mwigulu nchemba

Mwigulu Nchemba
Mwigulu Lameck Nchemba Madelu ni mwanasiasa na mwanachama wa chama cha kisiasa nchini Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mwigulu alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango tangu 31 Machi 2021, mpaka July 2023 ambapo wizara hiyo ilivunjwa na kuwa wizara mbili yaani Wizara ya Fedha inayoongozwa na Mwigulu Nchemba na Wizara ya Mipango na Uwekezaji inayosimamiwa na Waziri Kitila Mkumbo.
  1. Jidu La Mabambasi

    Waziri Mwigulu Nchemba akiwa na maongezi na Wafaransa, kujenga viwanda vya madawa

    Natazama hapa Waziri Mwigulu Nchemba akiwa na maongezi na Wafaransa, ati kujenga viwanda vya madawa. Kwanza, Kuna kiwanda cha madawa ya kukuua vidudu vya mbu Kibaha. Kiwanda hiki kimejengwa kwa ushirikiano na nchi ya Cuba. Kiwanda vile vile kinazalisha dawa za binadamu. Serikali yenyewe...
  2. Mindyou

    Waziri Mwigulu Nechemba aishukuru Italia kwa kuipa mkopo Tanzania kujenga SGR

    Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ameishukuru Italia kwa kutoa dhamana ya mkopo wa kujenga Reli ya Kisasa (SGR), kipande cha Kwanza na cha pili kuanzia Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma hadi Makutupora mkoani Singida, ambavyo ujenzi wake umekamilika na treni imeanza kutoa huduma kuanzia Dar es...
  3. Mindyou

    Picha: Baada ya kimya kingi, Freeman Mbowe aibukia kwenye msiba wa mkwe wa Mwigulu Nchemba

    Huyu akibanwa vizuri atatoa hadi kadi yake ya CCM. ================================ Mwenyekiti mstaafu wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe akisalimiana na kumpa pole Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba leo Jumanne Machi 25, 2025 kwa kufiwa na mkwe wake katika Kanisa la KKKT Usharika wa Boko jijini...
  4. Waufukweni

    Klabu ya Singida Black Stars yamtangaza Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Mlezi wao

    Klabu ya Singida Black Stars imemtangaza Waziri wa Fedha na Mbunge wa Iramba Magharibi, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kuwa mlezi wao rasmi. Awali, Dr. Mwigulu alikuwa akishiriki kama mdau wa kawaida kwa kutoa michango yake kusaidia timu hiyo, lakini sasa atakuwa na nafasi kubwa katika kuiunga...
  5. Doug Stamper

    Pre GE2025 Siasa chafu dhidi ya Mwigulu ni woga wa 2030

    Katika kila zama za siasa, kuna wanasiasa wachache wenye dira, msimamo, na rekodi safi ambao wanapopata umaarufu na kuwa tishio kwa wapinzani wao, huanza kushambuliwa kwa propaganda chafu, uvumi na hila ili kuwaharibia taswira yao kwa umma. Leo hii, Tanzania inashuhudia smear campaign ya wazi...
  6. G Sam

    Harakati za Mwigulu Nchemba ni kama za hayati Edward Lowassa na mzee "Jumanne" kwenye urais

    Huyu jamaa ni waziri wa wizara nyeti ya fedha ila anafanya mambo ambayo hayaeleweki kabisa kwenye hizi mbio za kwenda ikulu mwaka 2030. Mara aage jimboni kuwa hatagombea tena mwaka 2030 bali anafikiria nafasi ya juu zaidi na anaweka na mrithi kabisa. Mara wachezaji wa timu yake B wapewe uraia...
  7. T

    Pre GE2025 DSM Waziri anayejifanya mzalendo anayetuhumiwa kujilimbikizia mamilioni ya hela kwa ajili ya Urais 2030 ni Mwigulu Nchemba?

    Akizungumza na Wasafi Radio kupitia kipindi cha goodmorning mhariri wa gazeti la Radar aliyejitambulisha kwa jina la Mjema ameeleza kuwa waziri anayejifanya mzalendo kwa kuvaa hadi mavazi yenye bendera, anajilimbikizia mali kwa njia ya Bureau de change kwa ajili ya maandalisi ya uchaguzi wa...
  8. Mindyou

    Pre GE2025 Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba: Serikali imeanza kuondoa makato ya miamala

    Wakuu, Akizungumza katika kumbukizi hiyo waziri wa fedha Dkt mwigulu nchemba amesema kwa sasa serikali imeanza kuchukua hatua ya kuondoa baadhi ya makato ya miamala unapolipia huduma kwa njia za dijitali ili kuwezesha watanzania wengi kufanya malipo ya kidijitali "Sisi kama Serikali...
  9. Cute Wife

