Uchaguzi 2020 Je, wajua kuna watu wazuri, waadilifu wenye uwezo, wanaotaka kuingia Bungeni kulisaidia Taifa, Bunge na kumsaidia JPM kwa dhati, lakini kwa vile...

Wanabodi,

Kila nipatapo fursa, huja na makala elimishi kuhamasisha uzalendo kwa taifa letu kupitia makala elimishi hizi za " Kwa Maslahi ya Taifa"

Swali katika mada yangu ya leo ni katika kuwapata wagombea wa CCM, Jee Vikao vya uteuzi vya CCM, vitazingatia tuu matokeo ya kura za maoni, ambayo ndio maslahi ya CCM, au navyo vitangulize mbele maslahi ya taifa kwa kutupatia wagombea wazuri, watu safi, waadilifu na wenye uwezo wa uongozi hata kama kwenye kura za maoni, wamepa kura sifuri?.

Vikao vya uteuzi vya CCM, vinakaa wiki hii, kuteua wagombea ubunge na udiwani, hivyo hili ni bandiko la ushauri, info pack kwa chama changu cha Mapinduzi, CCM, kwa kuwajulisha kuwa miongoni mwa watangaza nia kupitia CCM, kuna watu wazuri, watu safi, watu waadilifu na wenye uwezo wa uongozi waliogombea kupitia CCM na kutaka kuingia Bungeni kwa lengo la kwenda kulisaidia Taifa, Bunge, na kumsaidia JPM kwa dhati kabisa ya kusaidia kufuatia kubaini madhaifu mbalimbali ya Bunge na serikali, na kufuatia uadilifu wao, watu safi wazuri, waadilifu hawa, hawakutoa hata senti tano!, na kwa vile watu hawa hawakutoa hata senti 5!, na kufuatia ule msemo wa Waswahili usemao "Mkono mtupu haulabwi", wajumbe walifanya yao!.

Kama sasa na vikao vya uteuzi vya CCM, vitazingatia tuu kura za wajumbe na matokeo ya kura za maoni pekee, then CCM, itapoteza watu wengi safi, wazuri, waadilifu na wenye uwezo wa uongozi, lakini watakosa kuteuliwa kwasababu hawakutoa chochote na matokeo yake hawakupigiwa kura zozote na wajumbe.

Mimi ni miongoni mwa kundi hili ambaye nilitangaza nia kugombea kupitia CCM, sikutoa hata senti tano kwa yoyote, na katika kura za maoni, nikavuna nilichopanda!.

Hizi ni baadhi ya agenda zangu zilizonivutia kwenda Bungeni.



Japo wajumbe walifanya yao, lakini kufuatia trends za siasa za Tanzania kwa sasa zinaonyesha Bunge lijalo linakwenda kuwa ni Bunge la CCM predominantly, bado naamini ili Bunge hili liwe na impact ya kuisaidia serikali, linahitaji baadhi ya mijitu bold na critical thinkers ambao watakuwa critical kule Bungeni, vinginevyo kama tutajaza wapiga meza tuu kuunga mkono kila kitu, then kiukweli kabisa, Bunge lijalo lita...

Naomba nisimalizie.

Mungu waongoze wajumbe wa vikao vya maamuzi, kutuchagulia watu wazuri, waadilifu wenye uwezo ambao sio tuu watawasaidia wananchi, watalisaidia Bunge na kuisaidia serikali ikiwa ni kumsaidia Rais John Pombe Joseph Magufuli.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki CCM.

Paskali
Kada wa CCM.
PASKO one thing unachokosea (labda kwa kujifanya haujui) ni kuwa ukishaingia bungeni kwa tiketi ya CCM unakuwa sio wewe tena. Huwezi kulisaidia taifa wala Serikali. Unakuwa ni daraja tu la kupitisha mambo ya Serikali kwa maagizo ya Serikali na kumsifia rais. Hiyo ndiyo kazi yako.

KUMBUKA
1. Suala la korosho Wabunge wote wa kusini waliambiwa wataondoka

2. Katika kupitisha bajeti katibu Mkuu wa CCM huwa anaenda kuangalia watoro wakiamini hawaiungi mkono bajeti

N.k

CCM siyo wajinga kuwafanyia wanachowafanyia....wanajua hata uwe na hoja vipi, hutazitumia kule bungeni. Hata uwe Profesa kule bungeni unakuwa ni darasa la tatu B
 
Pascal Mayalla,

Paskali acha lugha za kitapeli, kwanza kutokutoa rushwa hiyo haimaanishi ni dalili ya uadilifu. Huenda hukutoa kwakuwa huna cha kutoa. Pili unaweza kuwa muadilifu lakini usiwe unauzika kwa wapiga kura. Inaonekana Paskali uliingia mkenge kwa propaganda kuwa ccm ccm imedhibiti rushwa, hivyo ukaamini kuwa kisemwacho ni kweli. Hayo unayosema kwamba unataka kwenda bungeni ili umsaidie magu, yeye mwenyewe sio muadilifu linapokuja suala la rushwa, vinginevyo tusingeona watu kwenda kuunga juhudi, ama chaguzi za nchi zisingenajisiwa.

