kunawakati nakuwa mzito sana kuwatukuza na kywaheshimu hawa wana muungano wawili mzee Karume na Mwl Nyerere kunamambo ya kinyama sana waliyatenda kwa wenzao tena walio wapigania kupata madaraka
Mabaya waliyofanya Hawa Wawili waliyafanya kipindi ambacho habari ilikuwa bidhaa adimu sana!
Unyama wa Hawa Viumbe Wawili ni Mkubwa kuliko wa kina Yahya Jammeh tofauti ni kuwa walimiliki mifereji yote ya habari na kuchuja kila wasichotaka kuwafikia Raia na kweli hakikuwafikia!
Ulikuwa ukiandamwa unauawa na hata Mali chache ulizoacha zinataifishwa kumkomoa Wajane na Mayatima ulioacha! Oscar Kambona alivyokoswa koswa kuzimwa kwa kukimbilia Uingereza basi kuanzia Majumba mpaka Kandambili alizoacha Tanzania zilitaifishwa na mpaka Leo hatujawahi kuambiwa alikuwa na kosa gani?
Kuna Wazee wetu Mungu awarehemu ulikuwa ukiwatajia Hawa watu kwa kukuheshimu basi watakaa kimya wasitie neno kutuudhi lakini unaona wanakaza meno kwa chuki na hasira
Ilitakiwa ikifika April 7 na October 14 kila Mwaka Familia zao ziwe zinatuomba Radhi kwa dhulma zilizofanyiwa Wazee wetu na Hawa watu