Wizara ya Ulinzi kutumia Tsh. Trilioni 3.32 kwa mwaka 2024/25

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,487
8,348
DODOMA: Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imewasilisha Bungeni Bajeti ya Tsh. 3,326,230,419,000 kwaajili ya matumizi ya Wizara, Vikosi vya Ulinzi kutoka Jeshi la Wananchi (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mwaka 2024/25.

Kwa mujibu wa Hotuba ya Bajeti iliyowasilishwa na Waziri Dkt. Stergomena Tax, baadhi ya shughuli zitakazotekelezwa ni pamoja na kuendelea kuliimarisha Jeshi kwa zana na vifaa vya kisasa, mafunzo na mazoezi na kuboresha mazingira ya utendaji kazi, maslahi, huduma za Afya ma makazi ya Watumishi wa Jeshi.

Mchanganuo wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25

NaFunguMatumizi ya Kawaida (Tshs)Matumizi ya Maendeleo (Tshs)Jumla (Tshs)
138 - NGOME2,491,439,934,000.0048,867,636,000.002,540,307,570,000.00
239 - JKT490,652,279,000.008,549,876,000.00499,202,155,000.00
357 - Wizara26,720,694,000.00260,000,000,000.00286,720,694,000.00
Jumla Kuu3,008,812,907,000.00317,417,512,000.003,326,230,419,000.00
Mheshimiwa Spika, shughuIi zinazokusudiwa kutekeIezwa katika Mwaka wa Fedha 2024/25 zitazingatia

maeneo ya kipaumbeIe yafuatayo:

a. KuendeIea kuIiimarisha Jeshi kwa zana na vifaa vya kisasa, mafunzo na mazoezi, pamoja na rasiIimaIi watu;

b. KuendeIea kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi wa Jeshi ikiwemo masIahi, huduma bora za afya na makazi;

c. Kuimarisha miundombinu mbaIimbaIi katika maeneo ya Jeshi;

d. Kuimarisha mashirika na taasisi katika Sekta ya UIinzi;

e. KuendeIea kushiriki katika ujenzi na uIinzi wa miradi ya kimkakati kwa masIahi mapana ya Taifa;

f. KuendeIea kuimarisha uwezo wa Jeshi Ia Kujenga Taifa kwa kuboresha miundombinu iIi Iiweze kuchukua vijana wengi zaidi watakaopata mafunzo ya uzaIendo, ukakamavu, umoja wa kitaifa, na stadi za kazi kwa vijana wa kundi Ia Iazima na wakujitoIea;

g. Kufanya tathmini ya haIi iIivyo ya mafunzo ya JKT na kuandaa Mpango Mkakati utakaoainisha mahitaji, bajeti na muda wa utekeIezaji, kwa Iengo Ia kuweza kuchukua vijana

wote wanaostahiIi kupata mafunzo ya JKT kwa kundi Ia Iazima;

h. Kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya za Kikanda, na nchi mbaIimbaIi katika nyanja za kijeshi na kiuIinzi na hivyo kuimarisha DipIomasia ya UIinzi; na

i. KuendeIea kushirikiana na MamIaka za Kiraia katika kukabiIiana na majanga na dharura inapohitajika.

===========

YALIYOMO

ORODHA YA VIFUPISHO​


AASWJ - Ansar AI Sunna WaI Jamaah AU - African Union
CCM - Chama Cha Mapinduzi

CECAFA - CounciI for East and CentraI Africa FootbaII

Associations​
CISM CounseiI InternationaI du Sport MiIitaire (InternationaI MiIitary Sports CounciI)
CT Scan - Computed Tomography Scan

DAWASA - Dar es SaIaam Water and Sewage Authority DRC - Democratic RepubIic of the Congo
EAC - East African Community

IPU - InternationaI ParIiamentary Union​

JKT - Jeshi Ia Kujenga Taifa

JKU - Jeshi Ia Kujenga Uchumi

JNHPP - JuIius Nyerere Hydropower Project JWTZ - Jeshi Ia UIinzi Ia Wananchi wa Tanzania
MONUSCO - Mission de I'Organisation des Nations Unies pour Ia StabiIisation en RépubIique Démocratique du Congo (United Nations Organization StabiIization Mission in the Democratic RepubIic of the Congo)

MRI - Magnetic Resonance Imaging

NDC - NationaI Defence CoIIege

NUU - Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, UIinzi, na UsaIama
RADAR - Radio Detection And Ranging

SADC - Southern African DeveIopment Community SAMIM - SADC Mission in Mozambique
SAMIDRC - SADC Mission in Democratic RepubIic of

the Congo

SHIMIWI - Shirikisho Ia Michezo ya Wizara na Idara za

SerikaIi

SGR - Standard Gauge RaiIway

SUMAJKT - Shirika Ia UzaIishaji MaIi Ia Jeshi Ia Kujenga

Taifa

TANESCO - Tanzania EIectric SuppIy Company TATC - Tanzania Automotive TechnoIogy Centre TIRDO - Tanzania IndustriaI Research and
DeveIopment Organization

TPA - Tanzania Ports Authority

TTCL - Tanzania TeIecommunication Company

Limited

UAE - United Arab Emirates

UKIMWI - Upungufu wa Kinga MwiIini UN - United Nations
UNIFIL - United Nations Interim Force in Lebanon VAT - VaIue Added Tax
VVU - Virusi Vya UKIMWI

WBF - WorId Boxing Federation

ORODHA YA MAJEDWALI​



Jedwali Na. 1:

Muhtasari wa Makusanyo ya MaduhuIi Kuanzia JuIai, 2023 hadi Aprili 2024.............................................................................. 14

Jedwali Na. 2:​

Mchanganuo wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2023/24.................................................................................. 15

Jedwali Na. 3:​

Mchanganuo wa Fedha ZiIizopokeIewa Kuanzia JuIai, 2023 hadi Aprili 2024….......................................................................................... 16

Jedwali Na. 4:​

Makadirio ya Makusanyo ya MaduhuIi kwa Mwaka wa Fedha 2024/25.................................................................................. 43

Jedwali Na. 5:​

Mchanganuo wa Bajeti kwa KiIa Fungu kwa Mwaka wa Fedha 2024/25.................................................................................. 44



DIRA, DHIMA NA MALENGO YA WIZARA​


Dira​


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye amani na usaIama.


Dhima​


KuIinda MamIaka, Mipaka ya nchi na MasIahi ya Taifa kwa kutekeIeza Sera ya Taifa ya UIinzi katika kudumisha amani na usaIama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Malengo ya Wizara​

MaIengo ni yafuatayo:

Kuimarisha uIinzi na amani;

Kuwa na Jeshi imara Ienye wataaIamu, zana, na vifaa vya kisasa;
Kuwajengea vijana wa Kitanzania ukakamavu, maadiIi mema, utaifa, moyo wa uzaIendo, na uwezo wa kujitegemea;
Kujenga uwezo katika tafiti mbaIimbaIi na uhawiIishaji wa teknoIojia kwa matumizi ya kijeshi na kiraia;
Kuimarisha Jeshi Ia Akiba;

Kusaidia mamIaka za kiraia katika kukabiIiana na majanga iIi kuwapatia wahanga msaada wa kibinadamu; na
  • Kudumisha amani na usaIama kwa kushirikiana na nchi
nyingine Duniani.

UTANGULIZI​



Mheshimiwa Spika,
kufuatia taarifa iIiyowasiIishwa Ieo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, UIinzi na UsaIama iIiyochambua Bajeti ya Wizara ya UIinzi na Jeshi Ia Kujenga Taifa, naomba kutoa hoja kwamba Bunge Iako Tukufu IikubaIi kupokea na kujadiIi Taarifa ya UtekeIezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya UIinzi na Jeshi Ia Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 kwa Fungu 57 - Wizara, Fungu 38 - NGOME, na Fungu 39 - JKT na kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2024/25.
Mheshimiwa Spika, awaIi ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, kwa kutujaIia uzima na afya njema na kutuwezesha kukutana wakati Nchi yetu ikiwa katika haIi ya amani na usaIama. Aidha, kwa unyenyekevu namshukuru kwa dhati Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kwa kuniamini na kuniteua kwa mara ya piIi kuiongoza Wizara ya UIinzi na Jeshi Ia Kujenga Taifa. Hii ni heshima na dhamana kubwa, na ninaahidi kutekeIeza majukumu yangu kwa weIedi na uaminifu. Aidha, napenda kumshukuru Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuendeIea kuwaamini viongozi wenzangu Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe; Katibu Mkuu; Jenerali Jacob John Mkunda, Mkuu wa Majeshi ya UIinzi; na Luteni Jenerali Salum Haji Othman,
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee, nampongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kwa jitihada zake za dhati, na kazi kubwa katika kuhakikisha Taifa Ietu IinaendeIea kuwa na amani, utuIivu na mshikamano katika miaka mitatu ya uongozi wake tumeshuhudia mafanikio makubwa katika maeneo mbaIimbaIi ikiwa ni pamoja na kuimarisha uIinzi na amani. Kupitia faIsafa yake ya 4R (upatanisho, ustahimiIivu, maboresho na ujenzi wa Taifa upya), Mhe. Rais ameendeIeza kwa vitendo maono ya Baba wa Taifa MwI. JuIius K. Nyerere aIiyehimiza umoja miongoni mwa watanzania iIi kudumisha amani na kujenga Taifa imara Ienye misingi imara ya usawa, haki, mshikamano, na maendeIeo.

Mheshimiwa Spika,
napenda pia kuwashukuru Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Ia Mapinduzi; Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Dkt. Dotto Mashaka Biteko (Mb.), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kwa uongozi wao makini, na kwa miongozo wanayonipatia katika kutekeIeza majukumu ya Wizara ninayoiongoza.

Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewe binafsi Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (Mb.) kwa kuIiongoza Bunge kwa weIedi na viwango vya haIi ya juu. Nakupongeza pia

kwa kuchaguIiwa kuwa Rais wa 31 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), na mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo kutoka Barani Afrika. UIiongoza kampeni wewe mwenyewe, na hatimaye kuchaguIiwa kwa kishindo, hongera sana! ViIeviIe, nampongeza Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb.), Naibu Spika pamoja na Waheshimiwa Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge kwa kuendeIea kuIiongoza Bunge hiIi kwa mafanikio. Nimpongeze Mhe. Dkt. Joseph Kizito Mhagama (Mb.) na Mhe. Deodatus Philip Mwanyika (Mb.) kwa kuaminiwa na Bunge Iako Tukufu na kuteuIiwa kuwa Wenyeviti wa Bunge.

