Yajue maneno ya kibiashara na maana zake

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
459
643
BOOKKEEPING TERMS.

Tumesema bookkeeping sio kwaajili ya wafanya biashara tu, hata mtu binafsi anaweza kuweka rekodi zake kutokana na shughuli zake za kila siku.

Sasa kuna maneno madogo dogo ya msingi ambayo yanatumika sana na wahasibu.

1. ACCOUNTING PERIOD

Hiki ni kipindi ambacho kampuni au mtu binafsi hupitia report zake za kifedha ambazo zitamsadia kujua mzunguko wa pesa zake.

Kwenye Management Accounting hiki kipindi hufanywa kila mwisho wa mwezi au baada ya miezi mitatu, inategemea na office.

Kwenye Financial Accounting hiki kipindi hufanyika kila baada ya miezi 12.

Ni muhimu kwasababu kadri mda unavyokwenda unajua shughuli zako zipo katika muelekeo gani, kwahiyo usipokuwa unafatilia ni ngumu kujua biashara zako zina mtaji kiasi gani, zinaitaji investment kiasi gani, matumizi gani upunguze au uongeze nk.

2. ACCOUNTS PAYABLE/DEBTS/ LIABILITIES

Haya ni madeni ya biashara.

Ukiwa unaanda balance sheet yako basi madeni hurekodiwa kwenye liabilities za biashara.

3. ACCOUNTS RECEIVABLES

Hapa ni pesa ambazo biashara inadai wateja wake, wateja walionunua bidhaa kwa mkopo.

Ukiwa unaanda balance sheer basi hurekodiwa kwenye current assets za biashara.

4. ASSET

Hivi ni vitu ambavyo biashara inamiliki na ikiamini kwamba vitazalisha pesa katika biashara.

_Fixed Asset

Hizi ni mali za biashara ambazo ni za kudumu kama majengo, vifaa nk

_Current Asset

Hizi ni mali za biashara ambazo hutegemewa kuuzwa au kutumika baada ya mwaka mmoja kama stock ya bidhaa za kuuzwa na kampuni.

_Liquid Asset

Hizi ni mali za biashara ambazo zinaweza kubadilishwa kuwa fedha kirahisi kama pesa zilizowekwa kwenye bond, bank nk.

_Prepaid Expenses

Biahara inapolipa matumizi yake kwa miezi ijayo basi hii ni asset, mfano biashara ikilipa kodi ya mwaka mzima hii ni asset.

_Intangible Asset

Hizi ni mali ambazo huwezi kuzishika kama copyright, trademark nk

5.ARREARS/ OVERDUE/UNPAID

Haya ni madeni ya biashara ambayo mda wake wakulipa umeshapita.

Mfano: Ukipanga nyumba lakini usilipe unapoanza kukaa , ukaja kulipa mwisho wa mwezi hiyo tunaita Arrears au Overdue payment.

Hata mfanyakazi kulipwa mwisho wa mwezi baada ya kufanya kazi mwezi mzima ni payment in Arrears.

6. ACCRUALS

Ni kitendo cha biashara kurecord kitu bila kupata pesa au kutoa pesa.

_Accrued Revenues

Hapa biashara hurekodi pesa ambazo imepata kutokana na mauzo, au kutoa huduma kwa wateja ila bado haijapokea pesa zake.

Kitendo hiki kitaongeza Account Receivables za biashara.

_Accrued Expenses

Hapa ni vitu ambavyo vimerekodiwa kuwa vilitumika katika biashara japo havijalipiwa bado.

Arrears zinaingia hapa pia.
7. BALANCE SHEET/ STATEMENT OF FINANCIAL POSITION

Hii ni moja wapo katika zile financial statements ambayo inaeleza biashara inamiliki nini na inadaiwa nini.

Kama tunavyofanya check up kujua hali ya afya zetu basi ndio balance sheet katika biashara.

Hesabu ya Balance Sheet ni

ASSET= LIABILITY + EQUITY

_Asset tumesema ni mali zinazomilikiwa na biashara.

