#HISTORIA #YA #VITA #YA #KAGERA.

Majeshi ya uvamizi ya Nduli Iddi Amin yavunja daraja la Mto Kagera.

#Sehemu #ya - 4.

Jana tuliona jinsi majeshi ya Idi Amin wa Uganda yalivyoshambulia ardhi ya Tanzania na jinsi kiongozi huyo wa Uganda alivyokuwa akiiambia Dunia kuhusu mashambulizi hayo.

Kitendo hicho kilimuudhi sana Rais wa Tanzania wakati huo,Mwalimu Julius Nyerere ambaye aliamua kuitisha mkutano wa viongozi mkoani Dar es Salaam na kutoa ile hotuba maarufu ya “#sababu za kumpiga #tunazo, #nia ya kumpiga #tunayo na #uwezo wa kumpiga #tunao”.

Mwalimu Nyerere alielezea kwa kina jinsi Tanzania ilivyopuuzia madai ya Idi Amin hadi alipofanya uamuzi huo wa kujibu mashambulizi.

Sasa endelea................

Baada ya amri ya Rais Julius Nyerere aliyoitoa Jumatatu ya Oktoba 30, 1978 ya kutaka Jeshi la Wananchi (JWTZ) kuingia vitani, Brigedi ya Kusini ilipewa jukumu la kuanza kujibu mashambulizi.

Brigedi ya Kanda ya Kusini iliyokuwa na makao yake huko Songea,chini ya Brigedia James Luhanga, ilikuwa na wapiganaji kati ya 4,000 na 5,000 kwa mujibu wa gazeti The Citizen la Oktoba 14, 2014.

Halikuwa jambo la bahati mbaya kwamba brigedi hiyo kuwa tayari kwa vita.
“Brigade hii ilikuwa imeandaliwa ili baadaye iweze kutumwa nchini Namibia kujiunga na askari wa msituni wa Swapo,”linaandika gazeti hilo.

Brigedi hiyo ilianza safari Alhamisi ya Novemba 2, 1978, siku ambayo Mwalimu Nyerere alikuwa akilitangazia taifa kuhusu “uvamizi wa Idi Amin na uamuzi wa Tanzania kumpiga”.

Askari wa brigedi hiyo walilazimika kusafiri na zana zao za kivita kwa umbali wa kilometa 1,600 kutoka Songea hadi uwanja wa vita.

Baada ya safari hiyo ya tabu kubwa kutokana na mvua iliyokuwa inanyesha na barabara kuharibika vibaya, wanajeshi waliwasili na mara moja kuanza kuchimba mahandaki kwa ajili ya kujihifadhi kwa shambulizi lolote la anga ambao halikutarajiwa.

Mjini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine alitoa maelekezo kwa wakuu wote wa mikoa 20 ya Tanzania kuhamasisha matumizi ya mali za serikali na za watu binafsi kutumika katika vita.

Mabasi na malori kutoka serikalini na kwa kampuni binafsi yalitumika kupeleka wapiganaji na vifaa kwenye uwanja vya vita.Kwa watu waliokuwa na magari mabovu waliiona fursa hiyo kwa sababu magari yao yalifanyiwa matengenezo.

Ingawa yaliteka eneo la Kagera kwa urahisi, majeshi ya Idi Amin yalihofia sana Jeshi la Tanzania kujibu mapigo.

Waandishi wa kitabu cha "Deadly Developments" Stephen na Downs Reyna wameandika katika ukurasa wa 117 kuwa kwa kuhofia hilo, wanajeshi wa Uganda waliamua kulipua daraja la Mto Kagera eneo la Kyaka.

Toleo la 348 la jarida "New African" liliandika kuwa “huu ulikuwa mwanzo wa mwisho wa utawala wake (Idi Amin)” nchini Uganda.

Luteni Kanali Marajani wa Uganda alitumia ndege za MiG kulipua daraja hilo.Kazi hiyo ilifanyika Novemba 1 na 2, lakini walishindwa kuliharibu daraja hilo la Kagera.

Wanajeshi wa Tanzania walizirushia makombora na baadhi ya ndege hizo zilitunguliwa.Marubani waliobakia wakavunjika moyo wa kuendelea na kazi hiyo.

Baadaye Marajani akapata wazo la kutumia bomu la kutegwa.Akaenda machimbo ya shaba ya Kilembe,kiasi cha kilometa 225 kwenye milima ya Ruwenzori. Meneja wa machimbo hayo,ambaye alikuwa Mwingereza, alikubali na akatuma timu yake ya wataalamu kwenda kutega mabomu daraja la Mto Kagera.

Usiku wa Ijumaa ya Novemba 3, 1978, wategaji wa mabomu hayo walifika darajani na kufanya kazi hiyo bila kuonekana.Kabla ya kupambazuka daraja likawa limelipuliwa.Mmoja wa wanajeshi wa Uganda aliyekuwa na watega mabomu hayo ni Sajini Kifulugunyu.

Kifulugunyu aliliambia gazeti Daily Monitor la Uganda (Aprili 23, 2016) kwamba wataalamu hao wa mabomu walikuwa watatu, lakini utafiti wa gazeti hilo uligundua kuwa walikuwa wanne—Muitaliano mmoja na Waganda wanne.

Baada ya hapo, ilikuwa ni furaha tele.
“Tulifanya sherehe hapa hadi Kampala.Tuliridhika kuwa Jeshi la Tanzania halingeweza kutushambulia tena baada ya kuharibu daraja ambalo wangetumia kuvuka na kuingia Uganda,” Kifulugunyu aliliambia gazeti hilo.

Mmoja wa marubani waliotumika kujaribu kulilipua daraja hilo ni Meja John Amunga (maarufu kwa jina la Kassim Semugabi). Alikuwa mmoja wa marubani bora zaidi wa kijeshi wa Jeshi la Uganda, akiendesha ndege aina ya MiG-21. Wanajeshi wenzake walimbatiza jina la “Mharibifu wa Tanzania”.

Mwingine alikuwa ni John Carse kutoka Seychelles na ambaye alikuwa ni mtaalamu wa ubomoaji. Ndiye anayedaiwa kuwa alilipua daraja hilo.

Lakini, katika ukurasa wa 149-150 wa kitabu cha "Guardian Angel The Moshi Conspiracy" kilichoandikwa na Arnold Spero Bisase, kuna maelezo tofauti.

Aliyekuwa mfungwa wa Tanzania ambaye hakutaka jina lake litajwe, na ambaye wakati kitabu hicho kinaandikwa mwaka 2012 alikuwa anaishi nchi za Scandinavia, alimwambia mwandishi wa kitabu hicho kuwa aliwahi kuwa katika gereza moja na John Carse mkoani Dodoma ambako aligundua kuwa raia huyo wa Seychelles hakuhusika kulipua daraja hilo.

Siku daraja hilo lilipolipuliwa, JWTZ ilikumbana na kikwazo kingine.Ndege zake tatu zilikuwa zikitoka uwanja wa ndege wa Ngerengere mkoani Morogoro kuelekea Mwanza, zikapita juu ya Ziwa Victoria ambako askari wa JWTZ walishaambiwa wakae chonjo.

Kitengo cha Musoma hakikuwa na taarifa ya kuwasili kwa ndege hizo. Ndege zote tatu zililipuliwa kwa makombora na kuua marubani wake.

Akilitangazia Taifa tukio hilo, kwa masikitiko Mwalimu Julius Nyerere alisema: “Katika mambo ya vita ajali hutokea, na vijana hawa walikwishaambiwa ndege zikionekana zipigwe Wangeziacha?

Wanajuaje ni za adui? Kwa hiyo ikatokea bahati mbaya hiyo.
“Matukio haya hatukuyatangaza hata kule kupigwa kwa ndege za Amin hatukutangaza. Hatukutangaza kwa sababu hatukutaka jambo lenyewe kulipa uzito mno.Tulisema akiendelea endelea kuleta ndege zake, tutaendelea kuziangusha kila zinapokuja.”

Mara baada ya maneno hayo, alipanda ndege kwenda Beira, Msumbiji kukutana na Rais Samora Machel na kushauriana juu ya uvamizi wa Idi Amin.

Nyerere alimwambia Machel kuwa kikosi cha Jeshi la Tanzania kilichokuwa kwenye mpaka wa Msumbiji na Rhodesia (Zimbabwe) kilirudi Tanzania kwa ajili ya Vita ya Kagera.

Baada ya daraja mhimu la mto Kagera kulipuliwa na majeshi ya uvamizi ya Nduli Iddi Amini,unajua ni hatua gani Majeshi ya Tanzania yalifanya kuhakikisha yanavuka mto Kagera kwa ajili ya mapambano dhidi ya majeshi ya uvamizi!?

Itaendelea ...,
 
#HISTORIA #YA #VITA #YA #KAGERA.

