Uchaguzi 2020 Je, wajua kuna watu wazuri, waadilifu wenye uwezo, wanaotaka kuingia Bungeni kulisaidia Taifa, Bunge na kumsaidia JPM kwa dhati, lakini kwa vile...

Tatizo sio kuingia bungeni na kusaidia shida hata uwe mzuri vipi lakini kama ufanyi kazi kwa maagizo ni lzm uchezee tumbuzi,wote ni wazuri ila wanakuwa na chaguzi mbili either utii maagizo ili usife njaa au utumie taaluma yako ufe njaa kwa kuchezea utumbuzi.

Ukileta professenalism imekula kwao ni lzm uwe type ya musiba ili usifie njaa.Mfano maagizo yamekuja nunua wapinzani we ukihoji haiwezi leta tija hapa ni lzm uchezee utumbuzi,au hakuna mpinzani kuruhusiwa kufanya siasa wwe ukawaruhusu as per katiba hapa imekula kwako
Hahahaaa...
Kaabuud
Mwaki embe...
 
Kama kweli kuna watu waadilifu na wa maslahi ya taifa, watakumbukwa kwenye nafasi 10 za Wabunge wa kuteuliwa. Asilimia kubwa ya waliogombea ni wasaka vyeo tu, wazalendo ni wachache sana. Ndiyo maana tuhuma za rushwa zimetapakaa.
Hao wa maslahi ya taifa ndo hawatakiwi na Magu.Prof Assad aliishia kuambiwa anajifanya muhimili kwa kutetea maslahi ya taifa
 
Mfumo wenyewe wa kuwapata wagombea umejengwa kwenye misingi ya rushwa tangu awamu zilizopita kwa wajumbe wote wa ngazi zote.

Hakuna uwezo wa mgombea hapo bali ni nani katoa kiasi gani. Hii imepelekea baadhi ya wabunge kutumia vikao vya Bunge km vijiwe vya kupiga stori, makofi na wengine kusinzia tu sababu hawana uwezo wa kujadili hoja.

Ubunge kwa sasa ndiyo kazi rahisi kuliko zote na yenye masilahi makubwa kuliko kazi zote. Sifa kuu mi kusoma na kuandika na umahiri wa kuwekeza fedha kujiandaa kwa uchaguzi unaofuata. Kwa hali km hii sidhani km tutafikia uwezo wa mabunge ya wenzetu wanaojitambua na kuweka vigezo vya mtu kuwa na sifa za kugombea ubunge kulingana na wakati tulionao.

Rushwa ni mdudu hatari sana kwa mustakbali wa maendeleo ya Taifa lolote hasa hizi nchi za Dunia ya Tatu.
 
Kura za maoni ni moja ya indicator ya mtu kukubalika na jamii anayo omba kuiwakilisha. Aliyepata sifuri hakubaliki, na Kuna sabb nyingi za kutokukubalika, siyo uadilifu peke yake.

Hapa umenichanganya. Kama unajjua hukupanda mbegu bora basi jipange ukapande upya.

Kwenye hili mkuu naomba nitofautiane na wewe. Kuna kitu kinaitwa "party caucus" huwa kinawa-fix watu wenye nguvu ya hoja kinzani ndani ya chama kilichompa ubunge. Ungetaka kuyatekeleza haya basi ungegombea kupitia vyama vya upinzani. Hapa ndipo ingeweza kulikosoa bunge linaloongozwa na wanaccm.

Mkubwa salama,

Kura za maoni siyo kigezo kabisa cha kuonyesha kwamba fulani anakubalika.

Hicho unachokisema kukubalika ni kununulika kwa wajumbe ili uonekane unakubalika.

Wewe ukitaka kuangalia tizama magape ya kura kati ya mshindi wa kwanza hadi wa mwisho.

Niseme tu kwamba Morally and ethically upright leaders ni vigumu sana kupatikana kupitia michakato ya "wajumbe"

Shukrani!
 
Unawaza watu waadilifu wakumsaidia raisi ambaye vipindi vyake vyakuongoza vinaukomo badala yakuwaza Watu waadilifu wakulisaidia Taifa litakalokuwepo karne nyingi zijazo.

