Nemo,nimekusoma kwa makini sana mwandishi wa makala hii, hakika historia ya Tanganyika na Zanzibar zina ukakasi mkubwa hususani katika harakati za kugombania Uhuru, visasi na usaliti ulikua umetamalaki sana kipindi hiko, alafu kumbe usomi kwa waafrika ulikua mkubwa sana kipindi hiko sasa sijaelewa kwa mini hao wasomi hawakushirikiana kuleta maendeleo pamoja, alafu kuna hili la waislamu kuambiwa hawakusoma mbona naona wengi humu wamesoma tokea zamani hususani Zanzibar.
aksante
Hizo historia tulikuwa hatufundishwi mashuleni. Nimesoma history mpaka A Level, lakini hakufundishwa kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar na wasisi wake. Tulikuwa tunafundishwa zaidi kuhusu uhuru wa Tanganyika.
Ukicheki hata past exams papers, nadra kukuta swali kuhusu mapinduzi ya Zanzibar, maybe just in case, mtu asije akafunguka huko wakati anashuka mapoints. Labda historia ya Mapinduzi ya Zanzibar iliachwa kufundishwa kwenye somo husika ili tujifanyie "homework" wenyewe?
MUNGU AMUWEKE MAHALA PEMA PEPONI NA MADHWALIMU WOTE WALIO DHULUMU NAFSI YAKE WAANGAMIZWE KWA ADHABU KALI YA MOTO