Watumishi wa umma tulionyimwa mshahara wa Machi kwasababu ya PEPMIS tumeumaliza mwezi salama, hatujawa ombaomba

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,911
36,754
Hello!

Serikali ilikosea sana kutunyima mshahara wa Machi baadhi ya watumishi wa umma kwasababu ya kutokukamilisha PEPMIS.

Nikiri kuwa kazini kwetu hakuna aliyepata semina wala kidudu gani, tuliwekewa tu tangazo Whatsapp tujiunge wenyewe. Mimi binafsi niliona simple nikajiunga nikaona mchezo umeisha kwakuwa nawaza ku log in na out. Kumbe kuna vipengere vingine.

Mpaka HR wetu alinyimwa mshahara wa Machi. Ilikuwa uzembe wa makao makuu. Imagine uzembe wa makao makuu nanyimwa Mimi mshahara ambao ni kamshahara kadogo. Pia hata kama makao makuu walizembea mahali bado haikuwa haki mtumishi yeyote kunyimwa mshahara wake kwa issue za kitoto.

Binafsi huu mwezi nimeumaliza salama from 22 Machi mpaka 21 Machi. Nasubiri kesho kama nitapata mshahara maana nimejaza lote. Kama sitalipwa kwasababu labda nimechelewa kujaza au sababu nyingine nitamwomba boss anipe likizo ya mwezi mmoja maana nitaishia jela.

Maana hasira zangu zitanipeleka kutafuta mshahara kila siku. Yaani kila nikitoka kazini nitoke na mshahara wa mwezi. Hii itaniharibia. Kwa amani tu nitaomba likizo ya mwezi mpaka nianze kuona mshahara.
 
Safi sana, nyie mnafanya kazi kimazoea huku hamna jipya la kuongeza ufanisi huko mnakofanya kazi. Kitu kidogo kama hiko mnashindwa vp kukikamilisha
 
Hahahaha uzembe wenu bana, bongo hadi vitu vidogo mnataka mfundishweeee kama watoto wadogo,

Katika hili serikali imefanya vizuri sanaa
Watu wanataka posho za semina-elekezi.

Waulize sasa kutumia simu nani aliwafundisha? Simu-janja ni sawa na kompyuta tu lakini kwenye kompyuta watu wanasomaga kozi na kupata cheti, ila sijawahi ona kozi ya kutumia simu-janja. Sasa mtu wa dizaini hiyo analalamika kwamba hakufundishwa kujaza taarifa tu kwenye tovuti!
 
Tunajaza activity progress za PEPMIS kwa bei nafuu kabisa, tutengeneza Employee Performance Plan na ku-update daily performance kila week.

Karibu inbox
 
Back
Top Bottom