Majeshi ya uvamizi ya Nduli Iddi Amin yavunja daraja la Mto Kagera.

#Sehemu #ya - 4.

Jana tuliona jinsi majeshi ya Idi Amin wa Uganda yalivyoshambulia ardhi ya Tanzania na jinsi kiongozi huyo wa Uganda alivyokuwa akiiambia Dunia kuhusu mashambulizi hayo.

Kitendo hicho kilimuudhi sana Rais wa Tanzania wakati huo,Mwalimu Julius Nyerere ambaye aliamua kuitisha mkutano wa viongozi mkoani Dar es Salaam na kutoa ile hotuba maarufu ya “#sababu za kumpiga #tunazo, #nia ya kumpiga #tunayo na #uwezo wa kumpiga #tunao”.

Mwalimu Nyerere alielezea kwa kina jinsi Tanzania ilivyopuuzia madai ya Idi Amin hadi alipofanya uamuzi huo wa kujibu mashambulizi.

Sasa endelea................

Baada ya amri ya Rais Julius Nyerere aliyoitoa Jumatatu ya Oktoba 30, 1978 ya kutaka Jeshi la Wananchi (JWTZ) kuingia vitani, Brigedi ya Kusini ilipewa jukumu la kuanza kujibu mashambulizi.

Brigedi ya Kanda ya Kusini iliyokuwa na makao yake huko Songea,chini ya Brigedia James Luhanga, ilikuwa na wapiganaji kati ya 4,000 na 5,000 kwa mujibu wa gazeti The Citizen la Oktoba 14, 2014.

Halikuwa jambo la bahati mbaya kwamba brigedi hiyo kuwa tayari kwa vita.
“Brigade hii ilikuwa imeandaliwa ili baadaye iweze kutumwa nchini Namibia kujiunga na askari wa msituni wa Swapo,”linaandika gazeti hilo.

Brigedi hiyo ilianza safari Alhamisi ya Novemba 2, 1978, siku ambayo Mwalimu Nyerere alikuwa akilitangazia taifa kuhusu “uvamizi wa Idi Amin na uamuzi wa Tanzania kumpiga”.

Askari wa brigedi hiyo walilazimika kusafiri na zana zao za kivita kwa umbali wa kilometa 1,600 kutoka Songea hadi uwanja wa vita.

Baada ya safari hiyo ya tabu kubwa kutokana na mvua iliyokuwa inanyesha na barabara kuharibika vibaya, wanajeshi waliwasili na mara moja kuanza kuchimba mahandaki kwa ajili ya kujihifadhi kwa shambulizi lolote la anga ambao halikutarajiwa.

Mjini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine alitoa maelekezo kwa wakuu wote wa mikoa 20 ya Tanzania kuhamasisha matumizi ya mali za serikali na za watu binafsi kutumika katika vita.

Mabasi na malori kutoka serikalini na kwa kampuni binafsi yalitumika kupeleka wapiganaji na vifaa kwenye uwanja vya vita.Kwa watu waliokuwa na magari mabovu waliiona fursa hiyo kwa sababu magari yao yalifanyiwa matengenezo.

Ingawa yaliteka eneo la Kagera kwa urahisi, majeshi ya Idi Amin yalihofia sana Jeshi la Tanzania kujibu mapigo.

Waandishi wa kitabu cha "Deadly Developments" Stephen na Downs Reyna wameandika katika ukurasa wa 117 kuwa kwa kuhofia hilo, wanajeshi wa Uganda waliamua kulipua daraja la Mto Kagera eneo la Kyaka.

Toleo la 348 la jarida "New African" liliandika kuwa “huu ulikuwa mwanzo wa mwisho wa utawala wake (Idi Amin)” nchini Uganda.

Luteni Kanali Marajani wa Uganda alitumia ndege za MiG kulipua daraja hilo.Kazi hiyo ilifanyika Novemba 1 na 2, lakini walishindwa kuliharibu daraja hilo la Kagera.

Wanajeshi wa Tanzania walizirushia makombora na baadhi ya ndege hizo zilitunguliwa.Marubani waliobakia wakavunjika moyo wa kuendelea na kazi hiyo.

Baadaye Marajani akapata wazo la kutumia bomu la kutegwa.Akaenda machimbo ya shaba ya Kilembe,kiasi cha kilometa 225 kwenye milima ya Ruwenzori. Meneja wa machimbo hayo,ambaye alikuwa Mwingereza, alikubali na akatuma timu yake ya wataalamu kwenda kutega mabomu daraja la Mto Kagera.

Usiku wa Ijumaa ya Novemba 3, 1978, wategaji wa mabomu hayo walifika darajani na kufanya kazi hiyo bila kuonekana.Kabla ya kupambazuka daraja likawa limelipuliwa.Mmoja wa wanajeshi wa Uganda aliyekuwa na watega mabomu hayo ni Sajini Kifulugunyu.

Kifulugunyu aliliambia gazeti Daily Monitor la Uganda (Aprili 23, 2016) kwamba wataalamu hao wa mabomu walikuwa watatu, lakini utafiti wa gazeti hilo uligundua kuwa walikuwa wanne—Muitaliano mmoja na Waganda wanne.

Baada ya hapo, ilikuwa ni furaha tele.
“Tulifanya sherehe hapa hadi Kampala.Tuliridhika kuwa Jeshi la Tanzania halingeweza kutushambulia tena baada ya kuharibu daraja ambalo wangetumia kuvuka na kuingia Uganda,” Kifulugunyu aliliambia gazeti hilo.

Mmoja wa marubani waliotumika kujaribu kulilipua daraja hilo ni Meja John Amunga (maarufu kwa jina la Kassim Semugabi). Alikuwa mmoja wa marubani bora zaidi wa kijeshi wa Jeshi la Uganda, akiendesha ndege aina ya MiG-21. Wanajeshi wenzake walimbatiza jina la “Mharibifu wa Tanzania”.

Mwingine alikuwa ni John Carse kutoka Seychelles na ambaye alikuwa ni mtaalamu wa ubomoaji. Ndiye anayedaiwa kuwa alilipua daraja hilo.

Lakini, katika ukurasa wa 149-150 wa kitabu cha "Guardian Angel The Moshi Conspiracy" kilichoandikwa na Arnold Spero Bisase, kuna maelezo tofauti.

Aliyekuwa mfungwa wa Tanzania ambaye hakutaka jina lake litajwe, na ambaye wakati kitabu hicho kinaandikwa mwaka 2012 alikuwa anaishi nchi za Scandinavia, alimwambia mwandishi wa kitabu hicho kuwa aliwahi kuwa katika gereza moja na John Carse mkoani Dodoma ambako aligundua kuwa raia huyo wa Seychelles hakuhusika kulipua daraja hilo.

Siku daraja hilo lilipolipuliwa, JWTZ ilikumbana na kikwazo kingine.Ndege zake tatu zilikuwa zikitoka uwanja wa ndege wa Ngerengere mkoani Morogoro kuelekea Mwanza, zikapita juu ya Ziwa Victoria ambako askari wa JWTZ walishaambiwa wakae chonjo.

Kitengo cha Musoma hakikuwa na taarifa ya kuwasili kwa ndege hizo. Ndege zote tatu zililipuliwa kwa makombora na kuua marubani wake.

Akilitangazia Taifa tukio hilo, kwa masikitiko Mwalimu Julius Nyerere alisema: “Katika mambo ya vita ajali hutokea, na vijana hawa walikwishaambiwa ndege zikionekana zipigwe Wangeziacha?

Wanajuaje ni za adui? Kwa hiyo ikatokea bahati mbaya hiyo.
“Matukio haya hatukuyatangaza hata kule kupigwa kwa ndege za Amin hatukutangaza. Hatukutangaza kwa sababu hatukutaka jambo lenyewe kulipa uzito mno.Tulisema akiendelea endelea kuleta ndege zake, tutaendelea kuziangusha kila zinapokuja.”

Mara baada ya maneno hayo, alipanda ndege kwenda Beira, Msumbiji kukutana na Rais Samora Machel na kushauriana juu ya uvamizi wa Idi Amin.

Nyerere alimwambia Machel kuwa kikosi cha Jeshi la Tanzania kilichokuwa kwenye mpaka wa Msumbiji na Rhodesia (Zimbabwe) kilirudi Tanzania kwa ajili ya Vita ya Kagera.

Baada ya daraja mhimu la mto Kagera kulipuliwa na majeshi ya uvamizi ya Nduli Iddi Amini,unajua ni hatua gani Majeshi ya Tanzania yalifanya kuhakikisha yanavuka mto Kagera kwa ajili ya mapambano dhidi ya majeshi ya uvamizi!?

Itaendelea ...,
Safi sana!

