Gai da seboga
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 482
- 969
Wasalam mabibi na mababu...
Toka tarehe 14/4/2024 Tume huru ya uchaguzi imetoa tangazo la nafasi za kazi za muda katika kuboresha Daftari la kudumu la mpiga Kura.
Katika Jambo lililonishangaza ni kuona wimbi la walimu kuomba hizi nafasi, imani yangu inaniambia hizi ilikuwa n nafasi za kuomba graduates na jobless wapate chochote kitu lakini leo watumishi wa umma ndo wamejazana mno hususani walimu.
Katika utafiti mdogo katika shule zote nchini Tanzania walimu wameomba hizi nafasi za muda tena wengine ni mpaka walimu wakuu...
Hili la walimu hadi kunyang'anyiana hizi nafasi na graduates mtaani ni ishara tosha kuwa maslahi ya walimu ni Duni na mshahara hauwatoshei kabisa... Walimu wana njaa mpka wameamua kuvamia hivi vinafasi, yan Mwalimu hana ata kaposho anachopata katika mwezi hii ni hali mbaya saana.
Mheshimiwa Rais Mama Samia tunajua Zimebaki Siku chache watu waadhimishe siku ya Wafanya kazi Duniani ikikupendeza Mama wawekee walimu ata teaching Allowance kwa mwezi ata kama ikiwa ni laki tu kwa mwezi Hakika inaweza ikarahisisha maisha yao. Kuna walim wanaishi katika mazingira magumu hakuna nyumba, hakuna umeme, wako maporini tu ya I mtu muda wote anasikia sauti za Komba na Tetere.
Mama samia najua hili unaweza kabisa embu wawekee walimu posho uache Alama ya kweli ya Uongozi Wako, Hakika utakumbukwa Kizazi na Kizazi, kazi ya Ualimu sio kazi ya laana ni kazi ya kimitume, embu watunze upate thawabu hadi Akhera.
Aione Mama Samia Kwenye Faili....