Kamanda Sirro: Wema Sepetu, Nyandu Tozzy na TID bado wanashikiliwa na Jeshi la Polisi

Labda mi ni mjinga ama masikio yangu pia ya kijinga ama ushabik umewazid uwezo watoto wa dar binafsi najua wema aliitwa kwa tuhuma za uuzaji wa ngada Na ninavyowajua petiti nyandu na tid Na blue ni kweli ni wauzaj ushabiki wa kijinga tuuweke pemben bas mana wauzaj hawauzii chini ya shimo wala juu ya anga tunawaona Na tuna wajua Kinondoni mkwajun mpk manyanya pamechafuka soko la petiti blue Na nyandu pale jirani Na kwa kina bilali mashauz ni balaaa.... Ni ngada Na ma shoga
 
Kwenye hii inshu mimi kwa kweli siichekeli sana. Nchi yetu mi nadhani inaelekea kubaya. Mi nashauri hili suala lishughulikiwe kwa kufuata taratibu za nchi.

Yaani wakuu wa mikoa ndio wamegeuka Polisi na mara nyingine mahakama. Huwezi kumuita mtu Kituo cha polisi na kufika kumuweka ndani sasa ni bora angeseme wakamatwe na kuwekwa ndani.

Tunachekelea hii hali 'lakini kwa hali halisi yawezekana kesho au Siku nyingine mimi na wewe tunaweza kuwa Waathirika wa maamuzi haya kwa namna moja au nyingine.
 
Kada wa CCM na aliyekuwa miongoni mwa wana kampeni nguli wa rais Magufuli, msanii Wema Sepetu amejikuta katika wakati mgumu ndani ya kituo kikuu cha polisi Dar baada ya kubadilishiwa tuhuma alizoitiwa ndani ya kituo hicho hapo awali.

Awali Wema alitakiwa kuripoti kituoni hapo na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ndugu Paul Makonda kwa tuhuma za matumizi ya madawa ya kulevya sanjari na baadhi ya wasanii wenzake. Hata hivyo Wema alipofika kituoni hapo alibadilishiwa tuhuma na kutuhumiwa kuuza madawa ya kulevya na kuishia kutupwa mahabusu kwa mahojiano zaidi.

Wema ambaye hakuambatana na mtetezi yeyote amejikuta akiishia kushindwa kujibu tuhuma zake na kuishia kuangua kilio kila mara.

Msanii huyo huenda akapandishwa mahakamani hapo kesho kutwa jumatatu kwa tuhuma hizo zinazomkabili.

====================
Wakati macho na masikio ya Watanzania wakisubiri kusikia hatma ya wasanii wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya, wasanii wanne waliofika Kituo Kikuu cha Polisi bado wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi.

View attachment 467134

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa bado wasanii hao Wema Sepetu, Dogo Hamidu, Khalid Mohamed (TID), na mtangazaji maarufu wa Clouds TV Babuu wa Kitaa bado wanashikiliwa na jeshi hilo.

“Bado tunawashikilia kwa mahojiano zaidi,” amesema Sirro kwa kifupi.

Wasanii wengine waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambao wanatakiwa kufika kituoni Jumatatu ni Vanessa Mdee, Tunda na watu wengine Halidali Kavila, Amani, Kashozi na Omry Sanga.

Chanzo: Mwananchi
Halafu eti alitaka kuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Ma CCM.
Mangu Mulika Bungeni kuna Ma Dealer wengi sana wa Ngada wamekimbilia kuwa wabunge kwa ticket ya Chama Cha Majambazi ili kuzuga umma na kufanya Biashara yao bila Mizengwe
 
Makonda anakurupuka ishu za ukamatajj wa madawa ya kulevya haziendi kwa pupa namna alivyofanya yeye..

Lakn ngoja tuwe kimya labda ana ushahidi wa kutosha au exbiht itakayoweza kumtia hatian huyo wema...

Ingekuwa inaleta maana sana endapo wema angekamatwa akiwa na hayo madawa na sio...

Hii kesi ikienda kwa wanasheria inatupwa kapuni mchana kweupee
We uliona wapi walikamatwa kistaarabu Mkuu ???

Vitu vingine haviitaji ujuaji kwani ukikaa kimya utapungukiwa damu
 
Jeshi la polisi na wasanii wa wasanii haahaha patamu hapo wasanii wanatumikia wanasiasa polisi wanatumika na siasa kazi inogireeee.
 
