viwanda

  1. M

    Kwa nini sukari kwa upande wa zanzibar haizidi Tsh 1,800/= kwa kilo, Wao wana viwanda vingapi?

    Zanzibar kuna viwanda vingapi vya sukari wakuu, mbona wao bei iko chini.. huku kwetu chai imeshakuwa anasa sasa...
  2. L

    Tanzania ya Viwanda: Zaidi ya wafanyakazi 90% wafutwa kazi kwenye kiwanda cha Mihogo kwa Nape

    Wassalam wana-JF, Mwezi Machi mwaka 2019, waziri Mkuu wa JMT Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa alizindua kikubwa na inawezekana cha pekee Mkoani Lindi maeneo ya Mbalala jimboni Mtama kinachojulikana kwa jina la CASSAVA STARCH OF TANZANIA CORPORATION. Kiwanda ambacho kinajishughulisha na uzalishaji...
  3. Mzee Mwanakijiji

    Viwanda Gani Tanzania Vinatengeneza vifaa vya kujikinga (PPEs) kama barakoa, glovu n.k?

    Mojawapo ya changamoto kubwa zilizoletwa na baa la virusi vya Corona ni ukosefu au upungufu wa vifaa vya kujikinga binafsi. Glovu, kofia, barakoa, gauni kinga ni baadhi tu ya vifaa hivi. Mahitaji ya vifaa hivi duniani yameongezeka sana. Katika hali ya kufa kufaana ni viwanda gani Tanzania...
  4. jingalao

    Udhibiti na maandalizi ya COVID 19 Tanzania viwanda vifanye nini?

    Ni muhimu sekta ya viwanda nchini hasa vile vya nguo vikaja na mpango kazi maalumu wa kuzalisha PPEs haswa masks za N95 ,COVERALL GOWNS ,BOOTS,GOGGLES,N.K
  5. Superbug

    Serikali ya Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete hazikupika takwimu za uongo za viwanda

    Wachumi na wanahistoria naomba mnisaidie Serikali za Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Jakaya hazikufanya udanganyifu wa takwimu za uwepo wa viwanda vipya Tanzania. Naamini hata Serikali ya awamu ya tano haiwezi fanya kosa Kama Hilo la kupika data za kiuchumi. Hivyo wanavyosema ndani ya miaka minne...
  6. wanzagitalewa

    Tanzania ya viwanda inavyohitaji mazingira bora kukuza ubunifu wa kiteknolojia

    Wiki jana tumeona ufunguzi wa maonyesho katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya. Tukio hilo muhimu lilileta pamoja wanafunzi na waalimu wa vyuo na taasisi mbalimbali za mkoa wa Mbeya kuonyesha na kujadili fursa zitokanazo na ubunifu wa kiteknolojia. Katika hotuba yake, Mkuu wa Kitivo...
  7. Titicomb

    Nadandia kwa mbele hoja ya Rais kuhusu bima ya afya kuwekeza kwenye viwanda vya madawa

    Mh. Raisi J.P. Magufuli nakusalimu na kukupongeza kwa wazo au ushauri wako kwa Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya (NHIF) wa kuwekeza makusanyo yao ya michango ya wateja kwenye sekta ya afya hasa kwenye viwanda vya madawa n.k. Mimi nilikuwa na ombi moja ktk kuboresha wazo lako. Naomba NHIF itangaze...
  8. Victor Mlaki

    Je, unafahamu katika nchi zinazoendelea kila sekunde 15 mfanyakazi mmoja hupoteza maisha kutokana na ajali au magonjwa yatokanayo na kazi?

    Suala la Usalama na Afya mahali pa kazi ni muhimu kuangaliwa kwa makini tunakoelekea kwenye uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ili kuokoa maisha ya wengi. Shirika la kazi Duniani (ILO) limeonesha kuwa kila sekunde 15 mfanyakazi mmoja hupoteza maisha na ndani ya saa 24 wafanyakazi 5760...
  9. wanzagitalewa

    Kuelekea Tanzania ya viwanda yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025

    Mwanzo wa mwaka huu ni kengele ya miaka mitano kuelekea 2025 mwaka ambao Tanzania ilipanga kuwa imefikia lengo lake la kuwa nchi ya uchumi wa kati, ya viwanda.Dira hii ambayo Tanzania ilianza nayo mwanzoni mwa karne hii ya 21 inatambulika kuwa ni moja ya malengo makubwa ya Rais Dkt John...
  10. technically

    Tuache siasa, tuwekeze kwenye kilimo then viwanda then ndege

    Naomba nitoe ushuhuda kidogo. Mimi ni moja ya watu ambao najaribu kuwekeza kwenye kilimo ila naleta ushuhuda ili liwe somo kwa serikali na wananchi kwa ujumla. Maka jana nililima ekari 20 za mahindi mkoa wa Rukwa na nilipovuna mwezi wa 7 mwaka jana nilipata gunia 350 nikaweka store maana...
  11. J

    Mchungaji Msigwa viwanda vya kuchakata mazao ya misitu vinafungwa Mafinga, kulikoni?