    Bunge lapitisha nyongeza ya bajeti ya Tsh. Bilioni 945

    Wakuu, Bunge limepitisha nyongeza ya mapato na matumizi ya jumla ya shilingi bilioni 945.7 kwa ajili ya kuongeza kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka 2024/25 kutoka shilingi trilioni 49.346 iliyoidhinishwa awali hadi shilingi trilioni 50.291. Nyongeza hiyo imewasilishwa na Waziri wa Fedha...
  10. Waufukweni

    Pre GE2025 Mwigulu: Wanachama wa CHADEMA wenyewe ndio waliosema Lissu hatoshi hata kuwa Mwenyekiti wa Kitongoji. Sisi tunajua uwezo wake

    Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walikuwa wanafahamu kuhusu uwezo wa viongozi waliochaguliwa ndani ya chama lakini wanachama wa CHADEMA wao wenyewe ndio walikuwa wakiaminisha watu kwamba Mwenyekiti wao Tundu Lissu hatoshi katika nafasi hiyo...
  11. Mindyou

    Waziri Mwigulu Nchemba aeleza jinsi mgao wa umeme na barabara mbovu zilivyoipitisha serikali katika kipindi kigumu

    Wakuu, Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema bajeti ya Serikali ilikumbwa na changamoto mwaka jana na mwaka huu, hasa kutokana na uharibifu wa barabara chini ya Tarura na Tanroads pamoja na mgao wa umeme. Akizungumza bungeni Dodoma, Dk Mwigulu amesema Serikali ililazimika kuchagua kati...
  12. Doug Stamper

    DKT. Mwigulu Nchemba: Kiongozi mwadilifu na nguzo ya maendeleo ya taifa

    Tangu kuteuliwa kwake kama Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba ameendelea kuonesha uadilifu, uthabiti na umahiri wa hali ya juu katika usimamizi wa uchumi wa Tanzania. Licha ya juhudi za wapinzani wake kueneza kampeni chafu dhidi yake, ukweli unabaki palepale—hana doa la ufisadi, hana tuhuma...
  13. R

    Waziri Mwigulu Nchemba shughilika na hawa lazy customer care service

    Namba ya simu TRA Arusha inaita tu haipokelewi. Why taasisi nyingi za serikali kwenye mawasiliano ni sifuri??
  14. Mindyou

    Mliokuwa mnahoji kuhusu Tigo kubadilisha jina, Mwigulu amewajibu "Kubadilisha majina ya makampuni hakuathiri mchakato wa kodi"

    Wakuu, Hapa juzi juzi tuliona Tigo imebadilisha jina kuwa Yas na kukawa na tetesi kuwa wanakwepa kodi. Akijibu swali bungeni kuhusu makampuni yanayobadilisha majina ili kukwepa kodi Mwigulu amesema "Kupitia sheria ya usimamizi wa kodi ya 238, serikali imeweka sharti kwamba mamalaka ya mapato...
  15. Waufukweni

    Hii ndio sahihi ya Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba kwenye noti mpya zilizoanza kutumika Februari

    Wakuu Hii ndio sahihi ya Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba kwenye noti mpya zilizoanza kutumika Februari 2025 kama ilivyotangazwa wiki kadhaa zilizopita. Soma: Tanzania yazindua Noti Mpya toleo la 2010 zenye Saini ya Waziri Mwigulu Nchemba na Gavana Emmanuel Tutuba Noti ya elfu 5 (5,000/-)...
  16. Dalton elijah

    Tanzania yazindua Noti Mpya toleo la 2010 zenye Saini ya Waziri Mwigulu Nchemba na Gavana Emmanuel Tutuba

    Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba amesema kuwa Noti Mpya za Tanzania zenye Saini ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) na yeye mwenyewe, za toleo la mwaka 2010, zitaingia kwenye mzunguko kuanzia tarehe mosi Februari mwaka huu. Gavana Tutuba amesema hayo wakati...
  17. Li ngunda ngali

    Picha: Duma wakisikiliza Mkutano wa kampeni za Mwigulu

    Hivi, huo ujinga wa kuandika kila pahali hata ndani ya mbuga ya Nyumbu, Simba, Swala na Digidigi aliutoa wapi Nchemba?! Nchi yangu! Picha hapo juu ni Duma wakisikiliza Mkutano wa kampeni za mgombea u Rais bwana Dr. Mwigulu Nchemba.
  18. Mchochezi

    Nini kimemsibu Mwigulu? Uso wake umekosa nuru!

    Nimemuona mheshimiwa Dr. Mwigulu Nchemba ama hayupo sawa. Sio yule tuliyemzoea mwenye uso wenye nuru na bashasha. Nini kinamsibu?
  19. Waufukweni

    Pre GE2025 Mwigulu aahidi kuwahudumia watoto wawili wa aliyekuwa Mtumishi wa TRA

    Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba ameahidi kuwahudumia kimahitaji watoto wawili wa marehemu, Amani Kamguna Simbayao, aliyekuwa mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), aliyefariki Dunia katika Hospitali ya Taifa ya Mifupa Muhimbili-Moi- Dar es salaam, aliyefariki dunia kwa kushambuliwa...
Back
Top Bottom