hayo yamebainika siku chache baada ya Waziri Ndalichako, kuwasimamisha kazi vigogo wa TCU akiwamo Katibu Mtendaji, Profesa Yunus Mgaya, Mkurugenzi wa Udahili na Nyaraka, Rose Kiishweko, Mkurugenzi wa Ithibati, Dk. Savinus Maronga na Ofisa Mwandamizi wa Takwimu, Stambuli Kimboka.

Watendaji hao walisimamishwa Mei 25, mwaka huu kupisha uchunguzi wa kasoro katika udahili wa wananafunzi uliofanywa na Chuo Kikuu cha St. Joseph kwenye programu ya Shahada ya Ualimu katika Sayansi.

Chanzo cha kuaminika kiliiambia MTANZANIA kuwa awali, Mwenyekiti wa TCU, Profesa Awadhi Mawenya, alipokea barua kutoka kwa Waziri Ndalichako ikimtaka awapumzishe watendaji wakuu wa TCU.

Profesa Mawenya aliitisha kikao cha dharura cha Tume kujadili maagizo ya Waziri.

Inaelezwa kuwa kwa mujibu wa majukumu ya Tume, kikao kiliamua kufuata utaratibu wa sheria na kumwandikia barua Katibu Mtendaji kumtaka atoe maelezo katika masuala mbalimbali yaliyoainishwa kwenye barua ya Waziri.

Hata hivyo Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Mgaya, alijibu maelezo hayo kwa kina katika barua hiyo ya Mei 14, mwaka huu

Kutokana na majibu yake, kwa mujibu utaratibu uliowekwa na sheria, Tume ilijadili maelezo ya Katibu Mtendaji na kuridhika kwamba hakuna kosa lolote la utendaji na kwamba mengi yaliyotajwa yalishughulikiwa na Tume na Wizara ilihusishwa kwa ukamilifu.

“Hata hivyo kuna jambo la kushangaza kidogo, Waziri anajua sheria na suala hili lilikuwa ndani ya uchunguzi maalumu je, inakuaje anaingilia na kulijadili bila kufuata sheria zilizoanzisha TCU?

“… alisema hasara iliyopata Serikali kutokana na wanafunzi wasiokuwa na sifa ni Sh milioni milioni 700 wakati si sahihi.

“Hapa kuna jambo ambalo lipo limejificha nyuma ila tutaliona tu, watu wamekuwa wakionewa kinyume cha sheria.

“Hawa watendaji wa Rais nini wanafanya zaidi ya kufanya upotoshaji na kusigina sheria,” alisema mtoa habari huyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.

Baada ya hatua hizo na maelezo kutolewa kuhusu tuhuma hizo zilizoainishwa kwenye barua ya Waziri kwa Mwenyekiti wa Tume, majibu kamili yalitayarishwa na kuwasilishwa kwa Waziri kabla ya hotuba yake Bungeni.

Kutokana na mawasiliano hayo na Waziri Ndalichako, alitakiwa kujibu kwa maandishi kuwa amekubali ama kukataa mapendekezo ya Tume kama inavyotakiwa katika sheria.

Hii ingewezesha Tume kuliangalia suala zima kwa utaalamu na kumshauri Waziri iwapo maoni ya Tume yanakinzana na Sera ya Elimu au la.

“Kutokana na historia ya suala zima la maadili na viwango vibovu vya elimu nchini kwa muda mrefu, haikuwa mwafaka kulijadili suala hili bungeni kabla ya kulichunguza kwa mapana zaidi,” alisema.

Mtoa habari huyo alisema tatizo hilo kwa msingi limetokana na vigezo vya udahili kwenye programu ya Ualimu katika Sayansi iliyopitishwa na Tume mwaka 2013 na kuendeshwa na Chuo Kikuu cha St. Joseph, Kampasi ya Arusha.

Alisema programu hiyo ilibuniwa kusaidia kupunguza uhaba wa walimu wa Sayansi nchini na ililenga kudahili vijana waliomaliza kidato cha nne katika masomo ya sayansi na kwa wale wasiosoma sayansi, wawe wamefaulu Hisabati na Baiolojia.

“Huu si utaratibu mpya kwani ulianza tangu mwaka 2013 kwa makubaliano na Wizara ya Elimu. Kutokana na mwongozo mpya wa Wizara, vigezo vya udahili vilibadilishwa kwa kuviongeza kutoka ufaulu wa daraja la nne (division four) kwenda daraja la tatu (division three) ili kusimamia utekelezaji wa mwongozo huo

“Hatua hizo ilikuwa ni kuhakikisha kwamba vigezo vya Wizara vinatimizwa kwa kuchukua madaraka ya kudahili moja kwa moja badala ya kukiachia chuo jukumu hilo. Kitendo hiki kilifanyika mwaka 2015 ili kuondoa uhafifu katika masuala ya ufundishaji wa programu hii.