    Nakuuliza swali hili mh Peter Msigwa kwanza kama mbunge pekee wa upinzani mkoa wa Iringa lakini pia kama mwenyekiti wa Chadema kanda ya Nyasa. Nimetembelea Mafinga wadimi wanalalamika kukosa vibarua kwa kuwa viwanda vinafungwa na wamebakia Wachina ndio wanaotamba msituni. Kabla sijawasiliana...
  12. N

    Dodoma kuchele: Serikali ya viwanda inapiga kazi?

    Hatimaye Serikali umeamua kufungua kiwanda kikubwa na cha kisasa cha kusindika mbogamboga maana sasa hivi akina mama wengi wanafunga mboga zao, Serikali imeamua kuboresha na kuandaa kiwanda kitakachoajiri watu 100,000 na kupewa mishahara ya laki 5. Hakika hakuna kiwanda kilichokufa vyote vipo...
  13. J

    Kwa kasi hii ya Rais Magufuli nashindwa kuelewa mzee Mwinyi alifeli wapi hadi viwanda na mashirika ya umma yakafa!

    Nafuatilia kwa makini jinsi taasisi za serikali zinavyozidi kujitokeza kutoa gawio (dividends) kwa serikali. Nimeona hadi vyuo kama SUA, IFM nk vikitoa gawio sambamba na wakala mbalimbali za serikali na hata vitega uchumi vilivyoko jeshini na magereza mfano Suma JKT. Natafakari tu endapo...
  14. J

    TBS kuandaa viwango vya Mbege na Ulanzi katika kukuza viwanda vidogo vidogo

    Msemaji wa Shirika la Viwango TBS kanda ya kusini amesema taasisi yake inaandaa viwango vya pombe za kienyeji Mbege na Ulanzi ili zitengenezwe na kusindikwa katika ubora unaostahili. Msemaji huyo amesema viwangi hivyo vitasaidia Mbege na Ulanzi ziweze kushindanishwa na Chibuku na hivyo kusaidia...
  15. Patriot

    Viwanda hivi vilikufa, vingine ni mali ya wawekezaji wasanii Marais muliopita tuwaambie nini?

    Nimeweka list ya viwanda ninavyoweza kumbuka, ambavyo ilikuwa ni mkombozi wa ajira kwa TZ. Vingi viliajili zaidi ya watu 1000. Mbali na viwanda hivi, kuna mashirika ambayo sikuyaweka. Lakini hii ilikuwa enzi ya Mwalimu. Marais waliofuata walifanya nini? ni halali leo hii vijana kukosa ajira...
  16. Suley2019

    Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kumtunuku Rais Magufuli Shahada ya Falsafa

    Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kitamtunuku Rais wa Tanzania, John Magufuli Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa kutokana na uongozi wake hasa ujenzi wa uchumi wa viwanda. Akizungumza leo Jumatano Novemba 20, 2019 Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Faustine Bee amesema shahada hiyo itatolewa...
  17. elivina shambuni

    Viwanda vya Nguo, Glasi kujengwa Simiyu

    Mwekezaji kutoka nchini Uturuki, Bw. Mustafa Albayram ameahidi kujenga viwanda viwili kiwanda cha nguo na kiwanda cha kutengeneza glasi katika eneo la Isanga Mjini Bariadi Mkoani Simiyu mwaka 2020, mara baada ya kuridhishwa na mazingira ya uwekezaji ambapo viwanda hivyo vinatarajia kuajiri...
  18. elivina shambuni

    Viwanda vya juisi, pombe ya korosho vyaja

    WAFANYABIASHARA wakubwa wa korosho, wawekezaji na watafi ti 169 kutoka nchi 13 duniani zikiwamo nchi zinazoongoza kwa ununuzi wa korosho, India na Vietnam, wamekubaliana kuzuia uuzwaji wa korosho ghafi kutoka nchini kwenda nje ya nchi. Badala yake, wametaka korosho iendelezwe hapa hapa nchini...
  19. Ngwanakilala

    Tuna vyuo vya Kilimo lakini hatuna wakulima wakubwa, Tuna SIDO lakini hatuna viwanda vidogo

    Wakuu Hili suala nimekua nalifikiria mara kwa mara Tuna chuo Kikuu cha kilimo SUA lakini kwanini hakuna wanafunzi au walimu wanaotoka pale na kua wakulima wakubwa na bora. Wote wakimaliza pale wanaamini kwamba wanatakiwa waajiriwe maofisini. Ina maana hawa walienda chuo cha kilimo ili...
  20. Kaka Pekee

    Tanzania ya Viwonder...ni lini tutafika huku? (Tufanye nini?!)

    Kuelekea Tanzania ya Viwonder (Viwanda) ni lini tutafikia kutoa support kwa Wataalamu wetu wabuni na kutengeneza Vimashine vidogo au kubwa za kurahisisha kazi na kutengeneza ajira. Tukiwa na nia ya dhati ya kupata 'Viwanda' inabidi sapoti hizi ziwepo, fungu liwepo na hamasa iwepo. Yuko wapi...
Back
Top Bottom