Waadilifu wengi wenye uwezo mzuri wakufikiri nakutenda wako nje ya mfumo huu wa siasa za vyama lakini pia kwasababu jamii imejengewa uoga wakuhoji na kushauri nje ya mfumo uliopo nawao wameingia katika kundi ilo ndo maana wako kimya.

Wengine wengi walioko kwenye mfumo wa vyama tena kama hicho cha kwako wako kwa ajili ya matumbo yao.Ingekua sio hivyo leo usingekuja hapa na hii mada.
 
Kama kweli kuna watu waadilifu na wa maslahi ya taifa, watakumbukwa kwenye nafasi 10 za Wabunge wa kuteuliwa. Asilimia kubwa ya waliogombea ni wasaka vyeo tu, wazalendo ni wachache sana. Ndiyo maana tuhuma za rushwa zimetapakaa.
Kwani ili uweze kufanya mazuri kwa maslahi ya taifa ni lazima uwe mbunge? Kuna tatizo lakimfumo ambalo kimsingi ndilo linalotusumbua ila tunashindwa kulirekebisha ili kila mtu mwenye nguvu na mawazo mazuri ayatumie kwa ajili ya taifa ndo maana unaona wengi wanakimbilia kwenye siasa na mbunge. Sasa matokeo yake wanakimbilia wabovu uku wale werevu wakibaki kutazama.
 
Mkuu, Pascal Mayalla uzalendo na mapenzi ya dhati kwa taifa hayana masharti (unconditional love) kwamba ili uipende Tanzania na kumsaidia Mh. Rais lazima uwe Mbunge ama Diwani. That's pathetic!

Kuna tofauti kubwa sana katika ya kuwa mzalendo na kuwa kiongozi wa ngazi fulani katika taifa.

Mbona kuna watu humu JF wanaipenda sana Tanzania na wanaishauri serikali kila kukicha na system imewaweka kando? Na kamwe hawajawahi kuandika thread yoyote ya kulalamika.

Unless otherwise useme una maslahi yako binafsi na si yale ya taifa.

Do African political activists actually fight for democratic change or they simply keep alive the well-known old saying that "It's Our Turn to Eat"?
 
Mkubwa salama,

Kura za maoni siyo kigezo kabisa cha kuonyesha kwamba fulani anakubalika.

Hicho unachokisema kukubalika ni kununulika kwa wajumbe ili uonekane unakubalika.

Wewe ukitaka kuangalia tizama magape ya kura kati ya mshindi wa kwanza hadi wa mwisho.

Niseme tu kwamba Morally and ethically upright leaders ni vigumu sana kupatikana kupitia michakato ya "wajumbe"

Shukrani!
Mkuu yasemekana kuna watu waliwapa wajumbe pesa lkn wameangukia pua. Sasa hili nalo unaliongeleaje?

Kuna wanaosema ili wajumbe wamkubali mtia nia lazima awe na sifa zifuatazo:-
-awe ana Mahusiano chanya na watu wa eneo husika. Mfano awe mshiriki mtiifu wa misiba, harusi, harambee, n.k

-asiwe mjivuni

-tofauti yake kimaisha isimtenganishe na jamii. Mfano kama una gari basi gari lako liwe msaada na siyo msala kwa watu wako.

_ awe na ukwasi. Ukwasi unampa mjumbe Imani kuwa mtia nia ana akili ya maisha ndiyo maana ana ukwasi. Lkn ukiwa mwenzangu na mie (pangu pakavu), mjumbe anakutilia mashaka.
 
Pascal umeleta mada nzuri. Ni mada ambayo inakwenda na wakati huu tulionao.

Kwanza na mimi niseme wazi kabisa hapa kuwa nina maslahi na mada hii. Nilitia nia nyumbani kwetu na niliambulia kura "0". Kwa mazingira ya pale kwetu sikuona au kusikia tetesi za rushwa japo kwakusema hivyo haina maana ya mimi kudhibitisha kuwepo au kutokuwepo kwa rushwa. Hii ilinisukuma kuandika andiko hili:
Hongera sana CCM kwa mchakato wa kura za maoni

Kama ulivyoeleza, na mimi nilienda kwenye mchakato huu nikiwa na moyo wa dhati kabisa wa kuwatumikia watu wangu kwa nafasi hiyo. Kuhusu uadilifu, uwezo na uzoefu wangu, hilo sio jambo la kutilia shaka na wanaonifahamu wanajua hilo.

