Fahamu Kuhusu Taarifa za Fedha za Biashara

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,527
5,595
Angalizo:
Andiko Hili sio ushauri wa kitaalamu na wala sio mbadala wa ushauri wa kitaalam.Maudhui yaliyomo yanatokana na uelewa binafsi wa mwandishi.Ukihitaji ushauri kuhusu wa kitaalamu unaweza onana na muhasibu au mshauri wa kodi aliyesajiliwa na mamlaka husika.

Utangulizi.
Katika biashara lengo la muwekezaji/mfanyabashara/mjasiriamali ni kutengeneza Faida.Katika kutimiza lengo hili mfanyabiashara hutumia rasilimali zake na za wengine katika kutengeneza Faida.Hivyo katika wakati wowote Mjasiriamali au mfanyabiasha huwa anatazama maeneo makubwa matatu ambayo ni Kiwango cha Rasilimali,Kiwango cha Madeni na Uwekezaji wa Mmiliki. Kwa kiingereza huwa tunakutana na maneno Assets,Liabilities na Equity.Uchaguzi wa maana ya maneno hayo unaweza kuwa Tofauti hivyo basi kwa lengo la kuondoa Utata nitatutimia Neno Assets/Rasilimali kisha nitatumia Liabilities/Madeni na Equity/Uwezo wa Mmiliki.

Uwezo wa Mmiliki(Mtaji) na Mizania ya Fedha(Balance Sheet)

Ili simulizi yetu inoge nitafikiria unapoanzisha Kampuni au biashara Mpya.Mmiliki au wamiliki huwa wanakuja na Mtaji wao tu.Mtaji wao unaweza kuwa Pesa/muda/Wazo/Rasilimali Fulani au kitu chochote ambacho unaweza kukitumia kuzalisha thamani ambayo unaweza kuiuza kutengeneza Faida.Sasa ili kurahisisha Tutasema kwamba Mmiliki ana Pesa Taslim Milioni 10.Nimechagua Pesa Kwa sababu ni rahisi kuelewa.

Punde anapoamua kwamba hii milioni 10 ni mtaji wa biashara basi itaingia kwenye Biashara na Itaende Sehemu ya Equity ambapo itakuwa ni sawa na Milioni 10 lakini pia itaingia kwenye vitabu vya Kampuni kama Pesa Taslimu ambazo ni Assets.Huu ndio Msingi wa Kanuni ya Double Entry kwa wale ambao wamesoma Uhasibu.Hivyo Basi unapoanza kampuni yako Utakuwa Hesabu zinazoonekana kama hivi hapa Chini:

Assets=10M,Liabilities =0 Equity= 10M

Kwa nini nimeweka hii Milioni 10 kwenye sehemu Mbili?Msingi ni Kanunu ya Double Entry ambayo inasema kwamba Katika Biashara yako hakikisha kwamba Mizania yako inakuwa sawa. Assets zako ziwe na uwezo wa kulipa Madeni yako yote au Assets zako ziwe sawa na Jumla ya Madeni na Uwezo wa Mmiliki. Kihasibu huwa inaandikwa hivi:

Assets = Liabilities + Equity(Owner Claim to the Business)

Kanunu ya Double entry inataka kwamba kila unapofanya kitu upande wa kushoto basi na upande wa kulia lazima ufanye kitu ili jumla ya kila upande iwe sawa.

Sasa Tuendelee.Ukiwa na Hii milioni 10 yako unaamua kununua Pikipiki zako 4 kwa ajili ya Vijana wa boda.Pikipiki moja ni Milioni 2.5 hivyo pikipiki 4 jumla ni milioni 10.Il kwa sababu una m10 tu Mo dewji anaamua kukukopesha Piki piki moja ya ziada kwa Riba ya asilimia 5 kwa mwaka mzima.Kisha unabaki na milioni 2.5 kwa ajili ya gharama za uendeshaji.

