Zawadi Mkweru: Elimu ya matumizi sahihi ya mitandao ianzie shuleni

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,865
4,693


Zawadi Mkweru, mtumishi wa Jamiiforums, leo ikiwa siku ya wanawake Duniani yupo Mbashara EATV akizungumzia masuala mbalimbali kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao ya jamii.

Katika mjadala huo Zawadi anafafanua umuhimu wa Elimu ya matumizi sahihi na salama ya mitandao kuanza kutolewa kwa watoto tangu wakiwa shuleni ili watoto hao wasidhurike pindi wanapofikia ngazi za elimu ya juu.

Zawadi anasema, Tunahitaji kuwa na elimu itolewe kuhusu masuala ya matumizi sahihi ya mitandao na nadhani inatakiwa kuanzia tukiwa shuleni yaani tusimkurupue mtu kwa kuja kumpa smartphone. Hata nyumbani wazazi siku hizi tumekuwa wakisasa zaidi, tunawapa watoto simu mapema.

Kwahiyo mzazi hata kama imetokea umempa mwanao simu kutumia kusoma, tenolojia imekua, inaruhusu kuset time. Unaweza ukaweka utaratibu kwamba huyu mtoto kwa siku hii simu ataitumia kwa saa mbili tu na baada ya hapo hatoweza kufanya kitu kingine.

Mzazi fuatilia mtoto wako anaangalia nini mtandaoni, kitu gni anautana nacho kwenye hicho kifaa chake cha kielektroniki. Shuleni tutoe elimu kuhusu matumizi sahihi ya hivi vifaa vya kidijitali na matumizi sahihi ya mtandao ya kijamii.

Mitandao ya kijamii ina kanuni zake na sheria zake ambazo naamini wengi wetu hatusomi kwa sababu ya urefu na lugha inayotumika. Hujui kwamba unapoweka kitu chako hujui ni taarifa zako zipi zinachukuliwa. Ukienda Facebook unaweza kuchagua unataka nani aone picha zako na nani asione. Instagram pia siku hizi unaweza ukatumia ombi la kumfuata mtu, kabla ya kumfata mtu tazama maudhui yake kwanza.

Usimfollow kila mtu kwa sababu ya options ambazo zimepopo up tu kwenye simu yako. Kuna watu wanakosa kazi sababu ya kurasa zao mitandaoni na kuna watu wanapata kazi sababu ya kurasa zao za mitandaoni. Inabidi ujue future yako umefocus wapi. Mitandao ya kijamii inakutambulisha.

Mfano wanaoweka Whatsapp status unaweza kujua kitu ambacho mtu amekutana nacho ikiwa cha furaha, huzuni au hata kama anarusha kijembe kwa mwingine. Kwahiyp, unatakiwa ujue kwamba mitandao kwa siku hizi ni sehemu ya maisha inakutambulisha. Kabla ya kupost chochote kwenye mtandao wa kijamii jiulize kimetoka wapi? Kilipotoka panaaminika? Unaweka kwa sababu gani? Na uko tayari kuyaishi matokeo ya hiyo post unayoiweka? kama upo tayari basi unapublish kwa ajili ya watu.

Teknolojia haisahau, kuna vitu vingi vimepita au vimefutwa lakini ukikaa ukitulia ukavitafuta unaweza kuvipata. Kwahiyo, ni kuwa makini na nini unaweka mtandaoni. Kwahiyo elimu itolewe kwa watu.
 
Back
Top Bottom