Niliandaa kipeperushi changu na kukisambaza kwa watu wangu wa karibu, punde katibu wa NEC - Itikadi na Uenezi ndugu Polepole akatoa onyo juu ya Jambo hilo. Haraka sana nikatii na kuwataka ndugu, jamaa na marafiki waache kusambaza kipeperushi hicho. Na hilo lilifanyika "with immediate effect".

Ndugu Pascal na wasemaji, baada ya hatua hiyo sikufanya tena aina yoyote ya kampeni wala sikutoa rushwa. Siku ya kujieleza kwa wajumbe ikafika, nikajieleza, mwenyekiti anauliza, " Kuna swali lolote kwa mgombea?" Wajumbe wakajibu kwa sauti moja "hakunaaaa". Nikatoka. Kura zikapigwa na zikahesabiwa wazi kwa kila mgombea kupewa kura zake. Kika zikitajwa, sitajwi mpaka mwisho.

Basi msimamizi wa uchaguzi akawa anaita mtia nia mmojammoja kupita mbele na kusema amepata kura ngapi. Akaita " Amani Msumari" nikapita mbele na kusema " ninawashukuru ndugu wajumbe, sijapata kura yoyote, nimepata sufuri".

Baada ya mchakato huo, moyo wangu umefarijika kwani nimefanya kile ninachokiamini. Nilifurahi zaidi baada ya wazee flani watatu kuniita na kuniambia " kijana umeongea vizuri Sana, wewe ni kiongozi mzuri Ila kwasasa umegombea na mtu ambaye sisi tunamuamini Sana na ni muhimu kwa Jimbo letu, Mungu hakutaka iwe kipindi hiki". Kwakweli nilifurahi Sana.

Kama hakuna rushwa, ni vigumu Sana kumrudisha mtu aliyepata kura sifuri kwani wajumbe walikuwa na sababu kwanini wasimpe kura. Cha muhimu ni kuwa tumepata ya kujifunza kwenye mchakato huu.

Pascal, mimi na wewe tunazo shughuli zetu zinazotuingizia vipato halali, tena vizuri tuu. Ushauri wangu ni kuwa tuendelee kuonesha uzalendo kwa kuitumikia nchi yetu na chama chetu kwa nafasi nyingine.

Binafsi nimejivika kuwa balozi wa kuyasema mema ya chama na serikali. Kukosoa kwa staha pale inapobidi na sikosolei humu mitandaoni. Sio lazima tuwe wabunge kwenye jitihada za kuhakikisha nchi yetu inasonga mbele zaidi.

Amani Msumari
Tanga
 
Pascal Mayalla,

Kaka Pasco, heshima yako.

Miongoni mwa watu ninaowaheshimu humu ndani nawe ni wa juu sana naomba kudeclare hili wazi. Si kwa bahati mbaya hapana, kwa muda mrefu nimekuwa nikiguswa sana na uwasilishwaji wa mada zako hasa kabla ya kutoka kuhojiwa na kamati ile ya bunge kwani baada tu ya lile tukio ladha yako kiasi flani ilipungua(maana ulijiweka upande wa popo) na sasa inafifia zaidi kwa sababu umeamua kujipambanua zaidi kiitikadi(upande uliopo). Sikushangai mkubwa wangu ila umetuacha solemba wapenzi wafuatiliaji wa mada zako hususani jf tuliokuamini sana.

Narudi kwenye bandiko lako la leo. Mkuu leo umekaa upande wa kuhitaji huruma zaidi kutoka kwa kamati ile yenye dhamana maana unajinasibu kuwa una nia ya dhati ya kutaka kumsaidia mkuu ukiwa kule mjengoni ambapo sisi wafuatiliaji tumekwisha shuhudia mara kadhaa kuwa watu kama wewe waliwahi kuwepo na hata walipopewa nafasi zaidi hakuna maajabu waliyofanya zaidi walishusha reputations zao tu hapa sina haja ya kutoa mifano maana hakika unatambua hilo na hata katika mahojiano yenu kwenye hiyo clip na Nyanda wamejaribu kuligusia hilo.