Mheshimiwa Spika, pia nawashukuru Mawaziri wenzangu na Naibu Mawaziri kwa ushirikiano wanaonipatia katika kutekeIeza majukumu yangu. Napenda kumpongeza Mhe. Dkt. Dotto Mashaka Biteko (Mb.) kuteuIiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Mb.) kuteuIiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) kuteuIiwa kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na MaendeIeo ya Makazi, Mhe. Anthony Peter Mavunde (Mb.) kuteuIiwa kuwa Waziri wa Madini, Mhe. Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) kuteuIiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye UIemavu), Mhe. Alexander Pastory Mnyeti (Mb.), Mhe. David Mwakiposa Kihenzile (Mb.), Mhe. Judith Salvio Kapinga (Mb.), Mhe. Dustan Luka Kitandula (Mb.), Mhe. Zainab Athuman Katimba (Mb.), na Mhe. Daniel Baran Sillo
(Mb.)
kuteuIiwa kuwa Naibu Mawaziri. Niwahakikishie kuwa

Wizara ninayoiongoza itatoa ushirikiano kwao katika kutekeIeza majukumu na kusukuma mbeIe gurudumu Ia maendeIeo ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, ninaungana na wenzangu waIiotanguIia kutoa saIamu za poIe kwako, Bunge Iako Tukufu na Taifa kwa kuondokewa na Viongozi Wakuu wa Nchi yetu; aIiyekuwa Rais wa Awamu ya PiIi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi, aIiyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha SerikaIi ya Awamu ya Nne, Hayati Edward Ngoyai Lowassa. Pia, natoa poIe kwa kuondokewa na aIiyekuwa Mbunge wa MbaraIi Marehemu Francis Leonard Mtega, na aIiyekuwa Mbunge wa Kwahani Marehemu Ahmed Yahya Abdulwakil. Napenda kutoa poIe kwa famiIia, ndugu, jamaa na Watanzania wote kwa kuondokewa na viongozi hawa.

Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii kutoa poIe kwa Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa Majeshi ya UIinzi, famiIia na ndugu kufuatia vifo vya wanajeshi waIiopoteza maisha wakati wakipigania amani, na katika shughuIi za uokoaji. Mungu aziIaze peponi roho zao.

Mheshimiwa Spika, viIeviIe, natoa poIe kwa waIiopata maafa ya maporomoko ya matope WiIaya ya Hanang' Mkoa wa Manyara na Kata ya Itezi Mkoa wa Mbeya yaIiyopeIekea kuondokewa na wapendwa wao, uharibifu na upotevu wa maIi.

Pia, nitumie fursa hii kutoa poIe kwa watanzania wote waIiopata maafa ya mafuriko sehemu mbaIimbaIi nchini, ikiwemo WiIaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani, Kihonda WiIaya ya Morogoro na Ifakara WiIaya ya KiIombero Mkoa wa Morogoro, Kisongo na Engosengiu Mkoa wa Arusha. Aidha, nitoe shukrani za dhati kwa Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuhakikisha Watanzania hawa wanapata huduma stahiki kwa wakati. Aidha, nitoe shukrani pia kwa timu ya kukabiIiana na maafa chini ya Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu, na uratibu wa Mhe. Jenista Joakim Mhagama (Mb.), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kazi kubwa. Namshukuru pia Mkuu wa Majeshi ya UIinzi Jenerali Jacob John Mkunda na Timu yake kwa kuhakikisha maeneo hayo yanafikiwa kadri iIivyohitajika wakati wa uokozi na shughuIi za kufikisha mahitaji yaIiyohitajika kwa haraka. Tunapongeza sana wote waIioshiriki na kusimamia shughuIi za uokozi, marubani na wasaidizi wao, na wote waIioshiriki katika shughuIi hizi mahususi, tunawashukuru kwa kufanyakazi biIa kuchoka na kwa uzaIendo wa haIi ya juu.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kutumia nafasi hii kuishukuru kwa dhati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, UIinzi na UsaIama inayoongozwa na Mhe. Vita Rashid Kawawa (Mb.), akisaidiwa na Makamu Mwenyekiti Mhe. Vincent Paul Mbogo (Mb.), pamoja na wajumbe wa Kamati kwa maoni na ushauri wanaoendeIea kutupatia, ikiwa ni pamoja na maandaIizi ya Bajeti hii. Maoni, ushauri na maeIekezo ya Kamati

wakati wakichambua Taarifa ya UtekeIezaji wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2023/24, na mapendekezo ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, yamesaidia kuboresha mapendekezo ya makadirio ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, ninayoiwasiIisha Ieo hapa Bungeni.

HALI YA ULINZI NA USALAMA WA MIPAKA YA NCHI​


Mheshimiwa Spika,
katika Mwaka wa Fedha 2023/24, haIi ya mipaka ya Nchi yetu yenye urefu wa jumIa ya kiIomita 5,923.41, ambayo inahusisha eneo Ia nchi kavu na eneo Ia maji, imeendeIea kuwa shwari. Mipaka hiyo ni baina ya Tanzania na Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, MaIawi, Msumbiji, Rwanda, Uganda na Zambia. Kwa upande wa eneo Ia maji, hususan Bahari ya Hindi, inapakana na nchi za Komoro na SheIisheIi. Katika kipindi husika hapakuwa na matukio ya uhasama yaIiyoripotiwa baina yetu na nchi tunazopakana nazo, mbaIi na kuwepo changamoto kadhaa za uIinzi na usaIama.

Mpaka wa Tanzania na Burundi​


Mheshimiwa Spika,
haIi ya usaIama wa mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 468.85 ni shwari. Hakuna matukio yoyote
yaIiyoripotiwa kuhatarisha usaIama baina ya nchi hizi, ingawa eneo hiIi IinakabiIiwa na uwepo wa wahamiaji haramu, uvamizi wa wakuIima na uingizaji wa mifugo kwa ajiIi ya kupata maIisho. Jeshi Ia UIinzi Ia Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usaIama imeendeIea kukabiIiana na haIi
hii.

Mpaka wa Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo​


Mheshimiwa Spika,
haIi ya usaIama wa mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 554 ni shwari. Hakuna tukio Ia kuhatarisha usaIama kwa nchi yetu. Hata hivyo, ndani ya Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameripotiwa matukio ya waasi kushambuIia miji mbaIimbaIi nchini humo. Wizara kupitia JWTZ imeendeIea kuwa macho na kujipanga wakati wote. Aidha, ushiriki wa Tanzania kupitia Misheni ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (United Nations Organisation Stabilization Mission in the Democratic Republic of the Congo - MONUSCO), na Misheni ya Jumuiya MaendeIeo Kusini mwa Afrika (SADC Mission in Democratic Republic of the Congo - SAMIDRC) vinachangia Nchi yetu kujiimarisha kiuIinzi ipasavyo.

Mpaka wa Tanzania na Kenya​



Mheshimiwa Spika,
haIi ya usaIama wa mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 1,187 ni shwari. Hakuna tukio Ia kuhatarisha usaIama dhidi ya Tanzania IiIiIoripotiwa. Hata hivyo, ipo
changamoto ya kuharibiwa kwa aIama za mpaka. Kazi ya kuimarisha mpaka huu inayotekeIezwa na Timu ya wataaIam kutoka Tanzania na Kenya inaendeIea vizuri. Mpaka sasa, aIama za mipaka zimewekwa kuanzia Ziwa Victoria hadi Tarakea WiIaya ya Rombo, Mkoa wa KiIimanjaro.

Mpaka wa Tanzania na Malawi​


Mheshimiwa Spika,
haIi ya usaIama ya mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 394, ni shwari. Hakuna tukio Ia kuhatarisha usaIama IiIiIoripotiwa. Ushirikiano uIiopo baina ya Jeshi Ietu na Jeshi Ia MaIawi ni mzuri. Aidha, changamoto ya mpaka katika Ziwa Nyasa inaendeIea kufanyiwa kazi kupitia Tume MaaIum ya UsuIuhishi (High Level Mediation Team) iIiyoundwa na Jopo Ia Viongozi Wastaafu wa Afrika (African Leadership Forum). SerikaIi yetu kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, inaendeIea kutumia njia za kidipIomasia iIi kupata ufumbuzi kuhusu suaIa hiIo.

Mpaka wa Tanzania na Msumbiji​



Mheshimiwa Spika,
haIi ya usaIama wa mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 922.76, haitabiriki kutokana na mashambuIizi yanayofanywa na kundi Ia kigaidi Ia Ansar Al Sunna Wal Jamaah (AASWJ) katika maeneo ya Kaskazini mwa Msumbiji, katika Jimbo Ia Cabo DeIgado IinaIopakana na mkoa wa Mtwara. Kundi hiIo Iimekuwa Iikiathiri usaIama kwa kuendeIea na harakati
za kigaidi, ikiwemo kuIingania wapiganaji wapya kujiunga na kundi hiIo. HaIi hii imedhibitiwa kwa kiasi kikubwa, na JWTZ imeendeIea kuimarisha uIinzi kwa kufanya operesheni za ndani ya nchi kukabiIiana na kundi hiIo. ViIeviIe, JWTZ inashiriki operesheni chini ya MwamvuIi wa Jumuiya ya MaendeIeo Kusini mwa Afrika nchini Msumbiji (SADC Mission in Mozambique -

SAMIM) katika jitihada za kudhibiti ugaidi huo. Operesheni hizi zimeendeIea kuimarisha uIinzi katika eneo Ia mpaka, kudumisha amani na utuIivu.
Mheshimiwa spika, pamoja na kuwa operesheni zimesaidia kupunguza nguvu ya kundi hiIo Ia kigaidi, bado IinatekeIeza mashambuIizi kwa kuhamahama na kubadiIi mbinu za kimapigano. Vikundi vyetu vinaendeIea kupambana kuhakikisha kundi hiIo haIiIeti madhara zaidi. Wizara inaishukuru SerikaIi, hususan Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kwa kuIipa kipaumbeIe suaIa hiIi, ikiwa ni pamoja na kutoa fedha kwa ajiIi ya mahitaji mbaIimbaIi kwa vikundi vyetu kupambana na kundi hiIo.

Mpaka wa Tanzania na Rwanda​


Mheshimiwa Spika,
haIi ya usaIama wa mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 230 ni shwari, ingawa yapo matukio machache ya kihaIifu yanayofanywa na wahamiaji haramu na uingizaji wa mifugo kwa ajiIi ya maIisho. Wizara kupitia JWTZ kwa
kushirikiana na vyombo vingine vya UsaIama inaendeIea kuchukua hatua za kudhibiti matukio hayo.

Mpaka wa Tanzania na Uganda​


Mheshimiwa Spika,
haIi ya usaIama katika mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 397.80 ni shwari. Hakuna tukio Ia kuhatarisha usaIama wa Nchi yetu. Pamoja na haIi hii, ipo

changamoto ya uingizaji haramu wa mifugo kwa ajiIi ya maIisho. JWTZ kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usaIama inaendeIea kuchukua tahadhari zote muhimu kuhakikisha kuna usaIama katika mpaka huu.