_Liability ni madeni ya biashara.

_Equity ni vile vitu vya kwako ambavyo umeanza navyo katika biashara sio vya kukopa.

Kwa maana nyengine hata madeni nayo ni Asset, hapa ndio maana wanashauri ukikopa ni kheri kutumia huo mkopo katika biashara maana utakuzalishia faida kuliko kutumia kwaajili ya matumizi yako binafsi.

8. BANK RECONCILIATION

Hapa ni kitendo cha kukagua mahesabu yako ya pesa zilizopo bank kama zinaendana na balance ya kwenye record zako.

Kwahiyo utatakiwa kuchukua bank statement na kuangalia vipi ambavyo bado bank hawajarekodi na wewe kipi ambacho hujarekodi ila bank wamerekodi ili balance zifanane.

9. BILLING

Hiki ni kitendo cha mfanyabiashara kumtumia invoice mteja wake ambaye amenunua bidhaa kwake kumkumbusha kuhusu malipo.

Kwahiyo mteja ndio anapokea BILL na mfanyabiashara anatoa INVOICE.

Billing ni katika process za Account receivables.

10. BUDGET

Hapa ni makadirio ya shillingi ngapi biashara itaingiza na shillingi ngapi zitakazotumika kwa muda husika mara nying huwa kipindi cha mwaka 1.

11. BOOKKEEPING

Ni kitendo cha kurekodi mahesabu yote yanayofanyika katika biashara, rekodi zote za shughuli za kifedha zinazofanyika katika biashara au kwa mtu binafsi.

12. CAPITAL

Huu ni mtaji wa biashara, pesa au vitu ambavyo vinaweza kufanya biashara iendelee kuzalisha.

13. CASH FLOW

Hapa ni rekodi ya pesa zinazoingia na zinazotoka kwenye biashara.

Net Cashflow ni jumla ya pesa zote ambazo biashara imezalisha au imepokea.

14. CERTIFIED PUBLIC ACCOUNTANT (CPA)

Hawa ni wahasibu ambao wamekidhi vigezo vya kuwa katika chama cha wahasibu kwa kufaulu mitihani iliyoandaliwa kuwapima ili wawe katika kundi hilo la wahasibu.

15. CHART OF ACCOUNTS

Hii ni list ya shughuli zote za kibiashara zinazofanywa na kampuni, zimewekwa kimakundi ili kurahisisha ufatiliaji wa kila shughuli.

Huanza kutaja vipengele zilivyopo kwenye balance sheet vikifatiwa na vipengele vilivyopo kwenye Income Statement.

Huelezea Asset za biashara, Liabilities za Biashara, Equity, Income, Expenses nk.

16. CLOSING BALANCE

Hiki ni kiwango cha pesa ambayo hubaki baada ya kufunga mahesabu yako kwa kipindi flani, kama ni mwisho wa mwezi au mwisho wa mwaka.

17. CREDITORS

Wanaodai biashara, watu ambao uliwakopa.

18. COST OF GOODS SOLD

Hizi ni gharama za mauzo.

Hesabu yake ni

Beggining Inventory + Purchases - Ending Inventory

Kwa kiswahili ni bidhaa ulizoanzia nazo biashara + manunuzi uliyoyafanya katika biashara - bidhaa zilizobaki katika biashara

19. CREDIT

Ni uwezo wa kukopa bidhaa ukiahidi utalipa badae.

Kitu ambacho kinaongeza madeni au ambacho kinapunguza Asset za biashara.
20. DEBTORS

Mtu aliyekopa bidhaa au pesa basi huyu ndio Debtor.

21. DEBIT

Hizi ni shughuli ambazo zitaongeza pesa upande wa Asset, au kitapunguza madeni ya biashara.

Japo kwenye mabenki pesa ikiwa debited ina maana pesa imepungua kwenye account yako.

Kama ukienda ku withdraw pesa basi bank ita debit kile kiasi cha pesa unachokichukua.

