Je, Haki ya mtoto anayezaliwa nje ya ndoa kisheria imekaaje?

Care Giver

Member
Apr 2, 2024
51
177
Habari wakuu,
Swala la "single mothers" nadhani sio geni kulisikia maskioni mwetu, hapa nazungumzia mwanamke aliyezalishwa na kuterekezwa na mwanaume wake. Hali inayompelekea kulea mtoto peke yake bila mchango wa mwanaume aliyemzalisha.

Hoja yangu inakuja kwenye huyo mtoto aliyezaliwa haki zake kwa baba yake hapo imekaaje?

1. Je ikatokea huyo mwanaume akafunga ndoa na mwanamke mwingine. Sheria inamlinda vipi huyu mtoto?

2. Je kama ikitokea swala la kifo kwa baba sheria itamtambua huyu mtoto kweli? Au ndio imekukla kwake.

Maana naona kama wimbi la hawa watoto linaongezeka kwa kasi. Ebu wajuzi wa sheria mtusaidie kwa ufafanuzi kidogo ili kuwaokoa hawa watoto ili hawa single mothers wapate hints.

Kulea mtoto mzazi mmoja bila usaidizi wa upande wa pili ni changamoto mno, hakika tuwape maua yao.

Nawasilisha kwenu..
 
Sasa kama mama kamkimbia mume wake kijeuri kwa nini alete usumbufu wa kusaidiwa kulea mtoto? Akalee mwenyewe. Mwingine kajiona ana uwezo wa kulea peke yake katimua mume abaki peke yake
 
Kuongezeka kwa single mothers ni matokeo ya mmomonyoko wa maadili ya ndoa. Usomi umekuwa mwingi na wanawake wanataka uhuru wa kuishi peke yao bila mume ila kuzaa watoto wanataka
 
Kuna Single Maza wa aina mbili au Zaidi

1. Ulizaa Bila Ndoa na Mwanaume Single ambaye alikuja kuoa mke mwingine.

2. Ulizaa Bila ndoa na mwanaume anayezalisha wanawake ovyo ovyo na kuwaacha.

3. Ulizaa na Mume wa Mtu mwenye familia yake na watoto wake Wengi tuu Kwenye Ndoa yake.

4. Ulizaa Ndani Ya Ndoa inayotambulika Kiserikali lakini mkaachana ukiwa na m/watoto.

5. N.k

Katika Scenario Zote hapo Juu nadhani kwa mtazamo wangu Sheria itamuhusisha Mwanaume namba 4. Tuu na kwa mbaali namba 1.
 
Mkuu Care Giver

Mosi, Mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ana Haki zote za msingi za kurithi mali ya Baba yake. Kabla ya mwaka 2011 watoto wa nje ya ndoa hawakuwa na Haki ya kurithi mali za baba yao.

Lakini sheria ya mtoto mwaka 2019 mtoto wa nje ya NDOA ana haki zote za kurithi mali ya mzazi wake. Miaka ya nyuma kesi zilikuwa zikiamuliwa kwa kufata sheria za kimila kwamba watoto wa nje ya ndoa hawana haki ya kurithi mali.

1. Katiba ambayo inasema watu wote ni sawa.
2.sheria ya mtoto kifungu cha 5 ambacho kinakataza kubagua watoto
3.sheria ya mtoto kifungu cha 10 ambacho kinampa Haki ya ku-enjoy mali ya mzazi wake.
4.mikataba ya kimataifa kuhusu Haki za watoto ambazo Tanzania imeridhia.

Kiuhalisia katika sheria hakuna kitu kinaitwa “mtoto Haramu” sababu mtoto hapangi azaliwe wapi au asizaliwe wapi.
 
Mtoto analindwa kwa ushihidi ,hata watoto wako wewe ni kwa vile watu wana ushahidi na wewe umeonyesha kuwa ni wako .

Mtoto wa marehemu nje ya DNA, anaweza kuwatambulika kupitia wosia au hata kama ndugu wanamfahamu ...Ndugu wakijua au mtu baki akiwa na ushahidi ni mtoto au watoto wa fulani kwa damu anaweza kutetea maslahi ya mtoto huyo kama mzazi wake akifa.