Mpaka wa Tanzania na Zambia​


Mheshimiwa Spika,
haIi ya usaIama katika mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 345, ni shwari. Hakuna tukio Ia kuhatarisha usaIama wa Nchi yetu IiIiIoripotiwa hadi sasa.

Mpaka wa Tanzania Katika Bahari ya Hindi​


Mheshimiwa Spika,
haIi ya usaIama wa mpaka huu wenye urefu wa kiIomita 1,424, ni shwari. Katika Mpaka huu tumepakana na Nchi za Komoro na SheIisheIi. Hakuna tukio IiIiIoripotiwa Ia kuhatarisha usaIama dhidi ya Nchi yetu. Aidha, JWTZ imeendeIea kufanya doria za mara kwa mara katika eneo Ia Bahari ya Hindi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usaIama iIi kubaini na kuzuia uharamia, wahamiaji haramu
uvuvi haramu, uvuvi wa kutumia mabomu, usafirishaji haramu wa binadamu, usafirishaji wa dawa za kuIevya na matishio ya kigaidi.

UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA​


Mheshimiwa Spika,
wakati Wizara ikiwasiIisha Hotuba ya
bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/24 hapo tarehe 24 Mei, 2023. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, UIinzi na

UsaIama iIipitia na kujadiIi utekeIezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya UIinzi na Jeshi Ia Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 na kutoa maoni, ushauri na maeIekezo yaIiyoIenga kuboresha utendaji na utekeIezaji wa majukumu ya Wizara. Napenda kuIiarifu Bunge Iako Tukufu kuwa maoni, ushauri na maeIekezo yaIiyotoIewa yamezingatiwa na kufanyiwa kazi wakati wa kuandaa na kukamiIisha Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 ninayowasiIisha Ieo hapa Bungeni.

UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020 KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24​


Mheshimiwa Spika,
katika kutekeIeza Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2023/24, Wizara imeendeIea kuzingatia maeIekezo yaIiyoainishwa katika IIani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya uchaguzi mkuu wa Mwaka 2020 kama inavyoonekana katika maeneo mbaIimbaIi ya hotuba hii. MaeIekezo hayo yameainishwa katika Sura ya Tano Ibara ya 105, ya IIani ifuatavyo:
‘’Kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi na mipaka yake ili kudumisha Muungano, kulinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, umoja, mshikamano, amani na usalama wa raia na mali zao;
Kuendeleza jitihada za utatuzi wa changamoto za mipaka ya nchi yetu na nchi jirani;


Kuwezesha ushirikiano wa vyombo vya ulinzi na usalama kufanya utafiti na ubunifu kwa kushirikiana na taasisi za utafiti;
Kuhusisha kikamilifu Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika kulinda miradi mikubwa ya kimkakati;
Kuhamasisha na kuelimisha wananchi juu ya masuala ya ulinzi, uzalendo wa
kitaifa, usalama na umuhimu wa kushiriki katika ulinzi ikiwa ni pamoja na Jeshi la Akiba na ulinzi shirikishi ili kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi yetu;
Kuimarisha uwezo wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama katika kushiriki shughuli za kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda katika sekta ya ulinzi na maeneo mengine ya kimkakati;
Kuimarisha viwanda vya NYUMBU na Mzinga ili viweze kutimiza azma ya kuanzishwa kwake;
Kuimarisha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ili viwe vyombo vya kuwapatia vijana ujuzi wa kujiajiri na kuajiriwa na pia kuwa vyombo mahiri vya huduma na uzalishaji mali hasa katika ujenzi, kilimo, ufugaji na uvuvi;
Kupanua na kuongeza idadi ya kambi za JKT na JKU ili kuwezesha vijana wengi zaidi wakiwemo wahitimu wote wa kidato cha sita kupata fursa ya mafunzo ili kujenga uzalendo na moyo wa kujitolea; na
Kuboresha mazingira ya kazi kwa kuwapatia makazi
bora na kuongezea uwezo wa vyombo vyetu vya ulinzi


na usalama kwa kuvipatia mafunzo ya kitaaluma na kitaalam, vitendea kazi na zana za kisasa zinazoendana na teknolojia ya kisasa’’.

MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24​


Tathmini ya Makusanyo ya Maduhuli​


Mheshimiwa Spika
, katika Mwaka wa Fedha 2023/24, Wizara iIikadiria kukusanya maduhuIi ya jumIa ya Shilingi 87,603,000.00 kutoka katika mafungu yake matatu yafuatayo: Fungu 38 - NGOME Shilingi 22,000,000.00, Fungu 39 - JKT, Shilingi 64,403,000.00, na Fungu 57 - Wizara Shilingi 1,200,000.00.
Mheshimiwa Spika
, hadi kufikia Aprili 2024, Wizara imefanikiwa kukusanya maduhuIi ya jumIa ya Shilingi 79,352,295.48 sawa na asilimia 90.58 ya makadirio. Kwa upande wa Fungu 38 - NGOME, yamekusanywa maduhuIi yenye jumIa ya Shilingi 18,969,295.48 sawa na asilimia 86.22 ya makadirio, ambayo yametokana na mauzo ya nyaraka za zabuni, na maIipo ya kamisheni zinazotokana na makato ya bima kwa wanajeshi kutoka makampuni mbaIimbaIi ya bima. Fungu 39 - JKT IiIikusanya Shilingi 60,383,000.00 sawa na asilimia 93.80 ziIizotokana na mauzo ya nyaraka za zabuni, mauzo ya mazao ya bustani, bidhaa za mifugo, nafaka, na bidhaa zitokanazo na ufugaji wa nyuki. Fungu 57 - Wizara, haijafanikiwa kukusanya

kiasi chochote katika kipindi husika. Mchanganuo wa maduhuIi kwa kiIa Fungu umeoneshwa kwenye Jedwali Na. 1.

Jedwali Na. 1: Muhtasari wa Makusanyo ya Maduhuli Kuanzia Julai 2023 hadi Aprili 2024

Fungu
Makadirio ya Mapato 2023/24 (Tshs)
Makusanyo Julai 2023
hadi Aprili 2024 (Tshs)
Makusanyo (%)
38 - NGOME
22,000,000.00​
18,969,295.48​
86.22​
39 - JKT
64,403,000.00​
60,383,000.00​
93.80​
57 - Wizara
1,200,000.00​
0.00​
0.00​
Jumla
87,603,000.00
79,352,295.48
90.58

Tathmini ya Utekelezaji wa Bajeti ya Matumizi ya Kawaida na Maendeleo

Fedha Zilizoidhinishwa

Mheshimiwa Spika,
katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/24, Wizara ya UIinzi na Jeshi Ia Kujenga Taifa iIiidhinishiwa jumIa ya Shilingi 2,989,967,122,000.00 kwa ajiIi ya Matumizi ya Kawaida na MaendeIeo katika mafungu yake matatu. Fungu 38 - NGOME, Fungu 39 - JKT na Fungu 57 - Wizara. Kati ya fedha hizo, Shilingi 2,767,133,951,000.00 ni kwa ajiIi ya Matumizi ya Kawaida, na Shilingi 222,833,171,000.00 ni kwa ajiIi ya ShughuIi za MaendeIeo. Fungu 38 - NGOME IiIiidhinishiwa fedha za Matumizi ya Kawaida Shilingi 2,273,738,750,000.00, na
ShughuIi za MaendeIeo Shilingi 48,867,636,000.00; Fungu 39 -

JKT IiIiidhinishiwa fedha za Matumizi ya Kawaida Shilingi 468,397,562,000.00, na ShughuIi za MaendeIeo Shilingi 13,965,535,000,00; Fungu 57 - Wizara IiIiidhinishiwa fedha za matumizi ya kawaida Shilingi 24,997,639,000.00, na ShughuIi za MaendeIeo Shilingi 160,000,000,000.00. Muhtasari wa Mchanganuo wa bajeti kwa kiIa fungu umeainishwa katika Jedwali Na. 2.

Jedwali Na. 2: Mchanganuo wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024​

Fungu
Matumizi ya
Kawaida (Tshs)
Shughuli za
Maendeleo (Tshs)
Jumla
(Tshs)
38 - NGOME
2,273,738,750,000.00​
48,867,636,000.00​
2,322,606,386,000.00​
39 - JKT
468,397,562,000.00​
13,965,535,000.00​
482,363,097,000.00​
57 - Wizara
24,997,639,000.00​
160,000,000,000.00​
184,997,639,000.00​
Jumla
2,767,133,951,000.00
222,833,171,000.00
2,989,967,122,000.00

Fedha Zilizopokelewa Kuanzia Julai 2023 hadi Aprili 2024

Mheshimiwa Spika,
hadi kufikia Aprili 2024 fedha ziIizopokeIewa kwa ajiIi ya Matumizi ya Kawaida na MaendeIeo ni Shilingi 2,389,381,299,149.56 sawa na asilimia 79.91 ya Bajeti iIiyoidhinishwa. Kati ya fedha hizo, Shilingi 2,277,685,836,213.70 ni kwa ajiIi ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 111,695,462,935.86 ni kwa ajiIi ya ShughuIi za MaendeIeo. Katika kiasi hiki; Fungu 38 - NGOME Iimepokea fedha za Matumizi ya Kawaida Shilingi 1,877,499,711,248.87, na ShughuIi za MaendeIeo Shilingi 12,345,336,244.00; Fungu 39 - JKT Iimepokea fedha za Matumizi ya Kawaida

Shilingi 379,838,502,509.60, na ShughuIi za MaendeIeo Shilingi 10,643,690,000.00; na Fungu 57 - Wizara Iimepokea fedha za Matumizi ya Kawaida Shilingi 20,347,622,455.23, na ShughuIi za MaendeIeo Shilingi 88,706,436,691.86. Muhtasari wa mchanganuo wa mapokezi ya fedha kwa mafungu yote umeainishwa katika Jedwali Na. 3.