Lakini pili inawezekana umekuja na bandiko hili kwa sababu sasa katika fani yako ya uandishi unajua kabisa sasa hutakuwa na jipya, hutakuwa Pasco yule tuliyemzoea maana hadhira yako tayari umeipoteza sasa unafikiri utafanya nini zaidi ya kukomaa huko ulikoonesha muelekeo wako.

Kazi uliyokuwa unaifanya kaka Pasco watanzania tulikuhitaji zaidi ya huko ulikofikiri kwenda. Kiukweli "umebugi" kwa kiswahili chetu. Angalia sana utajikuta unapoteza kila kitu ambacho wewe umetumia muda mrefu wa maisha yako kukitengeneza. Nakusihi sana mkuu Pasco kabla mambo hayajaharibika sana "tuombe radhi" hadhira yako maana wewe ni mwanadamu kukosea ni kawaida nasi tutakusamehe tu na urudi kuwa Pasco yule tuliyemzoea na tunayemhitaji zaidi.

Nakuhakikishia heshima yako itabaki juu zaidi siku zote hata Mungu atakapokuchukua historia yako itaandikwa nchini kuliko huko unakotaka kwenda. Tatizo la hii nchi mkuu ni mfumo na sio mtu mmoja mmoja ndio maana hata Magufuli hataweza kama ana nia thabiti ila atapita na atayaacha tu kama yalivyo. Ila wewe una silaha kubwa ambayo ni kalamu. Andika Pasco na maandishi yako yataishi siku zote.

Asalaam!
 
Kama kweli kuna watu waadilifu na wa maslahi ya taifa, watakumbukwa kwenye nafasi 10 za Wabunge wa kuteuliwa. Asilimia kubwa ya waliogombea ni wasaka vyeo tu, wazalendo ni wachache sana. Ndiyo maana tuhuma za rushwa zimetapakaa.
Umeandika ukielekezwa na wivu..Pasco anawakumbusha viongozi hata kma kati ya watia nia wote zaid ya 10,000 wakiwemo 5 wasafi na waadilifu wanatosha kulisaidia bunge na taifa..ukiona mtu anaona ubaya zaidi kuliko wema, kichwan ana kasoro..lkn aliyoongea Pasco mengi ni kwa nia nzr kabisa, ni ajabu mtu kuona zaid tamaa ya vyeo kuliko watu wenye nia njema kwa taifa waliojitokeza kutia nia.
 
Pascal Mayalla,

Pascal Muogope Mungu. Mimi nimemaliza. Muogope Mungu tena Muogope hasa kipindi hiki. Usije ukatafuta shimo lakujichimbia Kwa kuandika vitu vinazuwa maswali magumu. Hii nchi itaendelea hata baada ya utawala huu. Hence tujifunze busara nawakati mwingine kukaa kimya.
 
Mkuu yasemekana kuna watu waliwapa wajumbe pesa lkn wameangukia pua. Sasa hili nalo unaliongeleaje?

Kuna wanaosema ili wajumbe wamkubali mtia nia lazima awe na sifa zifuatazo:-
-awe ana Mahusiano chanya na watu wa eneo husika. Mfano awe mshiriki mtiifu wa misiba, harusi, harambee, n.k

-asiwe mjivuni

-tofauti yake kimaisha isimtenganishe na jamii. Mfano kama una gari basi gari lako liwe msaada na siyo msala kwa watu wako.

_ awe na ukwasi. Ukwasi unampa mjumbe Imani kuwa mtia nia ana akili ya maisha ndiyo maana ana ukwasi. Lkn ukiwa mwenzangu na mie (pangu pakavu), mjumbe anakutilia mashaka.
Hizo ni sifa zako wewe, si za CCM zinazotumiwa kupata viongozi, wala hakuna sifa za wajumbe, kuna sifa za CCM.
 
Back
Top Bottom