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
Nzuri ila iko tifauti kidogo na ile ya shuleni hasa kwenye chanzo cha vita,yaweza kuwa umeenda deep zaidi
 
#HISTORIA #NA #KUMBUKUMBU #YA #VITA #YA #KAGERA:

Nyerere na Samora Machel wa Msumbuji wakubaliana kumpiga Iddi Amin.

#Sehemu #ya - 5.

Jana tuliona jinsi majeshi ya Tanzania yalivyoanza safari ya kwenda mpakani kukabiliana na majeshi ya Nduli Iddi Amin wa Uganda.Uhamasishaji wa taasisi na watu wengine kutoa magari yao ili yasaidie kusomba wanajeshi na kitendo cha Rais Julius Nyerere kulitangazia taifa kuhusu uvamizi na uamuzi wa kupambana nao na baadaye kuchukua ndege kwenda Beira,Msumbiji.

Muda mfupi baada ya Rais Julius Nyerere kulitangazia Taifa jijini Dar es Salaam kuhusu uvamizi wa Idi Amin na uamuzi wa Tanzania kumpiga,Alhamisi ya Novemba 2, 1978, alipanda ndege kwenda Beira, Msumbiji kwenye mkutano na mwenyeji wake, Rais Samora Machel.

Ilikuwa aahirishe safari hiyo lakini alilazimika kwenda kwa sababu alikuwa mwenyekiti wa Nchi za Mstari wa Mbele (FLS) katika ukombozi wa Nchi zilizo kusini mwa bara la Afrika,ambazo nyingine ni pamoja na Angola, Botswana, Msumbiji, Tanzania, Zambia na Zimbabwe n.k.

Wakati huo pia kulikuwa na mgogoro wa mpaka kati ya Zambia na Zimbabwe (zamani Rhodesia) uliosababishwa na Rais Kenneth Kaunda wa Zambia.Nyerere ndiye aliyekuwa ameitisha mkutano wa kushughulikia mgogoro huo.

Kaunda alikuwa amefungua mpaka wake na Zimbabwe, jambo lililomkera sana Nyerere na Samora.

Nchini Rhodesia, mwanasiasa aliyeitwa Ndabaningi Sithole, ambaye ni mwanzilishi wa chama cha Zimbabwe African National Union (Zanu - PF) kabla ya kuangushwa na Robert Mugabe, alikuwa mshirika wa karibu sana wa Idi Amin.

Kwa hiyo kufunguliwa kwa mpaka huo kulimfadhaisha Mwalimu Nyerere, hasa wakati huo ambao tayari alikuwa na mgogoro na Uganda.Kwa namna fulani Rhodesia ilikuwa na uhusiano wa kijeshi na utawala wa Idi Amin wa Uganda.

Katika ukurasa wa 114 wa kitabu chake cha "For the Sake of Argument: Essays and Minority Reports" mwandishi Christopher Hitchens anasema wakati fulani “akiwa ofisini, (Sithole) aliomba msaada wa Idi Amin wa kuunda jeshi lake binafsi”.

Jumatatu ya Julai 17, 1978, ikiwa ni miezi minne kabla ya kuzuka kwa Vita vya Uganda, jarida la Facts and Reports (volume 8), katika habari iliyoandikwa na David Martin iliyokuwa na kichwa kilichosomeka “Sithole Guerrillas Fly to Amin for Training”, kulikuwa na tuhuma za uhusiano huo wa kijeshi.

“Dikteta Idi Amin ameshutumiwa vikali kwa kutoa mafunzo ya kijeshi kwa maelfu ya vijana wa washirika wa Ian Smith (wa Rhodesia) kwa madhumuni ya kuwatumia kuvuruga harakati za ukombozi nchini Zimbabwe,” aliandika mwandishi huyo.

Jarida jingine la International Bulletin (volume 4) la Julai 1978, lilizungumzia suala hilo.
“Mshirika mweusi wa Ian Smith, Mchungaji Ndabaningi Sithole anafundisha jeshi lake binafsi nchini Uganda,” liliandika jarida hilo. Pia jarida la "Africa Research Bulletin’ likaripoti kuwa “Mchungaji Ndabaningi Sithole amepokea idadi kubwa ya wapiganaji kutoka Uganda kwa Idi Amin pamoja na vifaa vya mafunzo”.

Zilikuwapo pia habari kwamba ndege za Rhodesia zilikuwa zikitua katika viwanja vya ndege vya Uganda—Entebbe na Nakosongola.

Habari hizo na nyinginezo za ushirika wa Idi Amin na Sithole,zikijumlishwa na ile ya Zambia kufungua mpaka wake na Rhodesia, zilimfanya Mwalimu Nyerere kwenda Beira, Msumbiji, kujadili jambo hilo haraka kadri ilivyowezekana.

Nyerere na Samora walikutana jioni ya Novemba 2, 1978 kujadili jambo hilo na kuridhika kuwa Iddi Amin alitumiwa na mataifa mengine kuivamia Tanzania kwa lengo la kumuondoa Nyerere katika harakati zake za ukombozi wa Zimbabwe dhidi ya akina Ian Smith na mshirika wake, Mchungaji Ndabaningi Sithole, na kwamba huenda Uingereza ilikuwa nyuma ya mpango huo.

Baadhi ya wanazuoni wanaamini kuwa halikuwa jambo la bahati mbaya kwamba vita vya Kagera kuzuka wakati huo muhimu wa mazungumzo kati ya vikosi vya ukombozi na serikali ya wachache ya Ian Smith nchini Zimbabwe.
Walisema wapinzani wa ukombozi walitaka kudhoofisha jitihada za Mwalimu Nyerere “kwa gharama zozote”.

Baada ya kutafakari yote hayo, Nyerere alimhakikishia Samora kwamba Tanzania ingeweza kupambana na Idi Amin bila kupoteza lengo lake la harakati za ukombozi wa Zimbabwe.

Walikubaliana kuwa kikosi cha jeshi la Tanzania kilichokuwa katika mpaka wa Msumbiji na Rhodesia kirejee Tanzania na, zaidi ya hilo, Samora naye akaahidi kutoa kikosi chake kuja kusaidiana na Tanzania.

Ndani ya siku chache, wanajeshi wa Msumbiji wakawa wamewasili Kagera tayari kwa mapigano.Hakuna chombo chochote cha habari cha Tanzania kilichoandika taarifa zozote za wapiganaji wa Msumbiji kuwasili Kagera.

Hata hivyo, kitabu cha War in Uganda cha Tony Avirgan na ‎Martha Honey kinasema “ushahidi mdogo sana kwamba wapiganaji wa Msumbiji walikuwa Tanzania ni nakala ya gazeti Noticias iliyoachwa kwenye ukumbi wa mapumziko wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza.”

Waandishi wa kitabu hicho, ambao walikuwa uwanja wa vita, wamesema mbali na wapiganaji hao 800 kutoka Msumbiji, hakukuwa na wapiganaji wengine kutoka taifa jingine lolote duniani waliokuwa wakipigana bega kwa bega na wapiganaji wa Tanzania dhidi ya majeshi ya Idi Amin.

Katika lile juma la pili la Novemba 1978, pamoja na magumu yote waliyokumbana nayo kama mvua, Tanzania iliweza kuwaandaa vyema wapiganaji wake.

Soma Zaidi: Idi Amin avunja daraja la Mto Kagera sehemu ya 4 ya makala zangu.

Juma hilo ndipo alipowasili Meja Jenerali Tumainieli Kiwelu kuongoza mapambano.Pamoja na kwamba Tanzania ilisikitishwa sana na kuvunjwa kwa daraja la Mto Kagera, ilipata nafasi ya kufanya maandalizi ya kutosha bila hofu ya kuvamiwa na majeshi ya Idi Amin ambayo yangeweza kulitumia daraja hilo kushambulia upande wa pili.

Baada ya makamanda wa vikosi mbalimbali vya wanajeshi wa jeshi la wananchi kuanza kuwasili kwa makundi uwanja wa vita,vifaa na zana mbalimbali za kivita kuwasili uwanja wa mapambano,nini kilifuatia!?

Fuatilia makala zangu hizi kila siku kuanzia majira ya saa moja usiku au saa mbili usiku,na kuendelea ili kupata ufahamu juu ya vita hii ambayo imebakia kuwa kumbukumbu kwa taifa letu.

Usikose mwendelezo wa udambwi udambwi huu sehemu ya 6 , 7 , 8 , 9 na kuendelea.

Itaendelea.....
 
#KUMBUKUMBU #NA #HISTORIA #YA #VITA #YA #KAGERA:*

JWTZ waingia Uganda kwa mashua.

#Sehemu #ya - 6.