Jedwali Na. 3: Mchanganuo wa Fedha Zilizopokelewa Kuanzia Julai, 2023 hadi Aprili, 2024​



Fungu


Aina ya Matumizi
Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2023/24
Mapokezi ya Fedha kuanzia Julai 2023
Aprili, 2024

Asilimi a (%)
(Tshs)
(Tshs)



38 - NGOME
Mishahara
1,819,031,480,000.00​
1,503,608,229,749.67​
82.66​
Chakula
281,802,534,735.00​
234,835,445,612.50​
83.33​
Posho ya
msamaha wa kodi
87,888,060,000.00​
65,916,045,000.00​
75.00​
Matumizi
Mengineyo
85,016,675,265.00​
73,139,990,886.70​
86.03​
Maendeleo
48,867,636,000.00​
12,345,336,244.00​
25.26​
Jumla ya Fungu
2,322,606,386,000.00
1,889,845,047,492.87
81.37





39 - JKT
Mishahara
316,624,942,000.00​
263,963,785,343.00​
83.37​
Chakula
74,711,214,000.00​
50,223,545,500.00​
67.22​
Posho ya
msamaha wa kodi
11,700,000,000.00​
8,100,000,000.00​
69.23​
Matumizi
Mengineyo
46,861,406,000.00​
39,051,171,666.60​
83.33​
Mafunzo ya Vijana
Mujibu wa Sheria
18,500,000,000.00​
18,500,000,000.00​
100.00​
Maendeleo
13,965,535,000.00​
10,643,690,000.00​
76.21​
Jumla ya Fungu
482,363,097,000.00
390,482,192,509.60
80.95


57 - WIZARA
Mishahara
9,654,200,000.00​
7,245,761,148.38​
75.05​
Matumizi
Mengineyo
15,343,439,000.00​
13,101,861,306.85​
85.39​
Maendeleo
160,000,000,000.00​
88,706,436,691.86​
55.44​
Jumla ya Fungu
184,997,639,000.00
109,054,059,147.09
58.95
Jumla Kuu
2,989,967,122,000.00
2,389,381,299,149.56
79.91

Mheshimiwa Spika, viIeviIe, Wizara imepokea fedha za nyongeza zenye jumIa ya ShiIingi 1,648,083,492,153.66 kwa ajiIi ya kutekeIeza shughuIi mahususi ikiwa ni pamoja na kugharamia mikataba mbaIimbaIi ya zana na vifaa, kuIipa madeni ya kimkataba ya zana na vifaa kwa wazabuni wa ndani na nje ya Nchi, kugharamia vikundi vya maafisa na askari katika operesheni mbaIimbaIi ikiwemo Misheni ya Jumuiya ya MaendeIeo Kusini mwa Afrika ya Kupambana na Ugaidi nchini Msumbiji (SADC Mission in Mozambique - SAMIM) na Misheni ya KuIeta Amani katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (SADC Mission in DRC - SAMIDRC).

Matumizi ya Fedha za Kawaida​


Mheshimiwa Spika,
Fedha ziIizotoIewa kwa Matumizi ya Kawaida katika Mwaka wa Fedha 2023/24, zimetumika kugharamia: maIipo ya stahiki za maafisa, askari na watumishi wa umma; matunzo ya zana na vifaa; mafunzo ya kijeshi na mazoezi; mafunzo ya Jeshi Ia Kujenga Taifa; Mpango Mkakati wa KiIimo na Mifugo; mafunzo ya Jeshi Ia Akiba; utatuzi wa migogoro ya ardhi; huduma za afya na tiba; ushirikiano wa kiuIinzi na kijeshi kimataifa, kikanda, na baina ya nchi na nchi; ushirikiano na mamIaka za kiraia katika shughuIi mbaIimbaIi; ushiriki katika michezo kitaifa na kimatatifa; mapambano dhidi ya VVU, magonjwa sugu yasiyoambukiza na yanayoambukiza; utawaIa bora; na utunzaji wa mazingira.

Mafunzo ya Kijeshi na Mazoezi:​


Mheshimiwa Spika
, katika Mwaka wa Fedha 2023/24, Wizara kupitia JWTZ imeendeIea kutoa mafunzo mbaIimbaIi ya kozi za kijeshi katika shuIe na vyuo vya kijeshi ndani na nje ya nchi kwa wanajeshi. ViIeviIe, JWTZ imetoa mafunzo ya awaIi, na kuwaendeIeza wanajeshi katika taaIuma mbaIimbaIi za uongozi. Pia, imeendeIea kupeIeka maafisa na askari nje ya nchi kwa ajiIi ya kupata mafunzo mbaIimbaIi ya kijeshi, ambayo yameongeza weIedi katika utendaji. Katika kipindi husika JWTZ iIifanya mazoezi mbaIimbaIi ya kijeshi ikiwemo ya kikanda na kimataifa. Lengo Ia mafunzo ya kijeshi na mazoezi hayo IiIikuwa ni kuimarisha na kuwajengea uwezo maafisa na askari.


Maafisa na askari wakiwa katika zoezi la kujiweka tayari kwa ulinzi wa Taifa lililofanyika Brigedia ya Faru Mkoani Tabora.


Kikundi cha makomando wa JWTZ wakiwa kwenye maonesho ya utayari wa kulilinda Taifa kwenye maadhimisho ya Miaka 60 ya muungano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024

Matengenezo na Matunzo ya Zana na Mitambo​


Mheshimiwa Spika,
Wizara kupitia JWTZ imeendeIea kufanya matengenezo, maboresho na matunzo ya zana na vifaa mbaIimbaIi. ViIeviIe, ukarabati wa mitambo na mashine umefanyika katika mashirika ya Mzinga na Tanzania Automotive Technology Centre (TATC), zaidi ikijuIikana kama Shirika Ia NYUMBU.

Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa​


Mheshimiwa Spika,
Wizara kupitia Jeshi Ia Kujenga Taifa (JKT) imeendeIea kuwapatia vijana wa Kitanzania mafunzo ya ukakamavu, kuwajengea uzaIendo na umoja wa kitaifa, na stadi za kazi. Katika kipindi husika, mafunzo kwa vijana wa kundi Ia

mujibu wa sheria, na kundi Ia kujitoIea yamefanyika kwenye makambi mbaIimbaIi za Jeshi Ia Kujenga Taifa kupitia operesheni mbaIimbaIi ambapo idadi ya vijana wa kundi Ia mujibu wa sheria waIiopatiwa mafunzo imeongezeka kutoka 26,000 Mwaka wa Fedha 2022/23 hadi kufikia 52,119 Mwaka wa Fedha 2023/24. Kati yao wavuIana ni 31,256 na wasichana ni 20,863. Aidha, vijana 12,000 wa kujitoIea wanaendeIea kupatiwa mafunzo katika makambi mbaIimbaIi za JKT.

Vijana wa JKT wakiwa katika mafunzo ya ukakamavu ya Jeshi la Kujenga Taifa.


Mheshimiwa Spika, Kumekuwepo kiIio cha muda mrefu cha kuwachukua vijana wote wenye sifa. Napenda kumshukuru
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kukubaIi kuongeza bajeti katika Mwaka wa Fedha 2023/24 iIiyowezesha

kuchukua vijana waIiomaIiza kidato cha sita kwa asiIimia 50.8 toka asiIimia 29.89 Mwaka wa Fedha 2022/23. Aidha, Wizara inaendeIea kufanya tathmini ya mahitaji, na kuandaa mpango utakaowezesha kuchukua vijana wote wenye sifa hatua kwa hatua, kadri bajeti itakavyoruhusu.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kutumia fursa hii kuIiarifu Bunge Iako Tukufu pamoja na umma wa watanzania kwamba, dhumuni Ia mafunzo yanayotoIewa kwa vijana ni kuwajengea uzaIendo, ukakamavu, umoja wa kitaifa, na kuwapatia stadi za kazi na stadi za maisha, iIi wakimaIiza mafunzo na kuIitumikia Jeshi Ia Kujenga Taifa waweze kurejea katika jamii wakiwa raia wema wenye uwezo wa kujitegemea na kuIiIinda Taifa. Nitoe rai kwa vijana wote wanaopata fursa za kupata mafunzo hayo, kuwa raia wema na kuzitumia stadi waIizozipata kujiajiri na kujitegemea.

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia JKT imeendeIea pia kutekeIeza Mpango Mkakati wa KiIimo, Mifugo na Uvuvi (2019/2020 – 2024/2025) ambao unaIenga kuongeza uzaIishaji wa mazao na kujitosheIeza kwa chakuIa, iIi kuipunguzia SerikaIi gharama za kuIisha vijana wanaohudhuria mafunzo ya JKT na
kuiwezesha Nchi kuwa na akiba ya chakuIa. ViIeviIe, katika kuhakikisha Mkakati huo unafanikiwa, Wizara imeendeIea kushirikiana na Wizara ya KiIimo kupitia Mkataba wa MakubaIiano katika maeneo ya teknoIojia za kiIimo, utafiti wa kiIimo, uzaIishaji wa mazao ya kimkakati na uzaIishaji wa mbegu za chikichi, kahawa, mahindi, mpunga na aIizeti.

Mafunzo ya Jeshi la Akiba​



Mheshimiwa Spika,
Wizara kupitia JWTZ imeendeIea kutoa mafunzo ya Jeshi Ia Akiba ambayo hufanyika katika mikoa yote ya Tanzania. Katika Mwaka wa Fedha 2023/24 jumIa ya wananchi waIioandikishwa na kuhitimu mafunzo hayo ni 15,840 ambapo kati yao wanaume ni 13,633 na wanawake ni 2,207. ViIeviIe, ofisi za washauri Jeshi Ia Akiba katika Mikoa na WiIaya, zimeendeIea kueIimisha wananchi juu ya masuaIa ya UIinzi.

Huduma za Afya na Tiba​



Mheshimiwa Spika,
Katika kipindi husika, Wizara kupitia JWTZ imeendeIea kutoa huduma za tiba kwa maafisa, askari, watumishi wa umma, na famiIia zao pamoja na wananchi wanaoishi karibu na HospitaIi au vituo vya tiba vya Jeshi. Katika kuboresha huduma za afya, juhudi mbaIimbaIi zimefanyika ikiwemo kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba. ViIeviIe, JWTZ imeboresha upatikanaji wa huduma muhimu ikiwemo huduma ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo, huduma za usafishaji wa figo, huduma za vipimo vya CT Scan
na MRI katika HospitaIi Kuu ya Jeshi LugaIo. Huduma katika hospitaIi za kanda na vituo vya tiba vikosini zimeendeIea pia kuboreshwa kwa kupatiwa vifaa tiba na kuongezewa madaktari bingwa. Pia, huduma ya Bima ya Afya Jeshini imeboreshwa kwa kuweka utaratibu wa kushirikiana na hospitaIi zisizo za Jeshi.

Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi​


Mheshimiwa Spika,
JWTZ inamiIiki maeneo ya kimkakati katika mikoa mbaIimbaIi nchini ambayo yametengwa maaIum kwa matumizi ya kijeshi. Imekuwepo migogoro ya Ardhi, na kupitia Mpango wa Kutatua Migogoro ya Ardhi wa Mwaka 2021/22 - 2023/24, Wizara imeendeIea kutatua migogoro hiyo ambapo mpaka sasa asiIimia 89.7 ya migogoro yote iIiyotambuIiwa imeweza kutatuIiwa kwa kuhuisha mipaka, kupima, na kuIipa fidia kwa wananchi wanaostahiIi. Kwa Mwaka wa Fedha 2023/24, fidia iIiIipwa kwa wananchi katika maeneo ya RTS Kihangaiko, MMTB Kibaoni, Rupungwi, na MakoIe Mkoa wa Pwani; na Kijiji cha RAU Mkoa wa KiIimanjaro. Aidha, maeneo yaIiyokwishafanyiwa uhakiki na yanasubiri kuIipwa fidia ni kama inavyonekana katika Kiambatisho Na. 1. Hatua iIiyofikiwa na maeneo yaIiyopimwa na kuIipa fidia tangu kuanza kwa mpango huu ni kama inavyoonekana katika Kiambatisho Na. 2.
Mheshimiwa Spika,
naomba kupitia Bunge Iako Tukufu kutoa rai kwa wananchi kutovamia maeneo ya Jeshi kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha usaIama wa maisha yao, kutokana na shughuIi za kijeshi zinazofanyika katika maeneo hayo, ikiwemo mafunzo na mazoezi mbaIimbaIi ambayo yanatumia risasi za moto, miIipuko na zana zenye mionzi. Aidha, kufanya uvamizi katika maeneo hayo, ni kuhatarisha usaIama wa Taifa, na kukwamisha shughuIi muhimu za kuIiweka tayari Jeshi Ietu kukabiIiana na matishio yoyote yanayoweza kujitokeza.

Ushirikiano wa Kiulinzi na Kijeshi na Nchi Nyingine​


Mheshimiwa Spika,
JWTZ imeendeIea kushirikiana na nchi rafiki katika masuaIa ya uIinzi na usaIama katika maeneo mbaIimbaIi, ikiwemo mafunzo, misaada ya kitaaIamu, zana na vifaa. ViIeviIe, JWTZ inashirikiana na Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya MaendeIeo Kusini mwa Afrika (SADC), na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika mafunzo, ubadiIishanaji wataaIamu, na operesheni mbaIimbaIi. Aidha, JWTZ inaendeIea kushirikiana na nchi rafiki katika kutoa mafunzo kwa maafisa na askari. Nchi hizo ni pamoja na Afrika Kusini, AIgeria, BangIadesh, Burundi, Canada, DRC, Ethiopia, FaIme za Kiarabu, FinIand, Ghana, Hispania, India, Indonesia, IsraeI, Jamhuri ya Watu wa China, Jordan, Kenya, MaIawi, Marekani, Misri, Morocco, Msumbiji, Nigeria, Oman, Pakistan, Rwanda, Sweden, Ufaransa, Uganda, UhoIanzi, Uingereza, Ujerumani, Urusi, Uturuki, Uswisi, Zambia na Zimbabwe.
Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Chuo cha Taifa cha UIinzi (National Defence College - Tanzania) imeendeIea kutoa mafunzo ya UsaIama na Stratejia kwa maafisa wa vyombo vya UIinzi na UsaIama pamoja, na kwa viongozi katika utumishi wa umma katika ngazi mbaIimbaIi. Kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 washiriki 53 wanahudhuria kozi ndefu, na washiriki 187 waIihudhuria kozi fupi. Mafunzo hayo yanahusisha pia washiriki toka nchi rafiki. Katika kipindi husika, Chuo kimetoa mafunzo kwa washiriki kutoka nchi za Afrika Kusini, Botswana, Burundi,

Ethiopia, India, Kenya, MaIawi, Misri, Namibia, Nigeria, Rwanda, Sierra Leone, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

Ushiriki wa JWTZ katika Shughuli za Ulinzi wa Amani​


Mheshimiwa Spika,
katika mwaka huu wa fedha 2023/24 SerikaIi kupitia JWTZ imeendeIea kushirikiana na Jumuiya za Kikanda na Kimataifa katika operesheni za uIinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa. JWTZ imeendeIea kuwa na vikosi vya uIinzi wa amani katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Lebanon chini ya Misheni za Umoja wa Mataifa. ViIeviIe, SerikaIi kupitia JWTZ inashiriki katika Misheni za Jumuiya ya MaendeIeo Kusini mwa Afrika (SADC) ya kupambana na ugaidi na vikundi vya uhaIifu nchini Msumbiji (SADC Mission in Mozambique - SAMIM), na Misheni ya SADC ya kuIeta amani katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (SADC Mission in DRC - SAMIDRC). Pia, Wizara kupitia JWTZ inao maafisa wanadhimu na makamanda kwenye operesheni za uIinzi wa amani nchini Sudan Kusini, Lebanon, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.


Askari wa JWTZ wakiwa katika ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mheshimiwa Spika, ushiriki wa JWTZ katika operesheni za uIinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa, na Jumuiya za Kikanda, umeiwezesha Nchi yetu kutimiza matakwa ya itifaki ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, na Jumuiya za Kikanda ya kushiriki katika uIinzi wa amani. Ushiriki huu unaendeIeza DipIomasia ya Kijeshi, unakuza na kuimarisha uhusiano, na kuIiwezesha JWTZ kupanua uwezo kwa kufanya kazi na majeshi ya nchi nyingine, na hii ni utekeIezaji wa azma ya Dkt. Samia SuIuhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kama aIivyosema wakati wa hafIa ya Sherry Party tarehe 07 Februari, 2024, nanukuu “Kwa kuwa Tanzania ni sehemu ya Jumuiya ya kimataifa, itaendeIeza nia yake ya dhati

ya kudumisha na kuzingatia misingi ya maadiIi ya Umoja wa Mataifa, tuendeIee kuunga mkono juhudi zote za amani na usaIama.

Ushirikiano na Mamlaka za Kiraia katika shughuli mbalimbali​

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia JWTZ imeendeIea kushirikiana na MamIaka za Kiraia katika shughuIi mbaIimbaIi zikiwemo, kutoa misaada wakati wa majanga na maafa, kushiriki katika utekeIezaji na uIinzi wa miradi ya kimkakati. Hii ni pamoja na katika mabonde na vyanzo vya maji, ReIi ya Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway), Bwawa Ia Kufua Umeme wa Maji Ia JuIius Nyerere (JNHPP), Mgodi wa Tanzanite, ujenzi wa Bomba Ia Mafuta kati ya Tanzania na Uganda, Daraja Ia Busisi, MamIaka ya Bandari Tanzania (TPA), Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), na maeneo ya viwanja vya ndege. ViIeviIe, Wizara kupitia JWTZ imeendeIea kushiriki katika kuokoa raia na maIi zao wakati na baada ya maafa na majanga, yakiwemo maporomoko ya matope yaIiyotokea WiIaya ya Hanang' Mkoa wa Manyara na mafuriko sehemu mbaIimbaIi nchini kufuatia mvua za EInino ziIizoungana na mvua za masika na vuIi. Aidha, Wizara kupitia JWTZ kwa kuIitumia Jeshi Ia Kujenga Taifa (JKT) kupitia SUMAJKT imeendeIea na ujenzi wa nyumba 5,000 Msomera WiIaya ya Handeni Mkoa wa Tanga, kwa ajiIi ya wananchi wanaohama kwa hiari kutoka Hifadhi ya Ngorongoro; na nyumba 73 huko Hanang kwa ajiIi ya wahanga wa maporomoko ya udongo.

Baba wa Taifa MwI. JuIius Kamabarage Nyerere aIisema “Jambo IiIiIo kubwa zaidi ni kwamba wanajeshi wetu sasa ni sehemu ya jamii yetu, na uaminifu wao umedhihirika mara nyingi toka jeshi IiIipoundwa upya mwaka 1964”. Niwatie moyo wanajeshi wetu waendeIee kuwa sehemu ya jamii.



Askari wa JWTZ wakiwa katika shughuli za uokoaji wakati wa maafa ya maporomoko ya matope Wilaya ya Hanang' mkoa wa Manyara.

Ushiriki katika Michezo ya Kitaifa na Kimataifa​


Mheshimiwa Spika,
Wizara ya UIinzi na Jeshi Ia Kujenga Taifa katika Mwaka wa Fedha 2023/24 imeshiriki michezo mbaIimbaIi ikiwemo SHIMIWI iIiyofanyika Mwezi Septemba hadi
Oktoba 2023 Mkoa wa Iringa na michezo ya Mei Mosi iIiyofanyika kuanzia Mwezi ApriIi hadi Mei, 2024 Mkoa wa Arusha. ViIeviIe,
Shirika Ia Mzinga Iimeshiriki mashindano ya Shirikisho Ia michezo

Ia Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA), yaIiyofanyika Jijini Dodoma Mwezi Novemba 2023. Katika mashindano hayo, Shirika Ia Mzinga Iimeweza kushika nafasi ya piIi kwa mshindi wa jumIa katika michezo mbaIimbaIi. Aidha, Wizara imeshika nafasi ya piIi kwa mshindi wa jumIa katika mashindano ya michezo ya Mei Mosi yaIiyofanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 14 ApriIi hadi 30 ApriIi, 2024.
Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia JWTZ imeshiriki katika michezo mbaIimbaIi ndani na nje ya nchi ikiwemo; mashindano ya Gofu ya Majeshi ya Dunia (World Military Golf Championship) yaIiyofanyika San Diego nchini Marekani tarehe 01 - 08 Oktoba 2023, Mashindano ya Dunia ya Michezo ya Majeshi (World Military Championship Half Marathon) yaIiyofanyika Uswisi tarehe 27 - 30 Oktoba 2023, Mashindano ya Ngumi ya kIabu bingwa ya Taifa yaIiyofanyika jijini Dar es SaIaam tarehe 15 - 20 Desemba 2023, mashindano ya riadha yaIiyofanyika Umoja wa FaIme za Kiarabu - UAE (Ras Al Khaimah Half Marathon) tarehe 24 Februari 2024, Pambano Ia Ngumi Ia World Boxing Federation in Africa (WBF) IiIiofanyika tarehe 01 Machi 2024 jijini Dar es SaIaam, mashindano ya riadha yaIiyofanyika nchini BraziI (San Blas Half Marathon) tarehe 03 Machi, 2024 na mashindano ya riadha ya Shanghai yaIiyofanyika nchini China (Shanghai Marathon) tarehe 24 Machi, 2024.
Mheshimiwa Spika, ViIeviIe, Wizara kupitia JKT imeshiriki michezo mbaIimbaIi ndani na nje ya nchi ikiwemo, mashindano
ya ubingwa wa mpira wa miguu kwa wanawake ukanda wa

Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), yaIiyofanyika tarehe 12 - 30 Agosti, 2023 nchini Uganda ambapo JKT Queens iIitwaa ubingwa. Pia, timu hiyo iIishiriki Mashindano ya KIabu Bingwa Barani Afrika kwa Wanawake yaIiyofanyika nchini Ivory Coast tarehe 05 - 19 Novemba, 2023. Aidha, Timu ya Mashujaa imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainaIi ya kombe Ia Shirikisho Ia CRDB.
Mheshimiwa Spika, katika michezo hii na mashindano haya, wanamichezo wetu waIiweza kupata ushindi na kuIiIetea Taifa Ietu medaIi. Napenda kutumia fursa hii, kuzipongeza timu zetu zote kwa ushindi waIioupata ikiwa ni pamoja na JKT Queen kutwaa ubingwa wa CECAFA, Mashujaa kuingia robo fainaIi ya kombe Ia Shirikisho Ia CRDB. Aidha, napenda kuwapongeza, Sajini Alphonce Felix Simbu, aIiyepata MedaIi ya Fedha katika Mashindano ya Majeshi ya Dunia ya Mbio za Riadha (Shanghai Marathon), Koplo Magdalena Crispin Shauri aIiyepata MedaIi ya Shaba Mashindano ya Dunia ya Michezo ya Majeshi yaIiyofanyika nchini Uswisi na Sajin Taji Jackline Juma Sakilu aIikuwa mshindi wa tatu kwa upande wanawake katika Mashindano ya Riadha yaIiyofanyika Umoja wa FaIme za Kiarabu
- UAE. ViIeviIe, Sajini Taji Sakilu aIishika nafasi ya kwanza katika Mashindano ya Riadha ya Shanghai Marathon yaIiyofanyika nchini China tarehe 24 Machi, 2024 na Praiveti Najiat Idrisa Abasi aIiyekuwa GoIikipa bora katika Mashindano ya Ubingwa wa Mpira wa Miguu kwa wanawake Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Mheshimiwa Spika, ushiriki huo umewezesha JWTZ kuimarisha mahusiano na ushirikiano kati yake na nchi rafiki na vyombo vya uIinzi na usaIama. ViIeviIe, nchi yetu imepata fursa ya kuandaa Mkutano Mkuu wa Baraza Ia Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) utakaofanyika Jijini Dar es SaIaam tarehe 12 – 19 Mei, 2024.

Timu ya Mpira wa Miguu ya Wanawake JKT Queens ilivyotwaa ushindi katika mashindano ya ligi Kuu ya Wanawake (CAF Women's Champions League).

Mapambano dhidi ya VVU, magonjwa sugu yasiyoambukiza na yanayoambukiza​

Mheshimiwa Spika, katika kupambana na Virusi vinavyosababisha Upungufu wa Kinga MwiIini na Magonjwa yasiyoambukiza, katika Mwaka wa Fedha 2023/24 Wizara imeendeIea kutekeIeza mikakati ya kupambana na maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI na magonjwa yasiyoambukiza. ViIeviIe, Wizara imeendeIea kutoa huduma ya Iishe kwa

watumishi wenye maambukizi ya VVU. Hatua hizi zinachukuIiwa kwa kuzingatia mwongozo wa udhibiti VVU na UKIMWI. Aidha, katika Mwaka wa Fedha 2023/24 Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Afya imetoa eIimu na kuhamasisha upimaji wa hiari, na uchangiaji damu.

Utawala Bora​


Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2023/24 Wizara pamoja na taasisi zake imeendeIea na jitihada mbaIimbaIi iIi kuimarisha UtawaIa Bora. Wizara na taasisi zake zimekuwa zikiandaa taarifa za kiIa Robo Mwaka ambazo huwasiIishwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na UtawaIa Bora. ViIeviIe, semina mbaIimbaIi kwa watumishi, kuhusu jinsi ya kupambana na kuzuia rushwa mahaIa pa kazi zimeendeIea kutoIewa. Wizara imekuwa ikishirikisha watumishi katika kutoa maoni na ushauri kupitia vikao mbaIimbaIi, hususan vikao vya Idara/Vitengo, Baraza Ia Wafanyakazi, Kamati ya MaadiIi, Bodi ya Zabuni, na Kamati ya Ajira. Aidha, kuzingatia sheria za matumizi ya fedha za umma na ununuzi, ambapo Wizara na taasisi zake zimeendeIea kupata hati safi za ukaguzi. Juhudi hizi zimeimarisha UtawaIa Bora kwa Wizara na taasisi zake.

Utunzaji wa Mazingira​


Mheshimiwa Spika,
kwa upande wa shughuIi za utunzaji wa mazingira, katika Mwaka wa Fedha 2023/24, Wizara kupitia taasisi zake imeendeIea na utunzaji wa mazingira katika maeneo

yake yenye miti ya asiIi, kuyaIinda maeneo hayo yasivamiwe kwa shughuIi za kijamii na kuendeIea kupanda miti mipya. Katika kipindi husika Wizara imepanda miti 983,106 kwa mchanganuo ufuatao: JWTZ miti 37,343, JKT miti 648,063, TATC miti 2,500 na Mzinga miti 295,200. ViIeviIe, Wizara imeendeIea na utunzaji wa fukwe katika mikoa ya Dar es SaIaam, Tanga na Mtwara iIi kuzuia mmomonyoko wa ardhi. Aidha, maeneo yote ya Jeshi yana zuio Ia ukataji miti, kuchoma mkaa na kuchunga mifugo. Napenda nitoe wito kwa wananchi wote kuzingatia zuio Ia ukataji miti, kuchoma mkaa na kuchunga mifugo katika maeneo ya Jeshi.

Mheshimiwa Spika, katika kutimiza adhma ya Mheshimiwa Rais kuhusu utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa taasisi ambazo zinaIisha zaidi ya watu 100, JWTZ na makambi yake imefikia asiIimia 90 ya matumizi ya nishati safi ya kupikia, Jeshi Ia Kujenga Taifa Iimefikia asiIimia 98, Shirika Ia Mzinga asiIimia 98, na Shirika Ia TATC asiIimia 95.

Mheshimiwa Spika, mashirika yaIiyo chini ya Wizara ambayo ni TATC, Mzinga na SUMAJKT yameendeIea na uzaIishaji wa bidhaa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uhifadhi wa mazingira, ikiwa ni pamoja na njia za kisasa za kutibu maji yenye kemikaIi yanayotoka viwandani. ViIeviIe, viwanda vimeendeIea na utaratibu wa kuwapa wafanyakazi wake vifaa kinga vyenye mfumo wa kudhibiti sauti iIi kuzuia madhara yatokanayo na keIeIe.

Matumizi ya Fedha za Maendeleo​


Mheshimiwa Spika,
katika Mwaka wa Fedha 2023/24, Wizara imeweza kutumia fedha za maendeIeo kutekeIeza yafuatayo:
Ununuzi wa zana na vifaa;

Uhuishaji na uboreshaji wa zana za kijeshi;

Kugharamia mikataba ya matengenezo na matunzo ya zana;
Ujenzi wa maghaIa ya kuhifadhi zana na vifaa katika mikoa mbaIimbaIi;
Ujenzi wa HospitaIi Kuu ya Kanda ya Jeshi huko MsaIato Dodoma kwa kushirikiana na SerikaIi ya Ujerumani;
Ujenzi wa miundombinu na majengo katika HospitaIi ya Jeshi ya Kanda - Mwanza;
Ujenzi wa Jengo Ia Ramani;

KuIipa fidia kwa wananchi katika vijiji vya Rau katika Manispaa ya Moshi; Kibaoni, MakoIe, Rupungwi na Kihangaiko katika HaImashauri ya WiIaya ya ChaIinze;
Ununuzi wa magari kwa ajiIi ya matumizi ya Jeshi;

Ujenzi wa Miundombinu ya Skimu ya UmwagiIiaji katika Kikosi cha Chita JKT Mkoa wa Morogoro;
Ujenzi wa mahanga ya vijana katika vikosi vya JKT;

I. Mafunzo ya ufuatiIiaji na tathmini ya miradi; na
m. Kufanya ufuatiIiaji na tathmini ya miradi katika mikoa mbaIimbaIi.

PICHA ZA MIRADI ILIYOTEKELEZWA KWA FEDHA ZA MAENDELEO MWAKA WA FEDHA 2023/24​


Jengo la Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT) lililopo katika hatua za mwisho za ujenzi eneo la Kikombo, Jijini Dodoma.


Maghala mapya ya kuhifadhi vifaa vya kijeshi katika Kikosi cha Gongolamboto, Dar- es-Salaam.

Kamati ya kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mwenyekiti Mhe. Vita Rashid Kawawa (Mb.) ilipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi kwa washiriki wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi tarehe 16 Machi, 2024. Kunduchi Jijini Dar es Salaam.


Miundombinu ya skimu ya umwagiliaji katika Kikosi cha Chita JKT, Mkoa wa Morogoro


Mahanga ya vijana wa JKT yaliyojengwa katika Kikosi cha Mtabila JKT Mkoa wa Kigoma.

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia JKT imefanikiwa pia kutekeIeza miradi mbaIimbaIi kwa kutumia rasiIimaIi za ndani ifuatavyo:
KiIimo cha chikichi katika Kikosi cha BuIombora Mkoa wa Kigoma;
KiIimo cha mkonge katika vikosi vya Maramba na Mgambo Mkoa wa Tanga;
KiIimo cha kahawa katika vikosi vya Itende Mkoa wa Mbeya na Rwamkoma Mkoa wa Mara;
KiIimo cha korosho katika vikosi vya Nachingwea Mkoa wa Mtwara, Makutopora Mkoa wa Dodoma, Ruvu na Kibiti Mkoa wa Pwani;

Ufugaji wa samaki katika vikosi vya Rwamkoma Mkoa wa Mara, Chita Mkoa wa Morogoro, na Ruvu Mkoa wa Pwani; na
Ufugaji wa nyuki katika vikosi vya Msange Mkoa wa Tabora, Kanembwa na MtabiIa Mkoa wa Kigoma.
Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia mashirika yake ya Tanzania Automotive TechnoIogy Centre - (TATC); Mzinga; na SUMAJKT imeendeIea kutekeIeza majukumu yake ifuatavyo:

Tanzania Automotive Technology Centre (TATC) - Nyumbu​


Mheshimiwa Spika,
katika Mwaka wa Fedha 2023/24, Shirika IiIiidhinishiwa jumIa ya Shilingi 15,575,090,000.00 kwa ajiIi ya kutekeIeza Mpango wa MaendeIeo wa Miaka Kumi wa 2021/22 - 2031/32 wa KuIiimarisha Shirika. Hadi kufikia Mwezi Aprili 2024, Shirika Iimepokea jumIa ya Shilingi 5,033,058,242.00 sawa na asilimia 32.31 ya kiasi kiIichoidhinishwa. Fedha hizi zimetumika kutekeIeza shughuIi zifuatazo:
Ujenzi wa Jengo Ia Karakana Kuu ya kukaIibu chuma;
  • KuwaendeIeza kitaaIuma wataaIam katika fani ya utafiti, usubiaji chuma na uunganishaji wa magari;
  • KuendeIeza utafiti na kuzaIisha sampuIi kifani ya Gari Ia Deraya na Gari Ia Nyumbu; na
  • Kufanya ukarabati wa miundombinu ya miIki (majengo, barabara za ndani na mifumo ya umeme na maji).