“Hata hivyo Tume ilisimamisha udahili mpya na kukiagiza Chuo kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaishia kwenye ngazi ya diploma ya ualimu wa sayansi.

“Madhumuni ni kuhakikisha kwamba hii programu haiendelei tena kwa vile Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) lina uzoefu wa kutosha kusimamia elimu katika ngazi ya diploma vyuoni, Tume ililishirikisha Baraza kurekebisha mtaala wa programu hiyo kuwawezesha wanafunzi kumaliza masomo yao kwa ngazi ya diploma ya Chuo cha St. Joseph,” alisema.

Alisemna pamoja na hali hiyo tume ilichambua viwango vya ufaulu wa wanafunzi kwenye programu hiyo na kubaini wale wanaokidhi vigezo na wale wasiokidhi vigezo vya kudahiliwa.

Alisema yaliyoelezwa na Waziri Ndalichako hayahusiani na utovu wa nidhamu uliosababisha Waziri kuchukua hatua kali za kuivunja Tume na kuwaadhibu watendaji hata kabla ya matokeo ya uchunguzi wa Kamati aliyoiteua.

Mei 25, mwaka huu Profesa Ndalichako, alitangaza kumsimamisha kazi Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Mgaya, kwa kile alichodai ameshindwa kuisimamia shughuli za TCU na wajibu wake kama mtendaji mkuu wa taasisi hiyo.

Inaelezwa kuwa Waziri Ndalichako alichukua uamuzi huo kwa kumshauri Rais Magufuli moja kwa moja badala ya kusubiri maagizo na ushauri wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alikuwa Zambia kwa shughuli za kazi.

Chanzo:Mtanzania


Nahisi kuna jambo lipo nyuma ya maamuzi haya ya huyu waziri.


Mama Ndalichako alikuta Elimu ya kina Mulugo na Binam Shukuru iko kama jumba la sanaa kaole.

Huyu mama anakazi kubwa kuliko unavyoweza kufikiria. Ninachoomba asiondolewe kupisha uchunguzi kwa sababu hakuna cha kuchunguza. Kinachotakiwa aombwe atoe mwongozo wa mwelekeo wa elimu, atautekeleza naman gani kwa miaka mitano na apimwe kwa lipi. Kumshikia kasi kwa wizara hiii ilvyokuwa ni sawa na kuhalalisha watu wote wakiwa hyo wizara wawe kama mulugo na kawambwa, wafanye kama awamu ya jk ili wasiulizwe maswali.

Ninaomba watendaji wa wizara wampe ushirkiano sana. Tatizo na uzuri wa huyu mama si mtu wa maneno mengi. Ni mtu wa malengo na vitendo. Waliozoea talalilah wanaona hafanyi kwa kuwa hapigi domo.

Ninarudia tena kusema. Mama Ndalichako aachwe akomboe elimu ya taifa. Apewe muda aandae mpango wa kukabiliana na changamoto zilizopp ambazo kazikukuta likiwemo la ufaulu wa kubumbwa, kushuka kwa elimu, n.k. Apewe ushirikiano katika mahitaji ya raslimali za kutekeleza mpango huo na kwa uzito wa kipekee, usomi na umakini wake uheshimiwe.

Wabunge nawaomba sana watambue siyo kila mtu anapigiwa kura. Lazima wajue kama wangelikuwa wanachunguzwa wao kwa utaalamu, basi wenye vyeti fake wasingekuwemo bungeni. Wengye ufaulu kama wa Ms Marwa wasingekuwemo. Ni vizuri wtambue nafasi yao na inapoishia lakini waache maswala ya kitaalamu wasiyaingilie unless iwe ni katika kusaidia katika uboreshaji. Kama vile elimu ya jk na washikaji wake waliyvoua elimu na bunge halikuweza kupima wala kushtuka wala kuhoji na hata Mbatia aipojitahidi kuwaeleza hawakuelewa, ni dhahiri haya mambo kwao ni makubwa sana.