22. DEPRECIATION

Jinsi gani mali yako imeshuka thamani.

Mfano:

Ulinunua gari 2021 kwa lengo la kulifanyia biashara ya Uber. Ulinunua IST yako shillingi milllion 12.

Una mpango wa kuifanyia kazi miaka 6.

Ukaipigia kila mwaka ita depreciate kwa million 2, ina maana mpaka mwaka 2027 litakuwa na thamani 0.

Japo,

Hilo IST lako ukapanga ikifika mwaka wa 5, utaliuza kwa thamani ya shillingi million 2.

Ina maana tukitumia Straigh line Depreciation method

Annual depreciation expense= (Asset - Residual cost)/ useful life on an asset

Kwa kiswahili kirahisi ni

Gharama za depreciation = (bei ya gari - gharama utakayouza gari baada ya miaka 5) / miaka 5

Gharama za depreciation = (12,000,000 - 2,000,000) / 5

Gharama za depreciation = 10,000,000/ 5

Gharama za depreciation = 2,000,0000

Ina maana kila mwaka thamani ya gari yako itashuka kwa kiasi cha Shilllingi milllion 2.

Kwenye Balance Sheet, depreciation itarekodiwa upande wa Asset kuonyesha kushuka kwa thamani ya Asset.

Inarekodiwa kama Accumulated Depreciation ambayo ikitolewa kwenye original amount ya Asset kinachobaki kinaitwa BOOK VALUE.

Kwa kutumia mfano wetu wa IST mwaka 2022 kwenye Balance Sheet itakuwa itakuwa hivi:

Cost of Asset 12,000,000

Less: Accumulate depreciation 2,000,0000

Book value 10,000,000

Kwenye Income Statement, depreciation hurekodiwa pamoja na expenses nyengine mara nyingi ni kwa mwaka.

Depreciation ipo complicated kidogo, tutaielezea kiundani badae.

23. DIVIDEND

Ukiwekeza kwenye kampuni, na kampuni ikaanza kupata faida basi lile gawio ambalo muwekazaji hupewa ambalo ni katika faida zilizopatikana ndio tunaita Dividend.

Mfano:

UTT ukiwekeza kwenye Bond Account kiasi cha Shillingi Million 5 basi kila mwezi utapewa Dividend za Shillingi 50,000.

24. DIVERSIFICATION

Hiki ni kile kitendo cha kutokuweka mayai yote kwenye beseni moja.

Kitendo cha kuamua kuwekeza pesa yako kwenye miradi tofauti ili kupunguza kupata hasara kwa pamoja kama mambo yakifeli.

25. DEDUCTIBLE

Haya ni matumizi ya biashara ambayo yanapunguza faida kwenye biashara.

26. DOUBLE ENTRY

Hii ni principle ya biashara ambayo inasema kwa kila pesa iliyorekodiwa upande wa Debit basi lazima irekodiwe upande wa Credit and vice versa.

Mfano:

Umenunua IST million 12.

Inamaana Cash imetoa 12,000,000 (CREDIT)

IST Car imepokea 12,000,000 (DEBIT)
27. EQUITY

Hii ni balance inayobakia baada ya kulipa madeni yako na kuuza mali za kampuni.

EQUITY = ASSET - LIABILITIES

Hiki ni kile kiasi ambacho wewe umewekeza kwenye biashara, au watu wengine walichowekeza kwenye biashara yako.

28. EXPENSES

Hizi ni gharama zinazotumika kuendesha biashara.

Kama mnavyokumbuka kuna fixed na variable cost.

29. FINANCIAL STATEMENTS.

Hizi ni ripoti ambazo huandaliwa na muhasibu wa kampuni ili kuelezea maendeleo ya biashara, biashara inatakiwa kulipa kodi kiasi gani,nk

30. FACTORING

Hiki ni kitendo cha biashara kuuza madeni yake kwa mtu mwengine kwa bei ya chini.