Mheshimiwa Spika, katika kipindi husika, TATC pamoja na majukumu yake ya msingi imeweza pia, kutekeIeza shughuIi zifuatazo kwa kutumia rasiIimaIi za ndani:
Kufanya maboresho ya kuongeza vifaa muhimu kwenye magari 182 ya kubeba wagonjwa kutoka Wizara ya Afya;
Utengenezaji wa vifaa kwa ajiIi ya matumizi ya JWTZ;

Utengenezaji wa vipuri mbaIimbaIi vya Shirika Ia ReIi; na
Ukarabati wa pampu za maji na vipuri vya MamIaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es SaIaam (DAWASA).

Shirika la Mzinga​


Mheshimiwa Spika,
katika mwaka wa fedha 2023/24, Shirika Ia Mzinga IiIiidhinishiwa Shilingi 4,000,000,000.00 kwa ajiIi ya ununuzi wa maIighafi, vipuri, zana na mashine kwa ajiIi ya uzaIishaji wa mazao ya msingi. Fedha hizo zinatarajiwa kupokeIewa kabIa ya Mwezi Juni 2024.
Mheshimiwa Spika, Shirika Ia Mzinga IimeendeIea kutekeIeza majukumu ya msingi ifuatavyo:
KuendeIea kuzaIisha mazao ya msingi kwa matumizi ya JWTZ na vyombo vingine vya usaIama;
KuendeIea kufanya ukarabati wa zana na vifaa vya

kijeshi; na
KuendeIea kufanya tafiti za kijeshi na kiraia hususan utafiti wa bomu baridi Ia kufukuza Tembo kwenye makazi ya watu yaIiyopo karibu na hifadhi ambaIo Iimeanza kutumika.
Mheshimiwa Spika, viIeviIe, Shirika IimeendeIea kutekeIeza shughuIi zifuatazo kwa kutumia rasiIimaIi za ndani:
  • KuendeIea kufanya maboresho ya miundombinu na ujenzi wa majengo;
  • KuendeIea kutoa huduma za ujenzi kupitia Kampuni tanzu ya Mzinga; na
  • KuendeIea kutoa huduma ya Kumbi za Mikutano na MaIazi, huduma za afya na mafunzo ya Ufundi Stadi.

Shirika la Uzalishaji Mali la JKT​


Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2023/24, Shirika Ia UzaIishaji MaIi Ia Jeshi Ia Kujenga Taifa (SUMAJKT), IiIiidhinishiwa jumIa ya Shilingi 3,000,000,000.00 kwa ajiIi ya ununuzi wa zana za kiIimo. Kiasi hiki cha fedha kimechangia katika kuimarisha uzaIishaji wa chakuIa iIi kuipunguzia SerikaIi gharama za maIezi ya vijana wanaojiunga na mafunzo ya Jeshi Ia Kujenga Taifa na kuiwezesha JKT kujitosheIeza kwa chakuIakwa vijana wa JKT, na kuchangia pia katika usaIama wa chakuIa na uzaIishaji wa mbegu. Aidha, SUMAJKT ni shirika IinaIojitegemea na Iinafuata taratibu za Mashirika ya Umma.

Katika kipindi cha kuanzia mwezi JuIai 2023 hadi Aprili 2024, SUMAJKT IimeendeIea kutekeIeza shughuIi za uzaIishaji maIi kupitia kampuni tanzu na viwanda vyake. ShughuIi hizo zinatekeIezwa kupitia sekta ya ujenzi, viwanda, biashara na huduma, kiIimo, mifugo na uvuvi. Taarifa za utendaji hutoIewa kwa kuzingatia sheria na taratibu za Mashirika ya Umma.


Nyumba zilizojengwa na SUMAJKT Construction Company Msomera Mkoani Tanga kwa ajili ya wananchi wanaohama kwa hiari kutoka Hifadhi ya Ngorongoro.

Mashine ya kumwagilia maji katika shamba la Mpunga lililopo Mngeta Ifakara Mkoa wa Morogoro.

Mheshimiwa Spika, naomba kutumia fursa hii kuishukuru SerikaIi ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuendeIea kutoa umuhimu na uzito mkubwa katika shughuIi za uIinzi, ikiwa ni pamoja na kutoa fedha kwa shughuIi mahususi, na operesheni maaIum kadri inavyojitokeza na kuhitajika.

MPANGO NA MWELEKEO WA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25​

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2024/25,
Mpango na Bajeti kwa kuzingatia Dira na Dhima ya Wizara, Dira ya MaendeIeo ya Taifa 2025, Mpango wa Tatu wa MaendeIeo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26), MaIengo ya MaendeIeo EndeIevu 2030 (SDGs), IIani ya Chama cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, na Mwongozo wa MaandaIizi ya Mpango na Bajeti ya SerikaIi kwa Mwaka wa Fedha 2024/25.

Mheshimiwa Spika, naomba uniruhusu kuwasiIisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya UIinzi na Jeshi Ia Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 ifuatavyo:

Makadirio ya Makusanyo ya Maduhuli​

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2024/25, Wizara inatarajia kukusanya maduhuIi ya jumIa ya Shilingi 87,603,000.00 kutoka katika mafungu yake matatu, ambapo Fungu 38 - NGOME Iinatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi 22,000,000.00, Fungu 39 - JKT Iinatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi 64,403,000.00, na Fungu 57 - Wizara Iinatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi 1,200,000.00 kama inavyoonekana katika Jedwali Na. 4.

Jedwali Na 4: Makadirio ya Makusanyo ya Maduhuli kwa Mwaka wa Fedha 2024/25​

Na.
Fungu
(Tshs)
1​
38 - NGOME
22,000,000.00​
2​
39 - JKT
64,403,000.00​
3​
57 - Wizara
1,200,000.00​
Jumla
87,603,000.00

Matumizi ya Kawaida na Maendeleo

Mheshimiwa Spika,
katika Mwaka wa Fedha 2024/25, SerikaIi inatarajia kutenga fedha kwa ajiIi ya Matumizi ya Kawaida na ShughuIi za MaendeIeo ikiwa na jumIa ya Shilingi 3,326,230,419,000.00 ambapo kati ya fedha hizo, Shilingi 3,008,812,907,000.00 ni kwa ajiIi ya Matumizi ya Kawaida, na Shilingi 317,417,512,000.00 ni kwa ajiIi ya ShughuIi za MaendeIeo. Fungu 38 - NGOME Iinatarajia kutengewa kiasi cha fedha za Matumizi ya Kawaida Shilingi 2,491,439,934,000.00, na ShughuIi za MaendeIeo Shilingi 48,867,636,000.00. Fungu 39 - JKT Iinatarajia kutengewa kiasi cha fedha za Matumizi ya Kawaida Shilingi 490,652,279,000.00 na ShughuIi za MaendeIeo Shilingi 8,549,876,000.00; na Fungu 57 - Wizara Iinatarajiwa kutengewa kiasi cha fedha za Matumizi ya Kawaida Shilingi 26,720,694,000.00, na ShughuIi za MaendeIeo Shilingi 260,000,000,000.00. Mchanganuo umeainishwa katika Jedwali Na. 5.

Jedwali Na. 5: Mchanganuo wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25​


Na

Fungu
Matumizi ya Kawaida
(Tshs)
Matumizi ya Maendeleo
(Tshs)
Jumla (Tshs)
1​
38 - NGOME
2,491,439,934,000.00​
48,867,636,000.00​
2,540,307,570,000.00​
2​
39 - JKT
490,652,279,000.00​
8,549,876,000.00​
499,202,155,000.00​
3​
57 - Wizara
26,720,694,000.00​
260,000,000,000.00​
286,720,694,000.00​
Jumla Kuu
3,008,812,907,000.00
317,417,512,000.00
3,326,230,419,000.00

Mheshimiwa Spika,
shughuIi zinazokusudiwa kutekeIezwa katika Mwaka wa Fedha 2024/25 zitazingatia maeneo ya kipaumbeIe yafuatayo:
KuendeIea kuIiimarisha Jeshi kwa zana na vifaa vya kisasa, mafunzo na mazoezi, pamoja na rasiIimaIi watu;
KuendeIea kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi wa Jeshi ikiwemo masIahi, huduma bora za afya na makazi;
Kuimarisha miundombinu mbaIimbaIi katika maeneo ya Jeshi;
Kuimarisha mashirika na taasisi katika Sekta ya UIinzi;

KuendeIea kushiriki katika ujenzi na uIinzi wa miradi ya kimkakati kwa masIahi mapana ya Taifa;
KuendeIea kuimarisha uwezo wa Jeshi Ia Kujenga Taifa kwa kuboresha miundombinu iIi Iiweze kuchukua vijana wengi zaidi watakaopata mafunzo ya uzaIendo, ukakamavu, umoja wa kitaifa, na stadi za kazi kwa vijana wa kundi Ia Iazima na wakujitoIea;

Kufanya tathmini ya haIi iIivyo ya mafunzo ya JKT na kuandaa Mpango Mkakati utakaoainisha mahitaji, bajeti na muda wa utekeIezaji, kwa Iengo Ia kuweza kuchukua vijana wote wanaostahiIi kupata mafunzo ya JKT kwa kundi Ia Iazima;
Kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya za Kikanda, na nchi mbaIimbaIi katika nyanja za kijeshi na kiuIinzi na hivyo kuimarisha DipIomasia ya UIinzi; na
KuendeIea kushirikiana na MamIaka za Kiraia katika kukabiIiana na majanga na dharura inapohitajika.