Sasa Baada ya ya kufanya manunuzi yako ya Pikipiki za Milioni 7.5 Mizania yako itakuwa hivi:

Assets zako zitakuwa sasa sio Pesa Tu bali utakuwa na

Pikipiki 4 ambazo thamani yake ni Milioni 10
Fedha Taslim ambazo zitakuwa ni Milioni 2.5

Lakini Pia Utakuwa na Madeni ambayo ni Milioni 2.5 za pikipiki moja na Uwekezaji wako utabaki ule ule wa Milioni 10.Mizania yako itakuwa kama ifuatavyo:

Assets=12.5M,Liabilities =2.5 M Equity= 10M

Unaona Bado Asset=Liabilities+Equity

Hiki tunachozungumzia Hapa Katika Taarifa ya Fedha Huwa Kinaitwa Balance Sheet(Mizania ya Fedha)

Kama Umeelewa Hapa sio mbaya ila kuna mambo mengi sana humu ndani ambayo nitayaweka ila kwa sasa ili uelewa kidogo nafikiri tuachie Hapa.

Taarifa ya Mapato(Income Statement)
Baanda ya kuanzisha Biashara yetu na kuanza uendeshaji sasa inabidi uikatie Pikipiki ya BIMA,UIWEKEE Mafuta Full Tank na Pia Uwakabidhi vijana waanza kazi.Lakini Pia utahitaji ukubaliane na vijana Hesabu kwa siku ni Bei ngap?Ubajeti gharama za Marekebisho ya pikipiki.

Bima ya Piki Piki moja ni 50,000 kwa kawaida ila unaweza kukata pia bima kubwa.Mafuta Full Tak tuseme ni lita 15 na Ghara za Oil change na 15000 kwa mwezi.Hivyo Jumla za Gharama kwa Pikipiki moja kwa kuanzia ni 50000+45000+15000 ambapo Jumla ni 110,000 kisha kila mara utahitaji kurudia gharama ya 60,000 tuseme kwa wiki.Hii ina maana kwamba Pikipiki yako unaweza mafuta full tank kila wiki a kufanya oil change kila wiki au kila unapomaliza full tank unabadilisha na OIL.So Gharama zako kwa wiki ni 60,000 ambayo kwa mwaka ni 60,000*54=3240,000 kwa pikipiki moja ambapo kwa pikipiki zako 4 ni 12,960,000 ukiongeza na 50,000 ya BIMA una Milioni 13,160,000

Sasa Ili Uweze kuhakikisha Biashara yako inakuwa na Faida ina maana kwamba lazima pikipiki zako 4 zikutengenezee mapato ambayo yanazidi haya matumizi.Na hapo bado kijana wako hajajilipa.

Sasa huyu kijana wako hapa unamwambia kwamba unataka hesabu kwa option moja kati ya hizi
  1. 15000 kwa siku na kila baada ya siku saba anakuja unamfanyia service na kumjazia mafuta full tank atajilipa Mwenyewe.
  2. Au unamwambia kwamba Akuletee Hesabu ya 25000 kwa siku na kila baada ya siku 7 anakuja unamwaga OIL unamjazia Full Tank na Kumlipa Shilingi 40,000 kwa wiki.
Tukitumia njia ya Pili ambayo imekaa kijanja zaidi:Mapato yako kwa kila Pikipiki kwa wiki ni 175000 ambayo kwa mwaka ni 9,450,000 na kwa pikipiki 4 ni 37,800,000.Usisahau kwamba kwa sababu huyu kijana kila wiki utakuwa unamlipa 40,000 basi kwa pikipiki 4 utalipa jumla 120,000 kwa wiki ambayo kwa mwaka ni 6,480,000

Kama Unakumbuka Tulikopa Piki Piki Moja ya Milioni 2.5 kwa riba ya 5% ambayo ni sawa na 125000 ambayo kwa wiki utapaswa kulipa shilingi 48,650 ambapo riba ni 2350 na Principal ni 46300.


