Abdullah Kassim Hanga: Kutoka Kiongozi hadi adui wa mapinduzi ya Zanzibar

Kumbe haya mambo ya kuuwana hayajaanza leo, ni wakati wa kuyakomesha haya mauaji utawala wa ccm damu za watu mliowauwa unawalilia
 
Kumbe haya mambo ya kuuwana hayajaanza leo, ni wakati wa kuyakomesha haya mauaji utawala wa ccm damu za watu mliowauwa unawalilia
 
Mabaya waliyofanya Hawa Wawili waliyafanya kipindi ambacho habari ilikuwa bidhaa adimu sana!

Unyama wa Hawa Viumbe Wawili ni Mkubwa kuliko wa kina Yahya Jammeh tofauti ni kuwa walimiliki mifereji yote ya habari na kuchuja kila wasichotaka kuwafikia Raia na kweli hakikuwafikia!

Ulikuwa ukiandamwa unauawa na hata Mali chache ulizoacha zinataifishwa kumkomoa Wajane na Mayatima ulioacha! Oscar Kambona alivyokoswa koswa kuzimwa kwa kukimbilia Uingereza basi kuanzia Majumba mpaka Kandambili alizoacha Tanzania zilitaifishwa na mpaka Leo hatujawahi kuambiwa alikuwa na kosa gani?

Kuna Wazee wetu Mungu awarehemu ulikuwa ukiwatajia Hawa watu kwa kukuheshimu basi watakaa kimya wasitie neno kutuudhi lakini unaona wanakaza meno kwa chuki na hasira

Ilitakiwa ikifika April 7 na October 14 kila Mwaka Familia zao ziwe zinatuomba Radhi kwa dhulma zilizofanyiwa Wazee wetu na Hawa watu

Nyerere na Karume ni watu waovu sana kupata kutokea kwenye Taifa hili. Makatili na Wauwaji
 
EMT;

Shukrani. Nilimsoma Kassimu Hanga baada ya kununua kitabu cha mtoto wake aliye Urusi. Katika historia ya Tanzania hayumo lakini ni mtu mashuhuri. Mtoto wake alikuja Tanzania, anasema hali aliyokuta bibi yake ilikuwa pathetic.

Kuhusiana na historia ya Tanzania, kulikuwa hakuna uhuru wa kujieleza. Hivyo waandishi wengi wameandika kufuata mistari ya watawala.

Naomba kutaka kujua habari za icho kitabu. Kinaitwaje? nakinahusiana na nini?
 
Naomba kutaka kujua habari za icho kitabu. Kinaitwaje? nakinahusiana na nini?

Kitabu kinaitwa: Soul to Soul: A Black Russian American Family, Yelena Abdulaevna Khanga.

Yelena Khanga (Hanga) ni mtoto wa Kassimu Hanga ambaye alizaa na mwanamke aliyechanganya (mzungu na mmarekani mweusi).

Kitabu kinaelezea makuzi ya Yelena na jitihada zake za kutafuta asili ya wazazi.
 
Akhsante.
Bila shaka wengi tumefaidika japo muda ulopangiwa haukutosha kumalizia historia hii

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Bopwe,
Nakuwekea hapo chini video ya niliyozungumza katika mkutano ule:
Mohamed Said: WOMEN LEADERSHIP SUMMIT 2018 MLIMANI CITY 27 FEBRUARY 2018

Mwandishi katika video hii anaanza kuzungumza katika dakika ya 40:40

Hii ni simulizi ya mkasa wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ilipodhaniwa kalishwa chakula kilichotiwa sumu kwa nia ya kutaka kukatisha maisha yake nyumbani kwa Abdulwahid Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu katika miaka ya kati 1950 baada ya Mwalimu kutoka UNO safari ya kwanza 1955.
 
