DodomaTZ
Member
- May 20, 2022
- 72
- 108
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax, Machi 31, 2024 ameungana pamoja na Waumini wa Dini ya Kikristu katika ibada ya kusherekea Sikukuu ya Pasaka katika Kigango cha Shishani, kilichopo Parokia ya Mtakatifu Kizito Kabila, Magu, chini ya Jimbo Kuu la Mwanza.
Akitoa salamu za Pasaka Parokiani hapo, WaziriTax, ameshukuru kwa kupata wasaa wa kujumuika na Waamini katika Sikukuu hiyo muhimu kwa Wakristu duniani kote kukumbuka Ufufuo wa Yesu Kristu.
Waziri Stergomena amechukua fursa hiyo kumshukuru Mungu kwa baraka anazoendelea kulipatia Taifa letu ikiwa ni pamoja Na mshikamano, amani, na maendelea katika sekta mbalimbali za m kijamii na kiuchumi.
Aidha, ametoa rai kwa waumini wa Parokia ya Mtakatifu Kizito kuendelea kuiombea Tanzania pamoja na Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na viongozi wanaomsaidia katika nafasi mbalimbali. Waziri Tax ameshiriki ameahidi kuendelea kuchangia kwenye ujenzi wa Kanisa unaondelea kila apatapo nafasi kuwa yeye ni sehemu ya Kata ya Shishani.
Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Kizito Kabila, Padri Andrea Buhembo, amemshukuru Waziri Stergomena Tax kwa moyo wa upendo na ukarimu aliounyesha wa kujiwekea utaratibu wa kukumbuka kwao, katika hali zote amekuwa akishiriki kwa namna moja ama nyingine katika shughuli za kijamii na kiimani.