Jifunze mapishi na namna mbalimbali za kupika mkate

Dadaa samahani naomba kuuliza kama hauna hiyo ARKI je waweza tumia nini kingine au je bila iyo mkate hupoteza radha au hutoka vibaya? nataka niujaribu ila hiyo kitu ni ngumu kupatikna

Vanilla powder tumia.....ila ukikosa haina tatizo weka tu hiliki mkate utakua na ladha nzuri tu...
 
Natamani kupika ila mayai huwa sili kabisa je, naweza kupika bila kuweka yai?
 
Hahahaha ukimaliza lete tule....lol

Chila tayari.

Kisimu hakitaki ku upload picha, angalau tukala kwa picha.

Next week nataka nijaribu mkate wa ufuta kwa cooker mana mm sina seredani.

Jee lazima iwe plate ya coil au hata ya kawaida tu?
 
Chila tayari.

Kisimu hakitaki ku upload picha, angalau tukala kwa picha.

Next week nataka nijaribu mkate wa ufuta kwa cooker mana mm sina seredani.

Jee lazima iwe plate ya coil au hata ya kawaida tu?

Plate yeyote tu ilimradi inaleta moto..mie yangu coil..ila ukiugeuza itabidi kuzidisha moto ili mkate usije kuanguka...
 
Mahitaji
Mchele kikombe 1
Hiliki kiasi
Sukari 1/2-3/4
Yai 1
Tui la nazi vikombe 2
Hamira kijiko cha chai kimoja

Namna ya kutaarisha

1)Osha mchele na roweka hadi uwe laini kiasi.
2)weka mchele,hiliki,yai,hamira na tui la nazi kwenye blenda....saga hadi viwe laini
3)mimina kwenye bakuli...subiria uumuke

Namna ya kupika

1)weka chuma cha kuchomea(usitie mafuta) katika jiko moto kiasi... kikipata moto chota upawa mmoja wa mchanganyiko wako na mimina kwenye chuma chako...zungusha ili utandazike
2)funika na ufunikio juu..ukiona mkate wafanya vitundu tundu toa na weka pembeni.
3)fanya hivo hadi umalizie zilobaki


Mkate wa chila tayari kwa kuliwa

Farkhina....u r blessed dada! endelea kutulisha:smile-big:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom