Ikulu yatoa marekebisho kwenye majina ya wakurugenzi wa halmashauri walioteuliwa na rais

Kwani mmesahau yule mzee wa watu aliyejiandaa na suti yake mpaka Ikulu kuapishwa baadae akaambiwa "utupishe" jina lako limeletwa kimakosa!

Kuna kitu hakipo sawa upande wa kitengo cha habari na mawasiliano Ikulu.Na hii inatokana na siasa kuingilia taaluma,yaani mwandishi uliyekuwa nae bega kwa bega akakusifia kwenye kampeni za uraisi ndio unampa nafasi kusimamia kitengo muhimu kama hicho.

Tutafika tu!
 
Aliefanya hizo blunders bado yupo ofisini? Si bora Hata Anna Kilango arudishwe, nae alikosea kusoma orodha ya vibarua hewa
Binadamu Kama wewe ndio walipanga majina hayo kukosea sio dhambi
 
Mbona teuzi kila mara kuna makosa...!! Kabla ya kutangaza rudieni mara 3 au 4 hv, sio nzuri unatangaza kisha marekebisho hapo hapo..!! Relax...!!
 
Huenda Magufuli bado anaandika majina kwa mkono na kalamu kama alivyofanya kwa mawaziri. Huu utawala ndo kwanza miezi tisa! Tutafika kweli? Hataaa!!! Hatufiki hata kidogo!!
 
Kuna watu wanamhujumu Rais...hii ni hatari sana...Yaani majina ya walioteuliwa hayahakikiwi? Huu ni utendaji wa kazi wa ajabu...Najua sababu mojawapo ni kutaka kusiwepo na 'leak' kwa majina hayo,,,lakini mtu mwenye majina inabidi awe makini kabla hayajawasilishwa kutangazwa...
Mkuu nimewaza kama wewe kuna uhujumu with in.Lazima Raisi awe makini na watu wanaomzunguka.this is too much
 
Si unajua jamaa hawana database na wala hawafanyi proof reading. Wanasubiri muwashtue tena watoe PR nyingine. Hii nchi umaskini sio kwa bahati mbaya, huwezi kutudanganya kuwa hao watu wamefanyiwa VETTING, hakuna kitu kama hicho
Wametoa tamko eti wale makatibu tawala wamebadilishiwa kazi na sasa watatumikia kazi ya ukurugenzi. Sasa tija hapo iko wapi, mtu kaapishwa juzi kuwa katibu tawala, leo amebadilishiwa kazi kuwa mkurugenzi wa mji/halmashauri, etc. Huo uteuzi ni wazi unafanyika bila umakini wowote.
 
Kuna watu wanamhujumu Rais...hii ni hatari sana...Yaani majina ya walioteuliwa hayahakikiwi? Huu ni utendaji wa kazi wa ajabu...Najua sababu mojawapo ni kutaka kusiwepo na 'leak' kwa majina hayo,,,lakini mtu mwenye majina inabidi awe makini kabla hayajawasilishwa kutangazwa...
Hivi unaweza kumteua mtu bila kumhusisha kama yupo tayari kuchukua huo wadhifa??? Ina maana hii nchi ni ya kijeshi ambayo ni amri moja na amri ya mwisho??? Wewe utanipaje cheo na mimi sina hata uwezo nacho? Hawa watu kama ni siri na huyo mvujishaji anafanyaje kugeuza majina tena? Jibu ni kwamba Mapad hawajui hao na hajui walioteuliwa ila anaapisha tu otherwise angepitia na kujiridhisha kabla ya kuyatoa kwenye vyombo vya habari. Hii ni mara ya kwanza kwenye historia ya Tanzania kusikia kituko kama hiki tangu tupate uhuru. Hasa kwa sisi tuliokulia wakati wa uhuru na muungano na kunywea vikombe vya kijani vyenye picha ya mikono ya watu na mwenge.
 
Back
Top Bottom