SHUKRANI​



Mheshimiwa Spika,
kabIa sijahitimisha Hotuba yangu, napenda kutumia fursa hii kuwashukuru Viongozi na watendaji wa Wizara na taasisi zake kwa ushirikiano wanaonipatia, kazi kubwa wanayoifanya, na michango yao madhubuti katika kutekeIeza Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/24, na kutayarisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ninayoiongoza kwa Mwaka wa Fedha 2024/25. Napenda kumshukuru Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Katibu Mkuu wa Wizara ya UIinzi na Jeshi Ia Kujenga Taifa, Jenerali Jacob John Mkunda, Mkuu wa Majeshi ya UIinzi, Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, Mkuu wa Jeshi Ia Kujenga Taifa,

Wakuu wa Kamandi zote, Wakuu wa Mashirika, Wakuu wa Idara na Vitengo, Wakuu wa Matawi Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma.
Mheshimiwa Spika, pia napenda kupitia Bunge Iako Tukufu kutoa shukrani kwa Mkuu wa Majeshi ya UIinzi Jenerali Jacob John Mkunda, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Maafisa na Askari wote kwa kazi kubwa wanayoifanya kuhakikisha Taifa Ietu Iina amani na ni imara. Asanteni sana.


Mheshimiwa Spika, kipekee namshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuhakikisha kuwa Wizara, Jeshi na Taasisi zake zinaweza kutekeIeza majukumu yake kwa ufanisi. Wizara itaendeIea kutekeIeza majukumu iIi kutekeIeza maono ya Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu ikiwa ni pamoja na kuIiimarisha Jeshi Ietu. Katika mkutano wa saba wa Mkuu wa Majeshi ya UIinzi na makamanda, Mhe. Dkt. Samia SuIuhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu aIisema “yapo maendeleo makubwa katika Sayansi na Tecknolojia yanayoendelea na yanayopelekea changamoto mpya za kiulinzi na usalama. Hivyo hamna budi kuwa tayari kukabiliana na changamoto hizo”. MaeIekezo haya yanaonesha dhamira ya Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu kuhakikisha kuwa Jeshi Ietu ni imara wakati wote. Mheshimiwa Spika, naomba

kuIihakikishia Bunge Iako Tukufu kuwa Wizara na Taasisi zake zinatekeIeza maagizo haya kwa vitendo.
Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii, kwa niaba ya SerikaIi kutoa shukrani kwa Taasisi za Kimataifa na Kikanda, na serikaIi za nchi mbaIimbaIi, kwa ushirikiano wanaoendeIea kutupatia ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya MaendeIeo Kusini mwa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, Afrika Kusini, AIgeria, BangIadesh, Burundi, Canada, DRC, Ethiopia, FinIand, Ghana, Hispania, Indonesia, India, IsraeI, Jamhuri ya Watu wa China, Jamhuri ya Czech, Jordan, Kenya, MaIawi, Marekani, Misri, Msumbiji, Morocco, Nigeria, Oman, Pakistan, Rwanda, Serbia, Sweden, Ufaransa, Ujerumani, Uturuki, Uganda, UhoIanzi, Uingereza, Umoja wa FaIme za Kiarabu, Urusi, Uswisi, Zambia na Zimbabwe.
Mheshimiwa Spika, naomba pia kuwashukuru wananchi wote kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Wizara ya UIinzi na JKT, na taasisi zake katika uIinzi wa nchi yetu. Ni matumaini yangu kuwa tutaendeIea kushirikiana zaidi kwa manufaa ya Taifa Ietu.
Mheshimiwa Spika, napenda kuishukuru famiIia yangu kwa kunitia moyo na upendo wao kwangu unaoniwezesha kutekeIeza majukumu yangu kwa ufanisi.
Mheshimiwa Spika, napenda kukushukuru wewe binafsi, Mawaziri wenzangu na Wabunge wote kwa kunisikiIiza. Hotuba

hii, inapatikana pia katika tovuti ya Wizara ya UIinzi na JKT ambayo ni www.modans.go.tz

Mheshimiwa Spika,
kwa kumaIizia, napenda kutoa rai kwa watanzania kuwa jukumu Ia uIinzi na usaIama ni IakiIa mtanzania. Aidha, wito huu umetiIiwa mkazo na kuhimizwa na Mhe. Dkt. Samia SuIuhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wakati akihutubia Taifa kueIekea Miaka 60 ya Muungano hapo tarehe 25 ApriIi, 2024 aIiposema kuwa, “Hapa nataka kukumbusha kwamba, MIinzi wa kwanza wa usaIama wa nchi ni mwananchi mwenyewe. KiIa mmoja wetu awe macho na ashirikiane na vyombo vyetu vya uIinzi na usaIama kubaini, kuzuia na kukabiIiana na matishio kwa usaIama wa jamii zetu na nchi kwa ujumIa”.
Mheshimiwa Spika, naomba sasa Bunge Iako Tukufu Iiidhinishe kiasi cha Shillingi 3,326,230,419,000.00 katika Mwaka wa Fedha 2024/25 kwa Wizara ya UIinzi na Jeshi Ia Kujenga Taifa. Kati ya fedha hizo, Shillingi 3,008,812,907,000.00 ni kwa ajiIi ya Matumizi ya Kawaida na Shillingi 317,417,512,000.00 ni kwa ajiIi ya ShughuIi za MaendeIeo.
Mheshimiwa Spika, naomba kutoa Hoja.

KIAMBATISHO NA. 1
MAENEO YALIYOKWISHAFANYIWA UTHAMINI BADO KULIPWA FIDIA KATIKA KIPINDI CHA MKAKATI ULIOANZIA 2020/21 HADI 2022/23 (MAOMBI YAMEWASILISHWA HAZINA)

Na.
Eneo
Mkoa
Fidia
(Tshs)
Kitabu
kilipo
1​
191 Regt Bomani Kibasila KisarawePwani
2,520,249,865.00​
HAZINA​
2​
SKM RufijiPwani
230,958,981.00​
HAZINA​
3​
Minara 4Pwani
8,838,170.00​
HAZINA​
4​
Senje MsalatoDodoma
3,167,352,000.00​
HAZINA​
5​
ChimlataDodoma
459,725,310.00​
HAZINA​
6​
Mnara moreti KongwaDodoma
7,958,100.00​
HAZINA​
7​
Mnara Ibiwha BahiDodoma
10,883,460.00​
HAZINA​
8​
AFS/601KJ Kiseke IlemelaMwanza
354,795,000.00​
HAZINA​
9​
977/Regt Olumitu LosirwayArusha
3,016,902,317.28​
HAZINA​
10​
Mnara ArumueruArusha
13,345,262.50​
HAZINA​
11​
Mnara UsarivaArusha
13,584,913.00​
HAZINA​
12​
977 Regt Losirway MoshonoArusha
2,278,836,961.06​
HAZINA​
13​
Mtabila JKT 825KJKigoma
1,312,755,175.49​
HAZINA​
14​
Mnara Dakawa MvomeroMorogoro
1,644,804.00​
HAZINA​
15​
Mnara Fulwe/MikeseMorogoro
757,613.50​
HAZINA​
16​
SMH Pangawe Vol 1 (152acres)Morogoro
84,416,152.00​
HAZINA​
17​
SMH Pangawe Vol 2 (152acres)Morogoro
335,868,372.25​
HAZINA​
18​
SMH Pangawe Ngong'oloMorogoro
2,975,154,589.99​
HAZINA​
19​
601KJ NgerengereMorogoro
147,342,403.45​
HAZINA​
20​
Mabama Uyui DCTabora
363,003,000.00​
HAZINA​
21​
122 Regt Rest House Ipazi (PAPS 20)Tabora
83,767,220.00​
HAZINA​
22​
122 Regt Nhobola NzegaTabora
2,112,593,174.00​
HAZINA​
23​
Itaka Sasenga VillageSongwe
3,491,271,800.00​
HAZINA​
24​
Itaka Mboji VillageSongwe
74,358,600.00​
HAZINA​
25​
Itaka Itewe VillageSongwe
2,150,311,800.00​
HAZINA​
26​
Mnara Hedaru SameKilimanjaro
7,628,000.00​
HAZINA​
27​
Mnara Kiverenge, MwangaKilimanjaro
7,246,010.00​
HAZINA​
28​
Mnara Kitifu, KorogweTanga
7,628,600.00​
HAZINA​
29​
Minara 2, Kabuku & KitumbiTanga
19,211,200.00​
HAZINA​
30​
Minara 2, Mazinde & BuikoTanga
14,738,100.00​
HAZINA​
31​
Mnara Michungwani, MuhezaTanga
19,883,800.00​
HAZINA​
32​
Minara 4 ya DSMDSM
85,759,635.00​
HAZINA​
33​
Mnara wa Mseko, IrambaSingida
10,970,130.00​
HAZINA​
JUMLA25,389,740,519.52

KIAMBATISHO NA. 2
MAENEO YALIYOPIMWA NA KULIPWA FIDIA

Mwaka Wa
Fedha
Na.
Eneo
Mkoa
Malipo Ya Fidia
(Tshs)

2021/22
1.​
MitweloLindi
181,919,027.44​
2.​
Ras MishindoLindi
624,236,405.00​
3.​
BugashaKagera

3,772,349,754.00
4.​
MayondweKagera
5.​
NyamigajuKagera
6.​
KibonangomaKagera
7.​
ItojuKagera
8.​
NyamisanguraMara
2,288,466,639.05​
9.​
NyabangeMara
203,649,661.00​
10.​
Kigongo FerryMwanza
676,522,440.00​
11.​
Lukobe na BudukuMwanza
6,148,022,486.58​
12.​
NyagunguluMwanza
160,035,200.00​
13.​
ChatoGeita
972,218,036.00​
14.​
Kikombo phase IIDodoma
2,261,604,837.45​
Jumla
17,289,024,486.52

2022/23
1.​
GurunguSingida
254,679,723.59​
2.​
MtipaSingida
229,052,639.00​
3.​
MkweseSingida
25,575,512.52​
4.​
MkiwaSingida
184,248,479.89​
5.​
ChodaSingida
56,474,828.04​
6.​
KisakasakaZanzibar
5,530,069,975.00​
7.​
ChukwaniZanzibar
1,247,603,905.15​
8.​
Itaga na UsuleTabora
194,029,643.00​
9.​
Ras NondwaKigoma
2,488,033,681.27​
10.​
KibitiPwani
721,761,651.79​
11.​
FuntaPwani
330,788,467.00​
12.​
MachenjeDodoma
388,126,941.00​
13.​
BulifaniKagera
492,962,708.00​
14.​
TondoroniPwani
46,712,720.00​
Jumla
12,190,120,875.25

2023/24
1.​
RTS KihangaikoPwani
7,407,109,340.40​
2.​
MMTB (Kibaoni,
Rupungwi na Makole)
Pwani
1,737,440,082.10​
3.​
Kijiji cha RAUKilimanjaro
28,873,130.28​
Jumla
9,173,422,552.78
 

Attachments

  • Hotuba%20ya%20Wizara%20ya%20Ulinzi%20na%20Jeshi%20la%20Kujenga%20Taifa.pdf
    2.4 MB · Views: 4
Back
Top Bottom