Jana tuliona jinsi Rais wa Tanzania,Mwalimu Julius Nyerere na wa Msumbiji,Samora Machel walivyozungumzia kwa kina uvamizi wa majeshi ya Idi Amin Dada na hatari iliyokuwepo baada ya Rais wa Zambia,Kenneth Kaunda kufungua mpaka wake na Zimbabwe,wakati huo ikiitwa Rhodesia.

Kimsingi,Nyerere na Samora walikubaliana kupambana na majeshi ya Uganda na namna watakavyotumia vikosi vyao.Makala iliishia wakati Meja Jenerali Tumainieli Kiwelu alipofika uwanja wa mapambano tayari kwa vita.

Sasa endelea......

Usiku wa Jumanne ya kuamkia Novemba 15, 1978, kikosi cha kwanza cha askari wa Tanzania,kikiwa chini ya Luteni Kanali Benjamin Noah Msuya, kilivuka Mto Kagera kwa mashua ndogo na kuingia ng’ambo ya pili.

Hadi kufikia wakati huo (wa kuvuka mto),zaidi ya Watanzania 1,000 walikuwa wameuawa na majeshi ya Nduli IddiAmin Dadaa.
Alisema Msuya katika mahojiano na gazeti The Monitor la Uganda la Jumamosi ya Mei 3, 2014 nyumbani kwake Kunduchi, Dar es Salaam.

Msuya aliongoza Bataliani ya 19 ya JWTZ iliyokuwa chini ya Brigedi ya 208 iliyoongozwa na Brigedia Jenerali Mwita Marwa.Kazi yake ilikuwa ni kuivamia na kuitwaa Kampala,lengo ambalo hatimaye lilifikiwa Jumanne ya Aprili 10, 1979.

Baada ya kufanikiwa, Luteni Kanali Msuya akaitawala Kampala kama meya wake na pia kama rais wa Uganda kwa siku tatu hadi nchi hiyo ilipompata Yusuf Kironde Lule kuwa rais.

Alfajiri ya Jumapili ya Novemba 19,Luteni Kanali Msuya alituma kikosi kingine cha askari kwenda ng’ambo ya Mto Kagera,kikitumia mashua nyingine ndogo.
Huko walishangazwa sana kuona uporaji na mauaji yaliyofanywa na askari wa Idi Amin.

Miili ya Watanzania waliouawa na majeshi ya uvamizi ilikuwa imeshaanza kuoza.Kikosi hicho kiligundua kuwa miili mingine ilikuwa imekatwa viungo,ishara kwamba wengi wao waliteswa kabla ya kuuawa.

Serikali ya Tanzania ilisema kiasi cha wakazi 40,000 walivuka Mto Kagera kukimbia majeshi ya Uganda, wakiacha kiasi cha raia kati ya 5,000 na 10,000 wakihofiwa kuuawa.

Miongoni mwao,kwa mujibu wa gazeti la Serikali la Daily News,walikuwako Watanzania 485 waliopelekwa gereza la Mutukula upande wa Uganda,ambako waliuawa kwa kulipuliwa kwa baruti.

Habari iliyoandikwa na John Darntonnov kwenye gazeti "The New York Times" la Alhamisi ya Novemba 23, 1978 inasema katika maeneo yaliyovamiwa na majeshi ya Idi Amin,hasa ya biashara, “kitu pekee chenye uhai kilichoonekana (baada ya uvamizi) ni mbwa mweusi aliyekonda” baada ya raia Watanzania wengi kuyakimbia majeshi ya Idi Amin.

Maduka yote, kwa mujibu wa gazeti la "The New York Times", yaliporwa.
“Katika duka moja lililoporwa,kilichokuwa kimesalia dukani hapo ni picha ya harusi ya mmiliki wa duka,Zaharan Salum na bibi harusi wake,ambayo ilikuwa inaning’inia ukutani,” liliandika gazeti hilo.

Kati ya ng’ombe 12,000 waliokuwa ranchi ya Narco, ni ng’ombe 100 tu walisalia baada ya wengine kuporwa. Wamiliki wa ranchi hiyo, ambao ni raia wa Australia, hawakuonekana baada ya uporaji huo na ilihofiwa kuwa nao waliuawa.

Kiwanda ha sukari cha Kagera na shamba la miwa viliteketezwa kwa kulipuliwa na mizinga na mabomu ya wavamizi

Doria ya Luteni Kanali Msuya ilifika hadi mpakani mwa Uganda Jumatano ya Novemba 22,na kwa wakati wote huo askari wa Amin hawakuonekana.Lakini doria hiyo ilipofika eneo la Minziro,iliona kiasi cha askari 30 wa Amin na vifaru viwili vikiwa eneo la kanisa.

Askari hao wa doria hawakufanya shambulio lolote bali walirudi hadi Kyaka.
Ijumaa ya Novemba 24, vikosi kadhaa vya JWTZ, vikiongozwa na mabrigedia watatu; James Luhanga, Mwita Chacha Marwa na Silas Mayunga vikawa vimetanda kuzingira maeneo yaliyotekwa.

Siku hiyo hiyo daraja la dharura la Mto Kagera likaanza kujengwa kwa ajili ya kuvusha vifaru na zana nyingine za kivita.Kazi hiyo ilikamilika na siku iliyofuata na zana za kivita zikaanza kuvushwa kwenda ng'ambo ya pili ya mto Kagera.

Wakati daraja la dharura likijengwa, Rais Nyerere alizuru eneo hilo.Ingawa awali makamanda wa JWTZ walitaka kumzuia.

Akiwa uwanja wa vita, alitumia darubini kutazama wapiganaji wa Amin wakiwa vilimani,umbali wa kilometa kumi kutoka mpakani,tayari kuishambulia Tanzania.

Ziara hiyo ya Nyerere ilimshawishi kukubaliana na makamanda wa JWTZ kuwa eneo la Kagera haliko salama na kwamba ili usalama uwepo,ilikuwa ni lazima jeshi la Tanzania livuke mpaka.

Usiku wa Jumapili ya Novemba 21, 1971 askari wa Tanzania walivuka mpaka na kuingia Uganda. Kikosi cha kwanza kilisaidiwa na vifaru na kiliongozwa na Luteni Kanali Salim Hassan Boma.

Vikosi kadhaa vilijizatiti maeneo ya misitu kuzunguka mji wa Mutukula.Kabla ya kupambazuka,kikosi kimojawapo kilichoongozwa na Luteni Kanali Salim Hassan Boma, kikisaidiwa na vifaru, kilitembea katika barabara kuu ya kuelekea Mutukula.Hii ilikuwa ni mbinu ya kuwavuta adui na ilifanikiwa.

Wakati majeshi ya Idi Amin yakifuatilia nyendo za kikosi cha Luteni Kanali Boma kilichokuwa mbele yao, yalishtukiwa yakishambuliwa na kikosi kingine cha JWTZ kutoka nyuma yao.

Kwa jinsi askari wa Idi Amin walivyopagawa, walilazimika kukimbia na kutelekeza silaha zao.
Kwa njia hiyo JWTZ ikajipatia silaha mbalimbali kuanzia vifaru hadi bunduki za kawaida.Katika mapambano hayo, kikosi cha Luteni Kanali Boma kilipoteza wanajeshi watatu na wengine kadhaa kujeruhiwa.Hata hivyo,bila ujasiri huo ilikuwa ni vigumu kuvunja ngome ya jeshi la Uganda katika vilima vya eneo hilo.

Kwenye mapigano ya Mutukula,idadi kubwa ya raia waliuawa.
“Kila kitu kiliharibiwa na kila kilichokuwa na uhai kiliuawa,” imeandikwa katika kitabu cha "War in Uganda."

“Mabuldoza yalifukia nyumba zote za udongo. Vikongwe ambao hawakuweza kukimbia waliuawa kwa kupigwa risasi. Kufikia mchana (Jumatano ya Novemba 22, 1978) Mutukula haikuwapo tena isipokuwa kwenye ramani.”

Jeshi la Tanzania “lilianza kulipiza kisasi kwa namna isiyotofautiana na ile ya Idi Amin” wakati akiteka eneo la Kagera.
Habari za ushindi wa kuitwaa Kagera zilimfariji Mwalimu Nyerere, lakini inasemekana, hakufurahishwa na habari za mauaji yaliyofanywa na jeshi lake.

Baadaye Nyerere alitoa amri ya maandishi kwa jeshi lake litofautishe jeshi na raia na mali zao. Vyovyote iwavyo, ushindi wa kwanza ukawa umepatikana kwa kuikomboa Mutukula na sasa eneo lote lililotekwa na majeshi ya Idd Amin Dadaa kutoka mpaka wa Mutukula hadi mto Kagera ilikombolewa na majeshi yetu

Siku JWTZ ilipovuka mpaka, Serikali ya Uganda ilitangaza kuwa wanajeshi zaidi ya 1,000 wa Tanzania wameingia maili 100 ndani ya Uganda na kuteka miji mitatu ya Kyotera, Kakuto na Kalisizo.