Mfano:

Una mdai mtu laki 5 ila anakusumbua kulipa, unaamua kumuuzia mtu huyo mdaiwa wako kwa 450,000.

Kwahiyo wewe unakuwa umepokea 450,000, na yule uliyemuuzia ataenda kudai 500,000 yako uliyokuwa unaidai.

31. GROSS PROFIT/SALES PROFIT/ GROSS INCOME

Hii hupatikana kwa kuchukua mauzo (sales) toa gharama za mauzo (cost of goods sold)

32. GROSS MARGIN

Tunaweza sema ni gross profit in percentage.

Hii hupatikana kwa kuchukua gross profit/revenue x 100%

Gross margin hutumika na ma manager kuandaa promotion, kujua bei za bidhaa nk

33.GENERAL LEDGER

Hapa utakuta kila aina ya shughuli ya kifedha imerekodiwa vizuri kwaajili ya kutengeneza financial statements.

Kutengeneza general ledger ni lazima utumie double entry.

34. INCOME STATEMENT/PROFIT AND LOSS STATEMENT

Hii ni ripoti ya kampuni inayoonyesha mapato na matumizi kwa kipindi flani.

Hutumika na wawekezaji kujua kama kampuni inapata faida ama hasara.

35. INVENTORY

Hapa ni vitu ambavyo mfanyabiashara anavimiliki kwaajili ya kuuza au kutengenezea bidhaa yake ambayo anaiuza.

Haishauri Inventory kuwa kubwa sana kuepuka ikitokea vikapitwa na wakati ina maana atauza kwa hasara, pia kuharibika ,na pia gharama za kutunza hizo bidhaa kwa mda mrefu huwa kubwa.

36 .INTERIM REPORTS

Hizi ni zile ripoti ambazo hutengenezwa chini ya mwaka mmoja, labla baada ya mwezi, miezi 3 ama miezi 6.

Hizi ripoti husaidia wawekezaji, wakopeshaji, na mwenye biashara kujua kampuni inaendeleaje.

37. JOURNAL ENTRY

Bookkeepers hutumia journal kurekodi matukio ya kifedha ya kila siku.

Hapa ni kurekodi muamala wako ulikuwa unahusu nini, ni tarehe ngapi, kiasi gani, ni upo upande wa Debit ama credit.

38. LIABILITIES

Haya ni madeni ya biashara.

Kama biashara ilinunua vitu bila kulipa, ilichukua mkopo wa aina yoyote tunaita liabilities.

Kuna short term liabilities, haya ni madeni ambayo yapo chini ya mwaka mmoja.

Long term liabilities, haya ni madeni yaliyozidi mwaka mmoja.

39. LIQUIDITY

Kitendo cha kuweza kubadilisha mali yako kiuharaka kukupa pesa.

40. LOSS

Hii ni kitendo cha matumizi kuwa makubwa kuzidi mapato yanayopatikana katika biashara.
41. MARGIN

Ni ile faida unayoipata katika uuzaji wa bidhaa.

Mfano:

Umenunua gauni kwa shillling 20,000 ukafika nyumbani mtu akalipenda akakwambia umuuzie wa shilling 30,000.

Inamaana 10,000 ndio margin yako.

42. NET INCOME/NET EARNINGS

Hii ni balance ambayo kampuni hupata baada ya kutoa matumizi yote na kodi zote kutoka kwenye gross profit ya biashara.

Hii hutumika kujua kampuni inauwezo wa kukopeshwa kwa kiasi gani.

43. OPENING BALANCE.

Hii ni rekodi ya vitu ambavyo unaanzia navyo mwaka kutoka mwaka uliopita wa biashara.

44. OVERHEADS

Hizi ni gharama zinazotumika kuendesha biashara, sio lazima ziwe zinatumika katika kutengeneza bidhaa ila zinahitajika ili mauzo yaweze kufanyika au biashara iweze kufanyika.

Ni muhimu muuzaji kupigia mahesabu ya overheads katika upangaji wa bei pia kuyaweka kwenye budget zake.