Bopwe,
Nakuwekea hapo chini video ya niliyozungumza katika mkutano ule:
Mohamed Said: WOMEN LEADERSHIP SUMMIT 2018 MLIMANI CITY 27 FEBRUARY 2018

Mwandishi katika video hii anaanza kuzungumza katika dakika ya 40:40

Hii ni simulizi ya mkasa wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ilipodhaniwa kalishwa chakula kilichotiwa sumu kwa nia ya kutaka kukatisha maisha yake nyumbani kwa Abdulwahid Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu katika miaka ya kati 1950 baada ya Mwalimu kutoka UNO safari ya kwanza 1955.
Si mchezo kwa kweli...
 
Boaz,
Kwanza nikupe picha.
Abdul Sykes kafa kijana miaka 44, 1968.
Soma kitabu cha maisha yake jibu limo humo.
 
Boaz,
Kwanza nikupe picha.
Abdul Sykes kafa kijana miaka 44, 1968.
Soma kitabu cha maisha yake jibu limo humo.

Sheikh Mohamed Said sijasoma hichi kitabu ila nitajitafuta.
Lakini jee umegusia kwa nini Ali, Abdul Sykes waliachana na siasa ? Na kifo cha Abdul akiwa kijana Bado akiwa maaruf na Abbas kupelekwa Ubalozi miaka yote ya Nyerere jee kuna conspirancy theory ? Wenyewe walili zungumziaje hili.
 
Bopwe,
Nadhani sote tujiulize maswali.

Kwa nini Abdul tayari akiwa Secretary wa TAA na Acting President kuanzia 1950/51 alikuwa anamshawishi Chief Kidaha Makwaia ajiunge na TAA wamchague president kisha waunde TANU na baada ya kushindwa kumshawishi Chief Kidaha alimsaidia Nyerere kuchukua uongozi wa Tanganyika.

Hii mosi na pili tujiulize kwa nini baada ya uhuru zilipoanza kejeli ndani ya TANU kuwa TAA hakikuwa chama cha siasa bali chama cha starehe Abdul hakujibu kejeli zile ingawa rafiki zake walimtaka sana afanye hivyo.

Tatu kwa nini Abdul juu ya kupata admission ya kuingia Princeton University 1953, Abdul hakwenda akabakia Dar es Salaam hadi akaunda TANU 1954 na baada ya kufanya hivyo akajivua uongozi wa kushikilia nafasi ndani ya chama akawa amejikita zaidi katika ufadhili yeye pamoja na mdogo wake Ally, Dossa Aziz na John Rupia.

Nimezungumza na Abbas Sykes mambo mengi sana na mchango wake katika serikali.

Sikupata hisia zozote kuwa hakuwa anapenda kazi ya ubalozi kwa hiyo naamini hapakuwa na njama.

Nilichogundua ni kitu kimoja tu.

Walikuwapo watu ndani ya uongozi wa TANU na serikali wakichomwa sana na historia ya akina Sykes katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Haya nimeyaeleza kwa kirefu katika kitabu.
 
Unashangaa watu waliopotea kwenye 60ś kuna masheikh wetu wako Tanganyika hadi leo ambao bado wako hai. Halafu anatokea mjinga anasema tumuombee raisi ... shwain!
 
Picha za Mwisho za Kassim Hanga Makamu wa Rais wa Zanzibar kabla hajapotea.
Hanga ni katika wa hanga wa mwanzo kupotea na mpaka leo miaka 50 wapi kazikwa wanajua walio mpoteza na hakuna alietoa siri

Jee unafikiri Azory atapatikana ?

Mwenye kujua zaidi historia yake tunaomba atujuze hapa nimeikuta tweeter
IMG_20180530_081025.jpg
IMG_20180530_081004.jpg
IMG_20180530_081012.jpg


Historia yake ni hii baada ya member mwenzetu kutupa hii habari

Tuendelee kujikumbusha na Mapinduzi !

