Kama ulishawahi kukaa Uswazi(Uswahilini )tukutane hapa

Hapa nikiwa na washikaji kwenye hitma. mimi ni huyo mwenye fulana yenye ?
IMG_1477.JPG

Dah, umenikumbusha mbali sana, hapo sinia kabla halijafika chini mchele umeshaisha
 
Maisha ya uswazi ukikosa miongozo bora tu ya maisha basi lazima uangukie kwenye kati ya mojawapo hapa chini
Kutumia mihadarati bange, unga nk
Wizi
Ulevi
Umalaya hii kwa watoto wa kike
Kuzaa kila mtoto na baba yake au mama yake
Kutomaliza masomo ukibahatika msingi basi sekondari humalizi


So kama umekulia uswazi na umepuka hayo yote mpigie makofi mlezi wako na shukuru mungu wako.
Mi nmeeepuka yote hayo,bahti nzuri hujauweka mmea kwenye hyo listi yako.manake nlifanya sensa mtaa wangu pekee una mapusha 13 wa todi
 
Dah, umenikumbusha mbali sana, hapo sinia kabla halijafika chini mchele umeshaisha
Tru dat,hii nliishuhudia kwa macho yangu kipindi niko mdogo mitaa ya gongo la mboto.enzi hizo wali ni chakula adhimu,sio skuiz sembe ina bei kuliko nchele
 
Uswazi raha sana wala hatuna magaga ya miguuni maana nikitoka kuoga tu nakutana na jiwe nje la kusugulia magaga
 
Supu ya uswazi hata ikitengenezwa katika mazingira machafu utamu upo pale pale watu tunajazana katika banda la mama lishe
 
Uswazi, uswazi ili mradi eti unaishi DAR. No thanks. bora ukaishi kijijini kwenu
 
Back
Top Bottom