We sema hivi, umeona maisha ya huku mtaani ni magumu, huku ukiona watu wenye elimu duni wakila keki ya taifa huko bungeni. Hivyo unatumia gia lile lile la wapigania tumbo kumtajataja rais ili upate ulaji. Huo mchango wako unaotaka kuupeleka bungeni, changia huku huku mitandaoni utaonekana na kufanyiwa kazi. Ni kweli ww una point za kuridhisha, ila huna mvuto wowote wa kisiasa. Kama unataka kumsaidia huyo John Magufuli, nenda nyumbani kwake ana kazi nyingi.

Sikutegemea kama utaishiwa kiasi cha kujidhalilisha na siasa za kumtumikia mtu. Hata Mrema umri ulivyomtupa mkono na yeye akaanza haya haya ya kwako ya kutaka cheo ili amsaidie rais! Hii ni bonge la aibu kwa mwanaume anayejitambua. Kwa taarifa yako magu hahitaji watu waadilifu, bali anahitaji wanaonmnyenyekea na kutii kila anachoamini. Hivyo we hutaki kwenda kumsaidia kwakuwa ni muadilifu, bali ni kuwa unafit hizo sifa nyingine.
 
Pascal Mayalla,

Hili bandiko limejaa ukweli mtupu. Tulioenda na mikono mitupu tuliambulia tulichopata. Wajumbe walitumia sawasawa ule msemo mkono mtupu haulambwi. Lakini wakasahau kuwa uongozi haununuliwi.
 
Japo wajumbe walifanya yao, lakini kufuatia trends za siasa za Tanzania kwa sasa zinaonyesha Bunge lijalo linakwenda kuwa ni Bunge la CCM predominantly, bado naamini ili Bunge hili liwe na impact ya kuisaidia serikali, linahitaji baadhi ya mijitu bold na critical thinkers ambao watakuwa critical kule Bungeni, vinginevyo kama tutajaza wapiga meza tuu kuunga mkono kila kitu, then kiukweli kabisa, Bunge lijalo lita.
Ukweli mnauona lakini mnaufumbia macho. Siioni mbunge wa CCM atakae iambia serikali ukweli kama ana wazo mbadala. Wanaweza wakawapo wachache lakini sioni kama watakuwa na sauti ya kutosha.

Kukosekana kwa wapinzani kama itakuwa hivyo unavyotabiri, maana yake kutakuwa na vacuu na wale wabunge wa CCM watakao jifanya wana kiherehere watakuwa considered kama wapinzani wa serikali, na speaker ata deal nao. Party caucus itafanya kazi yake, utaingizwa serikalini a le Bashe na hapo utanyamaza.

Kwa mfumo wa CCM sioni pa kutokea. Labda kama mna resources watu waanzishe an independent think tank ya kushauri serikali. Bahati mbaya hapa mtahitaji fedha na mtaambiwa ni vibaraka wa mabeberu. Hakuna ubishi kuwa kwa sasa CCM ni sauti moja na hapo bila upinzani tutaendeshwa na sauti moja kama nchi.

Fikiria SGR na Elimu bure walipoongelea CDM wakati wa Kikwete CCM waliwacheka na kuwaita wenda wazimu, sasa kati ya majigambo ya CCM ni hivyo vitu viwili.
 
Pascal kama unahisi umeonewa na wajumbe na unafaa zaidi ya wengine, kata rufaa mapema na uwe nasababu kwann wengine hawafai
 
Pascal Mayalla,

Uncle nakukubali saana japo nilisikitika sana nilipofahamu umekua kada wa CCM.

Sababu zilizonisikitisha kwa wewe kuwa kada wa CCM ni namna utakavyopoteza weledi wako was jicho la tatu (uono) katika chambuzi zako zakisiasa na uongozi.

Kiukweli mtu Kama wewe unatakiwa uendelee kutofungwa na upande wowote kwa maslai ya taifa.

Uncle whatever made you become mwanachama wa ccm kwangu nimeshindwa ku justify kua ni sahihi otherwise kwakua wewe ni mkubwa labda kuna usalama unautafuta Kutoka kwenye system.

Dua yangu kamati kuu isikufikirie kabisa ikiwezekana ufutwe na uanachama ili utumikie taifa lako Kama Mzalendo halisi tuliyekufahamu.
Usiogope maisha Mwenyezi Mungu atakupigania palipo haki.