Baada ya majeshi yetu kulikombea eneo lote lililotekwa na majeshi ya uvamizi,nini hatua zaidi na kipi kiliamuriwa na Ameir jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama wakati huo,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere!?

Endelea kufuatilia ......
 
#KUMBUKUMBU #NA #HISTORIA #YA #VITA #YA #KAGERA:

Mwalimu Nyerere ahamasisha wapiganaji.

#Sehemu #ya - 7.

Jana tuliona habari za ushindi wa kwanza wa wapiganaji wetu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania dhidi ya majeshi ya wavamizi wa Nduli Iddi Amin Dadaa,kwa kuitwaa Kagera zilivyomfariji Mwalimu Nyerere,lakini inasemekana hakufurahishwa na habari za mauaji yaliyofanywa na jeshi lake.
Baadaye Nyerere alitoa amri ya maandishi kwa jeshi lake litofautishe jeshi na raia na mali zao.Vyovyote iwavyo,ushindi wa kwanza ukawa umepatikana kwa kuikomboa Mutukula.

Siku JWTZ ilipovuka mpaka, Serikali ya Uganda ilitangaza kuwa wanajeshi zaidi ya 1,000 wa Tanzania wameingia maili 100 ndani ya Uganda na kuteka miji mitatu ya Kyotera, Kakuto na Kalisizo.

Miezi miwili ya mwanzo wa vita ilikuwa ni ya kuongeza idadi ya wanajeshi jeshini.Katika lile juma la kwanza vikundi vya wanamgambo vilianza kufanya mazoezi baada ya saa za kazi.

Miongoni mwa wanamgambo hawa walikuwamo wakulima wadogo na wale ambao hawakuwa na ajira.Jeshi la Polisi lilichangia askari wake kiasi cha 2,000.

Juma moja baada ya uvamizi wa Uganda wakuu wa mikoa yote 20 ya Tanzania walikutana mjini Dodoma kujadiliana kuhusu uandikishaji wa wapiganaji.

Kila mkoa ulipewa idadi ya kikomo cha wapiganaji 2,000 na wakuu hao walipewa maelekezo ya kuwapokea wale tu ambao walikuwa wamehitimu mafunzo ya mgambo.

Pamoja na hayo,mkuu wa Mkoa wa Mara alipotangaza mkoani mwake kuwa yeyote ambaye anataka kujiunga na jeshi ajitokeze,wananchi wengi walimiminika kwenye vituo vya kuandikishwa.

Vituo vya kijeshi mkoani Mara vilielemewa na idadi kubwa ya waombaji,mwishowe Rais Nyerere alikwenda mwenyewe mkoani humo kulikabili tatizo hilo.

Hatimaye mkoa huo ulikubaliwa kuandikisha wapiganaji 4,000 badala ya 2,000 wa kikomo waliokubaliwa awali, ilimradi tu hawakuwa na tatizo la akili,wana elimu ya angalau darasa la saba na ni wanachama wa CCM.

Kwa kutumia utaratibu huo wanamgambo 40,000 waliingizwa jeshini na kufanya idadi ya wapiganaji kufikia 75,000 na zaidi.

Hatimaye wapiganaji 45,000 wa Tanzania wakaingia Uganda.

Ingawa wanamgambo wanawake nao walipata mafunzo ya kijeshi sawasawa na wale wa wanaume, hakuna mgambo mwanamke aliyeingia jeshini kupigana vita isipokuwa tu wale waliotumika kama wauguzi.

Mara baada ya uvamizi wa Kagera, Tanzania ilianza kuwahamasisha Waganda waliompinga Idi Amin kupigana dhidi ya Idi Amin.

Kufikia hatua hii,mkataba wa Mogadishu ambao ulilitaka jeshi letu kukaa umbali wa kilomita 16 au zaidi kutoka kwenye mpaka wa Uganda ukawa umekufa rasmi.

Mkataba huo ulioitwa ‘Mazungumzo ya Mogadishu’ uliafikiwa nchini Somalia Alhamisi ya Oktoba 5, 1972. Ulikuwa ni sehemu ya usuluhishi wa mgogoro kati ya Tanzania na Uganda.

Somalia iliepusha vita kati ya Tanzania na Uganda kwa miaka sita tangu 1972 hadi ilipokuja kuzuka baadaye mwaka 1978 na sasa, wakati vita inaendelea, ukawa hauna kazi tena.

Walioshiriki katika mazungumzo hayo ni mawaziri wa mambo ya nje ambao ni John Samuel Malecela (Tanzania), Joshua Wanume Kibedi (Uganda) na Umar Arteh Ghalib au Omer Carte Qalib (Somalia). Mwingine aliyeshiriki ni Katibu Mkuu wa OAU, Nzo Ekangaki.

Kufikia hatua hii Rais Nyerere alisema waziwazi kuwa anaunga mkono wanaompinga Idi Amin na kwamba angetoa mafunzo,silaha na fedha kwa Waganda wowote ambao wangekuwa tayari kwenda Uganda kumpiga Iddi Amin.

Wito huo uliitikiwa na makundi mbalimbali na wengine walikuwa wanaishi nchini Tanzania, Kenya, Zambia,nchi za Ulaya na Amerika pamoja na Waganda waliokuwa ndani ya Uganda kwenyewe.

Baadhi ya hawa hawakuwa wapiganaji wengine walikuwa wafanyabiashara, walimu au waandishi wa habari.Kwa hiyo hawakuwahi kubeba silaha wakati wowote.

Sehemu kubwa ya hawa ilitokea Tanzania, hususan kwenye kambi ya wakimbizi ya Tabora.
Wengi wao walikuwa katika jeshi la Obote,lakini tangu waliposhindwa katika jaribio lao la mwaka 1972 la kumwangusha Idi Amin hawakuendelea tena kupata mafunzo ya kijeshi.

Baadhi ya wengine hawangeweza tena kuingia kwenye mapambano ya kivita kwa sababu ya uzee.
Hata hivyo, siku chache baada ya uvamizi wa Iddi Amin,Obote ambaye alikuwa amekwenda Zambia, alirejea Tanzania haraka na kuanza kuwakusanya makomandoo wa kijeshi kutoka Dar es Salaam na kwingineko.

Wanajeshi wote wa zamani wa Uganda walitakiwa kukutana Tabora kwa mkakati maalumu dhidi ya Idi Amin.Ndani ya wiki moja tu ya wito huo wakakutana 800 chini ya Kanali Tito Okello, ambaye ndiye alikuwa kamanda wa lile jaribio la mapinduzi la mwaka 1972.

Kufikia katikati ya Novemba 1978 kiasi cha wapiganaji 300 miongoni mwao wakawa wamepewa sare za kijeshi na kupelekwa Mwanza ambako walikutana na wenzao wengine ili wapelekwe vitani Uganda.

Mwalimu Nyerere alitaka kikosi cha Waganda hao kiende vitani haraka iwezekanavyo, lakini Obote akapinga akidai kikosi chake cha Tabora kimegawanyika na kilihitaji muda kuwekwa sawa. Lakini wengine walisema Obote alihisi kikosi hicho kinamtii zaidi Kanali Okello kuliko yeye.

Okello na wapiganaji wengi walikuwa wa kabila la Acholi na ingawa wakati mmoja Obote alidai kuwa watu hao wa Tabora walikuwa watiifu kwake, wakimbizi wengi wa kabila la Acholi waliona kuwa Obote aliwapuuza wakati wa utawala wake kabla ya kupinduliwa na Idi Amin mwaka 1971.

Wengi wao walikuwa wakidai kuwa wakati Obote akiwa madarakani aliwapendelea watu wa kabila lake la Langi kwa kuwapa ajira na fursa nyingine ambazo wao walinyimwa.
Hata hivyo Nyerere alimsikiliza sana Obote na hivyo aliamuru wapiganaji 300 waliokuwa wameshawasili Mwanza warudi Tabora ambako Obote na Okello wangekubaliana kuwa hao wawe kwenye Batalioni moja.

Kwa mujibu wa kitabu cha "War in Uganda" Tanzania iliwapatia silaha na makamanda wa Uganda wakaanza kutoa mafunzo mara moja.
Wakati huohuo, Nyerere alianzisha kambi ya mafunzo ya Uganda huko Tarime karibu na Musoma. Ilikuwa na uwezo wa kutoa mafunzo kwa wapiganaji 1,200. Nyerere aliwataka Waganda wengine, akiwamo Robert Serumaga na Roger Makasa.

Wengine ni Andrew Adimola wa chama cha Ugandan Redemption and Reconciliation Union. Robert Bellarmino Serumaga ambaye alikuwa mwandishi, aliukimbia utawala wa Idi Amin mwaka 1977. Adimola alikuwa waziri kabla hajakimbia. Mwingine ni Aleker Ejalu.

