ngafu.fijo
JF-Expert Member
- Oct 3, 2015
- 1,237
- 1,099
Utajutaaa kuomba ushauri jf.....kuna wama huku ni noooma..
mumie huyu wala sio mwanaumemjinga sana .. wamekaa kimya as if hawapo .. kazi tunayo wadada kupata mwanaume anayejielewa ni sawa na kuokota almasi barabarani
Haaaahaaaaa.mie leo nachamba kwa niaba ya huyo dada.
anajitia uzuri wa kachumbari, kujitia napendwa, kuwekwa juu ya pilau, kumbe ya kwanza kuliwa.
hana lolote wala si chochote asubiri zamu yake ifike
and yet he is a manDah, Binadamu Bwana, kwahiyo hata shule ulikuaga hukomai sana kwakua unajua unasura nzuri???
Duh sasa mwanaume uwe na sura nzuri ili umvutie nani?Dah, Binadamu Bwana, kwahiyo hata shule ulikuaga hukomai sana kwakua unajua unasura nzuri???
Akome kabisa, anamvua dada wa watu kyupi mpaka sasa mtoto, halafu eti yeye mbaya lakini pesa zake tamu.Eh wakina dada punguzeni hasira mweeeee! Mmekuja km nyuki..kijana ukome kuomba ushauri wa vitu obvious
acha kashfa wee nan aliye kwambia kwamba huyo ndo mwenye sura mbaya kulikow wanawake wengine?Acha utoto ww hata mama Anna mkapa alikuwa 1st lady ujue
mdogo wake ampokee ..ukiona mwanaume unalishwa na kulelewa wee ni mita ya luku bila chanji umekwisha.
na asubiri sasa yeye kumbe ndo kaaza kuliwa hili.
bidada alishajionea mzigi ivi alikuwa anatafuta pa kutokea. akirudi leo atakutana na mafurushi yake apeleke kwa mama yake mzaz
mjinga sana .. wamekaa kimya as if hawapo .. kazi tunayo wadada kupata mwanaume anayejielewa ni sawa na kuokota almasi barabarani
naona hajawaeleza kinaga ubaga .. sasa awaeleze then aone kama atapata sapoti ya kumwacha dubwana
ni kichefu chefu hikiKwanza kanichefu pyeeeee
atuwekee hapa iyo sura yake anayoinadi kwamba ni nzuri tuione.Eh wakina dada punguzeni hasira mweeeee! Mmekuja km nyuki..kijana ukome kuomba ushauri wa vitu obvious
acha niseme tu jirani .. haya ni mambo ya aibu na fedheha khaaaaaJirani, Taratiibu jamani. Usiue inzi kwa gobole
ni kichefu chefu hiki
Wadau naomba niwasalimu
Kuna huyu dada tulisoma wote high school, hatukuwahi kuwa marafiki wala hatukua na ukaribu wowote, yy alikua msongo sana, ni yy na kitabu, kitabu na yy, hata hivyo hakua mzuri kama mabinti wengine, ndio maana wengi hatukuhangaika nae
Yy aliendelea na chuo, mm nilikwama sikupata principle pass za kuweza kuchaguliwa nikaazimia nitaunga unga unga hela ikipatikana
Almost 7 yrs later tukagongana mjini, akiwa kwenye usafiri wa nguvu, in short since that day akawa resi sana, mara tutoke usiku, mara movie, akawa anajitongozesha, tukawa wapenzi, mapenzi yaliponoga tukahamia kwenye nyumba yake aliyokua anajenga, tumekaa humo kwa miaka 2 na tuna mtoto sasa wa mwaka na nusu
Sasa analazimisha tuhalalishe uhusiano wetu kwa kufunga ndoa, kwa kweli amenitoa juu ya mawe hadi somewhere, nimekua mtu wa maana, yy yupo kazini, mm nasimamia biashara za kwake ambazo sasa ni kama zimekua za kwangu,
Shida ni kuwa kwa kweli alichukua sura ya baba yake, yaani huyu mtoto wetu kama isingekua ni mm sijui angefananaje, thank god alifanana na mm kila kitu, nyumbani kwetu pamoja na kuwa nimewafanyia mengi kwa hela za huyu dada lakini kuna minong`ono mingi sana, kwamba G alimtoa wapi huyu binti, hata marafiki zangu tukikaa sehem tukiondoka nyuma ni maneno hadi nakosa raha, nakua na avoid kutoka nae
Sasa hili la kufunga ndoa ndio bomb shell, nimekua nakwepa hoja hiyo kila mara, sasa kuna huyu mdogo wangu wa kike ni wa mwisho kwetu, amem recommend rafiki yake kipenzi kwangu, nimeshakaa kunywa nao mara kibao, ampapo sister kila mara ananishauri achana na hilo dubwana umuoe rafiki yangu katulia,
Sasa wadau mlikua mnasemaje? Maana huyu rafiki wa mdogo wangu ni mzuri hasa, amejazia, kifuani kumenyooka wima sidiria haiitajiki, halaf ana adabu sana, huniamkia shikamoo kila tukikutana hata tukiwa wawili tu, ila hatujafanya chochote zaidi ya kutoka out tu
Sasa sijui mlikua mnasemaje?
atakuwa anatumia kalio kufikiriSijui anafikiria kwa kutumia kichwa cha chini.
huyu ni fungu la kukosa.Utajutaaa kuomba ushauri jf.....kuna wama huku ni noooma..