Mbunge Shonza Afunguka Miaka Mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassa Katika Mkoa wa Songwe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,960
954

MBUNGE SHONZA AFUNGUKA MIAKA MITATU YA RAIS MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA MKOA WA SONGWE

"Kwa bahati nzuri nimekuwa Mbunge kwa awamu ya pili Mkoa wa Songwe, tangu Mkoa wa Songwe uanzishwe mimi nilikuwa Mbunge, ninaujua vizuri Mkoa wa Songwe. Najua wapi tumetoka, wapi tumefika na wapi tunakwenda" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Kimsingi nichukue nafasi hii kumshukuru sana na kumpongeza sana Rais wetu. Sisi kama wabunge tumeona namna ambavyo utekelezaji wa Ilani unavyotekelezwq kwenye Mkoa wetu wa Songwe, tuna kila sababu ya kumpongeza. Suala la kumpongeza Mheshimiwa Rais ni suala endelevu kwasababu kazi tumeiona. Mkoa wa Songwe kwa sasa umekimbia" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Miaka Mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa ndani ya Mkoa wa Songwe, Mkoa ni Mpya na kwa Miaka mingi tulikuwa hatuna hospitali ya Mkoa lakini mpaka sasa tuna Hospitali ya Mkoa ya kisasa, majengo yamekamilika ikiwemo jengo la Mama na Mtoto, Wanawake wa Mkoa wa Songwe tunajivunia sana" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Tumeshuhudia ndani ya Miaka mitatu ya Mama Samia Suluhu Hassan kila Mkoa umepatiwa CT-Scan. Mkoa wa Songwe ilikuwa likija suala la CT-Scan ilikuwa lazime uende Mkoa wa Mbeya palipo Hospitali ya Kanda. Sasa tuna vifaa na watumishi na majengo mazuri ya kisasa" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Mkoa wa Songwe unazo Wilaya Nne, ni Wilaya ya Mbozi tu ndiyo ilikuwa na Hospitali ya Wilaya ambayo ni Wilaya kongwe lakini ndani ya Miaka mitatu ya Mama Samia Suluhu Hassan ukienda Wilaya ya Songwe, Momba, Ileje kuna Hospitali nzuri zimejengwa, zimekamilika na zimeanza kufanya kazi" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Huwezi kujenga Hospitali za Mikoa na Wilaya bila kujenga vituo vya afya kwasababu vituo vya afya vinapunguza msongamano kwenye Hospitali kubwa. Mkoa wa Songwe karibu kila Wilaya, kila Kata imepata vituo vya afya. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kubeba agenda ya kupunguza vifo vya Mama na Mtoto.
maxresdefaultQAWSDEAXFDR.jpg
 
Namuomba pia Mheshimiwa Juliana Daniel Shonza apiganie kujengwa kwa kituo cha afya kata ya Mlowo. Maana haiwezekani kata ina wakazi takribani elfu 66 lakini haina kituo cha afya .wakati kata ya isansa iliyo na watu wachache ukilinganisha na Mlowo inakituo cha afya na gari la wagonjwa.

Hali hii ya kutokuwepo kwa kituo cha afya ndio ambayo inachochea wagonjwa wengi kwenda hospitali ya wilaya Vwawa ,ambao kama kituo cha afya kingekuwepo Mlowo basi wengi wangepatiwa huduma na matibabu Mlowo na kuishia Mlowo badala ya kwenda kusongamana Vwawa.
 
MBUNGE SHONZA AFUNGUKA MIAKA MITATU YA RAIS MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA MKOA WA SONGWE

"Kwa bahati nzuri nimekuwa Mbunge kwa awamu ya pili Mkoa wa Songwe, tangu Mkoa wa Songwe uanzishwe mimi nilikuwa Mbunge, ninaujua vizuri Mkoa wa Songwe. Najua wapi tumetoka, wapi tumefika na wapi tunakwenda" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Kimsingi nichukue nafasi hii kumshukuru sana na kumpongeza sana Rais wetu. Sisi kama wabunge tumeona namna ambavyo utekelezaji wa Ilani unavyotekelezwq kwenye Mkoa wetu wa Songwe, tuna kila sababu ya kumpongeza. Suala la kumpongeza Mheshimiwa Rais ni suala endelevu kwasababu kazi tumeiona. Mkoa wa Songwe kwa sasa umekimbia" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Miaka Mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa ndani ya Mkoa wa Songwe, Mkoa ni Mpya na kwa Miaka mingi tulikuwa hatuna hospitali ya Mkoa lakini mpaka sasa tuna Hospitali ya Mkoa ya kisasa, majengo yamekamilika ikiwemo jengo la Mama na Mtoto, Wanawake wa Mkoa wa Songwe tunajivunia sana" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Tumeshuhudia ndani ya Miaka mitatu ya Mama Samia Suluhu Hassan kila Mkoa umepatiwa CT-Scan. Mkoa wa Songwe ilikuwa likija suala la CT-Scan ilikuwa lazime uende Mkoa wa Mbeya palipo Hospitali ya Kanda. Sasa tuna vifaa na watumishi na majengo mazuri ya kisasa" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Mkoa wa Songwe unazo Wilaya Nne, ni Wilaya ya Mbozi tu ndiyo ilikuwa na Hospitali ya Wilaya ambayo ni Wilaya kongwe lakini ndani ya Miaka mitatu ya Mama Samia Suluhu Hassan ukienda Wilaya ya Songwe, Momba, Ileje kuna Hospitali nzuri zimejengwa, zimekamilika na zimeanza kufanya kazi" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Huwezi kujenga Hospitali za Mikoa na Wilaya bila kujenga vituo vya afya kwasababu vituo vya afya vinapunguza msongamano kwenye Hospitali kubwa. Mkoa wa Songwe karibu kila Wilaya, kila Kata imepata vituo vya afya. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kubeba agenda ya kupunguza vifo vya Mama na Mtoto.
Wameanza kutapatapa..
 
Back
Top Bottom