Kama insurance nk

45. ON CREDIT/ ON ACCOUNT.

Kama mtu kununua bidhaa kutumia credit card, ni makubaliano ya mteja kulipa pesa badae.

46. PAYROLL

Huu ni mchakato unaotumika kulipa wafanyakazi wa kampuni husika, kulingana na masaa waliyofanya kazi, taarifa zao za mafao, bima, mikopo, kodi nk

47. PETTY CASH

Tunaweza sema pocket money ili iwe rahisi kuelewa, hiki ni kiasi cha pesa ambacho kampuni hukitenga pembeni kwaajili ya matumizi madogo madogo ya office.

48. PURCHASE.

Hiki ni kitendo cha mfanyabiashara kununua vitu kwa lengo la kuviuza tena ili aweze kupata faida.

49.PRESENT VALUE.

Thamani ya pesa leo huongezeka kadri siku zinavyozidi kuongezeka .

Present value ni kupigia hesabu kuwa thamani ya pesa leo kwa mwaka au miezi 3 mbele itakuwa kiasi gani.

Present value = Future value/ (1 + rate of return) power number of payment periods.

Mfano:

Unataka kuwa na kiasi cha million 100 baada ya miaka 10 katika bong account yako ya UTT, sasa kitendo cha kupiga hesabu sasahivi uwekeze shilling ngapi ila miaka 10 ijayo iweze kuwa million 100 ndio tunaita PRESENT VALUE.

50. RECEIPT.

Hii ni hati ya ushahidi wa mauzo au manunuzi.

51. RETAINED EARNINGS/ RETAINED SURPLUS.

Hiki ni kasi cha fedha kinachobaki baada ya kugawa Dividend kwa wawekezaji.

Uongozi wa kampuni utaamua kuendelea kufanyia kazi hizi retained earnings au wagawie wawekezaji wao.

52. RETURN ON INVESTMENT (ROI).

Tunaweza sema ni Faida ya uwekezaji.

Ni kitendo cha kuchukua thamani ya uwekezaji wako kwa sasa kutoa thamani ya mwanzo ulivyoanza kuwekeza, gawanya kwa gharama ya kuwekeza.

Mfano:

Ulinunua kiwanja kwa Shillingi million 1 ila kwasasa hiko kiwanja thamani yake ni million 11.

RETURN ON INVESTMENT =( 11M - 1M)/1M

RETURN ON INVESTMENT = 10M/1M

RETURN ON INVESTMENT = 10%

53. REVENUES.

Haya ni mapato yanayopatikana kutokana na shughuli zinazofanyika katika biashara husika.

54. SUBSISTENCE ALLOWANCE.

Hizi ni kiasi cha pesa ambacho office humpa mfanyakazi wake ambacho ni tofauti na mshahara ili aweze kujikimu kama amepata safari za ki office. Kama gharama za usafiri, gharama za chakula, gharama za sehemu ya kulala nk.

55. SINGLE ENTRY.

Hii ni kinyume cha double entry.

Huku utarekodi kitu mara moja, ila ubaya wa hii system ni rahisi kuwa na makosa kwasababu hauwezi ku match kujua kama kuna kosa lilifanyika kama kwenye double entry.

56. TRIAL BALANCE.

Hii hutengenezwa na watumiaji wa double entry ili kuangalia kama debit side ina matcha na Credit side, kabla ya kuanza kutengeneza financial statements.

57. TURNOVER.

Hapa tunapima ufanisi wa kampuni, jinsi gani kampuni inaweza kukusanya madeni yake kwa wakati, jinsi gani biashara inavyouza bidhaa zake kwa wakati mfupi.

Basically, ni jinsi gani kampuni inauwezo wa kutengeneza pesa kwa muda mfupi.

58. WRITE OFF.

Haya ni wale madeni ambayo ushayakatia tamaa, yani vichwa ngumu ambao hutarajii kama watakulipa. Umeyatoa sadaka.

Karibuni sana kuongezea vocabularies za wahasibu.
 
Back
Top Bottom