Majungu hayatalisaidia taifa. JK aliharibu sana hii nchi na kwa kuonyesha mauaji ya taifa ni pale alipoua elimu. Huyu mama hana kazi ndogo. NINARUDIA KUSEMA APEWE USHIRIKIANO LAKINI SI KUMWABIA APISHE UCHUNGUZI. UCHUNGUZI WA NINI? MBONA JESHI LA POLISI PAMOJA NA KASHFA YA LUGHUMI HAKUNA ALIYEPISHA UCHUNGUZI? HABARI ZA MAKONTEINA YA BANDARINI, NANI ALIPISHA UCHUNGUZI? HABARI ZA ESCROW HATUJASIKIA UCHUNGUZI WOWOTE?

TUNAOMBA SERIKALI IANZA KUCHUNGUZA HAYA MAUFISADI SUGU, KABLA HAIJAANZA KUWAVURUGA WATAALAM WANAOFANYA KAZI YA ZIADA KULIKOA TAIFA.
 
Swali ni je ukiachilia kuvunjwa sijui kukanyaga kanuni, walikuwa na makosa? Kama wana makosa achana na hizo Kanuni watumbuliwe tu.
 
Kichwa maji wa Bawacha weka hapa hiyo sheria!

Halafu hebu twambie kama wanakosa au lah...
Kwenye masuala ya nidhamu Waziri anaweza kumsimamisha CEO ila kufukuzwa ni Chief Secretary. Alivyofanya Prof Ndalichako ni sahihi kulingana na Standing Order. Standing Orders haziwezi kutangulia hiyo sheria Salary Slip
 
Ukweli gani wakati makosa yako wazi kabisa watu wana division four wanakwenda kusomea ualimu pale St Josephu....watu wameishia Form fou wana kwenda kujiunga na degree! Hivi mna hitaji nini?
Hapa kuna vyeti feki wengi, wanataka kutibua juhudi za waziri kuinyoosha elimu yetu.
 
unajua nahisi atatumia weledi wake kama prof kumbe nae amepata maradhi ya kutumbua kila kitu. hata alivo handle issue ya TCU was poor
 
Hahaha.. Wewe ni Mwalimu wangu wa shule ya msingi nini?
Make nakumbuka huyo mwalimu ulikuwa ukituhumiwa aidha kupiga kelele hata kama hujapiga lazima akuadhibu kwanza ndo ujietetee. Alikuwa na Kamsemo kake kuwa "Pokea adhabu halafu baadaye ndo ujitetee". Nawe unasema hayo hayo, "Wenye vyeti feki watumbuliwe kwanza halafu baadaye ndo sheria ziangaliwea'. Hahahahahah
 
Hiz inawezekana ni figisu figisu za wadananda wa nchi hii, huyu Mama mm bado nna imani nae.
 
unajua nahisi atatumia weledi wake kama prof kumbe nae amepata maradhi ya kutumbua kila kitu. hata alivo handle issue ya TCU was poor
Hebu niambie kosa la Ndalichako hadi sasa!
Akina dada wa siku hizi husema "yametushuka"

Ikumbukwe kwamba ni sisi tuliopiga kelele humu mpaka rais akakuteua na hata kipindi anasoma jina lako alitabasamu akimaanisha yule mnaemtaka nimewaletea, bila wanajf kupiga kelele ulikuwa umesahaulika kwenye siasa za Tanzania hasa baada ya kuondoka pale NECTA ila kwa matukio haya unatutia aibu wanajf ingawaje tuna mengi tunajivunia kutoka kwako.
1.Mh. Ndalichako mitihani ya kidato cha sita imevuja mno binafsi baada ya kuona hoja hiyo ya kuvuja mitihani imeletwa humu nilifikiri ni wale wabaya wako wasiokutakia mema wanakutafutia sababu ndipo nikajitosa mtaani nikagundua kuwa ni kweli mitihani ilikuwa imevuja nimeongea na wanafunzi wa shule za sekondari Tabora na Shinyanga wamekiri kuwa walikuwa wanapata mitihani toka kwa wenzao,
Mh hii aibu karne hii mitihani inavuja tunatengeneza Taifa gani?
2.Ni namna unavyolitatua suala la wanafunzi wa UDOM kama mzazi hukutakiwa kuruhusu wanafunzi wale kufukuzwa chuoni kwa haraka namna ile bila kuwa na tatizo, ikumbukwe kuwa kosa ni lenu serikali sasa kwanini wanafunzi watimuliwe chuoni bila kuwapa pesa za nauli na kuwaambia hatma yao.
Kushindwa kwako ni aibu yetu wanajf.
 
ndalichako hakuna kitu anavuruga tu elimu huwezi kuwafukuza wanafunzi kijinga hiki...Serikali iwalipe fidia maana wao ndio wameanzisha hiyo kozi
 
Back
Top Bottom