Kamanda Sirro: Wema Sepetu, Nyandu Tozzy na TID bado wanashikiliwa na Jeshi la Polisi

Haidary Kavira mshua wake mwenyewe si nguli wa hizo mambo ? Tokea wanaishi Mwananyamala na huko China sijui wana mjomba wao au ndugu yao ndio mkubwa wa hizo mambo .Nadhani alikutana na Mercy Galabawa China kwa jinsi dogo alivyokuwa ana floss demu akajaa mazima

Mara ya mwisho nawaona na Range Sports ya Silver sijui kama bado wapo wote

Haidary natamani kufahamu anakaa mwananyamala hipi?
 
Kada wa CCM na aliyekuwa miongoni mwa wana kampeni nguli wa rais Magufuli, msanii Wema Sepetu amejikuta katika wakati mgumu ndani ya kituo kikuu cha polisi Dar baada ya kubadilishiwa tuhuma alizoitiwa ndani ya kituo hicho hapo awali.

Awali Wema alitakiwa kuripoti kituoni hapo na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ndugu Paul Makonda kwa tuhuma za matumizi ya madawa ya kulevya sanjari na baadhi ya wasanii wenzake. Hata hivyo Wema alipofika kituoni hapo alibadilishiwa tuhuma na kutuhumiwa kuuza madawa ya kulevya na kuishia kutupwa mahabusu kwa mahojiano zaidi.

Wema ambaye hakuambatana na mtetezi yeyote amejikuta akiishia kushindwa kujibu tuhuma zake na kuishia kuangua kilio kila mara.

Msanii huyo huenda akapandishwa mahakamani hapo kesho kutwa jumatatu kwa tuhuma hizo zinazomkabili.

====================
Wakati macho na masikio ya Watanzania wakisubiri kusikia hatma ya wasanii wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya, wasanii wanne waliofika Kituo Kikuu cha Polisi bado wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi.

View attachment 467134

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa bado wasanii hao Wema Sepetu, Dogo Hamidu, Khalid Mohamed (TID), na mtangazaji maarufu wa Clouds TV Babuu wa Kitaa bado wanashikiliwa na jeshi hilo.

“Bado tunawashikilia kwa mahojiano zaidi,” amesema Sirro kwa kifupi.

Wasanii wengine waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambao wanatakiwa kufika kituoni Jumatatu ni Vanessa Mdee, Tunda na watu wengine Halidali Kavila, Amani, Kashozi na Omry Sanga.

Chanzo: Mwananchi
wote makada kutoka magambani hawa. hadi radio pendwa magambani (kilaudisi) imewakilishwa.

tukisema CCM ilichaguliwa kwa sponsorship ya wana mihadarati 2015 tutakuwa tumekosea?
 
Back
Top Bottom