Zitto Kabwe asema Kikwete alimwambia CCM hakina muda mrefu madarakani na kumshauri abaki upinzani. Aliahidiwa uwaziri wa fedha iwapo angejiunga CCM

Zitto Kabwe amesema mwaka 2012 alipata changamoto chama chake cha wakati huo cha CHADEMA akidai ilikuwa juhudi ya kumzuia kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Zitto amesema kulikuwa na makubaliano baada ya kugombea uchaguzi wa nyuma yake kwamba amuachie kijiti Freeman Mbowe na atampokea miaka mitano ijayo na badala yake miaka miwili kabla aliondolewa nyazifa zote za uongozi Chadema na wapo katika kundi lao walisema waende CCM.

Zitto Kabwe amesema Jakaya Kikwete alimuita na kumwambia ana machaguo mawili kwa kuwa alikuwa anachipukia kwenye siasa, kwanza kujiunga na chama tawala cha CCM na endapo angefanya hivyo angempa uwaziri wa fedha siku inayofata.

Rais mstaafu Kikwete alimpa angalizo Zitto Kabwe kwamba kwa maono yake CCM haitakuwepo madarakani muda mrefu ilhali Zitto bado kijana mdogo na kumshauri kutafuta jukwaa lingine lakini sio la chama tawala.

Zitto amesema kwenye hicho kikao mmoja wa waliokuwepo ni rafiki yake Deo Fulikunjombe naye akamshauri asiende CCM.

Mtasema mengi
 
Zitto siyo wa kumwamini hata kidogo!

Once a traitor always a traitor!

Screenshot_20240213_074126_Gallery.jpg

Screenshot_20240428_081610_Samsung Internet.jpg
 
Zitto sio wa kumuamini saana maneno yake
CCM miaka yote inahonga vyeo kuvutia wapinzani. Kina Gekul, Patrobas, Kitila, Mollel, Shonza, Waitara n.k wote walipewa uwazir au unaibu waziri walipohamia CCM!! so sishangai kama zitto aliahidiwa pia
 
So baada ya Zitto kuamua kwenda upinzani ndio akaelekea Chadema, baadae ndio akaanza kutumiwa na Kikwete kukivuruga Chadema kwa mikutano yao ya usiku akiulizwa akasema Kikwete ni sawa na baba yake..
Lema alimpigia mzee kikwete kuhusu kurudi nyumbani
 
Hili la Zitto kutumika na Kikwete hakuna asiyelifahamu na ndio maana alitimuliwa Chadema mapema sana , Hata Mahakamani alikuwa analindwa na Walinzi waliolipwa na Kikwete , nani amesahau ?
Utasema uliziona hizo pay slip za kikwete kwa hao walinzi,chakubimbi Sana wewe
 
Zitto Kabwe amesema mwaka 2012 alipata changamoto chama chake cha wakati huo cha CHADEMA akidai ilikuwa juhudi ya kumzuia kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Zitto amesema kulikuwa na makubaliano baada ya kugombea uchaguzi wa nyuma yake kwamba amuachie kijiti Freeman Mbowe na atampokea miaka mitano ijayo na badala yake miaka miwili kabla aliondolewa nyazifa zote za uongozi Chadema na wapo katika kundi lao walisema waende CCM.

Zitto Kabwe amesema Jakaya Kikwete alimuita na kumwambia ana machaguo mawili kwa kuwa alikuwa anachipukia kwenye siasa, kwanza kujiunga na chama tawala cha CCM na endapo angefanya hivyo angempa uwaziri wa fedha siku inayofata.

Rais mstaafu Kikwete alimpa angalizo Zitto Kabwe kwamba kwa maono yake CCM haitakuwepo madarakani muda mrefu ilhali Zitto bado kijana mdogo na kumshauri kutafuta jukwaa lingine lakini sio la chama tawala.

Zitto amesema kwenye hicho kikao mmoja wa waliokuwepo ni rafiki yake Deo Fulikunjombe naye akamshauri asiende CCM.

Kichwa cha habari hakivutii kuendelea kusoma.
Yaani chama kitakufa lakini akaahidiwa uwaziri kama angejiunga nacho.!
 
Unakwenda Chama fulani sababu ya itikadi / ideology yako inaendana na hicho Chama au unakwenda sababu ni Platform ya wewe kupata Kula ?

Hizi siasa ni maigizo tu kwa taxpayers expense....
 
Back
Top Bottom