Sasa Taarifa yetu ya Mapato (Income Statement)itakuw kama ifuatavyo:

Revenue(Jumla ya Mapato)=37,800,000

Matumizi yatakuwa ni:
Bima = 200,000
Riba =125000
Mshahara = 6,480,000
Mafuta =9,720,000
Matengenezo = 3,240,000
Jumla ya Matumizi ni 19765000

Hivyo Basi Faida yako itakuwa ni sawa na 18,035,000.

Kumbuka Mfano huu haulengi kuonesha faida ya biashara ya pikipiki na wala hazina uhusiano na faida katika biashara ya Pikipiki.

Faida hii itatozwa kodi ya 30% ambayo ni sawa na 5,410,500

Faida yako kamili itakuwa ni Milioni 12624500.

Kwa hiyo Taarifa yako ya Fedha itaonesha hizo taarifa hapo juu pamoja na Taarifa zingine kama depreciation n.k.



Sasa nilieleza hapo mwanzoni kwamba Msingi wa hesabu zote ni ule mlinganyo wetu wa mizania ambao unasema Assets = Liabilities +Equity.

Kwa Kawaida Hii Faida huwa inaenda kwa Mmiliki hivyo basi


Asset =10,000,000 +12624500
Liabilities=0(Tumelipia Pikipiki yetu full)
Equity=10,000,000 +12624500

Zingatia pia kwamba kwenye hesabu zangu sijaweka punguzo la Uchakavu(Depreciation)

Hapa Tumemaliza Kuanda Taarifa ya Mapato(Income Statement) na Tayari Tumehamishia Pesa Zetu kwenye Balance Sheet(Mizania)

Taarifa ya Mwisho ni Taarifa ya Mtiririko wa Fedha(Cash Flow Statement)

Hii taarifa inaonesha Pesa Ziliingiaje kwenye Kampuni/Biashara na zilitokaje
Huwa kuna Mtiririko wa Fedha kwa Ajili ya Uwekezaji(Cash flow from Investing)
Kuna Mtiririko wa Fedha kwa Ajili ya Uendesha(Cashflow from Operations)
Kuna Mtiririko wa Fedha kwa ajili ya kuongeza Fedha(Cash flow from Financing)

Uwekezaji ni Pale ambapo unaponunua Assets kwa ajili ya kutengeneza Pesa/Faida Mfano kununua Pikipiki

Operation ni pale unapotumia Pesa kwa ajili ya Uendeshaji mfano kununua mafuta,kulipa wafanyakazi na pia unapopokea mapato kutoka katika uendeshaji

Financing activities ni pale ambapo unapoingiza Pesa kama mmiliki,au kulipa mikopo ya fedha au pikipiki



Kama nilivyoeleza katika utangulizi kwamba Andiko hili sio la kitaalamu na linalenga kuchongoza mjadala kuhusu uelewa wa watu kuhusu Taarifa za fedha.Lengo ni kuhamasisha watu kuwa na tabia ya kutunza kumbukumbu za Fedha na kuandaa taarifa za fedha ili waweze kufahamu hali yao ya kifedha.

Zingatia pia kwamba kila mwaka Tarehe 31Jun unapaswa kuwakilisha Taarifa za Fedha za Biashara yako Mamlaka ya Mapato TRA kwa ajili ya masuala yako ya Kodi na kwamba unapoandaa Taarifa ya Fedha Hakikisha kwamba Unafahamu kwa Hakika ni nini unapeleka TRA.

Kama mfanya biashara ni muhimu ukaelewa Jinsi Taarifa za fedha zinavoandaliwa na Jinsi ya Kuzisoma na Kuzitafsiri kwa wafanya biashara wengi hujikuta wakishangaa wanapoona kwamba Taarifa zao za fedha zinaonesha faida wakati wao wanaona Changamoto kede kede.

karibu Tujadili zaidi na kuongeza Maboresho ya Mjadala.

Nawatakieni Wakati Mwema

Kwa mawasiliano zaidi tumia email:masokotz@yahoo.co
 
Back
Top Bottom