Kamanda Sirro: Wema Sepetu, Nyandu Tozzy na TID bado wanashikiliwa na Jeshi la Polisi

Kwavita hii ya makonda chadema chali tena kifo cha Mende, yale mateja ya ufipa sijui watayaficha wapi.
 
duh mtandao huu wa madawa ya kulevya ni hatari, yaani wahusika wanazidi kuongezeka jumatatu mh. zungu, mtemvu na diamond wameitwa jumatatu tarehe 6 na polis kituo cha kati kwa mahojiano zaidi.

Mkuu, huo mtandao hauongezeki bali tayari ni mkubwa sana. Hao wanaoandamwa sasa ni tone tu la bahari.

Tatizo kubwa ni kuwa hili suala la madawa ya kulevya limeambatana na UNAFIKI usio wa kawaida sio Tanzania tu bali dunia nzima. Ukitazama kwa makini sana utagundua kuwa ule unaojulikana kama "utamaduni maarufu" yaani "popular culture" aka "pop" ambao ndio unaowatambulisha wasanii wakubwa, "mafashonista", celebrities, n.k. kwa kiasi kikubwa unawezeshwa na matumizi ya hayo madawa.

Vituko, vurugu, mbwembwe nyingi zinazofanywa na hao watu maarufu na kuwavutia wengi kiasi cha kuwa kwenye media kila siku zinatokana na hayo madawa. Ile stress tu ya kuwa juu kwenye chati; ku-perform kiwango cha juu na kuwa na kitu kipya kwenye media huwafanya wengi kunasa kirahisi kwenye chambo cha ma-pusher.

Wengine unaona kabisa mambo zao haziwiani na akili sober ya binadamu. Lakini sisi haohao tunaofurahia mbwembwe zao tunajidai kuchukia sana madawa ya kulevya! Na siku jamaa wakiishiwa au ku-overdose ndio utasikia masikitiko kibao jinsi jamaa alivyoharibu future yake kubwa.
 
Kama hujaelewa usikurupuke kujibu.. Simaanishi kukamatwa kwa ubabe ama kistaarabu nacho maanisha ni unapomkamata mtuhumiwa wa madawa ya kulevya lazma pawepo na vidhibiti na ushahidi uliojitosheleza...

Huwezi ukampeleka mtuhumiwa pasipo ushahidi wala kidhibiti..
Kama walikuwa na ushahidi kwamba wema anauza unga basi wangemkamata nao lakn sio hii ya kuitwa polisi na kuwekwa ndani hata kama anajihusisha na biashara hyo kwa mda huo aliopata taarifa ya kuitwa polis lazma atakuwa ameuhamisha mzigo...

Hii kesi ya akina wema kwautaratibu huu ulivyofanyika watatoka wote na hakuna atakayekutwa na hatia..
Kesi haziendeshwi kwa rumours au hearsay
Broza kuna ushahid wa kimazingira Na kunaushahid wa moja kwa moja ndo nnachoweza kukusaidia..... Kwa iyo we unahis makonda Na polis wamekurupuka sio Nani asiyejua babuu mitaa ya mikocheni nyuma ya hospital ya dr kahiruki mpk kwa warioba uko yeye Ndio supplier Mkuu nan asie jua tid nyandu blue petiti ndo wanayoiaribu Kinondoni mpk mwananyamala yote nan asie jua wema Ndio ana supplies mzigo kwa mastaa wa bongo movie Na bongo fleva Na kwa wale madada tunaowaona high class lkn wala ngada kina director Joan ,junaisa braza ka Upo mkoani we kaa kimya tulipo jijin tunaona mengi sana ata mi binafs ningepewa hii kaz ya kuwatafuta ningewapata kwa wing hayo mambo yenu ya kijinga ya haki za binadam Na ujinga ka huo ndo ulitudikisha apo kwa miaka mingi Sanaa
 
Hii kombinesheni kwasasa ndio habari ya MJINI
images

Naona kama Kamanda Sirro kapungua
 
hayo ni mahojiano tu, ni mahakama pekee ndio itathibitisha kama wanahusika au la ingawa wakati mwingine mahakama zinashindwa kuthibisha kutokana na udhaifu wa mawakili wa serikali na vyombo vyake vya upelelezi cha muhimu ujumbe umefika kwa wauzaji na watumiaji wa madawa mwisho ningependa wamhoji shigongo maana magazeti yake yamekuwa msitariwa mbele kuandika juu ya wasanii kutumia madawa labda wanaweza kuwapa ushahidi fulani
 
Wema na ile timu ya mama mkanye mwanao wote wataishia jela kudadeki.

Safi sana. Acha wote tuisome namba, bora wisi wengine tunaisomea uraiani, wao wqtaisomea jela.

Hqwa wanaojiita wasanii wa bongo karibu wote ni wauzaji wa dawa za kulevya.

Yule dogo aliesema Venessa mdee amesema hamjui baada ya kuomba kolabo sasa anacheka meno yote nje.
Kwani ukiwa mwana ccm ndo usifuate sheria?
 
Mwisho wa siku utasikia baadhi hawatafikishwa kabisa mahakamani kutokana na kukosekana ushahidi na wengine watashinda kesi mahakamani kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha,n.k.

Baadhi ya waliosimamishwa kazi utasikia wamerudishwa kazini kutokana na ama kushinda kesi au kushindwa kufikishwa mahakamani kutokana na wao kuonekana hawana kesi ya kujibu.
.
Hii ndio Tanzania bwana

Time will tell.
Mwisho wa siku utasikia baadhi hawatafikishwa kabisa mahakamani kutokana na kukosekana ushahidi na wengine watashinda kesi mahakamani kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha,n.k.

Baadhi ya waliosimamishwa kazi utasikia wamerudishwa kazini kutokana na ama kushinda kesi au kushindwa kufikishwa mahakamani kutokana na wao kuonekana hawana kesi ya kujibu.
.
Hii ndio Tanzania bwana

Time will tell.

Ingekuwa wewe "salary slip" umetajwa kuwa unabwia au unauza, halafu pasiwe na ushahidi wowote, ungekuwa tayari kufungwa? Polisi na mahakama wana fanya kazi kwa kufuata sheria na si maneno ya mitaani. Polisi wakisikia maneno ya mitaani wanafuatilia na kuchunguza kabla ya kupeleka kesi mahakamani..ndiyo maana hata Mhe. Makonda hakuagiza watuhumiwa wafungwe bali wahojiwe, ufanyike uchunguzi na taratibu za kisheria zifuatwe.
 
Back
Top Bottom