Waziri wa Ardhi hana imani na mahakama; wizara yake inawezaje kutoa hati, ikatuhumu, ikaweka wafu ndani, then ikahukumu?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
912
4,247
Waziri wa Ardhi anapojiona yeye ni zaidi ya mahakama siyo utumishi mzuri. Jukumu la wizara yake nikutoa haki ya umiliki wa ardhi. Yeye siyo mahakama kwamba anaweza akahukumu kuita watu majina ya ajabu ajabu.

Tunafahamu kwamba yeye ana chuki binafsi na baadhi ya watu. Ukitaka kufahamu ana chuki binafsi hakuna kiongozi yeyote wa wizara yake aliyetoa hati kimakosa amekamatwa wala kuhojiwa . Lakini pia ikumbukwe kwamba hawa wanaoitwa matapeli siyo wafanyakazi wa wizara ya ardhi. Hawa ni wafanya biashara ambao walifika ardhi wakapewa umiliki. Kama walitumia rushwa kupata umiliki hao waliopokea rushwa wako wapi?

Kwanini yeye asiishie kwenye jukumu lake la kisheria la kufuta miliki ya ardhi, then akaacha mahakama ifanye kazi pale ambapo aliyefutiwa miliki atapingana na matakwa yake.?

Kwanini anajiona so perfect kutukana na kudhalilisha watu na hataki kusikia hoja za mahakama ?

Nchi za wenzetu hakuna utaratibu wa waziri kuweka watu ndani; siyo kila mtuhumiwa lazima awekwe ndani. Some of watuhumiwa wanapaswa kuhojiwa na kufikishwa mahakamani then watakwenda kujitetea.

Tukisoma ripoti ya haki jinai haya yalipigwa marufuku lakini waziri anakuja kupinga hata maelekezo ya Tume ya haki jinai ambayo iliundwa na Rais. Kama waziri anapingana na mteule wake huo utumishi uliotukuka utapatikanaje?

Twende mbele tuache kurudi kule alipotupeleka Mzee JPM.. Ukiweka watu ndani siyo kigezo kwamba unafanya kazi ni kigezo cha kushindwa kutoa huduma. Mahabusu zinajaa kwa sababu ya mawaziri na viongozi ambao mambo yasiyohitaji nguvu kubwa wanatumia nguvu kubwa.

Tukubali kwamba hatuwezi kuwa mawaziri wa Ardhi, tukawa mawaziri wa mambo ya ndani then tukawa pia majaji kwa wakati mmoja......turidhike na madaraka tuliyopewa.
 
Matapeli wa viwanja safari hii mmepigwa na kitu kizito, mlizowea kucheza na Mahakama, kuzarau hadi Hukumu za Mahakama mnazichana mbele ya Majaji, safari hii ni tit for tat!!
 
Back
Top Bottom