Nyerere aliwasihi wote hawa wahamasishe wapiganaji.

Baada ya kuona namna makambi mbalimbali ya mafunzo yakianzishwa kwa ajili ya kuongeza nguvu kwa mashujaa wetu waliokuwa tayari mstari wa mbele kuhakikisha Nduli Iddi Amini anashikishwa adabu,endelea kufuatilia kujua nini kitaendelea baada ya Ameir jeshi mkuu wa wakati wa majeshi yetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,kuamuru majeshi yetu kusonga mbele mpaka Kampala
 
#HISTORIA #NA #KUMBUKUMBU #YA #VITA #YA #KAGERA:

Nyerere ahaha kutafuta marafiki na silaha.

#Sehemu #ya - 8

Jana tuliona Mwalimu Nyerere alivyoanzisha kambi za mafunzo ya kijeshi kwa Waganda huko Tarime mkoani Mara.Kambi ile likuwa na uwezo wa kutoa mafunzo kwa wapiganaji 1,200,pia aliwataka Waganda wengine wakiwemo Robert Serumaga,Roger Makasa na Andrew Adimola wa chama cha Ugandan Redemption and Reconciliation Union.

Serumaga ambaye alikuwa mwandishi aliukimbia utawala wa Idi Amin mwaka 1977.Adimola alikuwa waziri kabla hajakimbia, mwingine ni Aleker Ejalu.

Nyerere aliwasihi wote hawa wahamasishe wapiganaji.

Sasa endelea........

Hadi ilipofika Krismasi mwaka 1978,zaidi ya wafuasi 50 wa watu hawa wakawa wamewasili.Wiki chache baadaye wakawasili wengine zaidi ya 100 tayari kwa mafunzo.
Januari 1979 Serumaga na Ejalu walimwambia Nyerere kuwa katika miji ya Kampala na Jinja kuna maelfu ya wanajeshi wanaompinga Idi Amin na kwamba wakipata msaada kidogo tu wataasi.

Nyerere alikubaliana nao,akaruhusu Waganda 200 wapelekwe Uganda kwa kazi hiyo,50 kwa ajili ya Serumaga na Ejalu na 150 kwa ajili ya Tito Okello. Lakini walipokaribia ufukwe wa Ziwa Victoria upande wa Uganda baadhi ya mashua zao zilizama,baadhi walifanikiwa kurejea Mwanza.

Muda mfupi baadaye Ejalu na Serumaga wakatuma mashua za doria ziwani,lakini walipowasili karibu na mji wa Jinja wote walikamatwa na kuuawa.
Baada ya matukio haya,kambi ya mafunzo ya Tarime ikafungwa rasmi.

Kwa upande wa uchumi wa nchi, bidhaa zilianza kupaa bei.Hii ilitokana na kuongezeka kwa kodi ili kulipia mahitaji ya vita.Novemba 15, 1978, jarida la Africa Contemporary Record 1978-1979 lilimnukuu Waziri wa Fedha wa Tanzania, Edwin Mtei akitangaza kuwa vita vimeifanya Serikali kuongeza kodi kwa bidhaa za walaji.

Vita ilipoanza kupamba moto,Tanzania ilianza kuwatafuta marafiki na washirika wake,lakini ikaonekana kusingekuwa na msaada mkubwa kutoka kwao.Rafiki wa kwanza ambaye Tanzania ilimwona alikuwa ni Jamhuri ya Watu wa China (RPC).

Kwa mujibu wa kitabu cha "Routledge Handbook of Chinese Security" kilichohaririwa na Lowell Dittmer na Maochun Yu, mwaka 1963 kiongozi wa China, Mao Zedong alianzisha falsafa mpya ya kimkakati aliyoiita “mapinduzi ya dunia”.

Nadharia yake akaiita “Two Middle Areas” (liangge zhongjian didai) ambayo aliamini kuwa katikati ya mataifa mawili makubwa Marekani na Urusi kulikuwa na maeneo mawili makubwa katikati yake. Eneo la kwanza lilikuwa ni baadhi ya nchi za bara la Asia,Afrika na Amerika ya Kilatini ambazo ama zilikuwa tayari zimejipatia uhuru au zilikuwa katika harakati ya kujipatia uhuru.

Kwa kufuata falsafa hiyo, mwaka 1964 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Zhou Enlai aliitembelea Tanzania. China ilitoa misaada na mafunzo ya kijeshi.Hadi mwishoni mwa 1978, wakati Vita vya Kagera ilipoanza na kupamba moto, Tanzania ilikuwa imeshapokea misaada na zana mbalimbali za kivita kutoka China.

Katika ukurasa wa 42 wa kitabu hicho, waandishi Dittmer na Maochun Yu wanaandika kuwa katika bara la Afrika, nchi ambayo Mao aliipa ‘kipaumbele cha juu’ ni Tanzania,na kuanzia mwaka 1964 Tanzania ilipewa msaada wa silaha mbalimbali vikiwamo vifaru, ndege vita na mfumo kamili wa usalama.

Kitabu cha China into Africa: Trade, Aid, and Influence kilichohaririwa na Robert I. Rotberg (chapa ya mwaka 2008) katika ukurasa wake wa 159 kinasema “...Zana za kivita kutoka China kwenda Afrika tangu 1966 hadi 1977 ilikuwa ni pamoja na boti za doria, vifaru na ndege za kivita aina ya MiG-17, MiG-19 na MiG-21 kwa ajili ya Tanzania.

Katika ukurasa wa 110 wa kitabu chake, Arms for Africa: Military Assistance and Foreign Policy in the Developing World, mwandishi Bruce Arlinghaus ameandika “China ilitoa (kwa Tanzania) asilimia 60 ya mahitaji yote ya kijeshi.

Pamoja na historia yote hiyo ya urafiki kati ya Tanzania na China tangu 1964 hadi 1978, Tanzania ilipoiendea kwa ajili ya msaada wa zana za kivita za kupambana na Idi Amin,Jamhuri ya Watu wa China iliiambia Tanzania kuwa haitajihusisha kwa namna yoyote na mgogoro kati ya Tanzania na Uganda.
Zaidi ya hilo,
China iliishauri Tanzania ikae mezani na Uganda kumaliza mgogoro huo.

Kilichofanywa na Serikali ya China ni kuwasilisha tu zana za vita zilizokuwa zimenunuliwa kabla vita haijazuka lakini hakuna silaha za ziada ambazo China ilitoa hata vipuri. Jeshi la Wananchi wa Tanzania likaanza kutegemea vipuri kama betri za vifaru kutokana na silaha walizoteka kwa majeshi ya Idi Amin.

Kwa upande wa Uganda, zana za kijeshi ambazo ilikuwa ikizipata kutoka Urusi hazikuendelea tena kutolewa.Kufikia katikati ya mwaka 1978 Serikali ya Idi Amin ilikuwa inazidi kutengwa.

“Kati ya 1975 na 1978 Uganda ilipata zana za kivita kutoka Urusi, Libya, Iraq, Uswisi na Libya,” kinasema kitabu cha Arms and Warfare: Escalation, De- escalation and Negotiation (chapa ya 1994) cha Michael Brzoska na Frederic Pearson.

Jumatatu ya Novemba 10, 1975 Idi Amin alitishia kuvunja uhusiano na Urusi ndani ya saa 48 ikiwa hangepata alichokitaka kutoka kwao. Alitishia pia kuwa angemfukuza nchini mwake balozi wa Urusi, Andrei Zakharov.

Aliilaumu Urusi kwa kuingilia mambo yake ya ndani. Pia aliilaumu kwa kumnyima vipuri kwa ajili ya ndege zake za kijeshi aina ya MiG-17 na MiG-21.
“Novemba 11, 1975 Idi Amin akatangaza kuwa Urusi imlete balozi wake mwingine ambaye ‘hana ubeberu’ kama aliyekuwapo,” kinaandika kitabu cha Who Influenced Whom: Lessons from the Cold War cha Dale Tatum.
Katika matangazo ya Redio Uganda, Idi Amin alisikika akifoka, “Mimi si kibaraka na sishurutishwi na yeyote.”

Mara baada ya hapo, kinaandika kitabu hicho, “Urusi waliamua kuvunja uhusiano na Uganda, lakini cha kushangaza Urusi iliurejesha uhusiano huo siku nne baadaye Novemba 15, 1978.”

Huu ni ule wakati ambao Idi Amin alikuwa mwenyekiti wa Nchi Huru za Afrika (OAU).
Uganda ilipovamiwa na makomandoo wa Israel katika kile killichoitwa ‘Operation Entebbe’ au kama ilivyojulikana kwa wengine, ‘Operation Thunderbolt’, Jumapili ya Julai 4, 1976 na ndege zake za kijeshi kuharibiwa vibaya, Urusi iliahidi kuimarisha kikosi cha anga cha Jeshi la Uganda na kuwapa ndege nyingine za kivita.