unao wanahistoria wengi makini wanaoweza kueleza mambo haya kinaganaga kuliko tunavyofanya katika makala za magazetini, lakini ama hawajapata jukwaa au hawako tayari kufanya hivyo. Namuunga mkono Issa bin Nasser kwa aliyosema katika kitabu chake, ‘Zanzibar: Kinyang’anyiro na Utumwa’. Aliandika: “Mwenyezi Mungu ndiye mjuaji wa yote.” Sentensi inayotangulia maneno hayo, ambayo ndiyo imenikopesha maneno ya kichwa cha habari ya mada hii, inatia uchungu hata zaidi inaposomeka hivi: “…Mwenyezi Mungu mwenyewe anaelewa namna ya kuihukumu dhuluma hii iliyotendeka…”

Naiandika mada hii kwa ufupi sana kutokana na ufinyu wa nafasi. Kassim Hanga alikuwa rafiki mkubwa wa kisiasa wa Oscar Kambona. Kama Kambona alivyopoteza nyadhifa zake katika siasa, ndivyo Hanga naye alipoteza nyadhifa zake katika Serikali ya Muungano wakati yalipofanyika mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri.

Hanga hakujua mambo mengi kuhusu Tanzania kama Kambona alivyojua. Baada ya kwenda Guinea, Hanga alihakikishiwa na Rais wa nchi hiyo, Ahmed Sekou Toure, na Nyerere wa Tanzania, kwamba angekuwa huru na salama akirejea nchini. Hanga alirejeshwa Tanzania kutoka Guinea.
Hanga hakuuona uhuru alioahidiwa na, badala yake, Desemba 1967 alikamatwa kwa tuhuma za uhaini. Alipohoji sababu ya kukamatwa alijibiwa kuwa alikula njama za kuwarubuni maofisa wa jeshi ili aweze kuiangusha serikali ya Sheikh Abeid Karume. Katika mahojiano aliyoruhusiwa kufanyiwa akiwa rumande, kwa mujibu wa jarida Africa Confidential, Hanga alikana kuhusika kwa vyovyote katika kula njama na maofisa wa jeshi na akasisitiza kwamba siku zote jitihada zake zilikuwa ni katika kutaka kuwapatanisha Kambona na Nyerere.

Mapema mwaka 1969, Kassim Hanga aliachiwa huru kutoka rumande. Badala ya kurejea Zanzibar, aliondoka na kwenda kuishi katika mojawapo ya nyumba zilizomilikiwa na Kambona mjini Dar es Salaam ambayo ilikuwa bado kutaifishwa.

Lakini matatizo yake na serikali za Tanganyika na Zanzibar hayakuwa yamemalizika. Kuna Watanzania ambao hawakuridhishwa na hali ya kisiasa nchini. Miongoni mwa mengi waliyohoji ni suala la Kassim Hanga na ‘udikteta wa Zanzibar’ wakidai kuwa Karume hakutaka uchaguzi kufanyika Zanzibar.

Baada ya kupinga sana sera za serikali, Oktoba 1968, wabunge kadhaa walitimuliwa Bungeni na baadhi ya watu wengine wakakamatwa na kutiwa kizuizini. Hawa walikuwa ni pamoja na Eli Anangisye, Joseph Kasella-Bantu, Christopher Kassanga Tumbo, Ndugu Choga, Ndugu Bakampenja na Ndugu Kaneno.
Taarifa za watu kutiwa kizuizini zilipochapishwa katika gazeti Daily Nation (Okt. 2, 1968) la Kenya, serikali ya Tanzania iliamuru kukamatwa kwa mwandishi wa Kitanzania aliyevujisha habari hizo, Melek Mzirai Kangero.
Baadaye ikajulikana kuwa Hanga na Othman Sharif walikamatwa mjini Dar es Salaam kutokana na shinikizo la Karume aliyewataka watu hao kwa gharama zozote—hata kama ni kwa kuuvunja Muungano. Othman Sharif, msomi kutoka Chuo cha Makerere, alikuwa mmoja wa waasisi wa Afro-Shirazi na kiongozi wa chama Bungeni wakati Karume akishikilia Urais wa chama.

Mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa kudhani kuwa Othman alikuwa na tamaa ya mamlaka ya kisiasa na uwezekano wake wa kula njama za kuiangusha serikali yake, akisaidiwa na Nyerere, Karume alimwondosha Othman Unguja na kufanywa kuwa Balozi.

