mwenge wa uhuru

Mwenge wa Uhuru
Mwenge wa Uhuru una muundo wa tochi ya mafuta ya taa ambayo inaashiria uhuru na mwanga. Mwenge wa uhuru ulinyanyuliwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro mnamo Desemba 9, 1961 na shujaa Brigedia Alexander Nyirenda ikiashiria kuangaza nchi na kuvuka mipaka kuleta matumaini palipo kukata tamaa, upendo palipo uadui na heshima palipo chuki.

Sababu ya huyu brigedia kunyanyua mwenge huu ni kuonesha fahari ya nchi na pia kuleta matumaini kwa Watanzania wote kwa kutokata tamaa, kupendana, kuheshimiana na kutogombana ikimaanisha kuwa na ushirikiano.

Mbio za Mwenge wa Uhuru hufanyika kila mwaka kuanzia maeneo mbalimbali nchini.
  1. C

    Mwenge wa Uhuru wafikishwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro, waimba Wimbo wa Taifa

    Wakuu, Mbio za mwenge zilihitimishwa tar 14, Oktoba na wakimbiza mwenge huo kutakiwa kukamilisha zoezi hilo kwa kufika katika kelele cha mlima huo pamoja na kuweka bendera ya taifa. Wajuba walikamilisha zoezi na hapa wanaimba wimbo wa taifa kwa uzalendo mkubwa uliotukuka! Pia soma: Rais...
  2. Venus Star

    Kuwasha Mwenge kunaashiria "Illumination, enlightenment, and guidance." Mwenge wa Uhuru ni muhimu sana katika taifa letu

    Ishara kumi na mbili za dunia zimeunganishwa katika makundi manne (Moto, Ardhi, Hewa na Maji) Kwakuwa tunataka tuijue nchi yetu zaidi kwa leo sitaongelea kwa undani zaidi hizo ishara Kumi na Mbili na makundi yote hayo manne, bali leo nitaongelea pekee kuhusu Moto Kuwasha mwenge kunaweza...
  3. Roving Journalist

    Waziri Kikwete azindua zoezi la kupandisha Mwenge wa uhuru mlima Kilimanjaro kama ilivyoelekezwa na rais Samia

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Tanzania inapeleka mwenge wa uhuru juu ya mlima Kilimanjaro ili kuitangazia dunia kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni imara na pia itaendelea kulinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar...
  4. Waufukweni

    Video ya LIVE ya Rais Samia kwenye kilele cha mbio za Mwenge yaondolewa YouTube. Je, sababu ni kukohoa kwenye hotuba?

    Leo nilitaka kurudia kutazama tukio la jana la kilele cha Mbio za Mwenge na Kumbukumbu ya Miaka 25 ya kifo cha Hayati Mwalimu Nyerere, Oktoba 14 pale Mwanza, nimejiuliza maswali mengi kuhusu hili, kwanini video hiyo imeondolewa YouTube au kwasababu Rais Samia wakati akihutubia alikohoa mara...
  5. M

    Kiongozi wa Mwenge kawa mkweli

    Muhtasari wa taarifa ya mbio za Mwenge 2024 imejaa ukweli mwingi. Wamejitahidi kubainisha kero na mahitaji ya wananchi kutoka mikoa mbalimbali. Sikusikia kero za wakazi.wa Dar ila kwa mujibu wa ripoti Wazanzibari wengi wameonyesha kuridhishwa na utendaji wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano na wa...
  6. Roving Journalist

    Rais Samia akishiriki kilele cha Mbio za Mwenge na Kumbukizi ya Miaka 25 ya kifo cha Hayati Mwalimu Nyerere

    Fuatilia yanayojiri kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 25 ya kifo cha Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kutoka uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, leo Oktoba 14, 2024. https://www.youtube.com/live/v8nSt4aSfdM?si=xHhzHPZ8Cjbg-3m9
  7. K

    Maajabu kumbukumbu ya Hayati Mwalimu Nyerere kila mwaka Mwanza na sio Mara

    Nyerere anatumika kwa kiki za kisiasa na familia yake haifurahishwi na siasa kwenye swala la kitaifa. Sherehe za Nyerere zifanyike alikotokea Mara au kama kama ni kwa mzunguko basi zifanyike sehemu tofauti. Lakini hizi sherehe zimekuwa kama ni za Mwanza day! kufanya kampeni za siasa Mwanza...
  8. ngara23

    Mwenge una Siri Gani? Viongozi Mwanza wanafanya miradi usiku kucha

    Mwenge wa uhuru tunavouchukulia inaweza ikawa tofauti na tunavyodhani. Nadhani viongozi wa mbio za Mwenge wanaenda ku report Kwa Rais mambo mazito, hawajali Mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi n.k. Wao wakikuta mambo ya ovyo wanakulipua juu. Mwenge kesho unaingia Ukerewe ila viongozi...
  9. Jumanne Mwita

    Toka nakua na mpaka sasa sioni faida ya Mwenge wa Uhuru

    Kwa vyovyote vile nitakuwa wa mwisho na wakwanza kuajua faida za mwenge. Sioni faida wala umhimu wa huu mwenge kuwepo, mwenge umekuwa na karaha pale unapoenda sehemu yeyote. Kuna siku nimeitwa na mkuu wa Wilaya, wilaya flani akisema nitoe mchango wa mwenge nikamwambia mwenge unabajeti yake...
  10. Stephano Mgendanyi

