Kama ulishawahi kukaa Uswazi(Uswahilini )tukutane hapa

Uswazi wapi unapopazungunzia wewe penye nyumba zisizo na mpangilio au unazungumzia uswazi maeneo yanayojulikana haswa ni uswahilini km tandale buguruni kwa mnyamani temeke mikoroshini mwananyamala kwa kopa kwa mama zakaria nk
Mana ninavyojua mimi 80% ya watu wa dsm wanaishi USWAZI tu kwenye nyumba za kupanga chumba kimoja au viwili hata humu JF
Wengi wanaishi uswazi tu ila kupretend tu HIGH LIFE nashauri kila anayetoa ushuuda aseme sasa anaishi wapi
Nafikiri anamaanisha Uswazi kwenye nyumba zisizo na mpangilio na kuwa na wingi wa watu .
 
10948698_923442091021152_904318190_n.jpg
 
Mbona uswazi poa tu, maisha safi kabisa ukitoka kwako unaslimia na kusalimiwa mpaka utakapofika kituo cha basi, maana kila nyumba utawakuta nje hata kama ni saa 12 asubuhi, jirani umeamkaje NAONA UNAKWENDA KAZINI, ee..kazi njema bwana, ukirudi unawakuta jirani NAONA UNARUDI pole na kazi tupo bwana yaani amani tupu.
Usisahau virungu vya sigara kwa wanaume, uswaz Rahaaaa!!!
 
Uswazi wapi unapopazungunzia wewe penye nyumba zisizo na mpangilio au unazungumzia uswazi maeneo yanayojulikana haswa ni uswahilini km tandale buguruni kwa mnyamani temeke mikoroshini mwananyamala kwa kopa kwa mama zakaria nk
Mana ninavyojua mimi 80% ya watu wa dsm wanaishi USWAZI tu kwenye nyumba za kupanga chumba kimoja au viwili hata humu JF
Wengi wanaishi uswazi tu ila kupretend tu HIGH LIFE nashauri kila anayetoa ushuuda aseme sasa anaishi wapi
Mi naishi kwa Mtogole
 
:D:D:D:D:D:D:D:D:D:DIna maana hiyo picha ya vitoto vinajisaidia, vyote vilishikwa haja kwa wakati mmoja!!!!
 
Uswazi kuna mengi kwanza kule jiko la mkaa ndio hutumika basi kama umewahi kuamka ukawasha mkaa wako mwenzio akiamka anaweka mkaa anakuja kuomba makaa ya moto au yuko radhi azunguke hata nyumba tatu atafute moto kuwasha bajeti mafuta ya taa ( mjini miti michache )
Uswaz ukipika ugali chumba chapili anatoka shoga ongeza maji nina kamboga kangu ka jana nimezee
Uswazi ugomvi huanza kwenye zamu za deki korido au choo au kufagia uwanja ( inasababishwa na masista duu au wafanyakazi maofisin wao wanakuwa tight )
Siku hzi imeboreshwa hufanyi usafi unatoa buku5 wanafanya wakaa nyumban
Uswazi nyumba nyingi wapangaji kuanzia 6 na kundelea basi lazima kuna mmoja mbishi kununua luku ya umeme yaani hapo anawasha taa friji kila kitu ikifika zamu yake anavuta domo kuleeee
Uswahilin ukichinja kuku jiandae kugawa kipapatio au kipande maana utaambiwa kabisa jiran usinisahau
Uswahilini kuombana mboga kawaida sana
Uswahili wanawake kwa mabinti wakienda kuoga tunafunga khanga au tenge haswa moja vibonge ndio wanafunga mbili au watu wazima
Linalonikera uswazi
Maji kujaa wakati wa mvua haswa ya choo yanaachiliwa makusudi
Watoto kujisaidia ardhin haswa wadogo chini ya miaka 3 sema siku hzi mapoti mengi na vile viti + poti vimesaidia
 
Matundu kwenye wavu wa mbu, usiniulize ni mbu au nini kimetoboa???
 
Dah kama ulikuja mjini kwa mbio za mwenge kama wengi wetu humu uswazi hakukwepeki. Sema kikubwa ni unajinasua vipi? Mimi nilikuja dar wakati nimechaguliwa chuo.....Kwa hiyo uswazi nilikaa. (ofcourse kama wewe ni wa kishua hizi habari huwezi zielewa)

..ila tukio sitakaa nilisahau kamwe ni pale nilipoingia mtaani...nimemaliza chuo....nililiwa timing nimetoka..nikaibiwa kila kitu! I mean kila kitu. Na hapo ndo nimetoka chuo nilikuwa nimetumia ile hela ya boom kununua kitanda, godoro, TV na Radio na mazagazaga mengine. Yaani nyumba nilikuta imesafishwa haswa! Kiukweli nililia sana ila sasa nilikuwa sina pa kuanzia. Kwenda polisi usiku huo naombwa Rushwa wakati mimi ndo nimeibiwa...Jamani hii nchi achana nayo kabisa. Sometimes wengine Magufuli tunamuelewa!

In any case, yale maisha nikiyakumbuka Kiukweli naona kama taifa tuna safari ndefu. Lakini somo kubwa nililolipata ni hili: Maendeleo ni juhudi binafsi. Hata kama ungelalamika mpaka Yesu arudi. Maendeleo yako ni wewe mwenyewe. Ukiendekeza Pombe (siku hizi ni viroba), mademu/wakaka, disco nk....katika yale mazingira aisee kutoboa ni ngumu.

All I call say to survive in Dar and evolve successfully you have to be a worrior!
 
Maneno mengiiiiiii sema niliingizwa mjini. Maneno mawili tu.
 
Uswazi ni sehemu ya kufichia umaskini, nyodo na viburi na kila aina ya ushenzi hufichwa humo, ukikosa sawa ukipata sawa ni maisha tu unasonga.
 
Back
Top Bottom