Waziri Mkuu Majaliwa: TANESCO imezalisha umeme zaidi ya mahitaji

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
400
1,004
Waziri Mkuu majaliwa ameipongeza TANESCO kwa kuzalisja umeme zaidi ya mahitaji yaliyopo sasa, "Leo tarehe 19 April 2024 uzalishaji wa umeme ni mkubwa, shirika letu la TANESCO limemudu kuzalisha umeme zaidi ya mahitaji tuliyonayo na bwawa la Nyerere limeanza kazi, tayari Megawati 235 ziko kwenye mfumo."

Ametoa pongezi hizo leo jioni, April 19, 2024 wakati akifungua maonesho ya Wiki ya Nishati yaliyofanyika kwenye viwanja vya bunge Dodoma.

Ameitaka Wizara ya Nishati iwwke mkakati wa kuhahakisha maonesho hayo yanakuwa endelevu ili wabunge waweze kupata fursa ya kuwasilisha hoja zao mahususi na kutatua kero za wananchi wanaowawakilisha

Ameitaka wizara hiyo iweme mkakati wa kuhahakisja wananchi wote wanapata ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu fursa zinazopatikana kutokana na miradi inayotekelezwa na sekta ya nishati

Wakati akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wadau mbalimbali walioshiriki maonesho hayo, Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko ameipongeza TANESCO kwa kuendelea kufanya kazi nzuri ya kuhahakisha wananchi wanapata nishati ya umeme

 
Hajasema chochote kuhusu ni wananchi wangapi wanafaidika na umeme huo na bado wangapi wanasikia tu kuwa kuna nishati ya umeme lakini hawajawahi maishani mwao kuitumia nishati hiyo, na wala hawajui kama wataitumia katika maisha yao yaliyosalia hapa duniani.

Majigambo ya aina hii yatawasaidia kitu gani watu kama hao?
 
Back
Top Bottom