nzalendo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 11,792
- 12,147
Alitupa vibarua na wamakonde fulani kina mandanga cha kupanda ukoka kwenye nyumba yake msasani,na yeye pia alikuwa anapanda pamoja nasi...Mara zote anatupa maneno ya kihekima hasa baada ya kugundua miongoni mwetu wanapiga stori za vinywaji na mademu....aisee alitupa usia sana yaani bado sauti yake bado naisikia masikioni......1. Kupenda Dini na Kusali sana.
2. Kupenda Utani na Ucheshi.
3. Kukitukuza Kiswahili na Kujivunia Kukiongea Kiufasaha.
4. Kuridhika na Maisha aliyonayo huku akipenda sana Kula Vyakula vya Kiasili na vya kuutunza Mwili kwa muda mrefu.
5. Kupenda mno Mazoezi hasa ya Kutembea kwa Miguu kwa Umbali mrefu.
6. Huruma,, Kusamehe na kutokiwa na Kinyongo na Mtu hasa hasa Adui.
7. Kutopenda Kujitukuza kama Kiongozi na kupenda Ushirikiano na Watu na kuwa mwepesi Kushaurika na Kujifunza.
Pumzika Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Alhaji Ali Hassan Mwinyi hakika Mwendo Umeumaliza na huna baya hata kama lipo Watanzania tulishakusamehe Kitambo na Uhai wako huu mrefu ulikuwa ni Zawadi na Faraja kwetu.
Ulale mahala pema. Peponi AHM.