Yawezekana Mkataba huu wa DP World ni malipo (Retribution) ya Waarabu dhidi ya Tanganyika kuikalia Zanzibar?

The Shah of Tanganyika

JF-Expert Member
Jul 2, 2023
602
1,571
Nimesoma na kusikiliza hoja nyingi zilizojaa hisia kali juu ya hili sakata la DP World ya Uarabuni (Imarati ya Dubai) kukabidhiwa bandari zote za bahari, maziwa, mito na hata nchi kavu, alimradi imehusiana na bandari. Ni mambo ya ajabu sana ukitulia na kusoma kwa kutafakari.

Lakini jambo linalojiyokeza kwa namna ya pekee ni kuwa kuna viashiria vya wazi kuwa kuna kikundi cha Wazanzibari walioamua kuzikabidhi bandari zote na vivutio vyote vya kiuchumi vya Tanganyika kwa kampuni moja ya Waarabu kwa mkataba wa milele na usiovunjika kwa namna yoyote ile mpaka pale Masiha atakaporejea kuuhukumu Ulimwengu.

Yawezekana kuna kikundi kilichochukizwa na madhila yote ya huu Muungano wetu ambao una sura ya ukoloni wa Taifa moja (Tanganyika) dhidi ya taifa lingine (Zanzibar). Hili siyo langu la kuzusha bali ni mtazamo uliopo mpaka leo na ambao umesababisha hasara kubwa na mauaji huko kwenye koloni la Tanganyika.

Mungu si Adhumani, kawapa wale wale wa kuuliwa na kuteswa na kutawaliwa, kawapa bahati ya mtende nao washike kwenye mpini (Astaqafirullah). Sasa watakaa kwa kutulia bila kulipiza kisasi cha maumivu na roho zilizoangamizwa za ndugu zao?

Kuendesha mauaji Tanganyika siyo jambo linalowezekana kwa haraka. Lakini kuifunga Tanganyika kwenye minyororo ya utumwa wa milele, hilo linawezekana kwa kuwatumia haohao watanganyika.

Basi na mimi nisizunguke mbuyu sana, bali nihitimishe kwa kusema kuwa yawezekana hii ni hujuma na kulipiza kisasi dhidi ya hila ya Mtanganyika ya kuipora mali halali ya mwarabu (Zanzibar).

Usiniulize kwanini nimewaza hivy bali wewe kwanini hukuwaza kama mimi nilivyowaza.
 
Kuna watu huwa wanasema kwa wizi huu bora mkoloni arudi

Hakuna nidhamu makazini, customer care zero, uadilifu ndio usiseme
Kama sisi wenyewe hata kusimamia kitu bila kuiba hatuwezi? Sasa leteni suluhu

Wengine wanasema tumechelewa na hatupigi hatua za maendeleo kwa sababu ya wachache
Naona ifike mahali tuambiane ukweli kuwa hatuwezi
 
Back
Top Bottom