Kwanza alikuwa Balozi wa Tanzania mjini London, Uigereza, kisha akapelekwa Washington, Marekani. Wakati mmoja, inadaiwa, Othman Sharif aliporudi Zanzibar kwa matembezi aliponyoka kuingia katika kucha za Abeid Karume. Karume alianza kumwandama kama simba anavyoandama windo lake. Kuona hivyo, Nyerere aliingilia kati mara hiyo hiyo akidai kwamba Othman Sharif alikuwa Balozi wa Muungano wa Tanzania, na si Balozi wa Zanzibar. Karume alipotambua kuwa hakuwa na mamlaka kisheria ya kumdhibiti Othman, alibadili mbinu ya kumtafuta. Nyerere alipogundua hilo alijaribu kufanya kila mbinu aliyoweza ili Othman asirudi Zanzibar.

Baada ya kupoteza wadhifa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mwalimu Nyerere alimpatia Othman kazi nyingine kwa kumteua kuwa afisa uganga wa mifugo mkoani Iringa. Lakini hiyo haikumzuia Karume kumwandama hadi mkoani Iringa na, kwa mujibu wa kitabu ‘Conflict and Harmony in Zanzibar’, Karume aliwashawishi Wazanzibari watatu waliokuwa marafiki wa karibu sana wa Othman ili wamsaliti.

Watu hao walikubali. Wakafikishwa mbele ya Baraza la Mapinduzi, wakatoa ushahidi kwa kiapo na kudai kwamba ni kweli Othman Sharif alikula njama za kutaka kuiangusha serikali ya Karume. Watu hao walipelekwa kwa Nyerere na kurudia madai hayo hayo. Wakati Nyerere anaelekea kuuamini huo ‘mchezo wa kuigiza’, tayari uhusiano kati yake na Karume ulianza kuingiwa na dosari nyingine. Muungano wa Tanganyika-Zanzibar ulikuwa majaribuni.

Hatimaye Nyerere akasema watu hao watapokea “hukumu ya haki” Zanzibar. Gazeti Ulimwengu (Nov. 19, 1967) katika tahariri yake liliandika kuwa lazima hukumu ya haki itolewe. Kisha likaonyesha kupinga suala la watu kuwekwa kizuizini. Kama matokeo, mhariri wa gazeti hilo, Otini Kambona, alikamatwa. Hata ndugu yake Otini, aliyeitwa Mathias, naye alikamatwa kwa sababu nyingine tofauti kwa madai ya kushiriki katika njama za kuiangusha Serikali.
Kikundi cha viongozi kutoka mkoani Iringa, ambako Sheikh Sharrif alikuwa akifanya kazi, walimsihi sana Nyerere asiruhusu watu hao wapelekwe Zanzibar kwani walijua hatima yao. Jawabu la Nyerere lilikuwa hivi: “…Hili si jambo la ubishi kwa sababu halina uzito wa kubishaniwa. Lakini kama kutakuwa salama, ni vizuri tukajua watu hawa watakuwa salama kiasi gani.” Lakini historia ni shahidi. Hakukuwa na usalama wa kiasi chochote. Wanadamu hawa walinyang’anywa haki yao ya kuishi.
Baada ya kuona kuwa mambo yameshindikana, na kwa kuwa Muungano wa Tanzania ndilo lililokuwa suala kuu katika akili yake, Mwalimu ‘alibwaga manyanga’. Septemba 1969 Nyerere akajikuta akiwapa idhini maofisa wake kuwatoa Kassim Hanga na Othman Sharif wakabidhiwe SMZ kama Abeid Karume alivyotaka.
Walipelekwa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Dar es Salaam (DIA), wakipewa maneno ya kuwafariji, na kisha wakasafirishwa kwenda Zanzibar. Hiyo ikawa ndiyo safari yao ya mwisho—angalau safari ya mwisho kutoka Dar es Salaam—tena, inadaiwa, wakiwa na wamefungwa pingu.
Huko ndiko walikokutana na mauti yao, pengine kwa kupigwa risasi—ingawa taarifa nyingine zilisema kuwa waliuawa kwa kuzamishwa katika maji. Lakini, kinasema kitabu ‘Conflict and Harmony in Zanzibar’, hata wale waliomsaliti Othman Sharif nao waliuawa mmoja baada ya mwingine. Machapisho mengine ya kihistoria yanaunga mkono madai hayo. Katika hotuba aliyoitoa Oktoba 1969, ukiwa ni mwezi mmoja baada ya kufanyika kwa mauaji hayo, Abeid Karume alitangaza kuwa watu wanne waliokuwa wakila njama za kuiangusha serikali yake “…wameuawa kwa kupigwa risasi.” Hili alilikiri mwenyewe. Vyanzo kadhaa vinasema kuwa Kassim Hanga, na aliyekuwa Waziri wa Elimu na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Sheikh Othman Sharrif, waliuawa Zanzibar na utawala wa Karume. Hata hivyo mauaji hayo hayakuwa mwisho wa mambo. Inaelekea kuanzia hapo, au kabla ya hapo, kulijengeka utamaduni wa kuwakamata watu, kuwaweka kizuizini na hatimaye wengine kuuawa.