Kwa ahadi hiyo uhusiano kati ya Uganda na Urusi ukaanza kuimarika tena. Marubani wa ndege za jeshi za Uganda walipelekwa mafunzoni Urusi.

Itaendelea............
 
#HISTORIA #NA #KUMBUKUMBU #YA #VITA #YA #KAGERA :

Nyerere aipuuza OAU,aamuru jeshi liingie Uganda.

#Sehemu #ya - 9

Sehemu iliyopita tumeona namna Uganda ilivyovamiwa na makomandoo wa Israel katika kile killichoitwa ‘Operation Entebbe’ au kama ilivyojulikana kwa wengine, ‘Operation Thunderbolt’, Jumapili ya Julai 4, 1976 na ndege zake za kijeshi kuharibiwa vibaya, Urusi iliahidi kuimarisha kikosi cha anga cha jeshi la nchi hiyo na kuwapa ndege nyingine za kivita.

Kwa ahadi hiyo uhusiano kati ya Uganda na Urusi ukaanza kuimarika tena.Marubani wa ndege za jeshi za Uganda walipelekwa mafunzoni Urusi.
Miongoni mwa hao ni Luteni David Omita,Luteni Atiku na Luteni Abusala ambao baadaye walikuja kuwa marubani wa kwanza kuishambulia Tanzania kwa ndege za kivita.

Pamoja na uhusiano huo kati ya Uganda na Urusi, wote hawa Urusi na nchi nyingine za Ulaya Mashariki walisema wako tayari kuendelea kuipa Uganda silaha na zana zingine za kijeshi,lakini sharti lilikuwa ni kulipa kwa fedha taslimu na si kwa mkopo.

Uingereza na Ujerumani Magharibi kwa upande wa Tanzania zilitoa msaada katika vita hiyo kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwa kutoa mamilioni ya dola kusaidia wakimbizi wa Kagera.

Kwa hiyo fedha ya Tanzania iliyokuwa itumike kwa wakimbizi hao ikatumika vitani badala yake.Canada ilikuwa ikitoa silaha kwa Tanzania zikiwamo ndege za kivita na kwa mujibu wa vyanzo fulani,hata baadhi ya marubani wa ndege za jeshi walipokea mafunzo yao nchini Canada.

Muda mrefu hata kabla ya vita kuanza,Tanzania ilikuwa imeagiza ndege zake kutoka Canada.
Wakati vita ilipozuka,kwa mujibu wa kitabu cha War in Uganda,Tanzania ilijaribu kuiharakisha Canada itume ndege hizo,lakini Canada haikufanya lolote.Hata hivyo ndege hizo zilifika baada ya vita kumalizika.

Kuhusu upatikanaji wa silaha nchini Uingereza, kitabu hicho kinaandika kuwa Tanzania ilimtegemea sana Amin Kashmiri ambaye wakati vita inaanza alikuwa London Uingereza, akifanya kazi ya uwakala wa ununuzi wa silaha kwa ajili ya Tanzania na nchi nyingine za Afrika.

Kashmiri au kama wengine walivyomuita Sheikh Mohamed Ameenullah Kashmiri,ilikuwa ateuliwe kuwa mkuu wa majeshi katika mabadiliko ya uongozi jeshini ya mwaka 1974, lakini iliaminika kuwa hakupewa wadhifa huo kwa sababu ya asili yake ya India.

Wasifu wake unaonyesha kuwa Luteni Kanali Kashmiri alizaliwa mwaka 1935 mkoani Tabora na kusoma Shule ya Sekondari ya Karimjee ya Tanga (1950-1956) na baadaye chuo cha kijeshi cha Royal Academy Sandhurst nchini Uingereza (1958 - 1960).
Yeye na Mrisho Sarakikya ndio walioshiriki kikamilifu kulisuka upya Jeshi la Tanzania mara baada ya uasi wa Januari 1964.

Hata hivyo, Serikali ya Uingereza haikutaka kujihusisha waziwazi katika mgogoro wa Tanzania na Uganda.Lakini angalau vifaa vya kujenga upya daraja la Mto Kagera vilitolewa na Uingereza.
Kashmiri alifanikisha kupatikana kwa mabuti ya jeshi,mahema na baadhi ya vifaa vingine, na vikapakiwa kuletwa Tanzania.

Kupita kote huko duniani ni katika Afrika tu ndiko ambako Tanzania ilipata marafiki wa kweli.Msumbiji na Zambia walitoa hadharani taarifa za kumlaani Idi Amin kuivamia Tanzania.
Msumbiji ilitoa kikosi cha wapiganaji wake kwenda vitani Kagera,nchi za mstari wa mbele nazo kila moja zikachangia silaha.Algeria nayo ilituma meli tatu za silaha.

Lakini katika yote hayo, walioiokoa Tanzania kwa maana ya zana za kivita ni silaha za Jeshi la Uganda.
Wanajeshi wa Uganda walipokuwa wakiwakimbia wapiganaji wa JWTZ waliacha silaha nyingi nyuma yao ambazo JWTZ ilizikusanya na kuzitumia.

Shida kubwa ya Tanzania ikawa si silaha tena,bali ni namna ya kusafirisha silaha walizopata. JWTZ ilikusanya silaha nyingi sana za jeshi la Idi Amin kiasi kwamba kuliibuka utani kuwa “Idi Amin alikuwa mgavi mkuu wa silaha kwa Tanzania.”

Awamu ya kwanza ya Vita vya Kagera ikawa imemalizika kwa kuyafukuza majeshi ya Idi Amin katika ardhi ya Tanzania.
Lakini Rais wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere hakuridhika tu na kuwaondoa katika ardhi yake kwa sababu aliamini akiwaacha watashambulia tena.

Baada ya kuwaondoa katika ardhi ya Tanzania kilichofuata ilikuwa ni uamuzi mgumu kuwaandama hadi ndani ya Uganda kwenyewe ili kuhakikisha hawabaki kuja kushambulia tena.
Lakini Nyerere alikuwa kwenye shinikizo kubwa kutoka kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) wakimtaka asitishe vita dhidi ya Uganda.

Aliyekuwa mwenyekiti wa OAU, Rais Jaafar Nimeiry wa Sudan, alianza kumkaba Rais Nyerere kuhusu vita ya Uganda akimtaka ayaondoe majeshi yake.Nyerere naye alimshutumu Nimeiry na OAU kwa kushindwa kulaani uvamizi wa Amin na kutaka kusitisha mapigano wakati Amin akiwa ameikalia ardhi ya Tanzania.

Nyerere alitangaza hadharani kuwa hafikirii kusitisha vita dhidi ya Uganda hadi awe na uhakika na usalama wa Tanzania.Msimamo huo alianza kuuonyesha siku ile alipotangaza vita,Alhamisi ya Novemba 2, 1978. Katika hotuba yake, Mwalimu Nyerere alisema: “

..Marafiki zetu wanaotuomba maneno ya suluhu waache maneno hayo.Kuchukua nchi ya watu wengine si kwamba majeshi yamekosea njia na kusema kuwa sasa sehemu hiyo umeichukua na kutangaza vita kwa nchi ile nyingine.Si sisi tuliofanya hivyo,amefanya hivyo mwendawazimu.

“Sasa rafiki zetu, kama ni marafiki wa kweli,watataka tumwondoe mtu huyu. Hawawezi kutuomba suluhu au jambo la ajabu kabisa turudishe majeshi yetu nyuma,niyarudishe wapi?”

Nigeria, ambayo huenda bado ilikuwa imekasirishwa na kitendo cha Tanzania kuitambua Biafra iliyojitenga nayo ilionyesha msimamo wake waziwazi dhidi ya Tanzania juu ya Vita vya Kagera.

Biafra ilijitenga na Nigeria Jumanne ya Mei 30 1967. Mwaka uliofuata, Jumamosi ya Aprili 13, 1968, Nyerere akaitambua.
Mkuu wa Jeshi la Nigeria, Luteni Jenerali Theophilus Yakubu Danjuma, akitokea Uganda alikokutana na Idi Amin,aliwasili Dar es Salaam Jumanne ya Novemba 14, 1978 na kukaa hadi Alhamisi ya Novemba 16.

Katika mazungumzo ya mjini Kampala, kwa mujibu wa jarida la Africa Research Bulletin, Idi Amin alimwambia Danjuma kuwa yuko tayari kuyaondoa majeshi yake mpakani iwapo tu OAU itamhakikishia kuwa Tanzania itasimamisha mapigano na “kuichokoza Uganda”.