    Ngara: Mwenge wa Uhuru Wazindua Mradi wa Maji wa Tsh. Bilioni 3

    Mwenge wa Uhuru Wilayani Ngara umetembelea na kuzindua Mradi wa Maji Wenye Thamani ya shilingi Bilioni tatu chini ya Ufadhilii wa Benki ya Dunia kupitia LADP (Local Area Development Program) inayosimamiwa na NELSAP (Nile Equatorial Lake Subsidiary Action Program). Mhandisi Simon Ndyamukama...
  11. B

    Mwenge wa Uhuru wamulika miradi ya maendeleo - Kibondo

    Jimbo la Muhambwe limepokea Mwenge wa Uhuru kutoka Halmashauri ya Kasulu Vijijini katika Uwanja wa Shule ya Msingi Busunzu 'B' ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa mbio za Mwenge wa Uhuru zinazoendelea nchini. Katika Jimbo la Muhambwe, Mwenge wa Uhuru umezindua Miradi ya Maji, Madarasa, Bweni na...
  12. I

    MSAFARA WA MWENGE WA UHURU

    Swala la kufungwa kwa barabara na kusimama kwa shughuli za usafirishaji kwa masaa kadhaa wakati wa msafara wa Mwenge wa Uhuru limezua mjadala nchini Tanzania. Wakati Mwenge wa Uhuru una umuhimu wa kihistoria na kitamaduni, ukihusishwa na kampeni za kitaifa kama vile vita dhidi ya malaria, ujenzi...
  13. Stephano Mgendanyi

    Mwenge wa Uhuru Wazindua Miradi Mingi Busokelo, Rungwe

    MBUNGE ATUPELE MWAKIBETE ASHIRIKI MBIO ZA MWENGE WA UHURU BUSOKELO, MIRADI MINGI YAZINDULIWA Mbunge Jimbo la Busokelo, Mhe. Atupele Fredy Mwakibete ameungana na Viongozi mbalimbali kushiriki mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ambao tarehe 29/08/2024 umekimbizwa Halmashauri ya Busokelo, Wilaya ya...
  14. Stephano Mgendanyi

    Mwenge wa Uhuru Musoma Vijijini Wazindua Miradi ya Bilioni 3.5

    MWENGE WA UHURU MUSOMA VIJIJINI: MIRADI YA THAMANI YA TSH 3.5 BILIONI YAKAGULIWA NA KUKUBALIKA Mwenge wa Uhuru ulipokelewa kwa shangwe nyingi mno kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) yenye Jimbo la Musoma Vijijini. Hiyo ilikuwa juzi, Jumatano, 31.7.2024 Miradi yote 7 ilikaguliwa...
  15. Lanlady

    Mwenge wa uhuru utafutiwe nishati mbadala ya kuuwezesha kuwaka badala ya kutumia mafuta ya taa na utambi unaotoa moshi

    Bila shaka kichwa cha habari kinajieleza vizuri sana. Binafsi sina tatizo na falsafa ya uanzishwaji wa mbio za mwenge wa uhuru. Tatizo langu kubwa ni namna wanavyoweza kuathiri afya za wanaoukimbiza. Nishati inayotumika sio rafiki kwa afya za wanaoukimbiza na hata walio karibu nao mahali...
  16. figganigga

    Kwanini Mkoa wa Mara wana Mwenge wao Tofauti na Mwenge wa Uhuru?

    Mkuu wa Mkoa wa Mara amewakaribisha viongozi, watendaji na wananchi wote kushiriki katika maadhimisho ya miaka 60 ya Mwenge wa Mwitongo yatakayofanyika nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwitongo tarehe 1 Agosti, 2024. Mwenge wa Mwitongo ni mwenge wa Kabila la Wazanaki...
  17. Mohamed Said

    Mwenge wa Uhuru na Kitabu Cha Mwenge wa Uhuru ("The Torch on Kilimanjaro") Cha Oxford University Press

    MWENGE WA UHURU NA KITABU CHA WATOTO CHA MWENGE WA UHURU ("THE TORCH ON KILIMANJARO") Mwaka wa 2007 Oxford University Press (OUP), Nairobi walianzisha mradi wa kusomesha Kiingereza na historia pamoja kwa shule za msingi Afrika ya Mashariki. Nia yao ikiwa wanafunzi wa shule za msingi katika...
  18. Stephano Mgendanyi

    Mwenge wa Uhuru 2024 Wilaya ya Ludewa

    Mwenge wa Uhuru 2024 umewasili Mkoani Njombe, na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva- Mwenge wa Uhuru kukimbizwa Wilayani Ludewa Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa kwa Umbali wa Kilometa 93 Wilayani Ludewa; ukipitia Miradi 7 yenye...
  19. uran

    Huu Mwenge usiwe unakimbizwa Dar es Salaam, unatuchosha na kutupotezea muda

    Imagine kwa muda wa karibia 2 hours sasa tuko kwenye foleni kupisha Mwenge. In this Millennium tunapotezeana muda kiasi hichi kisa Mwenge! Disappointment ya hali ya juu. Wakazi wa Kigamboni tunaotumia daraja kwenda mjini, Muda huu usijaribu. Bora ukapange foleni kwenye kivuko. Its worse
  20. B

    Hai, Kilimanjaro: Vurugu kubwa kwenye tukio la Mwenge, wananchi wadai kuporwa ardhi na mamlaka ya Bonde la mto Pangani

    MWENGE WA UHURU UNAOSEMEKANA UMILIKE PALE PASIPO NA HAKI, LEO 2024 KWA ZUKA TAFRANI YA HAKI Wananchi hao vijiji vya wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro wadai ardhi yao kuporwa na mamlaka ya Bonde la Pangani, hivyo walikuja na mabango kuonesha kero wanayopitia lakini mabango yao yalikumbana nguvu...
Back
Top Bottom