Zaidi ya watu kuwekwa kizuizini bila kufunguliwa mashitaka, kulikuwa na madai ya kuweko kwa zile kambi za mateso. Kwa mfano katika miaka ya 1960 na mwanzoni mwa 1970, inasemwa, Zanzibar kulikuwa na ile kambi iliyoitwa ‘Kwa Bamkwe’ au ‘Kwa Mandera’. Mkoani Mwanza kaskazini mwa Tanzania kulikuwa na (kambi ya) Kigoto. Hiyo ni moja ya kambi zilizokuwa mbaya. Baada ya kuwakamata watu kwa tuhuma za uchawi mwaka 1977 katika maeneo ya Mwanza na Shinyanga, ikijumlishwa na matendo waliyofanyiwa watu hao, ilitosha kumfanya Alhaj Ali Hassan Mwinyi kujiuzulu ‘kwa kuwajibika’.
Ingawa wengi walitarajia kuwa kuwajibika huko kungekuwa ndio mwisho wa Mwinyi katika siasa, Nyerere ‘alimpigia debe’ kuwa Rais wa Zanzibar (Jan. 30, 1984—Okt. 24, 1985) na hatimaye Rais wa Tanzania (Nov. 5, 1985—Nov. 23, 1995) kwa kura za NDIYO. Kwa mujibu wa kitabu ‘Zanzibar: Kinyang’anyiro na Utumwa’, mwanasiasa aliyekuwa Unguja wakati mambo yote hayo yakitokea, Issa bin Nasser Al-Ismaily, anaandika kuwa mwaka 1970 Wazanzibari tisa “walitiwa nguvuni na Serikali ya ASP kwa kisingizio cha kutaka kuipindua serikali hiyo.” Wazanzibari hao ni Salim Ahmed Busaidi, Abdallah Suleiman Riyami, Othman Soud, Aziz Bualy, Hemed Said, Muhammed Juma, Muhammed Hamza, Musa Ali na Said Hamoud.

Bila ya kufikishwa mahakamani, Karume aliwahukumu kutupwa gerezani na kupewa kazi ya kuchunga ng’ombe katika uwanda wa “Hanyagwa-Mchana”. Baada ya kifo cha Karume Aprili 1972, “wananchi hao waliuawa wakati wa utawala wa mrithi wa Karume, Aboud Jumbe.” Kitabu hicho kinaomboleza hivi: “…Mwenyezi Mungu mwenyewe anaelewa namna ya kuihukumu dhuluma hii iliyotendeka…; kwani Mwenyezi Mungu ndiye mjuaji wa yote.” Ni kweli kwamba “Mwenyezi Mungu ndiye mjuaji wa yote” kwa sababu hakuna mwanadamu atakayejua yote yaliyotendeka, hasa yale ambayo hayatajulikana kamwe.
 
Back
Top Bottom