Danjuma alikuwa na ujumbe kutoka kwa Rais wa Nigeria, Jenerali Olusegun Obasanjo kwenda kwa Mwalimu Nyerere ukimtaka kukubali mazungumzo na kusitisha mapigano.

Itaendele..
 
#HISTORIA #NA #KUMBUKUMBU #YA #VITA #YA #KAGERA:

Nyerere na Mkapa wacharuka OAU.

Sehemu ya - 10.

Jana tuliona awamu ya kwanza ya Vita vya Kagera ilivyomalizika kwa kuyafukuza majeshi ya Idi Amin katika ardhi ya Tanzania na jinsi Mwalimu Nyerere alivyoigomea OAU kuaitisha mapigano.

Nyerere hakuridhika tu kwa kuyaondoa majeshi ya Amin katika ardhi ya Tanzania, kwa sababu aliamini akiwaacha watashambulia tena Tanzania.

Nigeria, Sudan, OAU na Libya walimtaka Nyerere asitishe vita,lakini aligomea jambo hilo.Nigeria iliamua kumtuma mkuu wake wa majeshi,Luteni Jenerali Theophilus Yakubu Danjuma,kuja Tanzania kukabiliana na Nyerere,hata hivyo Nyerere hakuwasikiliza.

Mkuu wa Jeshi la Nigeria, Luteni Jenerali Theophilus Yakubu Danjuma,akitokea Uganda alikokutana na Idi Amin Dada aliwasili Dar es Salaam Jumanne ya Novemba 14, 1978 na kukaa hadi Alhamisi ya Novemba 16.

Luteni Jenerali Danjuma alitua Uganda kwanza kabla ya kufika Tanzania.
Katika mazungumzo ya mjini Kampala,kwa mujibu wa jarida "Africa Research Bulletin" Iddi Amin alimwambia Danjuma kuwa yuko tayari kuyaondoa majeshi yake mpakani iwapo tu OAU itamhakikishia kuwa Tanzania itasimamisha mapigano na “kuichokoza Uganda”.

Baada ya kuondoka Uganda ndipo akaja Tanzania kumletea Rais Nyerere ujumbe kutoka kwa Rais wa Nigeria,Jenerali Olusegun Obasanjo,ukimtaka kukubali mazungumzo na kusitisha mapigano mara moja.

Nyerere alimkabili Danjuma. Alimwambia, “Iddi Amin amefanya kitendo cha uvamizi dhidi ya Tanzania. Hebu fikiria ikiwa atayaondoa majeshi yake au kuyarudisha nyuma,sisi tuseme ‘imetosha’ halafu tumwache tu ajiendee zake? Si rahisi hivyo kumwachia mchokozi aende zake.”

Simon Chesterman katika kitabu cha "Just War Or Just Peace: Humanitarian Intervention and International Law (uk. 77) ameandika,
“Amin alidai kuwa uvamizi wake kwa Tanzania ulikuwa ni kitendo cha kujilinda dhidi ya matendo ya Tanzania kuunga mkono na kusaidia waasi wa Uganda ...

Novemba 8 (1978) aliahidi kuondoa majeshi yake iwapo tu OAU itamhakikishia kuwa Tanzania haitaivamia Uganda wala kuwasaidia wakimbizi wa Uganda waliopo Tanzania.Nyerere alilikataa sharti hilo na Novemba 12 (Nyerere) akatangaza kuwa Tanzania imeanza kushambulia (Uganda).”

Kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi naye akaingia vitani upande wa Idi Amin,alipomtaka Nyerere aache kuipiga Uganda

Nyerere alimjibu: “...Tumepigana kwa ajili ya usalama wa nchi yetu. Hatupigani kwa sababu ya kumng’oa (Idi Amin) … Sisi tunapigania usalama wa nchi yetu.”

Baadaye Kanali Gaddafi alimtuma mjumbe wake kumpelekea Nyerere risala iliyodai kuwa tangu mgogoro ulipoanza yeye (Gaddafi) alijitahidi sana kusuluhisha,lakini sasa baada ya uchunguzi wa muda mrefu,aliamini Watanzania ndio wachokozi.

Mwalimu Nyerere hakuchelewesha majibu.
Aliwaita wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuwapasha habari hizo. Aliwaambia: “...Vita tunavyopigana sisi ni vita vya usalama wa nchi yetu.

Hatukusudii kumtoa Amin … Tumeishi naye miaka minane,tunataka kuwa na hakika kuwa anajua kuwa vita si lelemama,vita si mchezo,kishajua hilo, nadhani tuliishi naye miaka minane,tuko tayari kuishi naye miaka mingine minane.”

Katika mkutano wa wakuu wa nchi za OAU mjini Monrovia, Rais Nyerere na Rais Gaafar Muhammad an-Nimeiry wa Sudan walirushiana maneno makali,Nimeiry akimtuhumu Nyerere kwa kuivamia Uganda.

Ajenda kuu ya mkutano ilikuwa ‘kitendo cha Tanzania kumpindua Idi Amin’.
Baada ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) kushindwa kutimiza sharti la Tanzania la kumlaani Idi Amin kwa kuitaka na kuiteka ardhi ya Tanzania, uliamua kuteua kamati ya mataifa tisa ya kujaribu kuleta suluhisho.

Ikiongozwa na Meja Jenerali Henry Edmund Olufemi Adefope wa Jeshi la Nigeria,kamati hiyo ilikutana mjini Nairobi,lakini katika kila kikao walichofanya kilikaribia kuvunjika kwa sababu ya kurushiana maneno makali.

Katibu Mkuu wa OAU, Edouard Kodjovi Kodjo (alijulikana zaidi kama Edem Kodjo) ndiye aliyetoa hadidu za rejea.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Benjamin Mkapa alikataa hoja iliyosema ‘Majeshi ya Uganda yameondoka kwa hiari katika ardhi ya Tanzania.’

Kisha akahoji, “Kusema kwamba majeshi ya Uganda yameondoka kwa hiari ni tusi kubwa kwa vijana wetu waliouawa wakipigana.”

Mkapa akaiambia kamati hiyo kuwa OAU ilishindwa kumlaani Idi Amin alipoteka sehemu ya ardhi ya Tanzania na pia ikashindwa kutofautisha kati ya mchokozi na aliyechokozwa.

Akijibu hoja za Mkapa, mwakilishi wa Uganda ambaye alikuwa ni Waziri wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje,Matias Lubega alipinga lakini Mkapa akasimamia msimamo wake.

Baada ya mjadala wa Nairobi kuwaka moto kamati hiyo iliamua kusafiri kwenda Kampala na Dar es Salaam kuonana na Idi Amin na Nyerere.

Walipofika Uganda,Idd Amin aliiambia kamati hiyo kuwa Uganda ilivamiwa na Watanzania,Wamarekani, Waisraeli na Wacuba.

Baada ya kumsikiliza kamati iliondoka Kampala kuelekea Dar es Salaam.
Nyerere alikuwa kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri wakati kamati ikiwasili.Mkapa aliwahakikishia wajumbe hao kuwa Nyerere alikuwa na shauku kubwa ya kukutana nao na kwamba angekutana nao jioni.

Kamati ilisubiri katika Hoteli ya Kilimanjaro,lakini Nyerere hakutokea.Hatimaye wakaamua kuondoka kurejea Nairobi.

Walipoondoka tu hotelini hapo ndipo Nyerere akatuma neno akisema sasa alikuwa tayari kukutana nao saa 11:30 jioni.

Mkapa alilazimika kuwakimbilia wajumbe hao hadi Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam kuwapasha habari hizo.Lakini walisema wameshachelewa na kwamba kama watafanya mkutano huo watachelewa ndege ya kuwarejesha Nairobi.

Ingawa Mkapa aliwaambia yuko tayari kuwapatia malazi na kila walichohitaji ili tu mkutano huo ufanyike, baadhi walimwambia hawakuja na miswaki na wengine wakasema hawakuja na nguo za ndani za kubadilisha,kisha wakapanda ndege wakaondoka zao,usuluhishi mwingine wa OAU ukawa umeshindwa.

Wakati Nyerere akikabiliana na kile alichodhani ni kuingiliwa matakwa yake na Nigeria,Sudan,Libya na OAU, zipo nchi ambazo hazikuishutumu Tanzania lakini ujumbe haukuwa tofauti na zile zilizoishutumu.

Waandishi Richard Bissell na Michael Radu katika kitabu chao, cha Africa in the Post-Decolonization Era (uk. 172) wameandika kuwa, “...baada ya OAU kushindwa kukemea na kuilaani Uganda kwa kitendo chake cha kuivamia na kuikalia sehemu ya ardhi ya Tanzania,Nyerere aliliamrisha jeshi lake kuingia Uganda.”

Awamu ya pili ya Vita ya Kagera ikaanza.

Itaendelea sehemu ya 11.
 
Back
Top Bottom