Ikulu yatoa marekebisho kwenye majina ya wakurugenzi wa halmashauri walioteuliwa na rais

Hawa watendaji wameamua kumhujumu rais
Hiiwezekani kila uteuzi kuwe na makosa,hii ni aibu kuu kwa nchi na kashfa ya kutupwa
NASHAURI SASA WAHUSIKA WAWAJIBIKE HATA KWA KUTUOMBA MSAMAHA
 
Ni jambo linaloshangaza sana na maswali mengi juu ya umakini wa taasisi nyeti km hii
 
Jukwaa la siasa sio Gym ya pushup, haya sasa ndiyo matokeo, lile jasho lilitoka ndiyo harufu yake inatutesa.
 
Nakubaliana na wewe kwamba kwa hakika hiki ni kituko...Hata mimi nimeona awamu zote tano, na katika awamu nne zilizopita jambo kama hili halijawahi kutokea...yaani watu wanaitwa IKULU kuapishwa kiapo cha maadili kuwa Ma-DC halafu mtu mzima na mwenye akili na ambaye ni senior Ofisa wa Ikulu anatokea na kutangaza hadharani kwa walioitwa kwamba 'so and so utupishe wewe haumo ..utupishe...' kwa hakika hii ni mpya...nakuthibitishia kuwa niliposikia hivyo nililengwa na machozi kuona kuwa wapo wasaidizi wa Rais ambao wanamharibia Rais...Kwani kuwepo na kosa mpaka mtu ameitwa na amepita mpaka getini pale IKULU kumbe hayumo kwenye orodha...halafu hata namna ya kumwambia huyo 'mvamiaji' nalo ni jambo la kushangaza kabisa na ina-defeat procedures zote za uongozi na utawala makini...kama kuna kosa mtu huyo anaitwa pembeni kwa siri na kuambiwa na kuombwa radhi na bila watu wengine kugundua what is going on...sasa hata wiki haijaisha mwingine tena anateuliwa kuwa Mkuurugenzi wa Halmashauri lakini wakati huo tayari alikuwa ameshateuliwa kuwa DC...halafu taarifa inakuja kuwa yametokea makosa huyu aendelee na u-DC...blah blah na kadhalika...Ni ajabu na kweli...


Of course mtu unaweza kuteuliwa bila kuarifiwa lakini kunakuwa na umakini wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na vetting...Uongozi makini duniani kote kwa maana ya nchi zote duniani...mara nyingi kunakuwa na 'bank' ya viongozi ambapo majina fulani ya watu wa kada mbalimbali yanakuwa yapo mahali yanasubiri tu 'uteuzi'...wakati wa Mwalimu Nyerere nina uhakika ndivyo ilivyokuwa ikifanyika na hata wakati wa Mwinyi na hata wakati wa Mkapa...


Lakini inavyotokea sasa inaonekana watu 'wanatafutwa' tu kwa dharura, na wengine kujipendekeza na kufanya lobbying... Na ndiyo maana kwa upande wa ma-DAS wapo baadhi ya watu walioteuliwa ambao hawakuwa watumishi wa serikali kabisa na hawajui hata maana ya utumishi, uongozi na utawala...wako walioteuliwa kwa kuwa tu walikuwa au walishiriki kampeni au waligombea ubunge....lakini u-DAS ni cheo kizito ambapo kuna taratibu zake za uteuzi...wapo kwenye utumishi miaka mingi ndani ya serikali...lakini wanakuja kupachikiwa mtu ambaye hana ABC za utumishi na wala hana uzoefu...ni aibu..hii inawavunja moyo hata watumishi waliopo kazini...


Kwa hakika kwa baadhi yetu tunaofahamu namna mambo haya yanavyopaswa kuendeshwa na ambao angalau tumepiga umande kiasi chake tunapata shida mno katika kulielezea hili...Ifike wakati kwa kiwango Fulani kuwe na namna ya 'separation' kati ya politics na administration...Ukifanya kila kitu kuwa politics na kuwaondoa professionals kwenye administration ni hatari...Ni kweli mabadiliko yanahitajika nchini mwetu katika masuala ya uongozi au administration kutokana na kushamiri kwa 'bureaucracy' inayokwamisha mambo...yaani kunahitajika reforms ya nguvu katika administration au bureaucracy, lakini mabadiliko na reforms hizi siyo kama inavyotokea sasa kwa uteuzi wa baadhi ya ma-DAS...na reforms hizi siyo hizi za kuteua mtu vyeo viwili viwili na kutangaza majina na within few hours unakuja kutangaza tena kuwa tulikosea...HII NI AIBU...