Ila mwisho kama ni mali ,ndugu wana nguvu kugawa kama wakijua damu ya ndugu yao basi atapata mali na kulelewa.

Yote hakuna mtoto haramu ,wazazi ndio wamempata kwa njia ya haramu mtoto hana hata chembe ya kosa .
 
Kuongezeka kwa single mothers ni matokeo ya mmomonyoko wa maadili ya ndoa. Usomi umekuwa mwingi na wanawake wanataka uhuru wa kuishi peke yao bila mume ila kuzaa watoto wanataka
Mabinti wamefanya swala la ngono kama kitu cha kawaida tu wakati zamani unatongoza binti unafuatilia miezi sita mpaka mwaka mmoja bila kufanya dating kwa sasa ukigusa siku ya kwanza siku ya pili walete.
 
Mkuu Care Giver

Mosi, Mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ana Haki zote za msingi za kurithi mali ya Baba yake. Kabla ya mwaka 2011 watoto wa nje ya ndoa hawakuwa na Haki ya kurithi mali za baba yao.

Lakini sheria ya mtoto mwaka 2019 mtoto wa nje ya NDOA ana haki zote za kurithi mali ya mzazi wake. Miaka ya nyuma kesi zilikuwa zikiamuliwa kwa kufata sheria za kimila kwamba watoto wa nje ya ndoa hawana haki ya kurithi mali.

1. Katiba ambayo inasema watu wote ni sawa.
2.sheria ya mtoto kifungu cha 5 ambacho kinakataza kubagua watoto
3.sheria ya mtoto kifungu cha 10 ambacho kinampa Haki ya ku-enjoy mali ya mzazi wake.
4.mikataba ya kimataifa kuhusu Haki za watoto ambazo Tanzania imeridhia.

Kiuhalisia katika sheria hakuna kitu kinaitwa “mtoto Haramu” sababu mtoto hapangi azaliwe wapi au asizaliwe wapi.
Umefafanua vizuri kiongozi ingawa kuna vitu fulani inatakiwa kungatiwa ili mtoto huyo asipate shida sana katika kupata haki yake hapo baadaye
#Cha kwanza ni muhimu mtoto awe na cheti cha kuzaliwa ambacho kinaonyesha baba wa huyo mtoto ndiyo mwanaume
# issue ya pili ni muhimu at least hata ndugu 1 yeyote yule awe amewahi kujulishwa na mhusika kwamba huyo ni mtoto wake
#Kwa hiyo kama una mtoto na mwanaume na hamuishi naye make sure atleast unampeleka kwa wazazi au ndugu yeyote amujue au unaweza kumuomba baba mtu amtambulishe mtoto kwa ndugu zake hii ni security kubwa sana na inarahisisha sana mtoto kupata haki zake..
 
Mkuu Care Giver

Mosi, Mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ana Haki zote za msingi za kurithi mali ya Baba yake. Kabla ya mwaka 2011 watoto wa nje ya ndoa hawakuwa na Haki ya kurithi mali za baba yao.

Lakini sheria ya mtoto mwaka 2019 mtoto wa nje ya NDOA ana haki zote za kurithi mali ya mzazi wake. Miaka ya nyuma kesi zilikuwa zikiamuliwa kwa kufata sheria za kimila kwamba watoto wa nje ya ndoa hawana haki ya kurithi mali.

1. Katiba ambayo inasema watu wote ni sawa.
2.sheria ya mtoto kifungu cha 5 ambacho kinakataza kubagua watoto
3.sheria ya mtoto kifungu cha 10 ambacho kinampa Haki ya ku-enjoy mali ya mzazi wake.
4.mikataba ya kimataifa kuhusu Haki za watoto ambazo Tanzania imeridhia.

Kiuhalisia katika sheria hakuna kitu kinaitwa “mtoto Haramu” sababu mtoto hapangi azaliwe wapi au asizaliwe wapi.
vipi mirathi ikiendeshwa kwa sheria/ kanuni za kiisram!
Ambapo mtoto wa nje hatambuliki ,,,ni haramu!
 
Back
Top Bottom