Juliana Shonza aitaka Serikali kuharakisha ujenzi wa Zahanati Kata ya Mmbebe na Wodi ya Akina Mama, Isansa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,994
961
"Serikali ina mkakati gani wa kuunga mkono juhudi za Wananchi wa Kata ya Mmbebe kukamilisha ujenzi wa kituo cha Afya" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Serikali imeendelea kutenga fedha kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya vilivyoanza kujengwa kwa nguvu za Wananchi sambamba na kujenga vituo vipya. Boma la kituo cha Afya Kata ya Mmbebe limejengwa kwenye Zahanati ya Mmbebe ambapo eneo lina ukubwa wa Ekari tatu. Eneo hilo halitoshi kwa kituo cha Afya. Halmashauri inapaswa kutafuta eneo litakalowezesha ujenzi wa kituo cha Afya wakati Serikali ikiendelea kutafuta fedha kwaajili ya ujenzi" - Mhe. Dkt. Festo Dugange, Naibu Waziri TAMISEMI (Afya)

"Tuko katika hatua za mwisho kupata eneo jipya katika Kitongoji cha Itanga. Naomba kupata msimamo wa Serikali endapo mchakato utakapokamilika, Je, Serikali itakamilisha mchakato haraka kwasababu wananchi wa Kata ya Mmbebe wanapata changamoto hasa kwenye masuala ya Afya?" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Tuna Kituo cha Afya katika Kata ya Isansa lakini kwa muda wa miezi sasa hakina wodi za kulaza wagonjwa hususani wodi ya akina Mama. Lini Serikali itatupatia wodi ya akina Mama katika kituo cha Afya cha Kata ya Isansa?" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Serikali Sikivu ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan itatafuta fedha na kupeleka kwenye Kata ya Mmbebe kwaajili ya kuwaunga mkono wananchi kwenye ujenzi wa kituo cha Afya. Serikali imeshafanya tathmini kwenye vituo vyote vya afya vyenye majengo pungufu ya yale yanayohitajika kwaajili ya kutoa huduma za afya. Tutahakikisha tunapeleka fedha katika kituo cha Afya cha Izaze kujenga jengo la wazazi na majengo mengine ili kiweze kutoa huduma nzuri kwa wananchi" - Mhe. Dkt. Festo Dugange, Naibu Waziri TAMISEMI (Afya)

Juliana Shonza.jpg
 
Back
Top Bottom