Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,033
- 974
DKT. STERGOMENA ASIMULIA KUANZISHWA KWA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ)
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax amesema Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) limepitia hatua mbalimbali za mabadiliko mara baada ya uhuru wa Tanganyika Disemba 9,1961 ambapo miongoni mwa mabadiliko hayo ni maasi ambayo waliyafanya kwenye Jeshi la wakoloni
Dkt. Stergomena ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Mungano wa Tanganyika na Zanzibar
Dkt. Stergomena amesema wakati huo Jeshi la JWTZ lilikuwa likiitwa Jeshi la Tanganyika hivyo Januari 20, 1961 katika kambi ya Colito ambayo sasa ni Lugalo wanajeshi wa Tanganyika walifanya maasi kwenye Jeshi ya kikoloni na maasi hayo ndio yaliyopelekea kuanzishwa kwa Jeshi la wananchi wa Tanzania(JWTZ)
Dkt. Stergomena amesema maasi hayo yalitokana na Jeshi la Mkoloni kuendelea kushikilia uongozi wa Juu wa Kijeshi kwa kutetea dola ya kikoloni japo kulikuwa na mabadiliko ya uongozi wa bendera ambayo waliwakabidhi Jeshi la Tanganyika