Inaonekana kuna watu wamejipanga kisawasawa kumdhibiti Makonda kwenye hii vita ya madawa.
Sikutegemea kuona baadhi ya Watanzania kumkashifu Makonda kwamba anatafuta sifa! Sifa jwa ajili ya nini?
Sikutegemea kuona baadhi ya wabunge kusimama na kuanza kumpinga Makonda.
Sasa kinachofuata, Makonda ataachana na hii operesheni na hapo madawa yatakuwa yameruhusiwa rasmi hapa nchini.
Na kwakuwa tumeshindwa kumasapoti Makonda kwa sababu ya mahaba yetu ya kisiasa, nisisikie mtu akilalamika kuhusu madawa ya kulevya tena.
Madawa ya kulevya ni janga la kitaifa na kwa ujumla wote tunatakiwa tupambane.
Lakini ili tushinde ni lazima tuwe na mkakati kwani hii vita si ya mchezo.Amerika pamoja na nguvu zake haijaweza kumaliza shida ya madawa ya kulevya.Iran na Saudi Arabia wana sheria kali lakini bado hajamaliza tatizo hili.
Makonda ameanzisha mfumo mwingine nje ya mfumo wa serikali katika vita hii na kwa mkakati huu mission itashindwa hata kabla ya kuanza.Hivi wangekamatwa kimya kimya bila media pangekuwa na shida gani?
-Hivi angeshirikiana na idara ya usalama wa taifa,polisi na tume ya kuzuia madawa ya kulevya angepoteza nini?
Waandishi wa habari wanaweza kukujenga lakini pia wanaweza kukubomoa.
Yetu macho!!!!!