JWTZ Yatoa ufafanuzi juu ya Mavazi ya Kijeshi aliyovaa Rais huko Arusha

Hongera mleta mada kwa kwenda na wakati. Sasa hv ni fashion kumsifia Magufuli kila afanyacho. Ila umeme ni janga na hali ya maisha ya mwananchi ni ngumu hasa mkulima. Tunachokiona ni hofu kwa watumishi wa umma ila mikakati haswa ya maendeleo ni kizungumkuti. Na watanzania walivyo wepesi hawaukizii maendeleo bali wanangoja kusikia habari za majipu.

Kichekesho kingine Magufuli anasisitiza hapa kazi tu lakini hawaulizi watu wanaoenda kumshangilia wanafanya kazi saa ngapi. Toka juzi ndio nimebaki hoi hapa Arusha. Barabara zinafungwa mpaka masaa mawili kisa Magufuli anapita!! Sasa hapa kazi tu huku unawafungia wananchi barabara wataenda kazini saa ngapi!!!
 
..mbona Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete, hawakuwahi kuvaa mavazi hayo.

..au, JWTZ wanataka kusema hii ni mara ya kwanza wanafanya mazoezi ya kijeshi?

Inawezekana hawakuwahi kuvaa kwa sababu labda walikuwa hawapendi tu.

Yaani kwenye hili sioni kabisa penye tatizo.

Kwanza hili tukio linanikumbusha kipindi flani hivi..2008 au 2009....Kikwete alionekana kwenye picha huko Songea kama sijakosea, akimpa mtoto pipi.

Watu walivyoshikia bango ile picha ungedhani ni kiama kinakuja.
 
Well, you said it. Kuna watu wameishikia sana bango hii issue.
Umemuelewa Nyani Ngabu au mzee umeingia kichwa kichwa nyavuni? Hebu angalia maana ya neno aliloliandika Nyani Ngabu halafu uone kama yuko upande wako au la!?

nontroversy ‎(plural nontroversies)

A debate in the press or the blogosphere where one side has been repeatedly demonstrated to be clearly wrong but vocally advocates for their position.
 
Nisingemuelewa nisingemjibu accordingly. Jeshi limejibu kwa kuelimisha UMMA na sio kwa Lengo jingine au Hilo unalotaka kulishinikiza kwenye mada yako.
Hujanielewa! Kwa jeshi kujibu ni ku-stir further discussions about the not-so-controversy. Jeshi lingekaa kimya tu! Watu wangeongea na kuchoka.

Kwa maana hiyo, wale waliokuwa wakishadadia hilo jambo wamefanikiwa. Kwani wamepata attention ya jeshi sasa. Lakini kwa jeshi kuongea, ina maana mjadala utaendelea na kuzidi kuwapa mileage washadadiaji.
 
..mbona Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete, hawakuwahi kuvaa mavazi hayo.

..au, JWTZ wanataka kusema hii ni mara ya kwanza wanafanya mazoezi ya kijeshi?
Umezaliwa 1990 nn...Nyerere keshapga xn zile gwanda km unabisha naenda maktaba ukapekuepekue
 
  • Thanks
Reactions: nao
Umezaliwa 1990 nn...Nyerere keshapga xn zile gwanda km unabisha naenda maktaba ukapekuepekue

..nimeshapekua maktaba.

..na sijamuona Mwalimu kavaa uniform mabaka-mabaka za jeshi wakati wowote.

..kuna picha wanadai kavaa magwanda ya JKT lakini siyo kweli. mimi magwanda ya JKT nayajua.

..Mwalimu na Kawawa waliwahi kuvaa nguo za mgambo, lakini ni kwasababu walipitia mafunzo ya mgambo.
 
Mimi sijui sana protocol za Kijeshi kwa kuwa sijapitia huko, lakini mbona CDF anapiga saluti kwa huyo Waziri?

Kupigiwa Saluti sidhani kama ni ishu kwani hata W.Mkuu pia anapigiwa Saluti, ila Raisi wa JMTZ ni Amiri Jeshi Mkuu yaani ni Mkuu wa Majeshi na ndiye anayeteua na kutengua CDF, ndiye anayetoa Amri ya majeshi yetu kwamba yaende vitani au yasiende!
 
Umemuelewa Nyani Ngabu au mzee umeingia kichwa kichwa nyavuni? Hebu angalia maana ya neno aliloliandika Nyani Ngabu halafu uone kama yuko upande wako au la!?

nontroversy ‎(plural nontroversies)

A debate in the press or the blogosphere where one side has been repeatedly demonstrated to be clearly wrong but vocally advocates for their position.
Umemeza dawa (Anti-psychotics) jioni hii mkuu!? Maana naona Kama umesahau..
Ukiisoma hiyo mada niliyoleta ndio utaelewa Kama it's a Controversy or Nontroversy. Meza dawa zako kwa wakati mkuu.
 
Kupigiwa Saluti sidhani kama ni ishu kwani hata W.Mkuu pia anapigiwa Saluti, ila Raisi wa JMTZ ni Amiri Jeshi Mkuu yaani ni Mkuu wa Majeshi na ndiye anayeteua na kutengua CDF, ndiye anayetoa Amri ya majeshi yetu kwamba yaende vitani au yasiende!
kwa hiyo hiko ndio kigezi cha kumfanya avae gwanda la Jwtz kirahisi vile.
 
Hujanielewa! Kwa jeshi kujibu ni ku-stir further discussions about the not-so-controversy. Jeshi lingekaa kimya tu! Watu wangeongea na kuchoka.

Kwa maana hiyo, wale waliokuwa wakishadadia hilo jambo wamefanikiwa. Kwani wamepata attention ya jeshi sasa. Lakini kwa jeshi kuongea, ina maana mjadala utaendelea na kuzidi kuwapa mileage washadadiaji.
Narudia tena JESHI HALIJAMJIBU MTU, JESHI LIMETOA ELIMU NA UFAFANUZI KWA UMMA.
 
Back
Top Bottom