Wizara ya Afya kuzindua Chanjo ya Saratani ya mlango wa kizazi Nov 26, 2022

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
575
2,559
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema Novemba 26, 2022 watazindua upya utoaji wa chanjo ya Saratani ya Mlango wa kizazi nchini kwa wasichana ili kuwakinga dhidi ya aina hii ya saratani.

A8801D9B-D4DE-4557-BD90-AE619097FEED.jpeg


“Tulianzisha sisi chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana (HPV vaccine), ikaanza vizuri. Lakini kukapita siasa na misconception, myth kwamba chanjo hii itawafanya wasichana wasizae au kupata watoto, tukarudi nyuma” amesema Waziri Ummy

Waziri Ummy amesisitiza kuwa chanjo hii imethibitika pasi na shaka kuwa ni salama na inao ufanisi wa kuwakinga watoto wa kike wasipate ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi.

Amesema wao kama serikali hawawezi kukubali kuona kati ya watanzania 66 wanaofariki kila mwaka kutokana na saratani, asilimia 21 wanakuwa na saratani ya mlango wa kizazi.

Alisema haya Novemba 3, 2022 kwenye Halfa ya kupokea mashine 50 za kutibu mabadiliko ya awali ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake kutoka Shirika la Clinton Health Access Initiatives (CHAI)

Jamii ya virusi vya Human papillomavirus (HPV) hupatikana katika aina zaidi ya mia moja, lakini aina ya 16 na 18 ndizo huhusika kwa zaidi ya 70% katika kusababisha maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi.
 
Back
Top Bottom