Ni maoni yangu binafsi kuwa RAIS anahujumiwa, whether ni kwa bahati mbaya au kwa makusudi siyo rahisi kufahamu...Lakini watu hawa wanaomwaibisha Rais they should be taken to task...haiwezekani mambo kama haya yamezewe mate tu na kusema kuwa eti 'ni makosa ya kawaida'...hakuna kitu kama hicho...IKULU ni Ofisi nyeti ni lazima iwe mfano kwa utendaji mzuri...IKULU ni taasisi ni institution ni lazima iwe na watu makini...wamsaidie Rais kwa moyo mmoja na kwa utendaji mzuri usio na chepe ya ubabaishaji....
Big up mkuu, you made my day!!!! I wish people responsible will pass and read your comments. Nakumbuka jinsi tulivyokuwa tuna aina ya watu toka mahali fulani waliokuwa wanasemwa ni wafanyakazi wa serikali. Ukiwaangalia ni watu waliokuwa hawana interest na politics na walikuwa wanafanya kazi kwa weredi. Recently watu wamekuwa wakiteuliwa kwa kuwa na unasaba na chama tawala. Hivi ile system ya kuwapeleka viongozi kule Kigamboni kupata msasa wa uongozi uliishia wapi. Nakumbuka hata ma Headmistress/masters walikuwa wakienda huko.
 
W
Kazi ya urais siyo rahisi kama tunavyodhani. Makosa kama haya si kitu cha ajabu sana. Tuwe na tabia ya kupuuzia vitu vidogo kama hivi.
Ww ni muongo kwahiyo kwenye mikataba ambayo tayari umesaini utasema kuwa ofisi ya rais ni nn tayari umeliwa tukiri rais hayuko makini
 
W

Ww ni muongo kwahiyo kwenye mikataba ambayo tayari umesaini utasema kuwa ofisi ya rais ni nn tayari umeliwa tukiri rais hayuko makini
Ni wazi rais anajiona ni jeshi la mtu mmoja na haombi usaidizi kwa watu ambao wako pale kwa ajili hiyo. Hakuna mtu Wa kumuhujumu . Nani asiyependa kibarua chake!?
 
Kwa mwendo huu kuna hatari siku moja ikatolewa taarifa kwamba tangazo la vita lilitolewa kwa makosa! Ilikuwa vikosi vielekee mpaka wa Kusini lakini vikaelekea Kaskazini. Hivyo, masaa machache yaliyopita imetolewa amri ya kubatilisha agizo hilo na muda huu vimeonekana vielekea Kusini-Magharibi kwa kasi.
 
Kazi ya urais siyo rahisi kama tunavyodhani. Makosa kama haya si kitu cha ajabu sana. Tuwe na tabia ya kupuuzia vitu vidogo kama hivi.

Kilaza tumia basi hata akili kidogo ulizo baki nazo. Yaani mambo makubwa ya nchi kama hayo eti tupuuzie ni vitu vidogo. Hivi unadhani mbuyu ulianzia hapo tu ukiwa mkubwa au ulianza kama mchicha.
 
Yetu macho...
Yetu macho ....Big Show kwa kuwa ujumbe wako wa Eid... Bakwata hawakuufikisha kwa Mzee wa li nchi hii...naona umepigwa tena katika uteuzi huu chalii..vip ame balance au?.....kwani nasikia aliwa promise Bakwata na Watanzania wote kwamba yeye si wa hivyo...hana ubaguzi...sasa sijui uteuzi huu Big show umetendewa Haki au umetiwa Kabali tena...

Big show mwaka huu utaisoma namba....itabidi mwaka huu ukamfanyie kisomo bagamoyo....poleni sana
 
Back
Top Bottom