Mwisho wa siku utasikia baadhi hawatafikishwa kabisa mahakamani kutokana na kukosekana ushahidi na wengine watashinda kesi mahakamani kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.

Baadhi ya waliosimamishwa kazi utasikia wamerudishwa kazini kutokana na ama kushinda kesi au kushindwa kufikishwa mahakamani kutokana na wao kuonekana hawana kesi ya kujibu.
.
Hii ndio Tanzania bwana

Time will tell.

Mlisema hayo hayo tukamuona Mramba na Yona wakilamba miaka.
 
Kama kweli anahusika na hizo tuhuma za kuuza madawa ya kulevya, mkondo wa sheria hauna budi kuchukua hatua stahiki
 
Kama wanahusika kweli sheria ichukue mkondo lakini kama hawasiki serikali itapoteza pesa nyingi kuwalipa fidia. Tatizo la madawa ya kulevya raisi mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete analifahamu siamini kama alishindwa kupambana nalo akiwa raisi. Makonda bhana sijui lakini ngoja tuone labda anapewa sapoti na Mtakatifu.
 
Wale wabunge wa CCM waliokamatwa na Takukuru kwa kuomba rushwa kesi imeishia wapi? Wale wabunge wa CCM kuhongwa milioni 10 kila mbunge wa CCM wapitishe muswada wa habari wamelipelekwa mahakama ipi?
Uwe unajiongeza
Mlisema hayo hayo tukamuona Mramba na Yona wakilamba miaka.
 
Ni mpaka waTanzania tutakapojua kua kwenda kufanya mahojiano unaweza kukaa kimya na kutojibu chochote mpaka wakili wako awepo na ukihitajika pande hizo ni vyema ukawa na wakili ndipo tutaepuka upuuzi wa kama aliofanyiwa huyu mtuhumiwa.
Right to remain silent for an appearance of your Advocate as per CRIMINAL PROCEDURE ACT.
 
sheria haichagui sura wala umaarufu, huko ndani ni vizuri wakitajana hadi mtu wa mwisho ajulikane! kwanini wewe uingie kwenye shida na kuwaacha wenzako mnaobwia pamoja wakila bata uraiani? kutajana ndo habari ya mjini manake kimenuka tayari , hupotezi kitu kwa kutaja wenzako, kifo cha wengi ni harusi! naamini kuna list ingine itaibuka soon, haya shime shime , waliokwisha kamatwa tajeni wenzenu waliosahaulika uraiani, msikubali kufa na tai singoni! ila pia ni vizuri wanaohusika ambao hawakutajwa wajipeleke wenyewe tu umwelani kuliko kusubiri kutajwa na maswahiba wao waliokwishafika umwelani! ni vizuri wajipeleke kuliko kusubiri defender nne , kamanda na virungu! wananchi tumpe moyo mkuu wa mkoa afike mwisho wa safari hii iliyotukuka kwa kuwasweka ndani drug lords wote ambao muda huu wanakula bata na upepo mwanana! kuna kitu wazungu wanaita POLITICAL WILL, yaani serikali ikiamua kwa dhati madawa ya kulevya, ufisadi, ujangili , ukabaji , ubakaji na ujambazi vinabaki historia nchini! siku zote ukiona jambo linaendelea na watu wanajiachia ujue serikali haijaamua!


huu msemo kifo cha wengi ni harusi siupendi ,kufa kufa tu hata mfe 100 umekufa hakuna cha sherehe hapo

kwahiyo mkifungwa watu wengi kifungo cha maisha ndio sherehe sababu mmefungwa wengi?

huu msemo siupendi ase kama vile shuleni eti mkichapwa wengi sherehe ,wakati maumivu yale yale tu unayapata

kifo cha wengi ujinga tafuta kila njia ukwepe kifo
 
Wakamatwe wasanii wote tu sasa wahojiwe, maana naona list itachukua wasanii Tz yote
 
Naungana na wale wanao pambana na madawa ya kulevya lakini kuwaweka mahabusu na kuwadhalilisha mbele ya jamii bila ya kuwa na ushahidi haikubaliki.

Imekuwa ni mazoea kwa vyombo vya ulinzi kuwakamata watu bila ya kuwa na ushahidi kamili, ingawa wananchi tunatoa taarifa, vyombo vya ulinzi na usalama Vinatakiwa kufuatilia kwa kina ndipo kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa.

Naamini bado hakuna ushahidi.
 
Back
Top Bottom