Zamani ukitembelea nyumbani kwa mtu unapewa albamu ya picha uangalie, siku hizi unapewa nini?

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
424
1,051
Hizi mambo za kupewa albamu kuangalia picha za wenyeji wako hivi bado zipo kweli ndugu zangu? Wewe ukienda kutembelea ndugu, jamaa na marafiki ukifika wanakupa nini au wewe ukitembelewa huwa unawapa nini?
 
Siku hizi pombe bange na out za kutafuta malaya...
Watoto wadogo wanataka hela waende disko toto au michezo gani sijui roulette
 
Siku hz hqkuna kutembeleana, zamani, kabla hata, simu za mkononi, unaibuka kwa ndugu yako, upo na watoto, mke, manpokewa kwa furaha, watoto mnagonga vyoda,wazazi,wana piga story, unatambulishwa kwa ndugu zako, freeesh tu, siku hz, tunakutanishwa na misiba, harusi,
 
Siku hizi mgeni ukifika wewe ndio unaomba chaja au kuwauliza wenyeji wako kama wana page za Instagram, mambo ya albamu za picha zilipendwa
 
Inategemea na sehemu na umuhimu wa mgeni, kwingine unapata password ya wifi hotspot kisha kila mtu anakamata simu yake, mpaka muda wa kula.
 
siku hizi ukienda kwa mtu unachopokelewa nacho ni sababu iliyokuleta na lini utaondoka na nilazima uende na kiroba cha mahindi na vitoto vy wenyeji havina adabu uzungu mwingi bora ukalishe kwenu kuliko kumtembeleq mtu siku hizi
 
Unapewa charger ya smartphone soda/bia/maji unawashiwa TV Kisha Kila mtu anakuwa busy na simu yake
 
Back
Top Bottom