Kila la heri Uncle pascal
 
Kwa hili umeongopa, mtunzi wa sheria zote ni Magufuli, kule bungeni wanataka watu wenye sauti za kusema "NDIYOOOO" hakuna mtu anayemsaidia Magufuli CCM.

Wanatafuta mavuvuzela sio wasaidizi.

Lini hao unaoita wenye uwezo walimsaidia, na utuambie walimsaidia sheria gani na ipi au hata kifungu kidogo cha sheria?

Au unaongelea kamati za Makinikia?! Na hawakuwa wabunge.

Ubunge ni ulaji tu na sio uwakilishi.

wewe umewakilushwa lini huko bungeni?

Lini umewahi kukaa au kukutana na mbunge ukampa issues za kukuwakilisha?

Lini na wapi zaidi ya kampeni za uchaguzi mbunge kakutana na anaowawakilisha zaidi ya kukutana na watu wa chama chake?
 
Mayallah, hufai kabisa. Mwanzo nivutiwa sana na uandishi wako. Lakini baadae haswa 2015 hadi leo uandishi wako waweza kukupeleka kuzimu. Nakuombea kwa Mungu akusamehe.
 
Kura za maoni ni moja ya indicator ya mtu kukubalika na jamii anayo omba kuiwakilisha. Aliyepata sifuri hakubaliki, na Kuna sabb nyingi za kutokukubalika, siyo uadilifu peke yake.


Hapa umenichanganya. Kama unajjua hukupanda mbegu bora basi jipange ukapande upya.


Kwenye hili mkuu naomba nitofautiane na wewe. Kuna kitu kinaitwa "party caucus" huwa kinawa-fix watu wenye nguvu ya hoja kinzani ndani ya chama kilichompa ubunge. Ungetaka kuyatekeleza haya basi ungegombea kupitia vyama vya upinzani. Hapa ndipo ingeweza kulikosoa bunge linaloongozwa na wanaccm.

Kuna wagombea hapo Paschal hajataka kuwaongelea lakini ila azunguuka sana.
 
unafurahisha eti kupata viongozi wazuri watakao msaidia magufuli,kazi ya bunge ni kuisimamia serikali MKuu wa Serikali ni Magufuli ambaye hapangiwi sasa wewe unataka ukamsaidie kivipi,tuache unafiki bunge la sasa hivi la utawala huu halihitaji mtu mwenye uwezo wala uadilifu hata Shilole anaweza akawa mbunge na mambo yakenda.
 
Kaka Pascal mayala Uzalendo wa Nchi kwa misingi ya kivyama Ni vigumu kuwapata watu wa namna hiyo. Vyama vya siasa Katika mitazamo hasi na mfumo tulionao, inachoangalia Ni:

1. Ushindi wa Chama thus means mgombea wa Chama kushinda bila kujali uadilifu wake
2. Wananchi wamemkubali na watampigia Kura na atashinda kwa Maslahi ya Chama

Kwahiyo Chama focus yake kubwa Ni kusoma saikolojia ya Mpiga kura ipoje. Chama kinampeleka mtu anayekubalika Sio uadilifu. Hatua za upatikanaji wa mgombea Katika ngazi mbali mbali tunazoziona ilikuwa na malengo mazuri Sana ya kupata watu tunaowaita wazalendo, lkn kwasasa sio ndio maana yake ila Ni kutimiza tu utaratibu na kuonyesha kwamba Katiba za Chama husika inafuatwa na demokrasia ipo ndani ya Chama.

Kwahiyo Mimi siamini Hali ya kisiasa iliyopo kwa Sasa hatuwez kupata wazalendo wa kweli zaidi ya wale wasio waadilifu na malengo Thabiti ya kuwatumikia wananchi.

Swali la msingi Nani alaumiwe Katika hili?
 
HUKO kamati kuu ya CCM Karibu wajumbe wote wanajua kwamba hata wakimpitisha Makonda kuwa mgombea wa Kigamboni,Ni lazima CCM itaibuka kidedea! Kigamboni HAKUNA upinzani mkubwa kiasi Cha kumshinda Makonda.Usiwafundishe kazi wajumbe wa kamati kuu ya CCM.Nyie wajumbe wa Kigamboni mlishamaliza kazi yenu.Mlichofanya nyie Ni maoni na mapendekezo tu. Kamati kuu ndo yenye final say ya kuteua mgombea. Makonda angefaa sana Kigamboni.
 
Kila nipatapo fursa, huja na makala elimishi kuhamasisha uzalendo kwa taifa letu kupitia makala elimishi hizi za " Kwa Maslahi ya Taifa"
Sio kweli, CCM imechokwa, inanuka, inatisha, inatia aibu. Nina sababu millions za kujustify hili. Pascal wewe si msafi kama mimi na huna moral authority ya kuandika kuielimisha jamii labda jamii ya CCM
 
Back
Top Bottom