Recent content by Mawele

  1. M

    UZUSHI Watu wenye Damu kundi B hawatakiwi kula kuku

    Nimesoma habari huko mtandaoni nimepata mtatiziko kidogo baada ya mwandishi kuandika watu wenye group B msile kuku, na wakati mimi kuku ndio moja ya kitoweo changu pendwa sana. Msaada hapo wa kuhakiki taarifa hii iwapo ni kweli kuku si salama kwa wenye damu group B
  2. M

    Sasa ni dhahiri kuna chama kilishaanza kampeni isiyo rasmi ya uchaguzi Mkuu 2025

    Kuna chama kilishaanza kampeni isiyo rasmi ya uchaguzi Mkuu 2025, huhitaji kuwaza kujua kuwa hii ni kampeni ya kum-"brand" mgombea wao na kujibrand wao wenyewe ili majina yao yatajwe kila siku na watu lakini pia wakumbukwe kuwa wapo kama walisahaulika. Kubwa zaidi ni kumuuza kwa lazima mgombea...
  3. M

    Daladala zilizochoka mpaka kuegemea upande mmoja zinahatarisha usalama wa abiria, kwanini zinaendelea kutumika?

    Umewahi kukutana na daladala imejaza abiria halafu upande mmoja unakuwa umeelewa utafikiri inataka kuanguka? Sijui nini kinasababisha hali hiyo na sina hakika iwapo hiyo ni salama kwa abiria, maana huwa nawaza likiyumba kidogo tu huenda likabinuka na kusababisha ajali. Kwanini magri haya...
  4. M

    Kwani Zanzibar wanawachukuliaje watu wa Bara?

    Video hii inaonesha mtu akichapwa fimbo huku akiambiwa "Hapa si bara" sababu za kuchapwa eti ni kwa kuwa amekula mchana chakula wakati wa Ramadhani. Hivi Zanzibar, mnawachukuliaje watu wa bara? Ni watu baki au ni watu wasio na haki ya kukaa Zanzibar? Maana hapo ni ubaguzi wa wazi, kupanda mbegu...
  5. M

    Mamba huyu mamba gani, mbona hawezi kung'ata?

    Kama si mamba mjusi, hatufai abadani, Anitia wasiwasi, kaziye ya kazi gani, Anamaliza ukwasi, wa kumtunza majini, Mjusi kafata nini, Nasi tulitaka mamba. Anaucheza mchezo, wenye swali lisojibu Anipatia mawazo, yupi wa kumuadhibu Kushindwa kazi ni kwazo, kwa tulompa wajibu. Mjusi kafata nini...
  6. M

    Mamba huyu mamba gani, mbona hawezi kung'ata?

    Ni kubwa sana kiumbo, ikiwa kwenye hadhira, Ni Mamba kama wa Mombo, Sema ye hana madhara, Yakichambuliwa mambo, yatakutia hasira, Mamba huyu mamba gani, mbona hawezi kung'ata? Hukaa kimya majini, hutoka mwingine mwaka. Huletwa vingi vitini, kusoma walo potoka, Vinasomwa kwa makini, imara bila...
  7. M

    Kwanini asisifiwe Mwananchi anayelipa kodi inayotekeleza miradi ya kitaifa?

    Umejengwa utamaduni wa ajabu kwa kutoa Sifa kwa viongozi wa kisiasa wanaposimamia utekelezwaji wa miradi ya kitaifa, na kusahaulika Mwananchi ambaye ndiye aliyemwaga jasho kutafuta pesa na kuipa kodi kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo. Sifa hizo kwa sasa zimeenda mbali zaidi kusifia hata pale...
  8. M

    KERO Ukilipia kuingia Magufuli stendi wanarudisha chenji nusu kwa kigezo cha "hatuna chenji"

    Ni mchezo mchafu wa wanaotoza hela kwa wanaotaka kuingia Magufuli stendi, ni mara kadhaa kila nikifika pale ukiwa na sh. 500 au 1000 nk watakwambia hawana shilini 100 au 200. Mara nyingi wanafaya mchezo huo wakati kukiwa na msongamano wa foleni wanakwambia uchukue chenji nusu au wakurudishie...
  9. M

    KWELI Vidonda vya tumbo(Ulcers) huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia mate au kinyesi

    Leo nimesoma mtandaoni kuwa Vidonda vya tumbo(Ulcers) huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Naomba kujua kama ni kweli maana siku zote mie najua vidonda vya tumbo huvipata mtu kutokana na mtindo wake wa maisha(kutokula) au kwa kutumia baadhi ya dawa ambazo zinaweza...
  10. M

    SI KWELI Mzazi akipata mimba wakati bado ananyonyesha hudhoofisha afya ya mtoto anayenyonya

    Lengo la post ni kuonesha ukweli kuwa hakuna madhara mtoto akinyonya kama ambavyo wengi walikuwa wanadai sijui mtoto anadhoofu ikiwemo kuharisha na walikuwa wanamtaka mama kumwachishwa mtoto kunyonya iwapo mama kabeba mimba bila kukusudia wakati akinyonyesha. Japo ni kweli kwa ajili ya afya ya...
  11. M

    DOKEZO Serikali, elezeni ukweli kuwa watoto chini ya miaka 5 wanalipia huduma, kama sivyo kituo cha afya Kimara wawajibishwe kwa kutoza pesa na huduma mbovu

    Mambo ya siasa yananihusu na naifatilia, kuhusu kuhoji hicho ulichosema nadhani tukutane kwenye hoja husika inayohusika na saa hiyo na si hapa panapojadiliwa kuhusu wajibu wa Serikali kutekeleza sera zake
  12. M

    DOKEZO Serikali, elezeni ukweli kuwa watoto chini ya miaka 5 wanalipia huduma, kama sivyo kituo cha afya Kimara wawajibishwe kwa kutoza pesa na huduma mbovu

    Hawana ufahamu kabisa, hawatambui wana haki na wajibu wa kuihoji Serikali pale ambapo inaahidi vitu ambavyo havitekelezwi.
  13. M

    DOKEZO Serikali, elezeni ukweli kuwa watoto chini ya miaka 5 wanalipia huduma, kama sivyo kituo cha afya Kimara wawajibishwe kwa kutoza pesa na huduma mbovu

    Tumia akili yako kidogo kuona kilichokusudiwa, lengo ni waseme kwa nini wanadanganya na hawaelezi ukweli
Back
Top Bottom